Nyumbani » 22/08/2017 Entries posted on “Agosti 22nd, 2017”

UNMISS yatowesha hofu kwa watoto Sudan Kusini.

Kusikiliza / Watoto wakicheza nchini Sudan Kusini. Picha kwa hisani ya video ya UNMISS.

Hofu,mashaka mtawalia! Haya ni baadhi ya madhila yaliyowakumba watoto nchini Sudan Kusini kabla ya operesheni ya kikosi cha ulinzi wa amani cha  Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kilichotowesha madhila hayo. Katika Makala ifuatayo, Joseph Msami anaeleza mustakabali wa watoto nchini Sudan Kusini taifa lililokumbwa na mizozo.

22/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Pande mbili husika zina wajibu katika jawabu la swala la Palestina- Jenča

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hali Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina. Picha: UM/Evan Schneider

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina. Akihutubia kikao hicho Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu maswala ya kisiasa Miroslav Jenča amewataka viongozi wa Palestina kuzingatia matokeo haribifu yanayotokana na migawanyiko Palestina na kufikia makubaliano ili kuwezesha mamlaka Palestina kutekeleza wajibu Gaza katika juhudi za [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa ubakaji wa ISIL lazima wapate msaada unaohitajika-UM

Kusikiliza / Mwanamke mYazidi Kurd kutoka Sinjar aliyenaswa na wanamgambo wa ISISL,. Yuko kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mamilyan nchini Iraq. Picha: Giles Clarke/ Getty Images Reportage

Leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI wametoa ripoti ikiitaka serikali ya Iraq kuhakikisha kwamba maelfu ya wanawake na wasichana manusura wa ubakaji na mifumo mingine ya ukatili wa kingono ulioteklelezwa na kundi la ISIL wanapata huduma, ulinzi, na haki na kwamba [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa EU kwa WFP kupunguza machungu kwa wakimbizi Algeria

Kusikiliza / Wakimbizi nchini Algeria. Picha:WFP/Algeria

Muungano wa Ulaya, EU umelipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP msaada wa dola milioni 5.5 kwa ajili ya mahitaji muhimu ya chakula kwa wakimbizi wa Sahrawi walioko kwenye kambi nchini Algeria. Kupitia fedha hizo wakimbizi watakuwa na uhakika wa mlo ambapo watapatiwa nafaka, mafuta, sukari na vyakula vilivyoongezewa virutubisho. Mwakilishi wa WFP nchini [...]

22/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha Burundi cha kulinda amani chawasili Somalia

Kusikiliza / Kikosi cha Burundi cha kulinda maani chawasili Somalia.(Picha:AMISOM/ ilyas AHmed)

Kikosi kipya cha ulinzi wa amani kutoka nchini Burundi BNDF, kimewasili nchini Somalia kwa ajili ya kazi hiyo itakayodumu kwa mwaka mmoja chini ya ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM. Kwa mujibu wa wavuti wa AMISOM, BNDF, chenye maafisa 45, kinachukua nafasi ya kikosi kingine cha 39 ambacho kimemaliza muda wake ambapo kimetimiza [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watoto wanaojilipua Nigeria yaongezeka- UNICEF

Kusikiliza / Watoto wanatumika katika kwenye mashambulizi ya kujilipua.(Picha:UNICEF / UN015784 / Prinsloo)

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limeeleza masikitiko yake kufuatia ongezeko la watoto wanaotumiwa kwenye mashambulizi ya kujilipua huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria. (Taarifa ya Kibego) Msemaji wa UNICEF huko Geneva, Uswisi Christophe Boulierac amesema katika kipindi cha mwaka mmoja idadi imeongezeka mara nne. Bwana Boulierac amesema kitendo cha kutumia watoto ni mauaji [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid apongeza kufutwa kwa sheria zinazolinda wabakaji

Kusikiliza / Wanawake waokumbwa na ubakaji husalia na msongo. Picha: UM

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein amekaribisha kitendo cha Lebanon, Tunisia na Jordan kufutilia mbali sheria ambazo zinalinda wabakaji dhidi ya mashtaka kwa kuwaruhusu kuwaoa wale waliowabaka. (Taarifa ya Assumpta) Zeid amesema kitendo cha wabunge katika nchi hizo kufuta sheria hizo kinadhihirisha azma yao ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake. [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waisaidia Libya kukabilii usafirishaji haramu wa binadamu:

Kusikiliza / Mmoja wa wahamiaji waliorejeshwa kwa hiyari kutoka Libya akifanya ujasiriamali. Picha na IOM

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM uko bega kwa bega na serikali ya Libya katika kukabili usafirishaji haramu wa binadamu. Kwa mujibu wa Maria do Valle Ribeiro naibu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Libya , hiyo ni biashara haramu na ya hatari [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930