Nyumbani » 31/08/2017 Entries posted on “Agosti, 2017”

UNIFIL yaongezewa mwaka mmoja, Guterres apongeza

Kusikiliza / UNIFIL2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kupitisha kwa kauli moja azimio linaoongeza muda wa ujumbe wa umoja huo nchini Lebanon, UNIFIL hadi tarehe 31 Agosti 2018. Muda wa ujumbe huo ulikuwa  umalizike leo na sasa kufuatia kuongezwa muda, Katibu Mkuu amesema UNIFIL [...]

31/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usipowezeshwa hata kama si mlemavu , utalemaa

Kusikiliza / Bi Rebecca Altsi na Bi Fatma Wangare wakihojiwa na Idhaa ya Kiswahili. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Kuwa mlemavu sio kulemaa isipokuwa la msingi na kujumuisha ili nawe uweze kutoa mchango wako katika familia, jamii n ahata taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imetolewa na Bi Rebecca Altsi anayefanya kazi katika shirika linalohusika na walemavu wenye mgongo wazi au spina bifida na vichwa vikubwa na Fatma Wangare anayefanya kazi na shirika la inclusion [...]

31/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita vya kunyakua Raqqa havipaswi kugharimu raia-Zeid

Kusikiliza / Uharibifu wa mji wa Tabqa city, jimbo la Raqqa, Syria.(Picha: UNICEF/Souleiman.)

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein, amesisitiza kwamba vita vya kunyakua Al-Raqqa na Deir-ez-Zor kutoka kwa kundi la ISIL havipaswi kugharimu maisha ya raia walioko katika maeneo yaliyozingirwa. Zeid ameongeza kwamba lengo la kushindwa kwa ISIL ni kulinda na kusaidia raia ambao wameteseka kupitia mfumo wa [...]

31/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu akaribisha hatua ya kuachiwa huru viongozi Cameroon

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha kuachiwa huru kwa baadhi ya viongozi wa Cameroon kutoka maeneo ya Kusini Magharibi na Kaskazini Magharibi na kutupiliwa mbali kwa mashataka dhidi yao Agosti 30 baada ya amri ya rais Paul Biya. Kupitia taarifa ya msemaji wake, Guterres ana matumaini kwamba hatua hii itapelekea katika kupunguza [...]

31/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasyria wasilipe gharama ya mkwamo wa kisiasa- O'Brien

Kusikiliza / Obrien1

  Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura akihutubia kwa njia ya video kutoka Geneva, Uswisi (Picha:UN/Kim Haughton) Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeshauriwa kusaka njia ya kuondokana na mwelekeo wa sasa huko Syria ambako raia wasio na hatia wanalipa gharama ya mkwamo wa mchakato wa kisiasa. Mkuu [...]

30/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyombo vya habari vyazidi kuminywa nchini Misri

Kusikiliza / Polisi wanajaraibu kutuliza maandamano kuhusu uhuru wa kujieleza na haki za binadamu nchini Misri. Photo: IRIN/Amr Emam (file)

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameeleza wasiwasi wao juu ya vitendo vya serikali ya Misri kubinya uhuru wa kujieleza wa vyombo vya habari nchini humo. Wataalamu hao ni David Kaye ambaye ni wa masuala ya uhuru wa kujieleza, na Fionnuala Ní Aloáin anayejikita katika kupambana na ugaidi. Katika taarifa yao, wataalamu hao wameshtushwa na [...]

30/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa usalama unatukwaza vijana DRC- Sehemu ya pili

Kusikiliza / Vijana kusambaratishwa na migogoro nchini DRC. Picha: UN News Center

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ghasia hususan mashariki mwa nchi hiyo zimesababisha maelfu ya watu kusaka hifadhi nchi jirani. Maisha ugenini ni ya kuwezesha mkono kwenda kinywani lakini mawazo ni kurejea nyumbani. Miongoni mwa raia waliokimbia ni Kiiza Serugendo Elwa kutoka mji wa Kiwanja, Jimboni Kivu ya Kaskazini . Sasa Kiiza ni mchuuzi [...]

30/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na wadau wahaha kudhibiti Kipindupindu Nigeria

Kusikiliza / Juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu kaskazini-mashariki mwa nchini Nigeria. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni, WHO na wadau wake wamechukua hatua za dharura kusaidia mamlaka nchini Nigeria kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Hadi sasa wagonjwa 69 wameripotiwa huku watano kati yao wamefariki dunia kwenye kambi ya Muna Garage iliyoko kwenye viunga vya mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri. Katika [...]

30/08/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zeid ataka hatua zichukuliwe dhidi ya Venezuela

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein. Picha: UM/Video capture

Uhuru wa kujieleza unabanwa nchini Marekani na hili lina madhara. Hii ni kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , Zeid Ra’ad Al Hussein wakati akihutubia waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi kuhusu hali inyaoendelea kuzorota nchini Venezuela. Katika mkutano huo kuhusu Venezuela, aliulizwa swali kuhusu matamshi dhidi ya [...]

30/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wailaani Korea Kaskazini kwa kurusha kombora

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili DPRK. Picha: UM/Evan Schneider

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa   limelaani vikali tukio la Jamhuri ya kidemkrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha kombora na kuvuka kisiwa cha Japan. Kupitia taarifa iliyosomwa na rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Agosti Balozi Amr Aboulatta mwishoni mwa kikao cha dharura kilichoitishwa Jumanne jioni, wajumbe wa baraza wamesema kitendo [...]

30/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wapalestina ungananeni kwa misingi ya PLO- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ziarani Mashariki ya Kati. Picha: UN Women/Eunjin Jeong

Katika siku ya mwisho ya ziara yake huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesihi kuwepo kwa umoja kati ya wapalestina wa eneo hilo la Gaza na wale wa Ramallah. Patrick Newman na ripoti kamili. (Taarifa ya Patrick) Leo Jumatano, Bwana Guterres ametembelea makumbusho ya wayahudi ya Kibbutz Nahal Oz [...]

30/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji na kupoteza makazi vyashamiri Kasai, DRC- WFP

Kusikiliza / Kasai-3

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limeelezea masikitiko yake juu ya janga linaloendelea kwenye majimbo yaliyoko eneo la Kasai nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC. (Taarifa ya Grace) WFP inasema maelfu ya watu wameripotiwa kuuawa na kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja na zaidi ya milioni moja wamekimbia vijiji vyao tangu mwezi Agosti mwaka [...]

30/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yalaani ofisi zake kuingiliwa na askari wa DRC bila ruhusa

Kusikiliza / Maman Sidikou, Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na mkuu wa MONUSCO.Picha:UM/Mark Garten

Mwakililishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC  Maman Sidikou amelaani vikali kitendo cha vikosi vya jeshi la nchi hiyo kuingia bila ruhusu kwenye ofisi za ujumbe wa umoja huo huko Kananga, jimbo la Kasai Kati. Katika tukio hilo la Jumatatu, askari wa jeshi la DRC chini [...]

29/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mataifa mawili ndio muarobaini kwa Israel na Palestina- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres awasili kwenye Kituo cha waathirika wa vurugu huko Ramallah, Palestina. Picha: Picha ya UN / Ahed Izhiman

Katibu Mkuu  wa Umoja wa mataifa António Guterres akiwa katika ziara ya siku tatu  huko Mashariki ya Kati amesema ni muhimu kuanzisha  upya mchakato wa amani unaoaminika. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Palestina, Rami Hamdallah Bwana Guterres amesema mchakato huo kati ya Israel na Palestina utasaka ufumbuzi [...]

29/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wa Asili kushirikishwa katika utekeleshwaji wa SDGs: Laitaika Sehemu ya 2

Kusikiliza / Familia ya watu wa Asili wakagua bwawa la maji. Picha: UM/Video capture

Mwaka huu ni miaka kumi tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kwenye Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Tangu wakati huo kuna hatua kubwa zimepigwa hususani barani Afrika has kuwatambua watu wa asili lakini pia kufahamu kuhusu azimio hilo la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji [...]

29/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 50 wa Ethiopia waliokwama puntland warejea nyumbani- IOM

Kusikiliza / Wahamiaji wa Ethiopia waliokwama puntland warejea nyumbani. Picha: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limewezesha wahamiaji 50 wa Ethiopia waliokuwa wamekwama kwenye eneo lililojitenga la Puntland huko Somaliland kurejea nyumbani. Miongoni mwao ni wanaume 29 , wanawake 5 na watoto 16 na walirejea nyumbani kwa hiari kwa ushirikiano baina ya wizara ya mambo ya  ndani ya Puntland , kituo cha dharura cha uhamiaji [...]

29/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maendeleo endelevu na amani haviwezi kuachana- Amina

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akihutubia Baraza la Usalama. Picha: UM/Kim Haughton

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao cha kuangazia mchango wa operesheni za ulinzi wa amani za umoja huo katika kuchagiza jitihada za kudumisha amani duniani. Akifungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema ni dhahiri shahiri kuwa ajenda ya maendeleo endelevu iliyopitishwa haiwezi kufanikiwa [...]

29/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dhoruba Harvey limeleta hali ya jinamizi jimboni Texas-WMO

Kusikiliza / Kimbunga Harvey limesababisha mafuriko katika maeneo kadhaa Texas. Picha: WMO

Dhoruba inayokumba jimbo la Texas nchini Marekani ni jinamizi ambalo linaendelea, limesema shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO. Joseph Msami na ripoti kamili. (Taarifa ya Joseph) Hofu ikiendelea kutanda huko Texas, baada ya mvua kubwa na upepo mkali kukumba eneo hilo na kusababisha vifo na mafuriko, WMO imetoa onyo ikisema kuwa [...]

29/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani jaribio la kombora kutoka DPRK

Kusikiliza / Mlipuko wa nyuklia. (Picha-Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani jaribio la hivi karibuni zaidi la kombora la masafa marefu lililofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa jaribio la kombora hilo lilifanyika jana na lilivuka kisiwa cha Japan. Kufuatia taarifa hizo, Bwana Guterres amesema kitendo hicho ni kinyume [...]

