UM waisaidia Libya kukabilii usafirishaji haramu wa binadamu:

Kusikiliza /

Mmoja wa wahamiaji waliorejeshwa kwa hiyari kutoka Libya akifanya ujasiriamali. Picha na IOM

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM uko bega kwa bega na serikali ya Libya katika kukabili usafirishaji haramu wa binadamu. Kwa mujibu wa Maria do Valle Ribeiro naibu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Libya , hiyo ni biashara haramu na ya hatari inayoathiri watu wengi wanaotaka kwenda kusaka mustalkhbali bora ughaibuni kupitia Libya.

Kwa kulitambua hilo Bi Ribeiro amesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yako msitari wa mbele kusaidia

(MARIA CUT 1)

"IOM na UNHCR bila shaka katika upande wa ulinzi pia katika kusaidia kurejea nyumbani kwa hiyari na kushirikiana na mamlaka ya Libya kuhakikisha kwamba huduma inayotolewa inatosheleza na inazingatia vigezo vya kimataifa."

Ameongeza kuwa unapolitazama suala la usafirishaji haramu ni muhimu kutizama pia mazingira yanayochangia

(MARIA CUT 2)

“Ndio maana ni muhimu kuangalia uhamiaji Libya au wahamiaji halali kwenda Libya , sio tu kama tatizo la ndani la Libya bali kama tatizo la kikanda na kuangalia changamoto za kiuchumi ambazo zinachagiza usafirishaji haramu na njia za kushirikiana na jamii husika kuwapa suluhu mbadala."

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031