Ghasia zinazoendeshwa na magenge El Salvador zatishia raia

Kusikiliza /

Baba na mwanae, familia ambayo walikimbia machafuko nchini El Savador.(Picha:ACNUR / Markel Redondo)

Mamlaka nchini El Salvador zinapaswa kuchukua hatua zaidi ili kusaidia raia wanaokimbia makazi yao kutokana na ghasia zinazosababishwa na magenge ya wahuni.

Hilo ni moja ya mapendekezo kutoka kwa mtaalamu huru wa haki za binadamu kuhusu watu waliokimbia makazi yao, Cecilia Jimenez-Damary baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tano nchini humo.

Amesema hali inayokabili watu hao ni sawa na janga lililofichika akisema kuna umuhimu wa kupata takwimu sahihi ingawa makadirio yanaonyesha kuwa maelfu ya watu wamekumbwa na hali hiyo.

Bi. Jimenez-Damary amesema magenge ya wahuni yanamiliki maeneo huku yakitishia raia na vitendo vya mauaji na utumiaji wa nguvu vikishamiri.

Amesema tatizo ni kubwa kuliko ambavyo serikali inafikiria akiongeza kuwa serikali inapaswa kukubali uwepo wa tatizo hilo la watu kusalia wakimbizi wa ndani kutokana na ghasia za magenge ya wahuni.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930