Nyumbani » 24/08/2017 Entries posted on “Agosti 24th, 2017”

Wakati wa viongozi kuchukua hatua nchini Sudan Kusini ni sasa

Kusikiliza / Naibu Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa El-Ghassim Waneakihutubia Baraza la usalama leo. Picha: UM//Kim Haughton

Mzozo wa Sudan Kusini umeanzishwa na binadamu na viongozi nchini humo wana wajibu wa moja kwa moja kuutatua. Hiyo ni kauli ya Naibu Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa El-Ghassim Wane aliyotoa wakati akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo jijini New York, Marekani. Kikao kilikutana  kujadili hali [...]

24/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha ripoti kuhusu Rakhine

Kusikiliza / Raia nchini Myanmar. Picha: UM

Umoja wa Mataifa umekaribisha ripoti ya kina iliyotolewa leo an kamisheni ya ushauri kuhusu jimbo la Rakhine huko Myanmar ambalo waumini wa dini ya kiislamu wanakabiliwa na sintofahamu ya utaifa. Ripoti hiyo ilitangazwa leo na mwenyekiti wa kamisheni  hiyo ya watu tisa, Kofi Annan ikisisitiza suala la uraia kwa wananchi na kutoa wito wa watu [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahitaji ya kibinadamu Raqqa nchini Syria ni zaidi ya inavyofikirika

Kusikiliza / Picha: UNICEF/Souleiman

Mahitaji ya kibinadamu kwa maelfu ya raia walionasa kwenye eneo linaloshikiliwa na magaidi wa ISIL huko Raqqa nchini Syria ni makubwa kuliko inavyofikirika. Hiyo ni kwa mujibu wa Jan Egeland ambaye ni mshauri maalum wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi hii leo baada ya kikao cha kikosi kazi [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shida haibagui wala haichagui, tusaidiane: Mugenyi

Kusikiliza / Unicef linasisitiza elimu kwa watoto wakimbizi. Picha: UNICEF

Shida haina adabu, haichagui , wala haibagui inapokufika imekufika, la msingi kusaidiana. Huo ni wito wa Iddi Mugenyi mkurugenzi wa shule ya sekondari ya East african Muslim High school iliyoko nchini Uganda. Shuleni kwake anasaidia watoto wakimbizi takribani 50 hususan masuala ya karo ili waweze kupata elimu ambayo ni ufunguo wa maisha. Anawaasa Waganda wenzie [...]

24/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Takribani watu milioni 41 waathiriwa na mafuriko na maporomoko Nepal, Bangladesh na India

Kusikiliza / Hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi Bangladesh, Nepal na India. Picha: UM

Ofisi ya Umoja wa mataifa  ya kuratibu msaada ya kibinadamu, OCHA imesema hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi huko Bangladesh, Nepal na India inaweza kuwa mbaya zaidi na kuleta madhara zaidi kutokana na uwezekano wa mvua kuendelea kunyesha na maji ya mafuriko kuelekea kusini. OCHA inasema tayari mvua kubwa imesababisha madhara ikiwemo vifo vya [...]

24/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ufugaji wa bata badala ya kuku wapunguza majanga Vietnam- UNISDR

Kusikiliza / Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa majanga, UNISDR Robert Glasser .(Picha:UM/Mark Garten)

Umoja wa Mataifa umesema ingawa majanga ya asili hugharimu serikali pesa nyingi bado kuna mikakati nafuu inayoweza kuepusha nchi kukabiliana au kuepusha hasara inayoweza kutokea. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa majanga, UNISDR Robert Glasser amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa siku moja kabla ya kuanza kwa [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wanaoingia Ulaya yapungua lakini ukatili wanaopata waongezeka

Kusikiliza / Wakimbizi na wahamiaji wanaosubiri kuokolewa baada ya chombo kinachobeba zaidi ya watu 700 kuzama. Picha: MOAS.eu2017

Idadi ya wakimbizi na wahamiaji waliowasili Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu kupitia moja ya njia tatu zinazotumika,  imepungua ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR iliyotolewa hii leo ikiangazia njia tatu za kuvuka kuingia barani [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Japan yatoa dola milioni 10 kusaidia wakimbizi, Uganda

Kusikiliza / Mhudumu wa afya anapima mtoto kutafuta ishara za utapiamlo katika kituo cha afya kambini Nyumanzi nchini Uganda. Picha: © UNHCR/Jiro Ose

Serikali ya Japan imetoa mchango wa dola milioni kumi kama uitikio wao kwa mahitaji yanangezeka katika jamii ya wakimbizi na wenyeji Kaskazini mwa Uganda kutokana na mmiminoko wa wakimbizi kutoka Sudan Kusini. John Kibego na maelezo Zaidi. (Sauti ya Kibego) Mwakilishi wa Shirka la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda,, Bornwell Kantande [...]

24/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ndege iliyokodishwa na WFP yaua mtoto Sudan Kusini

Kusikiliza / Ndege iliyokodishwa na WFP yaua mtoto Sudan Kusini. Picha: WFP

Nchini Sudan Kusini mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia na watu wengine wanne wamejeruhiwa baada ya ndege moja kugonga nyumba kwenye mji mkuu Juba. Joseph Msami na ripoti kamili. (Taarifa ya Joseph) Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ambapo iligonga nyumba hiyo wakati rubani akijaribu kutua [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Polisi Somalia wanolewa kuhusu ukatili wa kingono

Kusikiliza / Mafunzo3

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM unawapatia polisi nchini humo mafunzo kuhusu jinsi ukatili wa kingono unavyoweza kuzua mizozo na kuotesha mizizi ukatili kwenye jamii. Mafunzo hayo yanatolewa kupitia warsha ya siku tatu kwa kushirikiana na Wizara ya wanawake na haki za binadamu yataongeza ufahamu wa polisi kuhusu hatari za ukatili [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031