29/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bangladesh fungulieni mipaka warohingya wanaokimbia ghasia Myanmar

Kusikiliza / Baada ya kukimbia vurugu, idadi ya wakimbizi wa Rohingya imeongezeka kwa kasi katika kambi ya muda ya Cox's Bazar, Bangladesh. Picha: © UNHCR/Saiful Huq Omi

Umoja wa Mataifa umesema bado kuna tatizo kubwa kuwafikia waliokumbwa na ghasia kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar wakati huu ambapo hali ya usalama inazidi kuzorota kutokana mapigano kati ya waumini wa kibuda walio wengi na waislamu ambao ni wachache. Ghasia ziliibuka kwenye eneo la kaskazini-magharibi mwa jimbo hilo siku ya ijumaa baada ya majengo [...]

29/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maji yasalia ndoto kwa walio kwenye mizozo- UNICEF

Kusikiliza / Wamama wanakusanya maji. Picha: UNICEF

Zaidi ya watu milioni 180 walioko kwenye maeneo yenye vita na  mizozo hawana maji. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema hayo leo katika ripoti yake iliyotolewa kwenda sambamba na wiki ya maji. (Taarifa ya Patrick) Mkuu wa UNICEF anayehusika na masuala ya maji duniani,  Sanjay Wijesekera amesema watoto kwenye nchi hizo [...]

29/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afya ya vijana, UM wataka ushiriki kikamilifu

Kusikiliza / Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez. (Picha:UM-Tanzania)

Mkutano wa siku mbili wa vijana kitaifa kuhusu afya na maendeleo umeanza mjini Dar es Salaam Tanzania, ambapo Umoja wa Mataifa nchini humo umesema afya bora ambalo ni lengo namba tatu la malengo ya mendeleo endelevu ni lengo mtambuka na hivyo ushiriki wake ni muhimu sio tu kwa kundi tajwa bali jamii kwa ujumla. Akizingumza [...]

29/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walibya hawaamini kuwa ni hohehahe ndani ya nchi tajiri- Salamé

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo  Ghassan Salamé. Picha: UM/Video capture

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti kuhusu hali ya kiusalama, kiuchumi na kijamii nchini Libya ambapo wajumbe wamejulishwa kuwa hali ya kiuchumi inazorota. Akihutubia Baraza hilo kwa njia ya video kutoka Tripoli, Libya, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo  Ghassan Salamé amesema licha ya kuongezeka kwa [...]

28/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kila mtu ana wajibu wa kutatua changamoto ya maji- Thompson

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Peter Thompson akihutubia kongamano la kuadhimisha wiki ya maji duniani la 2017 huko mjini Stockholm, Sweden Picha: UNPGA Twitter feed

Wakati kongamano la kuadhimisha wiki ya maji duniani likiwa limeingia siku ya pili huko mjini Stockholm, Sweden rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Peter Thompson amesema suala la maji na huduma za kujisafi ni muhimu katika malengo 17 ya maendeleo endelevu  yaani SDGs. Maudhui ya wiki ya maji mwaka huu ni "Maji na [...]

28/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila uchao migogoro yaongezeka, mkakati wa uzuiaji ndio suluhu- O'Brien

Kusikiliza / Mratibu wa Umoja Mataifa katika masuala ya usaidizi wa kibinadamu Stephen O'Brien anazungumza na mwanamke katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dayniile Mogadishu, Somalia. Picha: UM/Tobin Jones

Mratibu wa Umoja Mataifa katika masuala ya usaidizi wa kibinadamu Stephen O'Brien, amesema licha ya juhudi za usaidizi wa kibinadamu, pengo la uhitaji limeongezeka hivyo jumuya ya kimataifa ina wajibu mkubwa wa kuongeza usaidizi. O'Brien ambaye amengoza ofisi hiyo kuanzia kwa takribani miaka mwili na nusu, amefanya mahojiano maaluma na redio ya Umoja wa Mataifa  [...]

28/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi Yemen waendelea kudhibiti Kipindupindu licha ya kukosa mishahara

Kusikiliza / Hao ni watoto wa Hemiar Mohammed. Mama yao Fauzia alikimbizwa hospitali kufuatia maradhi ya ghafla ya kipindupindu. Picha: © UNICEF Yemen/2017/Alzekri

Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF leo katika ripoti yake limesema kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen imepungua. Limesema hali hiyo inatokana na juhudi za wananchi kwa msaada wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine kupiga vita ugonjwa huo hatari. Naibu mkurugenzi wa kitengo cha kipindupindu katika hopitali Alsadaqah jijini [...]

28/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna hatua, lakini safari ni ndefu kutimiza haki za watu wa asili: Laitaika Sehemu ya 1

Kusikiliza / Watu wa Asili barani Afrika. Picha: Andi/Gitow

Mwaka huu ni miaka kumi tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kwenye Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Tangu wakati huo kuna hatua kubwa zimepigwa hususani barani Afrika has kuwatambua watu wa asili lakini pia kufahamu kuhusu azimio hilo la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji [...]

28/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 200 kusaidia Yemen kukabili Kipindupindu

Kusikiliza / Mama na mwanae aliyelazwa katika kituo cha afya kufuatia maradhi ya kipindupindu. Picha: UNICEF

Benki ya Dunia imetangaza mkopo nafuu wa dola milioni 200 kwa Yemen ili iweze kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Kristalina Georgieva, ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha mifumo ya maji, afya na majitaka nchini humo na pia kuepusha milipuko ya ugonjwa huo siku za usoni. Mathalani [...]

28/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatuna taarifa za wakimbizi kutoka Burundi kufurushwa kutoka Tanzania- Alvaro

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi. © UNHCR/Sebastian Rich

Hatma ya wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa nchini Tanzania itabainika Alhamisi wiki hii wakati mkutano wa pande tatu utakapofanyika. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Hiyo ni kwa mujibu wa Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alipohojiwa na Idhaa hii kufuatia ripoti za vyombo vya habari kuwa serikali ya Tanzania imetoa [...]

28/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres ashangazwa na wanaopigia chepuo chuki dhdi ya wayahudi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Ziarani Isarel. Picha: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ameeleza kushangazwa kwake na baadhi ya watu hata katika nchi zilizoendelea kupigia chepuo vitendo vilivyotekelezwa na manazi dhidi ya wayahudi. Joseph Msami na ripoti kamili. (Taarifa ya Joseph) Bwana Guterres amesema hayo baada ya kutembelea makumbusho ya Yad Vashem ya mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi huko [...]

28/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wapaswa kuchangamkia fursa: Kijana Fatma

Kusikiliza / Fatma-1

Uthubutu na kusaka fursa badala ya kusubiri miujiza ni nyenzo muhimu ya mafanikio kwa vijana, amesema Fatma Said Ahmed, Mwanzilishi wa taasisi ya StandforHumanity na pia mshiriki wa mwaka  2016 wa kundi la viongozi vijana la Michael Johnson. Katika mahojiano na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania, Fatma ambaye hujihusisha [...]

28/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres apongeza Kuwait kwa mchango wake katika maswala ya kiutu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azungumza na waandishi wa habari Kuwait.(Picha:UM/Stéphane Dujarric)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, amepongeza Kuwait kwa uongozi wake katika maswala ya kibinadamu na mchango wake katika kutatua mzozo ulioko maeneo ya Ghuba. Guterres amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na kiongozi wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah. Aidha amekumbusha ushiriki wa kiongozi huyo katika [...]

27/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inahitaji fedha zaidi kwa ajili ya wakimbizi walioko Tanzania

Kusikiliza / Baba na wanae katika kambi ya wakimbizi ya Nyargusu nchini Tanzania.(Picha:UM/Tala Loubieh)

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limelazimika kupunguza mgao wa chakula kinachotolewa kwa wakimbizi 320,000 wanaoishi katika kambi za Mtendeli, Nduta na Nyarugusu mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kwa sababu ya upungufu wa fedha. WFP inahitaji kwa haraka jumla ya Dola za Marekani milioni 23.6 kuanzia sasa hadi [...]

27/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vijana na amani na mustakhbali wao barani Afrika

Kusikiliza / Hujambo..ni ishara anaotoa msichana huyu wa Liberia na kijana mwenzake hapo pembeni wakipitisha ujumbe kwamba vijana wanaweza. Picha: UN Photo/Staton Winter (maktaba)

Kongamano la vijana barani Afrika  limefanyika wiki hii nchini Burundi. Katika kipindi cha siku tano,  vijana washiriki wapatao 350 kutoka mataifa mbalimbali  barani Afrika wameazimia  uanzishwaji wa fuko maalumu la kusaidia vijana kubuni ajira. Aidha  Vijana wamechagizwa kutotumiwa na wanasiasa kama ngazi ya kufikia  malengo yao. Bara la Afrika  lina idadi ya vijana takriban milioni [...]

25/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Makombora Sana'a yaua raia- OHCHR

Kusikiliza / Mama mkimbizi na mtoto wake akitizama mji mkuu wa Sana'a kutoka juu ya jengo liloharibika. Picha: Giles Clarke/UN OCHA

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema makombora yaliyorushwa kutoka angani siku ya Jumatano kwenye maeneo mawili tofauti mjini Sana'a Yemen, yamesababisha vifo vya raia 33 na wengine 25 wamejeruhiwa. Watu walioshuhudia matukio hayo wameieleza ofisi hiyo kuwa makombora hayo yaliangushwa kwa nyakati mbili tofauti kati ya saa tisa na saa kumi [...]

25/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM walaani mashambulizi ya jimbo la Rakhine, Myanmar Kaskazini

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini Myanmar. Picha: OCHA/P.Peron

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa huko Myanmar Bi. Renata Lok-Dessallien  amelaani vikali mashambulizi dhidi ya majeshi ya usalama katika Jimbo la Rakhine Myanmar kaskazini mapema Agosti 25. Bi Dessallien ameelezea kusikitishwa na kupoteza kwa maisha ya wananchi huku akituma salamu za rambirambi  kwa familia zote na kuwatakia heri   katika kipindi hiki kigumu Amezisihi pande zote [...]

25/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila wanayokumbana nayo watoto Syria hayatajiki- UNICEF

Kusikiliza / Mtoto asimama karibu na jengo lilioporomoka. Picha: UNICEF

Athari wanazopata watoto kutokana na vita vinavyoendelea nchini Syria ni za kusikitisha, amesema mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo Fran Equiza. Equiza akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi baada ya ziara yake kwenye maeneo ya Areesha Eza,  Ein Issa na Mabrouka amesema ameshuhudia watoto waliopoteza makazi [...]

