Grandi atolea wito jumuiya ya kimataifa kutambua ukarimu wa Sudan

Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi .(Picha:UM/Evan Schneider)

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi, amefanya ziara yake ya kwanza nchini Sudan wiki hii wakati huu ambapo wakimbizi wanaendelea kukimbia mzozo nchini Sudan Kusini.

Bwana Grandi amesifu ukarimu wa watu wa Sudan, mmoja ya nchi zinazowahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini, na kuwa mwenyeji wa wakimbizi wengine kwa miongo akitaja kushuhudia utayari wa nchi hiyo kupokea wakimbizi miaka 30 iliyopita wakati huo akiwa afisa wa mashinani wa UNHCR.

Ameongeza kwamba wakimbizi wanapata huduma mbali mbali ikiwemo uhuru wa kufanya kazi, hata hivyo ametolea wito kwa mamlaka nchini Sudan Kusini.

(Sauti ya Grandi)

"Inahuzunisha sana kwamba mmiezi yote hii ya watu kuteseka nje ya nchi, Sudan Kusini bado haijapata amani, na hili ni jukumu la viongozi, na upinzani kuanza kuchukua hatua stahiki."

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930