Nyumbani » 21/08/2017 Entries posted on “Agosti 21st, 2017”

Ghasia zinazoendeshwa na magenge El Salvador zatishia raia

Kusikiliza / Baba na mwanae, familia ambayo walikimbia machafuko nchini El Savador.(Picha:ACNUR / Markel Redondo)

Mamlaka nchini El Salvador zinapaswa kuchukua hatua zaidi ili kusaidia raia wanaokimbia makazi yao kutokana na ghasia zinazosababishwa na magenge ya wahuni. Hilo ni moja ya mapendekezo kutoka kwa mtaalamu huru wa haki za binadamu kuhusu watu waliokimbia makazi yao, Cecilia Jimenez-Damary baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tano nchini humo. Amesema hali inayokabili [...]

21/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wajipanga kuwasaidia maelfu wanaokimbia Telafar Iraq

Kusikiliza / Watoto hawa ni baadhi ya maelfu ya raia wanaokimbia kutoka Telafar. Picha: Iraqi Red Crescent/UNOCHA

Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu nchini Iraq wanajiandaa kwa ajili ya kuwasaidia maelfu ya raia watakaokimbia kutoka Telafar wakati jeshi la serikali likipambana kuukomboa mji huo ulioko Kaskazini mwa Iraq kutoka kwenye udhibiti wa kundi la kigaidi la ISIL au Daesh. Operesheni hiyo ya ukombozi ilianza Jumapili na hadi sasa [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa UNDP umewapa ujasiri sambamba na kuwawezesha wanawake wa Kimasaai

Kusikiliza / Wamama katika mradi wa kujikwamua wanawake kiuchumi. Picha: UNDP/Kenya_Video capture

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Kenya kwa ushirikiano na serikali ya nchi hiyo wameanzisha mradi kwa ajili ya kuwezesha jamii zinazoishi kusini magharibi mwa Kenya karibu na mbuga ya wanyama ya Amboseli. Miradi hiyo inayolenga jamii za watu wa asili hususan Wamasaai inanuia kuwawezesha wanawake sio tu kiuchumi lakini [...]

21/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yatangaza jopo la wataalam kwa mustakbali bora wa ajira

Kusikiliza / Guy Ryder Akizungumza katika tukio la uzinduzi wa jopo hilo mjini Geneva Uswisi mkurugenzi mkuu wa ILO. Picha: ILO/Marcel Crozet

Shirika la kazi ulimwenguni ILO, limetangaza leo kuanzishwa kwa tume ya ngazi ya juu ya kimataifa ya wataalamu 20 ambayo itaangalia taasisi, usimamizi na sheria zinazohitajika ili kuhakikisha ajira zinakidhi viwango vya kisheria ikiwa ni juhudi za ILO katika mikakati ya mustakabali wa kazi zilizoasisiwa na shirika hilo mwaka 2013. Akizungumza katika tukio la uzinduzi [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani angazieni pia elimu Pembe ya Afrika

Kusikiliza / Wanafunzi darasani. Picha: UNICEF

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yametoa wito kwa wahisani kufadhili kwa kina mahitaji ya elimu kwa nchi zenye mahitaji ya kibinadamu katika pembe ya Afrika. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la watoto UNICEF wamesema katika taarifa yao kuwa elimu ikienda [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uingereza yaendelea kuwasaidia wasiojiweza Sudan-WFP

Kusikiliza / Wakimbizi walioko nchini Sudan wapokea mgao wa chakula kutoka kwa WFP.(Picha:WFP)

Serikali ya Uingereza imetoa paundi milioni 4.5 sawa na dola milioni 5.8 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ili litoe msaada muhimu wa chakula kwa karibu wakimbizi wa ndani 370,000 kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan. Fedha hizo ambazo zitatosheleza kwa miezi miwli zitaruhusu WFP kuwasaidia watu hao kupitia [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu Burundi hazina dalili ya kuimarika:UM

Kusikiliza / Raia nchini Burundi. Picha UM

Wataalamu wa kimataifa wanaochunguza haki za binadamu Burundi wamesema hawajaona dalili zozote nzuri za kuimarika kwa hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika miezi ya karibuni nchini humo. John Kibego na ripoti kamili. (Taarifa ya Kibego) Hayo yamo kwenye ripoti mpya ya tume ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa iliyopewa [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kudhibiti kuenea kwa magonjwa Sierra Leone ni muhimu- WHO

Kusikiliza / UNFPA-Sierra Leone

Shirika la afya ulimwenguni, WHO linashirikiana kwa karibu na serikali ya Sierra Leone ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile Malaria na Kipindupindu kufuatia maporomoko ya udongo na mafuriko  nchini humo wiki iliyopita. Harakati hizo zinaenda sanjari na kuhakikisha huduma za afya kwa majeruhi na waliopoteza makazi zinapatikana, halikadhalika usaidizi wa kisaiokolojia na [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031