Afya ya wahamiaji Libya yaangaziwa

Kusikiliza /

Mkutano uliofanyika Tunis, Tunisiawa wa kujadili afya ya wahamiaji nchini Libya. Picha: IOM

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Libya ili kukabili changamoto za utoaji huduma za afya kwa wahamiaji.

Mkuu wa IOM nchini humo Othman Belbeisi, amesema hayo katika mkutano uliofanyika Tunis, Tunisia wakati huu ambapo wahamiaji wapatao milioni moja nchini Libya hawana huduma za uhakika za afya.

Amesema kwa kushirikiana na wadau mbali mbali likiwemo shirika la afya ulimwenguni, WHO wamechukua hatua hiyo kwa kuzingatia maazimio kadhaa ikiwemo azimio la mkutano wa mkuu wa 70 wa WHO ulioweka kipaumbele kwa afya ya wahamiaji.

Mradi huo wa kusaidia wahamiaji unatekelezwa pia Morocco, Misri, Libya, Tunisia na Yemen.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930