Nyumbani » 07/08/2017 Entries posted on “Agosti 7th, 2017”

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa muhimu UM:

Kusikiliza / Kituo cha kutoa huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu nchini Yemen. Picha na WHO

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa na umuhimu mkubwa wakati huu wakikabiliwa na zahma kubwa ya kibinadamu. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York hii leo. Mwishoni mwa juma mashambulizi ya anga yaliarifiwa [...]

07/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanariadha wakimbizi nchini Kenya wajiandaa kung'aa Olimpiki London

Kusikiliza / Wanariadha wakimbizi. Picha:VideoCapture

Wachezaji wakimbizi nchini Kenya wamejiunga na wachezaji wengine chini ya Jumuiya ya Kimataifa ya shirikisho la riadha ili washiriki katika mazoezi na michuano. Wakimbizi hao kutoka nchi jirani ikiwemo Sudan Kusini na Somalia, wamewekwa katika timu ya wanariadha wakimbizi waliochaguliwa na mfuko wa Tekla Loroupe nchini Kenya. Tekla Loroupe ni mwanariadha mstaafu na anashikilia rekodi [...]

07/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi wa kesho Kenya uwe wa salama na haki:OHCHR

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Albert Gonzalez Farran

Wataalamu huru watatu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameisihi mamlaka nchini Kenya kuhakikisha hali ya utulivu na uchaguzi salama, pamoja na mchakato wa uchaguzi uliowazi na wa haki. Ili kutorejelea hali ya machafuko na ukatili wa mwaka 2007, wataalamu hao wametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwahimiza wadau wote katika uchaguzi [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia bado inasuasua na haki za watu wa asili miaka 10 baada ya azimio:

Kusikiliza / Moja ya makabila ya watu wa asili nchini Ethiopia Picha ya UN/Rick Bajornas

Watu wa asili duniani bado wanakabiliwa na changamoto kubwa muongo mmoja baada ya azimio la kihistoria kuhusu haki za watu wa asili kupitishwa na baraza kuu limeonya leo kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa. Wakizungumza kabla ya siku ya watu wa asili duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 9 , kundi hilo la wataalamu [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wawili wa Iraq

Kusikiliza / Waandishi wa habari.(Picha:UM/Casey Crafford)

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, leo amelaani vikali mauaji ya waandishi wawili wa habari nchini Iraq. Ripota Harb Hazaa al-Dulaimi na mpiga picha Soudad al-Douri, maiti zao zilikutwa katika kijiji cha Imam Gharbi Kusini mwa Mosul Julai 20 . Bi Bokova amesema vifo vyao [...]

07/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uchunguzi Syria lazima uendelee licha ya kujiuzulu del Ponte

Kusikiliza / Wanawake, wanaume na watoto wapoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya ISIL. Picha: UM

Juhudi za kimataifa za ukuorodhesha ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria ni lazima ziendelee baada ya kujiuzulu mmoja wa wajumbe wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi , wamesema leo wajumbe wawili waliosalia wa jopo hilo la uchunguzi. Katika taarifa yao mjumbe Paulo Pinheiro na Karen AbuZayd, wamemshukuru Carla Del Ponte kwa huduma yake [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna kinachoweza kuhalalisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto Kasai:UNICEF

Kusikiliza / Mkimbizi wa ndani Bernard akiwa mji wa Idiofa, jimbo la Kwilu na wanae.(Picha:UNHCR/John Wessels)

Dunia isifumbie macho hali mbaya ya watoto na familia katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC . John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA KIBEGO) Onyo hilo limetolewa na mkurugenzi wa kanda ya Afrika ya Kati na Magharibi wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Marie-Pierre Poirie(MARI-PIERI_PORII) akisema [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dunia imetakiwa kutosahau ukatili wa ISIL dhidi ya Wayazidi

Kusikiliza / Familia ya waYazidi wapokea mgao wa chakula, Erbil, Iraq.(Picha:WFP/Chloe Cornish)

Miaka mitatu iliyopita mwezi huu kundi la kigaidi la ISIL lilishambulia mji waSinjar nchini Iraq, maskani ya Wayazidi walio wachache nchini humo na kuua raia na kuwafanya maelfu kukimbia. Pia maelfu ya wanawake na wasichana wa jamii hiyo walitekwa na kupelekwa Syria walikolazimishwa kuingia katika utumwa wa ngono. Wengi wao bado wanashikiliwa hadi leo. Katika [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031