25/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nimependa muziki tangu utotoni-Kiba

Kusikiliza / Mwanamuziki Ali Kiba. Picha: UM/Video capture

Mimi sikuchagua muziki, bali muziki ulinichagua! Hiyo ni kauli ya mwanamuziki Ali Kiba wakati alipohojiwa na Idhaa ya Kiswahili. Mwanamuziki huyu ambaye ni mashuhuri nchini mwake Tanzania na nje anasema safari ya kufikia wasanii katika fani mbali mbali kula jasho lao bado haijafikiwa, hata hivyo, hajakata tamaa. Kiba anazungumzia safari yake ya muziki ilipoanza na [...]

25/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki: Mlipuko na Mkurupuko

Kusikiliza / Neno-la-wiki_Mlipuko-na-Mkurupuko 1

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Mlipuko” na “Mkurupuko” Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Nuhu anasema neno “mlipuko” ni sauti ya ghafla ya kutisha ambayo inayotokana na moto au upasuaji ya mti na mengineyo, na [...]

25/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Feltman aelezea mshikamano wa UM na Somalia

Kusikiliza / Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khayre. Picha:  UM/ Tobin Jones

Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman, ameelezea dhamira ya Umoja huo kuendelea kufanya kazi na watu na serikali ya Somalia katika kukabiliana na baadhi ya changamoto ili kuwezesha Somalia kufikia uwezo wake kamili. Akizungumza mjini Mogadishu baada ya mazungumzo na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini [...]

25/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chuki dhidi ya jamii ya Igbo ni uchochezi wa machafuko: UM

Kusikiliza / Mutuma Rutere  ni mwakilishi maalumu dhidi ya mifumo yote ya kisasa ya ubaguzi.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Umoja wa Mataifa umelezea kusikitishwa kwake na vitisho na hatua ya kutakiwa kuondoka kwa watu wa kabila la Igbo huko Kaskazini mwa Nigeria, ifikapo Oktoba mosi mwaka huu. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Watalaamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kwamba  vitisho dhidi ya kabila la Igbo vimekwenda mbali zaidi ambapo vimeambatana na [...]

25/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Doria za usiku kufanyika Torit, Sudan Kusini- UNMISS

Kusikiliza / Sudan Kusini-2

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , UNMISS umepanga kuimarisha doria yake kwenye mji wa Torit kwenye jimbo la Imatong ili kuweka fursa nzuri ya ustawi na maendeleo. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer amesema hayo baada ya mazungumzo na gavana wa jimbo  hilo akisema [...]

25/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati wa viongozi kuchukua hatua nchini Sudan Kusini ni sasa

Kusikiliza / Naibu Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa El-Ghassim Waneakihutubia Baraza la usalama leo. Picha: UM//Kim Haughton

Mzozo wa Sudan Kusini umeanzishwa na binadamu na viongozi nchini humo wana wajibu wa moja kwa moja kuutatua. Hiyo ni kauli ya Naibu Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa El-Ghassim Wane aliyotoa wakati akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo jijini New York, Marekani. Kikao kilikutana  kujadili hali [...]

24/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha ripoti kuhusu Rakhine

Kusikiliza / Raia nchini Myanmar. Picha: UM

Umoja wa Mataifa umekaribisha ripoti ya kina iliyotolewa leo an kamisheni ya ushauri kuhusu jimbo la Rakhine huko Myanmar ambalo waumini wa dini ya kiislamu wanakabiliwa na sintofahamu ya utaifa. Ripoti hiyo ilitangazwa leo na mwenyekiti wa kamisheni  hiyo ya watu tisa, Kofi Annan ikisisitiza suala la uraia kwa wananchi na kutoa wito wa watu [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahitaji ya kibinadamu Raqqa nchini Syria ni zaidi ya inavyofikirika

Kusikiliza / Picha: UNICEF/Souleiman

Mahitaji ya kibinadamu kwa maelfu ya raia walionasa kwenye eneo linaloshikiliwa na magaidi wa ISIL huko Raqqa nchini Syria ni makubwa kuliko inavyofikirika. Hiyo ni kwa mujibu wa Jan Egeland ambaye ni mshauri maalum wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi hii leo baada ya kikao cha kikosi kazi [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shida haibagui wala haichagui, tusaidiane: Mugenyi

Kusikiliza / Unicef linasisitiza elimu kwa watoto wakimbizi. Picha: UNICEF

Shida haina adabu, haichagui , wala haibagui inapokufika imekufika, la msingi kusaidiana. Huo ni wito wa Iddi Mugenyi mkurugenzi wa shule ya sekondari ya East african Muslim High school iliyoko nchini Uganda. Shuleni kwake anasaidia watoto wakimbizi takribani 50 hususan masuala ya karo ili waweze kupata elimu ambayo ni ufunguo wa maisha. Anawaasa Waganda wenzie [...]

24/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Takribani watu milioni 41 waathiriwa na mafuriko na maporomoko Nepal, Bangladesh na India

Kusikiliza / Hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi Bangladesh, Nepal na India. Picha: UM

Ofisi ya Umoja wa mataifa  ya kuratibu msaada ya kibinadamu, OCHA imesema hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi huko Bangladesh, Nepal na India inaweza kuwa mbaya zaidi na kuleta madhara zaidi kutokana na uwezekano wa mvua kuendelea kunyesha na maji ya mafuriko kuelekea kusini. OCHA inasema tayari mvua kubwa imesababisha madhara ikiwemo vifo vya [...]

24/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ufugaji wa bata badala ya kuku wapunguza majanga Vietnam- UNISDR

Kusikiliza / Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa majanga, UNISDR Robert Glasser .(Picha:UM/Mark Garten)

Umoja wa Mataifa umesema ingawa majanga ya asili hugharimu serikali pesa nyingi bado kuna mikakati nafuu inayoweza kuepusha nchi kukabiliana au kuepusha hasara inayoweza kutokea. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa majanga, UNISDR Robert Glasser amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa siku moja kabla ya kuanza kwa [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wanaoingia Ulaya yapungua lakini ukatili wanaopata waongezeka

Kusikiliza / Wakimbizi na wahamiaji wanaosubiri kuokolewa baada ya chombo kinachobeba zaidi ya watu 700 kuzama. Picha: MOAS.eu2017

Idadi ya wakimbizi na wahamiaji waliowasili Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu kupitia moja ya njia tatu zinazotumika,  imepungua ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR iliyotolewa hii leo ikiangazia njia tatu za kuvuka kuingia barani [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Japan yatoa dola milioni 10 kusaidia wakimbizi, Uganda

Kusikiliza / Mhudumu wa afya anapima mtoto kutafuta ishara za utapiamlo katika kituo cha afya kambini Nyumanzi nchini Uganda. Picha: © UNHCR/Jiro Ose

Serikali ya Japan imetoa mchango wa dola milioni kumi kama uitikio wao kwa mahitaji yanangezeka katika jamii ya wakimbizi na wenyeji Kaskazini mwa Uganda kutokana na mmiminoko wa wakimbizi kutoka Sudan Kusini. John Kibego na maelezo Zaidi. (Sauti ya Kibego) Mwakilishi wa Shirka la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda,, Bornwell Kantande [...]

24/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ndege iliyokodishwa na WFP yaua mtoto Sudan Kusini

Kusikiliza / Ndege iliyokodishwa na WFP yaua mtoto Sudan Kusini. Picha: WFP

Nchini Sudan Kusini mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia na watu wengine wanne wamejeruhiwa baada ya ndege moja kugonga nyumba kwenye mji mkuu Juba. Joseph Msami na ripoti kamili. (Taarifa ya Joseph) Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ambapo iligonga nyumba hiyo wakati rubani akijaribu kutua [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Polisi Somalia wanolewa kuhusu ukatili wa kingono

Kusikiliza / Mafunzo3

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM unawapatia polisi nchini humo mafunzo kuhusu jinsi ukatili wa kingono unavyoweza kuzua mizozo na kuotesha mizizi ukatili kwenye jamii. Mafunzo hayo yanatolewa kupitia warsha ya siku tatu kwa kushirikiana na Wizara ya wanawake na haki za binadamu yataongeza ufahamu wa polisi kuhusu hatari za ukatili [...]

24/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Anti-Balaka na FPRC wapambana huko CAR

Kusikiliza / Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika ulinzi wa Amani. UM/Catianne Tijerina

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA umeripoti mapigano hii leo kati ya wanamgambo wa kikundi cha Anti-Balaka na wale wa FPRC awali wakijulikana kama Seleka. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema mapigano hayo yametokea kwenye eneo la Ngubi, karibu na mji wa Bria jimboni [...]

23/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa uhakika wa chakula huchochea uhamiaji- Ripoti

Kusikiliza / Wamama hao ni baadhi ya wahamiaji. Picha: WFP

Ripoti mpya ya utafiti wa pamoja wa mashirika mbali mbali ikiwemo lile la Mpango wa chakula duniani WFP , imebaini uhusiano uliopo kati ya ukame wa muda mrefu nchini El Salvador, Guatemala na Honduras uliochochewa na El Niño ya kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 na kuongezeka kwa wahamiaji kutoka nchi hizo kuelekea Marekani. Akizungumzia ripoti [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fursa na vikwazo katika juhudi za vijana kujikwamua nchini DRC 1

Kusikiliza / Kijana mfanyakazi wa kujitolea nchini DRC. Picha: UM/Sylvain Liechti (maktaba)

Katika mfululizo wa makala zinazomulika juhudi za vijana katika kujikwamua kiuchumi, tunakupeleka Afrika Mashariki kusikiliza mahojiano na  kijana mjasiriamali Kiiza Serugendo Elwa kutoka mji wa Kiwanja, Jimboni Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Ungana na John Kibego katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano na kijana huyu ambaye kwa sasa yuko [...]

