Najivunia kuwa polisi mwanamke nchini Sudan Kusini- Bi. Cynthia

Kusikiliza /

Afisa wa Polisi wa UNPOL. Picha:UNMISS/Daniel Dickinson

Kuelekea siku ya utu wa kibinadamu duniani tarehe 19 mwezi huu, imeelezwa kuwa uwepo wa polisi wanawake kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa huleta matumaini miongoni mwa makundi yanayokumbwa na mizozo.

Hiyo ni kwa mujibu wa Cynthia Anderson kutoka Ghana polisi anayehudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS.

Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kushiriki katika moja ya operesheni za kuondoa silaha katika kambi ya wakimbizi wa ndani amesema.

"Wengi wa watu walioko hapa ni wanawake na wana imani pale wanapoona operesheni inatekelezwa na polisi mwanamke, hiyo inawapa nguvu na hali ya kuwepo usalama."

Akiwa polisi mwanamke anahijisi vipi?

"Ni fursa kubwa kuwa hapa, na tunafanya kadri ya uwezo wetu katika kuchangia juhudi za amani na usalama kimataifa. Ninajivunia hilo kama mwanamke, kwa hiyo mwanamke kufanya kazi kwa pamoja na wanaume hilo ni jambo ambalo najivunia na ni fursa kubwa."

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930