Nyumbani » 16/08/2017 Entries posted on “Agosti 16th, 2017”

Azimio 2371 ni ujumbe dhahiri kwa DPRK kuwajibika kwa amani na usalama:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa New York Marekani. Picha:UM/Mark Garten

Kuna zahama nyingi hivi sasa duniani kote, hasa mvutano kuhusiana na rasi ya Korea ambao haujashuhudia katika kiwango hicho kwa miongo. Hayo yamesema leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alipozungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa New York Marekani. Amesema historia inakumbusha machungu ya miaka zaidi ya [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana kushirikiana katika kufanikisha SDGs: Tanzania

Kusikiliza / Vijana wa kike katika biashara ya ushirika ya kushona nguo nchini Tanzania. Picha: UN Women/Video capture

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo vijana kuwa bega kwa bega katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lile la kwanza la kutokomeza umaskini bila kusahau usawa wa kijinsia. Na ni kwa mantiki hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UNWomen nchini Tanzania mwaka 2015 lilizindua programu ya maendeleo endelevu kupitia [...]

16/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uharibifu wa silaha umekamilika katika kambi za FARC-Arnault

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia, Jean Arnault. Picha: UM/Colombia

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia, Jean Arnault amesema amefurahishwa na operesheni za kusalimisha silaha nchini humo. Katika taarifa yake ya Agosti 15, bwana Arnault amesema mchakato wa kuondoa silaha zote na risasi katika kambi 26 za kikundi cha FARC umekamilika. Ameongeza kwamba kando na operesheni ambayo inaendeshwa eneo Pondores [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM waonya kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi Marekani

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa Bwana Mutuma Ruteere. UN Photo/Evan Schneider

Visa vya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni vimeshamiri Marekani, kwa mujibu wa ripoti ya wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Onyo hilo limetolewa wakati huu ambapo maandamano na vurugu zimetanda katika mji wa Charlottesville jimbo la Virginia nchini marekani na mtu mmoja kupoteza maisha. Kwa mujibu wa wataalam hao, [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sierra Leone waomboleza kwa siku saba kufuatia maporomoko

Kusikiliza / Mamia ya watu wahofiwa kupoteza maisha baada ya maporomoko  ya ardhi nchini Sierra Leone. Picha: UNICEF

Nchini Sierra Leone, wananchi wakiendelea na maombolezo ya kitaifa kufuatia janga la maporomoko ya udongo na mafuriko siku ya Jumatatu, Umoja wa Mataifa unaendelea na harakati zake za uokozi na kuepusha mlipuko wa magonjwa. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Regent, mji ulioko milimani, takribani kilometa 16 kutoka mji mkuu wa Sierra Leone, [...]

16/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ILO kutangaza jopo la mustakabali wa ajira

Kusikiliza / Picha:ILO

Shirika la kazi ulimwenguni ILO, linatarajia kuanzisha tume ya ngazi ya juu ya kimataifa, tume itakayojumuisha wataalamu 20 ambao pamoja na mambo mengine wataangalia namna mabadiliko ya kazi yanavyoweza kukidhi viwango vya sheria. Katika taarifa yake hii leo, ILO imesema majina ya wanachama wa tume hiyo maaluma kwa ajili ya mustakabali wa kazi, yatatangazwa mnamo [...]

16/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yaanza kugawa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa ndani DRC

Kusikiliza / WFP wagawa msaada Kasai, DRC. Picha: WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na washirika wake World Vision wamezindua operesheni ya dharura leo ya kugawa chakula kwa wakimbizi wa ndani 42,000 kwenye majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Kwa mujibu wa WFP katika maeneo yanayofikika wanapanga kuwasaidia watu 25,000 Kasai ya Kati na [...]

16/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afya ya wahamiaji Libya yaangaziwa

Kusikiliza / Mkutano uliofanyika Tunis, Tunisiawa wa kujadili afya ya wahamiaji nchini Libya. Picha: IOM

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Libya ili kukabili changamoto za utoaji huduma za afya kwa wahamiaji. Mkuu wa IOM nchini humo Othman Belbeisi, amesema hayo katika mkutano uliofanyika Tunis, Tunisia wakati huu ambapo wahamiaji wapatao milioni moja nchini Libya hawana huduma za uhakika za afya. Amesema [...]

16/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dunia yashikamana kukabili sumu ya zebaki kupitia mkataba wa Minamata

Kusikiliza / mercury

Mkataba wa kwanza duniani wa kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya sumu ya zebaki umeanza kutekelezwa rasmi leo . Amina Hassan na taarifa zaidi (TAARIFA YA AMINA) Mkataba wa Minamata uliopigiwa upatu kwa karibu muongo mmoja, Mei 18 mwaka huu ulipata sahihi ya 50 iliyohitajika ili uanze kutekelezwa. Mkataba huo unaziwajibisha pande 74 [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterress alaani mfululizo wa mashambulizi Nigeria

Kusikiliza / Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Manuel Elias

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika Agosti 15 katika jimbo la Borno nchini Nigeria. Kupitia msemaji wake, ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Nigeria kufuatia vifo na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi. Katibu Mkuu pia ametoa wito waliotekeleza uhalifu huo nchini Nigeria na nchi jirani [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuna deni na kizazi kijacho kutoa msaada wa kibinadamu leo:O'Brien

Kusikiliza / Wakimbizi wahitaji misaada Syria. Picha: UNHCR

Kutoa usaidizi wa kibinadamu unaohitajika leo hii , ni uwekezaji wenye amana kubwa katika kizazi kijacho. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa operesheni za misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien katika kuelekea siku ya usaidizi wa kiutu duniani itakayoadhimishwa Agosti 19. Mwaka huu siku hiyo inajikita katika mashambulizi dhidi ya raia na [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930