23/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waikosoa Marekani kushindwa kukemea siasa za ubaguzi

Kusikiliza / Onyesho la upendo kwa wote. Picha:NICA/51602

Kamati ya Umoja wa mataifa ya kupiga vita vya ubaguzi wa rangi inayoendelea na kikao chake mjini Geneva Uswis (CERD) leo  imeikosoa serikali ya marekani pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa kwa kushindwa kukemea maandamano ya chuki, kibaguzi na uhalifu uliotokea Charlottesvilles Virginia na nchini kote. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tutokomeze ubaguzi tukiadhimisha kumbukizi ya utumwa: UNESCO

Kusikiliza / Hebu kumbukumbu na historia ya biashara ya watumwa na kufutiliwa kwake uendeshe majadiliano, kuvumiliana na kuelewa kwa pamoja. Picha: UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi  ya biashara ya utumwa na kutokomezwa kwake, Umoja wa Mataifa umetaka siku hii itumike kukemea aina zote za unyanyasaji na ubaguzi unaoripotiwa duniani hivi sasa. Assumpta Massoi na taarifakamili. ( TAARIFA YA ASSUMPTA) Katika ujumbe wake kuhusu siku hiyo , Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria nchini Jordan kupata ajira

Kusikiliza / Kituo cha kwanza cha ajira nchini Jordan kwa ajili ya wakimbizi wa Syria. Picha: ILO

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kazi ILO na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR wamezindua ofisi ya kwanza kabisa ya ajira ndani ya kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan. Ofisi hiyo iliyoanzishwa kwa uratibu na serikali ya Jordan itawezesha wakimbizi waishio kwenye kambi hiyo kupata ajira rasmi nchini humo. Mratibu wa ILO kuhusu janga [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yazindua mradi wa kuchagiza ajira ya vijana Burkina Faso

Kusikiliza / IOM yazindua mradi wa kuchagiza ajira ya vijana Burkina Faso. Picha: UN Migration Agency (IOM) 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limesema  limezindua mradi mpya unaoshughulika na uhusiano kati ya vijana, ajira na uhamiaji katikati na Mashariki Burkina Faso. Mradi huo unalenga kukuza uajiri wa vijana na ujasiriamali ili kupunguza hatari ya uhamiaji katika kanda hiyo  Burkina Faso, kama ilivyo nchi zingine za Afrika Kusini mwa Jangwa [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni dhidi ya ujangili ilileta mabadiliko- Kiba

Kusikiliza / Ali Kiba

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania Ali Kiba amesema kampeni ya kulinda wanyamapori ambayo alishiriki akiwa Balozi wa WILDAID ilikuwa ya mafanikio makubwa kwa kuwa ilijenga hamasa miongoni mwa makundi mbali mbali. Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Kiba ambaye ameshinda tuzo za kimataifa, kikanda na kitaifa [...]

23/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS yatowesha hofu kwa watoto Sudan Kusini.

Kusikiliza / Watoto wakicheza nchini Sudan Kusini. Picha kwa hisani ya video ya UNMISS.

Hofu,mashaka mtawalia! Haya ni baadhi ya madhila yaliyowakumba watoto nchini Sudan Kusini kabla ya operesheni ya kikosi cha ulinzi wa amani cha  Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kilichotowesha madhila hayo. Katika Makala ifuatayo, Joseph Msami anaeleza mustakabali wa watoto nchini Sudan Kusini taifa lililokumbwa na mizozo.

22/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Pande mbili husika zina wajibu katika jawabu la swala la Palestina- Jenča

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hali Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina. Picha: UM/Evan Schneider

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali Mashariki ya Kati na hoja ya Palestina. Akihutubia kikao hicho Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu maswala ya kisiasa Miroslav Jenča amewataka viongozi wa Palestina kuzingatia matokeo haribifu yanayotokana na migawanyiko Palestina na kufikia makubaliano ili kuwezesha mamlaka Palestina kutekeleza wajibu Gaza katika juhudi za [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa ubakaji wa ISIL lazima wapate msaada unaohitajika-UM

Kusikiliza / Mwanamke mYazidi Kurd kutoka Sinjar aliyenaswa na wanamgambo wa ISISL,. Yuko kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mamilyan nchini Iraq. Picha: Giles Clarke/ Getty Images Reportage

Leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI wametoa ripoti ikiitaka serikali ya Iraq kuhakikisha kwamba maelfu ya wanawake na wasichana manusura wa ubakaji na mifumo mingine ya ukatili wa kingono ulioteklelezwa na kundi la ISIL wanapata huduma, ulinzi, na haki na kwamba [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa EU kwa WFP kupunguza machungu kwa wakimbizi Algeria

Kusikiliza / Wakimbizi nchini Algeria. Picha:WFP/Algeria

Muungano wa Ulaya, EU umelipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP msaada wa dola milioni 5.5 kwa ajili ya mahitaji muhimu ya chakula kwa wakimbizi wa Sahrawi walioko kwenye kambi nchini Algeria. Kupitia fedha hizo wakimbizi watakuwa na uhakika wa mlo ambapo watapatiwa nafaka, mafuta, sukari na vyakula vilivyoongezewa virutubisho. Mwakilishi wa WFP nchini [...]

22/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha Burundi cha kulinda amani chawasili Somalia

Kusikiliza / Kikosi cha Burundi cha kulinda maani chawasili Somalia.(Picha:AMISOM/ ilyas AHmed)

Kikosi kipya cha ulinzi wa amani kutoka nchini Burundi BNDF, kimewasili nchini Somalia kwa ajili ya kazi hiyo itakayodumu kwa mwaka mmoja chini ya ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM. Kwa mujibu wa wavuti wa AMISOM, BNDF, chenye maafisa 45, kinachukua nafasi ya kikosi kingine cha 39 ambacho kimemaliza muda wake ambapo kimetimiza [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watoto wanaojilipua Nigeria yaongezeka- UNICEF

Kusikiliza / Watoto wanatumika katika kwenye mashambulizi ya kujilipua.(Picha:UNICEF / UN015784 / Prinsloo)

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limeeleza masikitiko yake kufuatia ongezeko la watoto wanaotumiwa kwenye mashambulizi ya kujilipua huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria. (Taarifa ya Kibego) Msemaji wa UNICEF huko Geneva, Uswisi Christophe Boulierac amesema katika kipindi cha mwaka mmoja idadi imeongezeka mara nne. Bwana Boulierac amesema kitendo cha kutumia watoto ni mauaji [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid apongeza kufutwa kwa sheria zinazolinda wabakaji

Kusikiliza / Wanawake waokumbwa na ubakaji husalia na msongo. Picha: UM

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein amekaribisha kitendo cha Lebanon, Tunisia na Jordan kufutilia mbali sheria ambazo zinalinda wabakaji dhidi ya mashtaka kwa kuwaruhusu kuwaoa wale waliowabaka. (Taarifa ya Assumpta) Zeid amesema kitendo cha wabunge katika nchi hizo kufuta sheria hizo kinadhihirisha azma yao ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake. [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waisaidia Libya kukabilii usafirishaji haramu wa binadamu:

Kusikiliza / Mmoja wa wahamiaji waliorejeshwa kwa hiyari kutoka Libya akifanya ujasiriamali. Picha na IOM

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM uko bega kwa bega na serikali ya Libya katika kukabili usafirishaji haramu wa binadamu. Kwa mujibu wa Maria do Valle Ribeiro naibu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Libya , hiyo ni biashara haramu na ya hatari [...]

22/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia zinazoendeshwa na magenge El Salvador zatishia raia

Kusikiliza / Baba na mwanae, familia ambayo walikimbia machafuko nchini El Savador.(Picha:ACNUR / Markel Redondo)

Mamlaka nchini El Salvador zinapaswa kuchukua hatua zaidi ili kusaidia raia wanaokimbia makazi yao kutokana na ghasia zinazosababishwa na magenge ya wahuni. Hilo ni moja ya mapendekezo kutoka kwa mtaalamu huru wa haki za binadamu kuhusu watu waliokimbia makazi yao, Cecilia Jimenez-Damary baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tano nchini humo. Amesema hali inayokabili [...]

21/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wajipanga kuwasaidia maelfu wanaokimbia Telafar Iraq

Kusikiliza / Watoto hawa ni baadhi ya maelfu ya raia wanaokimbia kutoka Telafar. Picha: Iraqi Red Crescent/UNOCHA

Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu nchini Iraq wanajiandaa kwa ajili ya kuwasaidia maelfu ya raia watakaokimbia kutoka Telafar wakati jeshi la serikali likipambana kuukomboa mji huo ulioko Kaskazini mwa Iraq kutoka kwenye udhibiti wa kundi la kigaidi la ISIL au Daesh. Operesheni hiyo ya ukombozi ilianza Jumapili na hadi sasa [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa UNDP umewapa ujasiri sambamba na kuwawezesha wanawake wa Kimasaai

Kusikiliza / Wamama katika mradi wa kujikwamua wanawake kiuchumi. Picha: UNDP/Kenya_Video capture

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Kenya kwa ushirikiano na serikali ya nchi hiyo wameanzisha mradi kwa ajili ya kuwezesha jamii zinazoishi kusini magharibi mwa Kenya karibu na mbuga ya wanyama ya Amboseli. Miradi hiyo inayolenga jamii za watu wa asili hususan Wamasaai inanuia kuwawezesha wanawake sio tu kiuchumi lakini [...]

