Pande mbili husika zina wajibu katika jawabu la swala la Palestina- Jenča

Kusikiliza /

Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hali Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina. Picha: UM/Evan Schneider

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina.

Akihutubia kikao hicho Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu maswala ya kisiasa Miroslav Jenča amewataka viongozi wa Palestina kuzingatia matokeo haribifu yanayotokana na migawanyiko Palestina na kufikia makubaliano ili kuwezesha mamlaka Palestina kutekeleza wajibu Gaza katika juhudi za kuunda serikali ya kidemokrasia Palestina.

Hivyo Bwana  Jenča amesema…

(Sauti ya Jenča,)

"Ni lazima Hamas ihakikishe utulivu unazingatiwa kwa kuzuia mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Israeli na kuhakikisha usalama katika mpaka na Misri. Israeli inapaswa kuimarisha juhudi kuondoa vizuizi na kuwezesha maendeleo Gaza wakati utulivu ukiendelea katika ukanda huo kwa mujibu wa azimio namba 1860 la Baraza la Usalama."

Aidha ametoa tahadhari kuhusu baadhi ya matamshi kutoka pande husika akisema

"Mnamo Agosti 3 waziri Mkuu wa Israeli alitoa hotuba katika uzinduzi wa makazi elfu moja katika eneo la Beitar Illit. Katika hotuba hiyo alisifu juhudi za serikali yake katika kuchagiza makazi hayo. Vitendo kama hivyo vinachangia dhana ya kwamba wanaopinga suluhu la mataifa mawili wanashinda."

Bwana Jenča amekumbusha kwamba kukaliwa kwa maeneo kunakwenda kinyume na sheria za kimataifa na ni kizuizi cha amani.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031