Nyumbani » 01/08/2017 Entries posted on “Agosti 1st, 2017”

Hali nchini yemen bado ni tete:UNDP

Kusikiliza / Hali nchini Yemen bado ni tete. Picha: UNDP

Hali nchini Yemen bado ni tete na inahitaji kuendelea kutupiwa jicho zaidi. Hayo ni kwa mujibu wa Auke Lootsma mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Yemen alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York kwa njia ya video. Bwana Lootsma amesema hivi sasa Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba [...]

01/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Busara na uzoefu wa wazee na vijana ni muhimu kwa SDG:Guterres

Kusikiliza / mjadala wa rika mbalimbali  wenye lengo la kuchagiza mchango muhimu wa wazee na vijana katika utekelezaji wa SDGs. Picha: UM/Manuel Elias

Busara, uzoefu, ari na mawazo ya wazee na vijana ni muhimu katika kuhakikisha utimizaji wa malengo yote 17 ya maendeleo endelevu yaani SDG's. Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, katika mwanzo wa siku ya mjadala wa rika mbalimbali wenye lengo la kuchagiza mchango muhimu wa wazee na vijana katika [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM uko hapa kuwasaidia Wasudan Kusini kupata amani: Lacoix

Kusikiliza / Mkutano kuhusu mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacoix leo amewasili Juba nchini Sudan kusini ili kutathimini hali halisi na mikakati ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS katika kuhakikisha taifa hilo linafikia lengo la amani ya kudumu. Lacoix amekutana na maafisa wa serikali na kujadili masuala mbalimbali [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkakati wa WFP Tanzania utasaidia kutokomeza njaa

Kusikiliza / WFP kutokomeza umasikini nchini Tanzania. Picha: WFP/Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP hivi karibuni limezindua mkakati wa miaka mine wa kitaifa nchini Tanzania (CSP). Walengwa wakubwa wakiwa watanzania wenyewe hasa wakulima wadogo wadogo na wakimbizi kutoka nchi jirani. Ili kuchambua zaidi kuhusu mkakati huo, faida na madhumini yake Flora Nducha amezungumza na Juvenal Kisanga afisa wa [...]

01/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumeshuhudia madhila ya Boko haramu kwa watu:IOM

Kusikiliza / Mtoto akiwa katika kambi ya Assaga, karibu na Diffa, Niger.(Picha:UNICEF/Sylvain Cherkaoui)

Tumeshuhudia madhila kwa watu yalkiyosababishwa na uasi wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing baada ya kuzuru eneo hilo. Karibu watu milioni mbili wamezikimbia nyumba zao sababu ya Boko Haram, huku zaidi ya nusu ya watu waliotawanywa [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji umewaangusha mama na mtoto katika unyonyeshaji:UNICEF/WHO

Kusikiliza / Watoto watano kati ya sita hawapati lishe muafaka. Picha: UNICEF/UNI116106/Pirozzi

Unyonyeshaji ni moja ya njia muafaka na uwekezaji wa gharama nafuu unaoweza kufanywa na taifa lolote katika afya ya kizazi kipya na mustakhbali bora wa kiuchumi na jamii amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataiofa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake. Katika mwanzo wa wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo kila mwaka huwa Agost [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lacroix yuko CAR kusaka suluhu ya machafuko mapya

Kusikiliza / Jean-Pierre-Lacroix

Mkuu wa operesheni za amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ili kusaidia kupata suluhu ya kuzuia kuendelea kwa machafuko yanayotishia mchakato wa amani. Katika ziara hiyo ya siku tatu inayomalizika leo Jumanne Lacoix amekutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo, viongozi wa serikali na [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031