Nyumbani » 02/08/2017 Entries posted on “Agosti 2nd, 2017”

Mfuko wa UM wasaidia tiba ya majeruhi wa shambulio la msikitini Afghanistan

Kusikiliza / Ali Ahmed, mmoja wa majeruhi aliyekuwa akisali msikitini, yuko katika hospitali wa Herat's nchini Afghanistan. Picha: UNAMA

Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa masuala ya kibinadamu umetenga dola 35,000 kwa ajili ya hospitali nchini Afghanistan inayotibu waathirika wa shambulio la kigaidi la msikitini umesema leo Umoja wa Mataifa. Fedha hizo zimekabidhiwa kwa hospitali kuu ya Herat iliyoko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambako takriban watu 44 waliuawa katika shambulio dhidi [...]

02/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni lazima kuhakikisha magaidi hawamili silaha:Fedotov

Kusikiliza / Yuri Fedotov, Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, akihutubia wanahabari jijini New York wakati wa kongamano la wadhamini katika kusaidia taasisi zinazopambana na uhalifu wa kuvuka mipala pwani ya Afrika Magharibi. (Picha:Maktaba/ UN /JC McIlwaine)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili tishio la ugaidi katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Baraza hilo ambalo limepitisha kwa kauli moja azimio nambari 2370 la mwaka 2017 la kuwazuia magaidi kumiliki silaha limesema ili kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa lazima nchi zishikamane kupambana na vitendo vyote vya kigaisi [...]

02/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana washirikishwe katika kutimiza SDGs: Sauli

Kusikiliza / Sauli 1

Umoja wa Mataifa unaendelelea kupigia chepuo ushirikishwaji wa vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Malengo hayo ni mtambuka ambapo vijana wana nafasi kubwa ya kuyafanikisha malengo yote iwapo watapewa fursa. Katika mahojiano na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kijana Sauli Paul Mwame wa kidato cha nne katika shule [...]

02/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yahimiza kuheshimu uhuru na haki ikiwataka wadau wote kujizuia na ghasia

Kusikiliza / Maman Sidikou, Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Maqtaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na mkuu wa MONUSCO.Picha:UM/Mark Garten

Maman S. Sidikou, mwakilishi maalimu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO, ameelezea hofu yake dhidi ya watu kukamatwa kiholea na kuwekwa rumande kunakofanyika katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo. Amesema kamatakamata hiyo ni kufuatia asasi za kiraia kuchagiza kuandamana [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama, kisiasa na changamoto Burundi yajadiliwa na baraza la usalama

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo kujadili hali nchini Burundi. Picha: UM/Manuel Elias

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali nchini Burundi. Katika kikao hicho kilichofanyika mjini New York Marekani wamezungumzia hali ya kisiasa, usalama, hali ya haki za kibinadamu na changamoto za haki za binadamu nchini humo. Akizungumza na waandichi wa habari kuhusu mkutano huo balozi wa kudumu wa Uingereza kwenye Umoja wa [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo na Kiir yamekuwa mazuri lakini bado tunawasiwasi: Lacroix

Kusikiliza / Jeane-Pierre Lacroix akikutana na Rais Salva Kiir. Picha:UNMISS

Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jeane-Pierre Lacroix, amesisitiza haja ya ushirikiano wa serikali ya Sudan Kusini katika kuhakikisha uhasama nchini humo unafikia ukomo. Akizungumza na waandishi wa habari,baada ya kukutana leo hii na rais Salva Kiir katika makao makuu ya jeshi la SPLA huko Bilpha Lacroix amesema baadhi ya [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq: FAO

Kusikiliza / Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq. Picha: FAO

Familia nyingi za vijijini nchini Iraq sasa zinafaidika na njia salama na ya uhakika ya kupokea fedha, asante kwa teknolojia ya kutuma fedha kupitia simu za rununu, iliyoanza kutumiwa kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo kama sehemu ya mpango wa malipo ya fedha kwa [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya 40 wafariki dunia kwenye shambulio msikitini Afghanistan:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa Antonio Guterres. Picha: UM

Waumini zaidi ya 40 wamearifiwa kuuawa wakiwemo watoto wawili na kujeruhiwa wengine zaidi ya 80 katika shambulio dhidi ya msikiti mjini Herart nchini Afghanistan. Amina Hassan na taarifa kamili (TAARIFA YA AMINA) Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio hilo la Agost Mosi na kusema mashambulizi ya makusudi dhidi ya raia [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031