21/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yatangaza jopo la wataalam kwa mustakbali bora wa ajira

Kusikiliza / Guy Ryder Akizungumza katika tukio la uzinduzi wa jopo hilo mjini Geneva Uswisi mkurugenzi mkuu wa ILO. Picha: ILO/Marcel Crozet

Shirika la kazi ulimwenguni ILO, limetangaza leo kuanzishwa kwa tume ya ngazi ya juu ya kimataifa ya wataalamu 20 ambayo itaangalia taasisi, usimamizi na sheria zinazohitajika ili kuhakikisha ajira zinakidhi viwango vya kisheria ikiwa ni juhudi za ILO katika mikakati ya mustakabali wa kazi zilizoasisiwa na shirika hilo mwaka 2013. Akizungumza katika tukio la uzinduzi [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani angazieni pia elimu Pembe ya Afrika

Kusikiliza / Wanafunzi darasani. Picha: UNICEF

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yametoa wito kwa wahisani kufadhili kwa kina mahitaji ya elimu kwa nchi zenye mahitaji ya kibinadamu katika pembe ya Afrika. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la watoto UNICEF wamesema katika taarifa yao kuwa elimu ikienda [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uingereza yaendelea kuwasaidia wasiojiweza Sudan-WFP

Kusikiliza / Wakimbizi walioko nchini Sudan wapokea mgao wa chakula kutoka kwa WFP.(Picha:WFP)

Serikali ya Uingereza imetoa paundi milioni 4.5 sawa na dola milioni 5.8 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ili litoe msaada muhimu wa chakula kwa karibu wakimbizi wa ndani 370,000 kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan. Fedha hizo ambazo zitatosheleza kwa miezi miwli zitaruhusu WFP kuwasaidia watu hao kupitia [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu Burundi hazina dalili ya kuimarika:UM

Kusikiliza / Raia nchini Burundi. Picha UM

Wataalamu wa kimataifa wanaochunguza haki za binadamu Burundi wamesema hawajaona dalili zozote nzuri za kuimarika kwa hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika miezi ya karibuni nchini humo. John Kibego na ripoti kamili. (Taarifa ya Kibego) Hayo yamo kwenye ripoti mpya ya tume ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa iliyopewa [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kudhibiti kuenea kwa magonjwa Sierra Leone ni muhimu- WHO

Kusikiliza / UNFPA-Sierra Leone

Shirika la afya ulimwenguni, WHO linashirikiana kwa karibu na serikali ya Sierra Leone ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile Malaria na Kipindupindu kufuatia maporomoko ya udongo na mafuriko  nchini humo wiki iliyopita. Harakati hizo zinaenda sanjari na kuhakikisha huduma za afya kwa majeruhi na waliopoteza makazi zinapatikana, halikadhalika usaidizi wa kisaiokolojia na [...]

21/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSCA yachukua hatua kudhibiti ghasia mpya Bria, CAR

Askari wa MINUSCA na wa taifa CAR wakipiga doria.(Picha:UN/Nektarios Markogiannis)

Kufuatia kuibuka kwa ghasia mpya kwenye mji wa Bria ulioko kilometa 450 kaskazini mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui, Umoja wa Mataifa umeanza kuchukua hatua ili kudhibiti hali hiyo. Ujumbe wa umoja huo nchini CAR, MINUSCA  umesema ghasia hizo ni kati ya watu wanaodaiwa kuwa masalia ya wanaopinga Balaka na [...]

19/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani shambulio huko Finland

Launch of the Regional Flash Appeal Folowing recent events in Libyan Arab Jamahiriya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulizi la kigaidi lililotokea jana Ijumaa kwenye mji wa Turku nchini Finland. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa shambulio hilo lilitokea baada ya kijana mmoja kushambulia watu kwa kisu na kusababisha vifo vya watu 9 na wengine wamejeruhiwa. Kufuatia tukio hilo, Bwana Guterres kupitia kwa msemaji wake, [...]

19/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wasigeuzwe ngao au silaha kwenye mizozo

Kusikiliza / NOT A TARGET 1

Leo ni siku ya usaidizi wa kibinadamu duniani ambapo suala la msingi linalopatiwa kipaumbele ni usalama kwenye maeneo yenye vita, wakiangaziwa raia na wale wanaowapatia misaada. Umoja wa Mataifa unasema mamilioni ya watu hivi sasa wanaishi kwenye maeneo yenye mizozo, wakiwemo watoto, wanawake na wanaume. Taswira ya miji yao awali ikiwa na huduma za msingi [...]

19/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana na jukumu lao katika amani na maendeleo

Kusikiliza / Vijana makala

Nguvu kazi ya taifa, taifa la leo, taifa la kesho! Ni baadhi ya kauli ambazo hutumika ili kuchagiza kundi hilo ambalo linatagemewa kwa maendeleo kwani idadi yake kwa sasa nikubwa kabisa katika historia ya dunia. Takwimu kwa sasa zinaonyesha kuwa vijana ni zaidi ya bilioni 1.8. Kundi hili linakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo ukosefu wa [...]

18/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya amani ya Yemen bado iko njia panda:Ould Cheikh

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed akihutubia Baraza la usama kwa njia ya video. Picha: UM/Kim Haughton

Hatima ya amani ya Yemen bado iko njia panda huku machafuko yakiendelea kushuhudiwa katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo ikiwemo mji mkuu Sa'ana. Akiwasilisha tarifa ya tathimini ya mchakato wa amani ya Yemen kwenye baraza la usalama hii leo mjini New York Marekani, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed [...]

18/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muziki waleta nuru kwa wakimbizi wa Syria nchini Ugiriki

Kusikiliza / Mwanamuziki mkimbizi kutoka Syria aliyeko Ugiriki ambaye anatumia ujuzi wake kuwafundisha watoto. Picha: UNHCR/Video capture

Vita nchini Syria vimeingia mwaka wa 7 na mamia ya maelfu ya raia wamekimbia nchi hiyo kwani si shwari tena. Maisha ambayo wananchi walikuwa wamezoa yametumbukia nyongo. Hata hivyo hata kule walipo wanatafuta mbinu ya kuweza kuishi na kutumia stadi zao ili kukabiliana na machungu. Miongoni mwao ni mkimbizi kutoka Syria aliyeko Ugiriki ambaye anatumia [...]

18/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunashikamana na Hispania kufuatia shambulio la Barcelona:UM

Kusikiliza / Tunashikamana na Hispania kufuatia shambulio la Barcelona:UM: UM

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio la kigaidi mjini Barcelona Hispania lililokatili maisha ya watu 13 na kujeruhi wengine zaidi ya 100. Shambulio hilo lilitokea Alhamisi kwenye wilaya ya Las Ramblas iliyo maarufu kwa watalii katikati ya mji wa Barcelona. Baraza limetoa tarifa ya kusisitiza kwamba vitendo vyovyote vya kigaidi ni [...]

18/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Sogi

Kusikiliza / Neno la wiki: Sogi

Wiki hii tunaangazia neno "Sogi" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema Sogi ni mifuko miwili anayebebeshwa punda, moja kila upande ambayo hutumiwa kubeba mizigo ndani yake.

18/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watoto 35,000 wapata chanjo ya polio Syria:UNICEF/WHO

Kusikiliza / UNICEF, WHO kwa kushirikiana na wadau wengine kuwapa watoto chanjo ili  kukabiliana na mlipuko wa karibuni wa polio nchini Syria. Picha: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO kwa kushirikiana na wadau wengine wamekamilisha duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo kukabiliana na mlipuko wa karibuni wa polio nchini Syria. Mashirika hayo yanasema kampeni hiyo imetoa kinga madhubuti dhidi ya polio kwa watoto zaidi ya 355,000 walio chini [...]

18/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yawaenzi wahudumu wa misaada ya kiutu duniani

Kusikiliza / Wakimbizi wakipokea msaada kwa furaha. Picha: UM

Wakati dunia ikishikamana Jumamosi Agosti 19 kuadhimisha siku ya usaidizi wa kiutu duniani mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP anaenzi mchango wa wahudumu wa kibinadamu kote ulimwenguni wakiwemo wafanyakazi wa WFP. David Beasley amesema kila kona ya dunia wafanyakazi wa WFP wanafanya kazi usiku na mchana bila kuchoka [...]

18/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baadhi ya nchi zaitikia wito wa kusaidia Sierra Leone

Kusikiliza / Maporomoko nchini Sierra Leone. Picha:UNICEF

Leo ni siku ya tano tangu Sierra Leone ikumbwe na maporomoko ya udongo na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo ambapo bado usaidizi wa kimataifa unatakiwa ili kuendelea kusaka mamia ya watu ambao bado hawajulikani walipo na pia kusaidia walioathiriwa na janga hilo. Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 400 wamefariki dunia [...]

18/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa sheria za kimataifa unaathari kubwa:UN women

Kusikiliza / Tuna jugumu la kuhakikisha kwamba kila msichana duniani kote ameweza kuishi maisha ya mafanikio na ya kiutu. Picha: UN Women

Ukiukwaji wa sheria za kimataifa katika maeneo yenye mizozo umesababisha zahma kubwa ya ulinzi na uslama kimataifa. Katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya usaizidi wa kibinadamu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women limesema athari zake hazisemeki, mabomu na makombora yakisambaratisha shule, hospital, masoko na maeneo ya kuabudu. [...]

18/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia na wafanyakazi wa misaada walindwe- Guterres

Kusikiliza / OCHA-4

Wanawake ni miongoni mwa walengwa kwenye mizozo na hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anataka walindwe. (Picha:WHD Video capture) Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya utoaji wa huduma za kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa wakazi wote ulimwenguni kulinda raia na wafanyakazi wa kibinadamu walio kwenye maeneo [...]

18/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Grandi atolea wito jumuiya ya kimataifa kutambua ukarimu wa Sudan

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi .(Picha:UM/Evan Schneider)

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi, amefanya ziara yake ya kwanza nchini Sudan wiki hii wakati huu ambapo wakimbizi wanaendelea kukimbia mzozo nchini Sudan Kusini. Bwana Grandi amesifu ukarimu wa watu wa Sudan, mmoja ya nchi zinazowahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini, na kuwa mwenyeji wa wakimbizi wengine [...]

17/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Al Mahdi kulipa fidia ya zaidi ya dola milioni 3 kwa uharibifu Timbuktu

Kusikiliza / 09-26-2015Mali_Timbuktu2

Hii leo mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Uholanzi imemtaka Ahmad Al Faqi Al Mahdi anayetumikia kifungo cha miaka 9 kwa makosa ya uhalifu wa kivita huko Timbuktu, Mali alipe fidia ya zaidi ya dola milioni 3. Mahakama hiyo imesema fidia hiyo ni kwa ajili ya watu na jamii ya Timbuktu kufuatia [...]

17/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usaidizi wa kibinadamu ni muhimu sana hasa kwa wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya. Picha: UM/Video capture

Wahenga walinena siri ya mtungi aijuaye kata, hawakukosea kwani madhila ya mtu anayejua ni amsaidiaye. Na hili limethibitishwa na Bi Khadija Hussein, afisa wa masuala ya ulinzi wa wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya. Baada ya kuhudumu hapo kwa miaka mingi. Leo Bi khadija amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii kwamba sasa anatambua ni [...]

