Nyumbani » 10/08/2017 Entries posted on “Agosti 10th, 2017”

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya pili

Kusikiliza / Picha: UNICEF/NYHQ2013-1031/Marinovich

Wiki ya unyonyeshaji duniani imehitimishwa juma hili, kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto ili kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora.  Katika sehemu ya pili ya makala hii Amina Hassan anaendelea kuzungumza na Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja wa [...]

10/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Stahamala muhimu kuhakikisha ulinzi kwa wakimbizi: Shearer

Kusikiliza / Raia nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Stahamala ni mbinu bora ya kuwalinda raia katika kwa kambi za wakimbizi dhidi ya uvamizi wa kijeshi, nchini Sudan Kusini, amesema mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, David Shearer. Kiongozi huyo alikuwa akizungumza mjini Bentiu, Kaskazini mwa Sudan Kusini, ambapo raia zaidi ya 115,000 wanaishi katika kituo cha ulinzi wa raia [...]

10/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya-UM

Kusikiliza / Dujarric2

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya, wakati huu ambapo matokea ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 yanatarajiwa kutangazwa. Akizungumza na waaandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, Marekani, msemaji wa katibu mkuu Stéphane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa haukuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi lakini.. (Sauti [...]

10/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chagizeni amani kwa kuchagiza uwezeshaji wa wanawake:Amina

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu mteule wa UM Bi. Amina J. Mohammed. (Picha:UM)

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa taarifa kwa baraza la usalama kuhusu ziara yake ya kwanza na ya aina yake aliyoifanya barani Afrika. Katika kikao cha baraza hilo lkilichokuwa kikijadili masuala ya amani na usalama Afrika, bi Amina Mohammed amesema aliambatana na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nigeria yasaidia watu wake kupitia WFP

Kusikiliza / Picha:WFP_Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limekaribisha msaada wa tani 5000 za mchele kutoka kwa serikali ya Nigeria. Shirika hilo linasema mchele huo utasaidia kulisha karibu watu nusu milioni wakimbizi wa ndani katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ililoghubikwa na machafuko na ambako tishio la baa la njaa [...]

10/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wengine 160 watoswa baharini leo Yemen:IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Wahamiaji wengi takribani 180 wametoswa baharini leo kwenye pwani ya Yemen na wasafirishaji haramu wa binadamu. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA YA AMINA) Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM maiti 6 wamepatikana huku wahamiaji wengine 13 hawajulikani walipo na 20 wakihofiwa kufa maji. Tukio hili limefanyika siku moja tu [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji katika huduma za afya wahitajika kunusuru watoto Iraq

Mwanamke mkimbizi akimbeba mwanae kusini mwa Mosul. Picha:UNICEF/USA

Miongo ya vita na uwekezaji duni vimeweka shinikizo kubwa kwenye mfumo wa afya nchini Iraq. Hali hiyo imewafanya wanawake wajawazito na watoto kulipa gharama kubwa ya maisha yao limesema shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, la afya WHO na la kuhudumia watoto UNICEF. Mashirika hayo yanasema ingawa kuna hatua zilizopigwa [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto zaidi ya 500,000 wanahitaji msaada Libya:UNICEF

Kusikiliza / Watoto katika shule ya tenti katika kambi ya muda ya Shousha mpakani mwa Libya. Picha:UNICEF

Miaka sita tangu kuzuka kwa machafuko Libya watoto zaidi ya 550,000 wanahitaji msaada wa kibinafdamu kwa sababu ya kutokuwepo utulivu wa kisiasa, machafuko yanayoendelea , watu kutawanywa, na kuporomoka kwa uchumi. Shirika la Umoja wa Mataifa a kuhudumia watoto UNICEF limesema machafuko katika baadhi ya sehemu nchini Libya yamelazimisha familia kuzikimbia nyumba zao. Watoto zaidi [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadilliko ya tabianchi yameathiri uchumi wa Malawi-Benki ya dunia

Kusikiliza / Watoto nchini Malawi ambao walikuwa waaathirika wakubwa wa nja.(Picha:WFP/Enoch Kavindelea JR.)

Shirika la fedha duniani, IMF na benki ya dunia wanafanya kazi kwa pamoja ili kusaidia nchi ya Malawi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi yameathiri pakubwa uchumi wa Malawi katika kipindi cha miaka miwili baada ya mafuriko yaliyofuatiwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo. Kwa mujibu [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031