Nyumbani » 23/08/2017 Entries posted on “Agosti 23rd, 2017”

Anti-Balaka na FPRC wapambana huko CAR

Kusikiliza / Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika ulinzi wa Amani. UM/Catianne Tijerina

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA umeripoti mapigano hii leo kati ya wanamgambo wa kikundi cha Anti-Balaka na wale wa FPRC awali wakijulikana kama Seleka. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema mapigano hayo yametokea kwenye eneo la Ngubi, karibu na mji wa Bria jimboni [...]

23/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa uhakika wa chakula huchochea uhamiaji- Ripoti

Kusikiliza / Wamama hao ni baadhi ya wahamiaji. Picha: WFP

Ripoti mpya ya utafiti wa pamoja wa mashirika mbali mbali ikiwemo lile la Mpango wa chakula duniani WFP , imebaini uhusiano uliopo kati ya ukame wa muda mrefu nchini El Salvador, Guatemala na Honduras uliochochewa na El Niño ya kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 na kuongezeka kwa wahamiaji kutoka nchi hizo kuelekea Marekani. Akizungumzia ripoti [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fursa na vikwazo katika juhudi za vijana kujikwamua nchini DRC 1

Kusikiliza / Kijana mfanyakazi wa kujitolea nchini DRC. Picha: UM/Sylvain Liechti (maktaba)

Katika mfululizo wa makala zinazomulika juhudi za vijana katika kujikwamua kiuchumi, tunakupeleka Afrika Mashariki kusikiliza mahojiano na  kijana mjasiriamali Kiiza Serugendo Elwa kutoka mji wa Kiwanja, Jimboni Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Ungana na John Kibego katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano na kijana huyu ambaye kwa sasa yuko [...]

23/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waikosoa Marekani kushindwa kukemea siasa za ubaguzi

Kusikiliza / Onyesho la upendo kwa wote. Picha:NICA/51602

Kamati ya Umoja wa mataifa ya kupiga vita vya ubaguzi wa rangi inayoendelea na kikao chake mjini Geneva Uswis (CERD) leo  imeikosoa serikali ya marekani pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa kwa kushindwa kukemea maandamano ya chuki, kibaguzi na uhalifu uliotokea Charlottesvilles Virginia na nchini kote. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tutokomeze ubaguzi tukiadhimisha kumbukizi ya utumwa: UNESCO

Kusikiliza / Hebu kumbukumbu na historia ya biashara ya watumwa na kufutiliwa kwake uendeshe majadiliano, kuvumiliana na kuelewa kwa pamoja. Picha: UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi  ya biashara ya utumwa na kutokomezwa kwake, Umoja wa Mataifa umetaka siku hii itumike kukemea aina zote za unyanyasaji na ubaguzi unaoripotiwa duniani hivi sasa. Assumpta Massoi na taarifakamili. ( TAARIFA YA ASSUMPTA) Katika ujumbe wake kuhusu siku hiyo , Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria nchini Jordan kupata ajira

Kusikiliza / Kituo cha kwanza cha ajira nchini Jordan kwa ajili ya wakimbizi wa Syria. Picha: ILO

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kazi ILO na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR wamezindua ofisi ya kwanza kabisa ya ajira ndani ya kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan. Ofisi hiyo iliyoanzishwa kwa uratibu na serikali ya Jordan itawezesha wakimbizi waishio kwenye kambi hiyo kupata ajira rasmi nchini humo. Mratibu wa ILO kuhusu janga [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yazindua mradi wa kuchagiza ajira ya vijana Burkina Faso

Kusikiliza / IOM yazindua mradi wa kuchagiza ajira ya vijana Burkina Faso. Picha: UN Migration Agency (IOM) 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limesema  limezindua mradi mpya unaoshughulika na uhusiano kati ya vijana, ajira na uhamiaji katikati na Mashariki Burkina Faso. Mradi huo unalenga kukuza uajiri wa vijana na ujasiriamali ili kupunguza hatari ya uhamiaji katika kanda hiyo  Burkina Faso, kama ilivyo nchi zingine za Afrika Kusini mwa Jangwa [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni dhidi ya ujangili ilileta mabadiliko- Kiba

Kusikiliza / Ali Kiba

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania Ali Kiba amesema kampeni ya kulinda wanyamapori ambayo alishiriki akiwa Balozi wa WILDAID ilikuwa ya mafanikio makubwa kwa kuwa ilijenga hamasa miongoni mwa makundi mbali mbali. Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Kiba ambaye ameshinda tuzo za kimataifa, kikanda na kitaifa [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930