17/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto zaidi ya 100 wapoteza Maisha kwenye maporomoko ya udongo Sierra Leon- UNICEF

Kusikiliza / Juhudi za kunasua miili nchini Sierra Leone.(Picha:UNICEF/Twitter)

Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ipo nchini Sierra leon ili kutoa msaada wa dharura kwa familia zilizoathirika na maporomoko ya udongo na mafuriko mjini Freetown . Grace Kaneiya na tarifa zaidi (TAARIFA YA GRACE) Shirika hilo linasema mamia ya watu wamepoteza maisha wakiwemo watoto 109 na idadi inatarajiwa kuongezeka [...]

17/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa Kipindupindu Yemen wahatarisha zaidi wajawazito

Kusikiliza / Mtoto muathirika wa kipindupindu anapatiwa matibabu katika kituo cha afya nchini Yemen. Picha: UNICEF

Nchini Yemen, kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu ni kubwa huku ikiripotiwa visa vipya 5000 kila siku. Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA linasema zaidi ya wajawazito milioni moja wako hatarini zaidi na wanahitaji huduma ya dharura. Miongoni mwao ni Ibsam ambaye anasema aliambukizwa Kipindupindu akiwa na ujauzito wa miezi [...]

17/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR na Tanzania wabainisha hatua za kukabili suala la wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Burundi walioko nchini Tanzania. Picha: © UNHCR/K. Holt

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na serikali ya Tanzania watafanyia tathmini sera ya taifa hilo kuhusu wakimbizi ili kuhakikisha inakidhi hali ya sasa ya ukimbizi. Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa kikao kati ya pande mbili hizo, kikao cha hivi karibuni zaidi cha ngazi ya juu kilichofanyika jijini Dar es salaam kikiangazia [...]

17/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mchele uliorutubishwa unaweza kabili ukosefu wa damu- Tafiti

Mwanamke anakagua mpunga. Picha: FAO/Daniel Hayduk

Utafiti mpya umebaini kuwa ulaji wa mchele ulioongezewa virutubisho unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa ukosefu wa damu na uhaba wa madini ya Zinki mwilini. Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema utafiti huo ulihusisha wanawake maskini zaidi huko Bangladesh ambao walipatiwa mchele huo kupitia mpango wa maendeleo wa serikali kwa watu walio hatarini zaidi, [...]

17/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Sudan Kusini walioingia Uganda sasa ni milioni 1:UNHCR

Kusikiliza / Tabu na mamake wa kambo(kati) na dadake pacha (kulia) wanakusanya misaada ya chakula cha familia. Picha: © UNHCR/Peter Caton

Idadi ya wakimbizi wa Sudan kusini waliokimbilia nchini Uganda sasa imefika milioni moja. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo leo limerejea kutoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa la msaada wa haraka ili kusaidia hali ya wakimbizi hao wa sudan Kusini na serikali ya Uganda inayowahifadhi. Flora [...]

17/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Najivunia kuwa polisi mwanamke nchini Sudan Kusini- Bi. Cynthia

Kusikiliza / Afisa wa Polisi wa UNPOL. Picha:UNMISS/Daniel Dickinson

Kuelekea siku ya utu wa kibinadamu duniani tarehe 19 mwezi huu, imeelezwa kuwa uwepo wa polisi wanawake kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa huleta matumaini miongoni mwa makundi yanayokumbwa na mizozo. Hiyo ni kwa mujibu wa Cynthia Anderson kutoka Ghana polisi anayehudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini [...]

17/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Azimio 2371 ni ujumbe dhahiri kwa DPRK kuwajibika kwa amani na usalama:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa New York Marekani. Picha:UM/Mark Garten

Kuna zahama nyingi hivi sasa duniani kote, hasa mvutano kuhusiana na rasi ya Korea ambao haujashuhudia katika kiwango hicho kwa miongo. Hayo yamesema leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alipozungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa New York Marekani. Amesema historia inakumbusha machungu ya miaka zaidi ya [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana kushirikiana katika kufanikisha SDGs: Tanzania

Kusikiliza / Vijana wa kike katika biashara ya ushirika ya kushona nguo nchini Tanzania. Picha: UN Women/Video capture

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo vijana kuwa bega kwa bega katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lile la kwanza la kutokomeza umaskini bila kusahau usawa wa kijinsia. Na ni kwa mantiki hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UNWomen nchini Tanzania mwaka 2015 lilizindua programu ya maendeleo endelevu kupitia [...]

16/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uharibifu wa silaha umekamilika katika kambi za FARC-Arnault

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia, Jean Arnault. Picha: UM/Colombia

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia, Jean Arnault amesema amefurahishwa na operesheni za kusalimisha silaha nchini humo. Katika taarifa yake ya Agosti 15, bwana Arnault amesema mchakato wa kuondoa silaha zote na risasi katika kambi 26 za kikundi cha FARC umekamilika. Ameongeza kwamba kando na operesheni ambayo inaendeshwa eneo Pondores [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM waonya kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi Marekani

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa Bwana Mutuma Ruteere. UN Photo/Evan Schneider

Visa vya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni vimeshamiri Marekani, kwa mujibu wa ripoti ya wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Onyo hilo limetolewa wakati huu ambapo maandamano na vurugu zimetanda katika mji wa Charlottesville jimbo la Virginia nchini marekani na mtu mmoja kupoteza maisha. Kwa mujibu wa wataalam hao, [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sierra Leone waomboleza kwa siku saba kufuatia maporomoko

Kusikiliza / Mamia ya watu wahofiwa kupoteza maisha baada ya maporomoko  ya ardhi nchini Sierra Leone. Picha: UNICEF

Nchini Sierra Leone, wananchi wakiendelea na maombolezo ya kitaifa kufuatia janga la maporomoko ya udongo na mafuriko siku ya Jumatatu, Umoja wa Mataifa unaendelea na harakati zake za uokozi na kuepusha mlipuko wa magonjwa. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Regent, mji ulioko milimani, takribani kilometa 16 kutoka mji mkuu wa Sierra Leone, [...]

16/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ILO kutangaza jopo la mustakabali wa ajira

Kusikiliza / Picha:ILO

Shirika la kazi ulimwenguni ILO, linatarajia kuanzisha tume ya ngazi ya juu ya kimataifa, tume itakayojumuisha wataalamu 20 ambao pamoja na mambo mengine wataangalia namna mabadiliko ya kazi yanavyoweza kukidhi viwango vya sheria. Katika taarifa yake hii leo, ILO imesema majina ya wanachama wa tume hiyo maaluma kwa ajili ya mustakabali wa kazi, yatatangazwa mnamo [...]

16/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yaanza kugawa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa ndani DRC

Kusikiliza / WFP wagawa msaada Kasai, DRC. Picha: WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na washirika wake World Vision wamezindua operesheni ya dharura leo ya kugawa chakula kwa wakimbizi wa ndani 42,000 kwenye majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Kwa mujibu wa WFP katika maeneo yanayofikika wanapanga kuwasaidia watu 25,000 Kasai ya Kati na [...]

16/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afya ya wahamiaji Libya yaangaziwa

Kusikiliza / Mkutano uliofanyika Tunis, Tunisiawa wa kujadili afya ya wahamiaji nchini Libya. Picha: IOM

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Libya ili kukabili changamoto za utoaji huduma za afya kwa wahamiaji. Mkuu wa IOM nchini humo Othman Belbeisi, amesema hayo katika mkutano uliofanyika Tunis, Tunisia wakati huu ambapo wahamiaji wapatao milioni moja nchini Libya hawana huduma za uhakika za afya. Amesema [...]

16/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dunia yashikamana kukabili sumu ya zebaki kupitia mkataba wa Minamata

Kusikiliza / mercury

Mkataba wa kwanza duniani wa kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya sumu ya zebaki umeanza kutekelezwa rasmi leo . Amina Hassan na taarifa zaidi (TAARIFA YA AMINA) Mkataba wa Minamata uliopigiwa upatu kwa karibu muongo mmoja, Mei 18 mwaka huu ulipata sahihi ya 50 iliyohitajika ili uanze kutekelezwa. Mkataba huo unaziwajibisha pande 74 [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterress alaani mfululizo wa mashambulizi Nigeria

Kusikiliza / Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Manuel Elias

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika Agosti 15 katika jimbo la Borno nchini Nigeria. Kupitia msemaji wake, ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Nigeria kufuatia vifo na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi. Katibu Mkuu pia ametoa wito waliotekeleza uhalifu huo nchini Nigeria na nchi jirani [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuna deni na kizazi kijacho kutoa msaada wa kibinadamu leo:O'Brien

Kusikiliza / Wakimbizi wahitaji misaada Syria. Picha: UNHCR

Kutoa usaidizi wa kibinadamu unaohitajika leo hii , ni uwekezaji wenye amana kubwa katika kizazi kijacho. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa operesheni za misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien katika kuelekea siku ya usaidizi wa kiutu duniani itakayoadhimishwa Agosti 19. Mwaka huu siku hiyo inajikita katika mashambulizi dhidi ya raia na [...]

16/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna ongezeko kubwa la machafuko CAR:UNICEF

Kusikiliza / 6-5-17car

Mwaka uliopita na hususani robo ya mwisho ya mwaka huo imeshuhudia ongezeko kubwa la machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Donaig Le Du msemaji wa shirika hilo akizungumza leo mjini Geneva Uswis amesema CAR ni moja ya nchi ambazo ni mbaya [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya tatu

Kusikiliza / Lilongwe, Malawi.

Wiki ya unyonyeshaji duniani imehitimishwa juma hili, kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto ili kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora.  Katika sehemu ya tatu ya makala hii Amina Hassan anaendelea kuzungumza na Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja wa [...]

