Polisi wanawake wana mchango mkubwa kwenye UM:Appelblom

Kusikiliza /

Maria Appelblom, mkuu wa kitengo cha polisi wa akiba cha Umoja wa Mataifa akisalimiwa na Maafisa wa Polisi wakati wa ziara yake MINUSCA huko Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Picha: UN / MINUSCA

Polisi wanawake wana mchango mkubwa katika miakakati ya ulinzi na usalama ya Umoja wa Mataifa hasa kwenye maeneo mbalimbali duniani waliko na operesheni za ulinzi wa amani.

Kauli hiyo imetolewa na Bi Maria Appelblom mkuu wa kitengo cha polisi wa akiba cha Umoja wa Mataifa akizungumza na UN News amesema ..

(MARIA CUT 1)

"Katika mazingira mengi tunayofanya kazi maafisa wa polisi wa kike huitajika kwa ajili ya wanawake wengi kuzungumaa nao endapo kuna mwanamke aliyebakwa na sio rahisi kuongea na afisa mwanaume na pia katika baadhi ya tamaduni ni vigumu kwa ujumla mwanamke kuzungumza na mwanaume."

Ameongeza kuwa pia ni muhimu kuwa na maafisa wa polisi wanawake kama mfano wa kuigwa kwenye Umoja wa Mataifa lakini kikubwa zaidi ni mchango wao katika jamii..

(MARIA CUT 2)

"Nadhani ni muhimu sana tuzungumzie wanawake kama wanaharakati, wanawake kama mawakala wa mabadiliko, tunatambua kutokana na utafiti kwamba kujumuisha wanawake katika michakato ya amani inasaidia kuwa na amani endelevu, hili ni eneo ambalo nadhani tunapaswa kujikita zaidi."

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031