UM waikosoa Marekani kushindwa kukemea siasa za ubaguzi

Kusikiliza /

Onyesho la upendo kwa wote. Picha:NICA/51602

Kamati ya Umoja wa mataifa ya kupiga vita vya ubaguzi wa rangi inayoendelea na kikao chake mjini Geneva Uswis (CERD) leo  imeikosoa serikali ya marekani pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa kwa kushindwa kukemea maandamano ya chuki, kibaguzi na uhalifu uliotokea Charlottesvilles Virginia na nchini kote. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kamati hiyo ambayo inafuatilia utekelezaji wa mkataba wa kimataifa kuhusu utokemozaji wa mifumo yote ya ubaguzi wa rangi imesema "popote duniani hakupaswi kuwa na fursa ya chuki za kibaguzi na fursa ya kuruhusu fikra za utukuzaji wa watu weupe au dalili yoyote inayopinga kanuni za msingi za haki na usawa wa kibinadamu duniani kote.

Kufuatia maandamo ya kibaguzi yaliyofanywa na makundi kama Ku Klux Klan (KKK)  na Neo Nazi yaliosababisha kifo cha Bi Heather Heyer, Mkuu wa kamati hiyo Bi Anastasia Crickley ameiomba serikali ya marekani kusimamia  sheria ya haki za kibinadamu kwa wote huku ikihakikisha inafanya uchunguzi wa kina kwa makundi hayo yenye mlengo wa kuwabagua watu wenye asili ya Kiafrica, dini  mbalimbali na haswa wahamiaji kutoka mataifa megine.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930