15/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mipango ya kikosi cha G5 ilandane na mchakato wa amani Mali- Wane

Kusikiliza / 16447005773_1eb4c1e33b_z2

Kadri hali ya usalama inavyozidi kuzorota kwenye mipaka ya nchi zilizo ukanda wa Sahel, Afrika Magharibi, ndivyo umuhimu wa kikosi cha pamoja cha nchi tano kwenye ukanda huo kinavyozidi kupata umuhimu. Hiyo ni kwa mujibu wa Naibu Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa El-Ghassim Wane wakati akipatia Baraza la Usalama [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya iko katika wakati muhimu, viongozi wawajibike-Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu  Zeid Ra'ad Al Hussein. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amepongeza wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi mkuu kwa njia ya amani huku akihimiza viongozi wa kisiasa kuwajibika na kuonyesha uongozi imara ili kuzuia machafuko zaidi. Zeid ameelezea wasiwasi wake kuhusu ripoti za vyombo vya usalama kutumia risasi za moto dhidi [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Manusura na maiti zaidi wapatikana pwani ya Yemen:IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Katika siku tatu zilizopita wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM wamewapata manusura lakini pia maiti zaidi kufuatia zahma ya boti wiki iliyopita. Tarehe 9 na 10 Agosti jumla ya wahamiaji 280 walikuwa wakielekea nchi za Ghuba walipotoswa baharini kutoka kwenye boti mbili Pwani ya Yemen jimbo la Shabwa na wasafirishaji haramu [...]

15/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maporomoko ya udongo Sierra Leone, juhudi za uokozi zaendelea

Kusikiliza / Juhudi za kunasua miili nchini Sierra Leone.(Picha:UNICEF/Twitter)

Nchini Sierra Leone, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana na serikali kupeleka huduma za uokoaji kwenye maeneo yaliyokumbwa na maporomoko ya udongo na mafuriko mapema jana Jumatatu. Zahma hiyo imekumba mji wa Regent na mji mkuu Freetown ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema wanahaha kunasua [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imeanza kuwahamisha wakimbizi wa DRC mpakani na Angola

Kusikiliza / Familia zilizokimbia machafuko jimbo la Kasai DRC zawasili katika kituo cha hifadhi cha Lóvua, Angola. (Picha:UNHCR/Rui Padilha)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake wameanza zoezi la kuwahamisha zaidi ya wakimbizi 33,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kutoka kwenye vituo vya mapokezi vilivyofurika Kaskazini mwa Angola na kuwapeleka kwenye kambi mpya iliyofunguliwa ya Lóvua . Takribani wakimbizi 1,500 wameshahamishwa kutoka kituo cha mapokezi cha Mussunge [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwepo wa UM jimboni Darfur umebadili maisha yetu- mkazi Darfur

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unatoa huduma mbali mbali za misaada jimboni Darfur, Sudan.(Picha:UNAMID Selemani Semenyu)

Wakati siku ya utu wa kibinadamu ikiadhimishwa tarehe 19 mwezi huu, wakazi jimboni Darfur nchini Sudan wameupongeza Umoja wa Mataifa kwa huduma wanazozipata kupitia Umoja huo.Taarifa kamili na Luteni Selemani Semunyu wa radio ya Umoja wa Mataida Darfur UNAMID (TAARIFA YA SELEMANI) Hii ni kufuatia ujio wa wawakilishi kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo [...]

15/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wazungumuzia msaada wa kibinadamu, Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi

Uganda ni moja ya nchi ambayo inahifadhi wakimbizi wengi barani Afrika na inasifika kwa namna serikali inawajumuisha wakimbizi na kuwapa ardhi kama moja ya mbinu ya kuwawezesha kujitegemea. Kando na hayo inatoa huduma muhimu kwa mfano elimu na huduma nyinginezo. Je ni vipi wakimbizi wanapokea ukarimu kutoka kwa serikali na jamii nchini Uganda? Ungana na [...]

14/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres astushwa na vifo vya maporomoko ya udogo na mafuriko Sierra Leone:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa kwenye kikao cha baraza la usalama. Picha na UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na vifo na athari zilizosababishwa na maporomoko ya udongo na mafuriko kwenye miji ya Regent na mji mkuu Freetown nchini Sierra Leone. Kupitia tarifa ya msemaji wake Guterres, ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Sierra Leone kufuatia vifo hivyo na uharibifu uliosababishwa [...]

14/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani wa UM na askari wa Mali wauawa katika shambulio

Kusikiliza / Mlinda amani nchini Mali.(Picha:UNIfeed/video capture)

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema leo asubuhi kumefanyiska shambuliop katika kambi mbili za Douentza jimbo la Mopti Kaskazini mwa Mali na kusababisha vifo na Majeruhi. Na mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo MINUSMA umelaani vikali shambulio hilo. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini New York Marekani Farhan Haq amesema.. (SAUTI YAFARHAN HAQ [...]

14/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani shambulio la kigaidi Burkina Faso

Kusikiliza / Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Manuel Elias

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulio la kigaidi lililotokea Jumapili kwenye mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou na kusababisha vifo vya watu 17. Kupitia Naibu msemaji wake, Farhan Haq, ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Burkina Faso huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi. Na zaidi ya hapo msemaji [...]

14/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Somalia yasherehekea miaka 3 bila polio, WHO yatoa tahadhari

Kusikiliza / Mtoa hudumu wa afya nchini Somalia.(Picha:UM/David Mutua)

Mjini Mogadishu kumefanyika tukio maaluma la kusherehekea miaka mitatu tangu kisa cha polio kugundulika nchini Somalia. Akizungumza katika tukio hilo lilohudhuriwa na wawakilishi kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Shirika la afya ulimwenguni, WHO na wizara ya afya ya Somalia, mkurugenzi wa kanda ya Mashariki mwa Mediterenea, WHO Dr Mahmoud [...]

14/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tulindeni ili tuweze kutoa huduma za kiutu #NotaTarget – Hussein

Kusikiliza / Gateway-Daadab2

Kuelekea siku ya utu wa kibinadamu tarehe 19 mwezi huu, wakimbizi ambao wanatumika kutoa huduma za kijamii kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya wamesema ukosefu wa usalama unakwamisha huduma zao. Hussein Issack mkimbizi kutoka Somalia ambaye hivi sasa ni mwalimu mkuu wa shule ya Gateway kambini hapo amesema wana uhaba wa vifaa vya kufundishia na [...]

14/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 7.7 wahitaji msaada wa haraka DRC: FAO/WFP

Kusikiliza / Picha:FAO

Wakati machafuko na watu kutawanywa kukiendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , watu milioni 7.7 wanakabiliwa na njaa kubwa yameonya mashirika ya Umoja wa Mataifa, la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP. Flora Nducha na taarifa kamili (FLORA TAARIFA) Katika ripoti yao mpya iliyotolewa leo mashirika hayo yanasema [...]

14/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Visa vya kipindupindu yemen vyafika 500,000:WHO

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wakipea matibabu watoto waaathirika wa ugonjwa wa kipindupindu.  Picha: UNHCR/John Wessels

Idadi ya visa vinavyoshukiwa kuwa ni kipindupindu nchini Yemen mwaka huu vimegonga nusu milioni, na watu takribani 2000 wamepoteza maisha tangu kuanza kusambaa wa ugonjkwa huo mwishoni mwa mwezi April. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO kwa ujumla visa vimepungua nchi nzima tangu mapema Julai hususani katika maeneo yaliyoathirika zaidi , lakini visa [...]

14/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mastercard na MediaCom zapiga chepuo harakati za WFP dhidi ya njaa

Kusikiliza / Sudan Kusini2

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limezindua kampeni iitwayo Kabiliana na Njaa kwa lengo la kuangazia mataifa manne yanayokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Taarifa ya WFP imesema uzinduzi huo uliofanyika Hispania, umetaja nchi hizo kuwa ni Sudan Kusini, Somalia, Nigeria na Yemen zikijumuisha zaidi ya watu milioni 20 walio hatarini kufariki dunia kutokana [...]

14/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi Kenya tumeni ujumbe wa wazi kwa wafuasi kuepusha vurugu- Guterres

Kusikiliza / Mkuu wa IEBC akitangaza matokeo ya urais nchini Kenya.(Picha:UNIC/Nairobi/Twitter)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amepongeza watu wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake, Guterres amesikia matokeo na hatimaye  Uhuru Kenyatta kutangazwa na Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwa rais mteule. Hata hivyo Bwana Guterres ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa wanaopinga matokeo [...]

12/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nitapaza sauti za vijana- Jayathma

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu maswala ya vijana, Jayathma Wickramanayake.(Picha:UNAMI/Sanaa Kareem)

  Umoja wa Mataifa uko pamoja nanyi na mimi mjumbe wenu, nitafanya kila niwezalo kuhakikisha sauti zenu zinasikika. Huo ni ujumbe wa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maswala ya vijana, Jayathma Wickramanayake akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya vijana duniani leo Agosti 12 iliyofanyika nchini Iraq. Kauli  mbiu ya [...]

12/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutawajumuisha vijana kwa maslahi yao:Guterres

Kusikiliza / Youth 5

Wakati siku ya kimataifa ya vijana ikiwadhimishwa kote dunia Agosti 12, Umoja wa Mataifa umesema umejizatiti kuliwezesha kundi hilo na kulijumuisha kote duniani. Katika ujumbe wake wa video kuhusu siku hiyo, Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia amamteua mwakilishi maalamu mpya wa vijana Jayathma Wickramanayake ambaye ni mjumbe [...]

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjadala kuhusu umuhimu wa unyonyeshaji watoto Burundi

Kusikiliza / Picha: UN Photo/B. Wolff

Ulimwengu  umehitimisha wiki ya kunyonyesha juma hili, wataalamu wa shirika la afya ulimwenguni  (WHO) wakichagiza kuwa faida za kunyonyesha sio tu kwa watoto lakini kwa jamii nzima hasa katika swala nzima la uzazi wa mpango. Ingawa kinamama wazazi wengi wanachangamkia utaratibu huu wa kunyonyesha watoto, baadhi ya wanawake wamejenga hoja nyingi za kutonyonyesha watoto. Burundi [...]

11/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sikuchagua muziki bali muziki ulinichagua mimi- mwanamuziki Jermain

Kusikiliza / James Germain.

Ni nadra sana kumuona mtu mwenye ulemavu wa ngozi yaani albino nchini Haiti, kwa kawaida kundi hili linakejeliwa sana. Hiyo ni kauli ya James Germain ambaye ni mwanamuziki mwenye ulemavu wa ngozi kutoka Haiti, anaesema kama mwanamuziki anatumia fursa hiyo kubadili mtazamo potofu wa jamii dhidi ya kundi la watu hao. Aidha anajikita katika kuchagiza [...]

