Nyumbani » 15/08/2017 Entries posted on “Agosti 15th, 2017”

Kuna ongezeko kubwa la machafuko CAR:UNICEF

Kusikiliza / 6-5-17car

Mwaka uliopita na hususani robo ya mwisho ya mwaka huo imeshuhudia ongezeko kubwa la machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Donaig Le Du msemaji wa shirika hilo akizungumza leo mjini Geneva Uswis amesema CAR ni moja ya nchi ambazo ni mbaya [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya tatu

Kusikiliza / Lilongwe, Malawi.

Wiki ya unyonyeshaji duniani imehitimishwa juma hili, kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto ili kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora.  Katika sehemu ya tatu ya makala hii Amina Hassan anaendelea kuzungumza na Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja wa [...]

15/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mipango ya kikosi cha G5 ilandane na mchakato wa amani Mali- Wane

Kusikiliza / 16447005773_1eb4c1e33b_z2

Kadri hali ya usalama inavyozidi kuzorota kwenye mipaka ya nchi zilizo ukanda wa Sahel, Afrika Magharibi, ndivyo umuhimu wa kikosi cha pamoja cha nchi tano kwenye ukanda huo kinavyozidi kupata umuhimu. Hiyo ni kwa mujibu wa Naibu Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa El-Ghassim Wane wakati akipatia Baraza la Usalama [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya iko katika wakati muhimu, viongozi wawajibike-Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu  Zeid Ra'ad Al Hussein. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amepongeza wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi mkuu kwa njia ya amani huku akihimiza viongozi wa kisiasa kuwajibika na kuonyesha uongozi imara ili kuzuia machafuko zaidi. Zeid ameelezea wasiwasi wake kuhusu ripoti za vyombo vya usalama kutumia risasi za moto dhidi [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Manusura na maiti zaidi wapatikana pwani ya Yemen:IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Katika siku tatu zilizopita wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM wamewapata manusura lakini pia maiti zaidi kufuatia zahma ya boti wiki iliyopita. Tarehe 9 na 10 Agosti jumla ya wahamiaji 280 walikuwa wakielekea nchi za Ghuba walipotoswa baharini kutoka kwenye boti mbili Pwani ya Yemen jimbo la Shabwa na wasafirishaji haramu [...]

15/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maporomoko ya udongo Sierra Leone, juhudi za uokozi zaendelea

Kusikiliza / Juhudi za uokozi nchini Sierra Leone.(Picha:UNICEF/Twitter)

Nchini Sierra Leone, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana na serikali kupeleka huduma za uokoaji kwenye maeneo yaliyokumbwa na maporomoko ya udongo na mafuriko mapema jana Jumatatu. Zahma hiyo imekumba mji wa Regent na mji mkuu Freetown ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema wanahaha kunasua [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imeanza kuwahamisha wakimbizi wa DRC mpakani na Angola

Kusikiliza / Familia zilizokimbia machafuko jimbo la Kasai DRC zawasili katika kituo cha hifadhi cha Lóvua, Angola. (Picha:UNHCR/Rui Padilha)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake wameanza zoezi la kuwahamisha zaidi ya wakimbizi 33,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kutoka kwenye vituo vya mapokezi vilivyofurika Kaskazini mwa Angola na kuwapeleka kwenye kambi mpya iliyofunguliwa ya Lóvua . Takribani wakimbizi 1,500 wameshahamishwa kutoka kituo cha mapokezi cha Mussunge [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwepo wa UM jimboni Darfur umebadili maisha yetu- mkazi Darfur

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unatoa huduma mbali mbali za misaada jimboni Darfur, Sudan.(Picha:UNAMID Selemani Semenyu)

Wakati siku ya utu wa kibinadamu ikiadhimishwa tarehe 19 mwezi huu, wakazi jimboni Darfur nchini Sudan wameupongeza Umoja wa Mataifa kwa huduma wanazozipata kupitia Umoja huo.Taarifa kamili na Luteni Selemani Semunyu wa radio ya Umoja wa Mataida Darfur UNAMID (TAARIFA YA SELEMANI) Hii ni kufuatia ujio wa wawakilishi kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930