Nyumbani » 04/08/2017 Entries posted on “Agosti 4th, 2017”

Uhaba wa maziwa na athari zake mkoani Kagera Tanzania

Kusikiliza / Mwanamke anakamua maziwa. Picha: UM/Eskinder Debebe (maktaba)

Shirika la afya ulimwenguni WHO, linasema maziwa ni miongoni mwa lishe muhimu hususani kwa ukuaji wa mtoto na afya ya mwanadamu. Kukosa maziwa hasa kwa watoto wa umri wa miaka mitano ni kukosa lishe muhimu na lishe duni huchangia vifo milioni 2.7 vya watoto kwa mwaka sawa na asilimia 45 ya watoto kote duniani. Binadamu [...]

04/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasanii Benin wapaza sauti dhidi ya ndoa za utotoni

Kusikiliza / Wasanii kutoka Benin. Picha:VideoCapture

Katika nchi zinazondelea, Umoja wa Mataifa unasema, msichana mmoja kati ya watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Ingawa kuna sheria kali dhidi ya hilo, desturi hizo bado zimetapakaa, zikisababishwa mara kwa mara na umasikini na ukosefu wa usawa wa kijinsia. Nchini Benin, wasanii kutoka jamii mbalimbali wamejitokeza na kushirikiana kwa pamoja kutumia [...]

04/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM kufunguliwa Liberia 2018

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour. Picha: MINUSCA

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu Andrew Gilmour leo amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Liberia. Lengo la zira yake ilikuwa ni kuanzisha ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini humo , na mkataba umetiwa saini na serikali kukubali kuanzishwa ofisi hiyo mpya mapema mwaka 2018. Mwisho wa ziara yake [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Venezuela lazima isitishe kuhukumu waandamanaji kijeshi na kuweka watu kizuizini

Kusikiliza / Waandamanaji wa amani nchini Libya. Picha: UNHCR

Serikali ya Venezuela ni lazima ikomeshe mfumo wa kuwakamata waandamanaji na ongezeko la matumizi ya mahakama za kijeshi kuwahukumu raia. Wito huo umetolewa leo na kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa . Kundi hilo pia limeitaka serikali ya Venezuela kuheshimu haki za waandamanaji wote na mahabusu na kuwahakikishia usalama wao [...]

04/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Libya yasalia kuwa kipaumbele cha IOM: Swing

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing zirani Libya. Picha: IOM

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing alienda Libya tena wiki hii ambako amerejelea kusema kwamba taifa hilo linasalia kuwa nchi inayopewa kipaumbele cha juu na IOM. Katika ziara hiyo ya pili mwaka huu ya Bwana Swing akiambatana na maafisa wengine wa IOM akiwemo mkuu wa ofisi yao [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki – KIAPO

Kusikiliza / NEnolaWikiKiapo

 Juma hili mchambuzi wetu ni Onni Sigalla mhariri mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akichambua neno “KIAPO”.

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Takribani asilimia 50 ya wanawake Tunisia waonja ukatili

Kusikiliza / Mkutano kati ya maafisa wa UN Women na ARP. Picha: UN Women

Tunisia imepiga hatua kubwa kwa kupitisha kwa mara ya kwanza sheria ya kitaifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake tarehe 26 July mwaka huu, ukatili unaoathiri asilimia 50 ya wanawake nchini humo, limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen . Taarifa kamili na Amina Hassan.. (Selina Amina) Sheria [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNDP, IOM na serikali kusaidia waathirika wa ukame Somalia

Kusikiliza / Mtoto kazaliwa wakati Somalia imepigwa na janga la ukame. Picha: IOM

Baada ya ukame mkali uliowatawanya na kuwaathiri watu zaidi ya laki nane nchini Somalia , sasa serikali ya nchi hiyo imeshikamana na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na shirika la Umoja wa Mataifa la mpangomwa maendeleo UNDP ili kuboresha juhudi na uwezo wa kukabiliana na ukame. Washirika hao watatu wameandaa mafunzo ya [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa Kasai DRC wachukua mwelekeo wa kikabila:UM

Kusikiliza / Eneo la Kasai. Picha: MONUSCO/Myriam Asmani

Machafuko katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yanaonekana kuchukua mwelekeo wa kikabila imeonya ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR. Taarifa kamili na John Kibego. (Sauti ya Kibego) Taarifa zilizokusanywa na timu ya uchunguzi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba baadhi [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031