Nyumbani » 09/08/2017 Entries posted on “Agosti 9th, 2017”

Mzazi ni mdau muhimu kuzuia mimba utotoni

Kusikiliza / Picha:UNICEF

Mzazi ni mdau muhimu katika kuzuia mimba za utotoni nchini uganda na kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto za maisha hayo. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego leo amejikita katika changamoto hiyo ya mimba za utotoni na nini wajibu wa mzazi kuahikisha tatizo hilo linapunguzwa au kukomeshwa kabisa. Ungana naye katika makala hii kwa udani zaidi.

09/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 50 wazamishwa makusudi na wasafirishaji haramu

Kusikiliza / Picha:IOM

Mapema leo asubuhi msafirishaji haramu wa binadamu aliyekuwa anahodhi boti aliwalazimisha wahamiaji zaidi ya 120 kutoka Somalia na Ethiopia kujitosa baharini walipokaribia pwani ya Shabwa, Yemeni kwenye mwambao wa bahari ya Arabia. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mastaifa la uhamiaji IOM wahamiaji hao walikuwa wakitumai kwenda nchi za Ghuba kwa kupitia Yemen. Muda [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Alison Smale kuwa mkuu mpya wa mawasiliano ya kimataifa UM

Kusikiliza / Alison Smale , Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu Mawasiliano ya Kimataifa. Picha:YouTube/Hertie School of Governance(UN News Centre)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres amemteua Alison Smale wa Uingereza kuwa msaidizi wa Katibu mkuu kuhusu mawasiliano ya kimataifa , kwenye idara ya habari kwa umma ya Umoja wa Mataifa (DPI). Bi Smale anakuwa mrithi wa  Cristina Gallach wa Hispania ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa utendaji wake na huduma aliyoitoa kwa Umoja [...]

09/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yakaribisha mchango wa dola milioni 1 kwa ajili ya wakimbizi wa Sahrawi

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sahrawi kambini Smara, Algeria. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni moja kutoka Marekani kwa ajili ya kusaidia wakimbizi walioko hatarini katika Mashariki mwa jangwa la Sahara nchini Algeria. Kwa takriban miaka 40, wakimbizi wa mzozo wa muongo mmoja wa eneo lililoko katikati ya Morocco wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu Kusini Mashariki mwa Algeria. [...]

09/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rasilimali zaidi zahitajika kuzinisuru nchi na baa la njaa:

Kusikiliza / Wanawake na watoto wao nchini Somalia wamebanwa na uhaba wa chakula
Picha: UN video capture

Rasilimali zaidi zahitajika haraka ili kuwalinda watu milioni 20 walio katika hatari ya baa la njaa Yemen, Somalia, Sudan Kusini na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa baraza la usalama hii leo , ambayo pia imetaja madhila kwa mamilioni ya watu yatokanayo na machafuko yanayoendelea kote duniani [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC yaalani mauaji ya watoa huduma wa msalaba mwekundu CAR

Kusikiliza / Picha:UNDOF

Shirika la Kimataifa la Hilali Nyekundu na Msalaba Mwekundu, ICRC, limeelezea kusikitishwa na vifo vya kikatili vya wafanyakazi wa kujitolea wa msalaba mwekundu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR wiki hii. Kwa mujibu wa taarifa, wafanyakazi hao walikuwa kwenye mkutano wa dharura katika kituo cha afya cha Gambo, Mbomou Kusini mashariki mwa CAR mnamo [...]

09/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanasanyansi DRC wazuia mlipuko wa mafua ya avian kwa kutumia nyuklia

Kusikiliza / Matumizi ya nyuklia DRC katika kutokomeza ugonjwa wa Avian.Picha:IAEA

Wanasayansi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamebaini mlipuko mpya wa mafua ya ndege aina ya avian kwa kutumia teknolojia ya nyuklia . Na kwa kubaini haraka na mapema mlipuko wa virusi hivyo kumesaidia kuchukua hatua za haraka na sasa mlipuko huo umedhibitiwa na kusalia tu katika jimbo la ziwa albert karibu na mpaka [...]

09/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado watu wa asili hawashirikishwi katika maamuzi-Dkt. Laitaika

Kusikiliza / Eli

Hatua kubwa zilizopigwa katika kutambua uwepo wa watu wa asili na kwamba wanastahili kupewa haki zao, lakini bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji wa haki hizo zilizopo katika azimio la watu wa asili. Hayo yamesemwa na Dr Elifuraha Laitaika kutoka Tanzania ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu mwakilishi wa UM Somalia ajadili usalama na viongozi

Kusikiliza / Raisedon Zenenga, Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia. Picha:UNSOM

Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Raisedon Zenenga leo amekuwa na mazungumzo na uongozi wa jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia kujadili hatua zilizopigwa na serikali katika sekta ya usalama. Ziara ya bwana Zenenga pia ilijikita katika ujenzi unaoendelea kwa makao makuu ya jeshi la Taifa la Somalia kikosi cha 60 na chuo [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSMA yachunguza makaburi ya pamoja na ukiukwaji wa haki Kidal

Kusikiliza / Picha: MINUSMA

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, katika ripoti yake iliyotolewa juma hili umesema unachunguza makaburi ya pamoja yaliyopatikana na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu katika jimbo la Kidal Kaskazini mwa Mali ambako machafuko na mapigano baina ya makundi mawili yenye silaha yaliyotia saini mkataba wa amani yameongezeka hivi karibuni na kutishia kuvuruga [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto ni zaidi, miaka 10 tangu kupitishwa kwa azimio la haki za watu wa asili

Kusikiliza / Mariam Wallet Aboubakrine, ambaye ni Rais wa Kikao cha Kudumu cha Umoja wa Mataifa juu ya Masuala ya watu wa Asili, UNPFII. Picha:UN Photo/Rick Bajornas

Ingawa ulimwengu unaadhimisha miaka 10 hii leo tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kuhusu haki za watu wa asili, Umoja wa Mataifa umesema kuwa kundi hili bado linabaguliwa, linatengwa na linakosa ulinzi ambao umedhihirishwa na ongezeko kubwa la mauaji ya watetezi wa haki za kibinadamu za watu wa asili na ongezeko la ukiukwaji wa haki [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031