11/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Yazidi kuwa tete Gaza mgao wa umeme ukiendelea:UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Yazuidi Iraq: Picha na UNICEF/Razan Rashid

Maelfu ya watu Gaza wako katika hali tete wakati huu mgao wa umeme ukiendelea na hali ya maisha kuzidi kuwa mbaya. Hii ni kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ambayo imeitaka Israel, mamlaka ya Palestina na Gaza kuzingatia haki za binadamu za watu katika eneo hilo. Msemaji wa ofisi [...]

11/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WaSyria 600,000 warejea nyumbani miezi 7 ya mwanzo 2017:IOM

Kusikiliza / Wakimbizi nchini Syria wanapokea msaada. Picha: UNHCR/Bassam Diab

Kati ya Januari za Julai mwaka huu , Wasyria zaidi ya laki sita waliotawanywa na machafuko wamerejea nyumbani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na wadau wengine. Takwimu zinaonyesha kwamba wengi wa watu wanaorejea takribani asilimi 84 walikuwa ni wakimbizi wa ndani Syria, huku asilimia 16 wanarejea kutoka Uturuki , [...]

11/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki – “Bakora” na “Mjeledi”

Kusikiliza / NenoLaWikiBakora

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Bakora" na "mjeledi" Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wajumuishwe kuleta maendeleo: Jayathma

Kusikiliza / Jayathma Wickramanayake kutoka Sri Lanka,mteule mpya wa kubeba bendera ya vijana kwenye Umoja wa Mataifa.(Picha:UM/Ofisi ya Katibu Mkuu)

Wakati siku ya kimataifa ya vijana ikiadhimishwa kote duniani Agosti 12, hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, leo vijana kutoka pembe mbalimbali za dunia wamejadili umuhimu wa kukabiliana na umaiskini na ujumishwaji pamoja mazingira. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Vijana hao wanaowakilisha kundi hilo linalokadiriwa kuwa [...]

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP yakaribisha mchango wa dola milioni 8 wa kusaidia wa Sudan Kusini

Kusikiliza / Wakimbizi waliokimbia machafuko na kuwasili Aburoc nchini Sudan Kusini.(Picha:OCHA/Gemma Connell)

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 8 kutoka kwa serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kuwasaidia watu nchini Sudan Kusini. Mchango huo utawezesha WFP kusaidia watu 180,000 kupitia msaada wa chakula na fedha taslimu. Takriban watu milioni 6 ambao ni nusu ya idadi ya watu nchini Sudan Kusini wanakabiliwa [...]

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa Amua wahitimisha awamu ya kwanza: UNFPA Tanzania

Kusikiliza / Picha:UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania limekamilisha ukusanyaji wa mawazo bunifu kutoka kwa vijana yahusuyo afya ya uzazi kupitia mradi uitwao Amua ambao umedumu kwa miezi sita. Mradi huo umehitimisha awamu ya kwanza ya uibuaji wa mawazo ambapo baada ya kupokea mawazo zaidi ya 300, mawazo ya makundi manne [...]

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafugaji walioghubikwa na ukame Ethiopia wahitaji msaada:FAO

Kusikiliza / Picha:FAO

Kusaidia wafugaji kurejea katika Maisha ya kawaida na kuzuia kupoteza zaidi mifugo yao ni muhimu sana nchini Ethipia kulikoghubikwa na ukame na njaa imekuwa ikiongezeka mwaka huu, limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO. Ukame nchini Ethiopia umewaathiri vibaya wafugaji na Maisha yao, wakikosa malisho na maji na kusababisha idadi [...]

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji kutoka Afrika Magharibi wakabiliwa na madhila makubwa:IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wanalala katika chumba kimoja kizuizini huko Tripoli's Tariq al-Sikka. Picha: UNHCR/Iason Foounten

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM leo imetoa ripoti mpya inayoainisha madhila yanayowakabili wahamiaji kutoka nchi za Afrika ya Magharibi wanaojaribu kwenda kusaka Maisha bora ughaibuni. Ripoti hiyo iliyoandaliwa na ofisi ya IOM Niger imefadhiliwa na Muungano wa Ulaya na inatokana na maelezo ya hiyari ya wahamiaji 6000 waliosaidiwa na IOM katika vituo [...]

11/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya pili

Kusikiliza / Picha: UNICEF/NYHQ2013-1031/Marinovich

Wiki ya unyonyeshaji duniani imehitimishwa juma hili, kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto ili kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora.  Katika sehemu ya pili ya makala hii Amina Hassan anaendelea kuzungumza na Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja wa [...]

10/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Stahamala muhimu kuhakikisha ulinzi kwa wakimbizi: Shearer

Kusikiliza / Raia nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Stahamala ni mbinu bora ya kuwalinda raia katika kwa kambi za wakimbizi dhidi ya uvamizi wa kijeshi, nchini Sudan Kusini, amesema mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, David Shearer. Kiongozi huyo alikuwa akizungumza mjini Bentiu, Kaskazini mwa Sudan Kusini, ambapo raia zaidi ya 115,000 wanaishi katika kituo cha ulinzi wa raia [...]

10/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya-UM

Kusikiliza / Dujarric2

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya, wakati huu ambapo matokea ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 yanatarajiwa kutangazwa. Akizungumza na waaandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, Marekani, msemaji wa katibu mkuu Stéphane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa haukuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi lakini.. (Sauti [...]

10/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chagizeni amani kwa kuchagiza uwezeshaji wa wanawake:Amina

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu mteule wa UM Bi. Amina J. Mohammed. (Picha:UM)

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa taarifa kwa baraza la usalama kuhusu ziara yake ya kwanza na ya aina yake aliyoifanya barani Afrika. Katika kikao cha baraza hilo lkilichokuwa kikijadili masuala ya amani na usalama Afrika, bi Amina Mohammed amesema aliambatana na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nigeria yasaidia watu wake kupitia WFP

Kusikiliza / Picha:WFP_Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limekaribisha msaada wa tani 5000 za mchele kutoka kwa serikali ya Nigeria. Shirika hilo linasema mchele huo utasaidia kulisha karibu watu nusu milioni wakimbizi wa ndani katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ililoghubikwa na machafuko na ambako tishio la baa la njaa [...]

10/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wengine 160 watoswa baharini leo Yemen:IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Wahamiaji wengi takribani 180 wametoswa baharini leo kwenye pwani ya Yemen na wasafirishaji haramu wa binadamu. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA YA AMINA) Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM maiti 6 wamepatikana huku wahamiaji wengine 13 hawajulikani walipo na 20 wakihofiwa kufa maji. Tukio hili limefanyika siku moja tu [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji katika huduma za afya wahitajika kunusuru watoto Iraq

Mwanamke mkimbizi akimbeba mwanae kusini mwa Mosul. Picha:UNICEF/USA

Miongo ya vita na uwekezaji duni vimeweka shinikizo kubwa kwenye mfumo wa afya nchini Iraq. Hali hiyo imewafanya wanawake wajawazito na watoto kulipa gharama kubwa ya maisha yao limesema shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, la afya WHO na la kuhudumia watoto UNICEF. Mashirika hayo yanasema ingawa kuna hatua zilizopigwa [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto zaidi ya 500,000 wanahitaji msaada Libya:UNICEF

Kusikiliza / Watoto katika shule ya tenti katika kambi ya muda ya Shousha mpakani mwa Libya. Picha:UNICEF

Miaka sita tangu kuzuka kwa machafuko Libya watoto zaidi ya 550,000 wanahitaji msaada wa kibinafdamu kwa sababu ya kutokuwepo utulivu wa kisiasa, machafuko yanayoendelea , watu kutawanywa, na kuporomoka kwa uchumi. Shirika la Umoja wa Mataifa a kuhudumia watoto UNICEF limesema machafuko katika baadhi ya sehemu nchini Libya yamelazimisha familia kuzikimbia nyumba zao. Watoto zaidi [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadilliko ya tabianchi yameathiri uchumi wa Malawi-Benki ya dunia

Kusikiliza / Watoto nchini Malawi ambao walikuwa waaathirika wakubwa wa nja.(Picha:WFP/Enoch Kavindelea JR.)

Shirika la fedha duniani, IMF na benki ya dunia wanafanya kazi kwa pamoja ili kusaidia nchi ya Malawi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi yameathiri pakubwa uchumi wa Malawi katika kipindi cha miaka miwili baada ya mafuriko yaliyofuatiwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo. Kwa mujibu [...]

10/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzazi ni mdau muhimu kuzuia mimba utotoni

Kusikiliza / Picha:UNICEF

Mzazi ni mdau muhimu katika kuzuia mimba za utotoni nchini uganda na kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto za maisha hayo. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego leo amejikita katika changamoto hiyo ya mimba za utotoni na nini wajibu wa mzazi kuahikisha tatizo hilo linapunguzwa au kukomeshwa kabisa. Ungana naye katika makala hii kwa udani zaidi.

09/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 50 wazamishwa makusudi na wasafirishaji haramu

Kusikiliza / Picha:IOM

Mapema leo asubuhi msafirishaji haramu wa binadamu aliyekuwa anahodhi boti aliwalazimisha wahamiaji zaidi ya 120 kutoka Somalia na Ethiopia kujitosa baharini walipokaribia pwani ya Shabwa, Yemeni kwenye mwambao wa bahari ya Arabia. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mastaifa la uhamiaji IOM wahamiaji hao walikuwa wakitumai kwenda nchi za Ghuba kwa kupitia Yemen. Muda [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Alison Smale kuwa mkuu mpya wa mawasiliano ya kimataifa UM

Kusikiliza / Alison Smale , Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu Mawasiliano ya Kimataifa. Picha:YouTube/Hertie School of Governance(UN News Centre)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres amemteua Alison Smale wa Uingereza kuwa msaidizi wa Katibu mkuu kuhusu mawasiliano ya kimataifa , kwenye idara ya habari kwa umma ya Umoja wa Mataifa (DPI). Bi Smale anakuwa mrithi wa  Cristina Gallach wa Hispania ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa utendaji wake na huduma aliyoitoa kwa Umoja [...]

09/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yakaribisha mchango wa dola milioni 1 kwa ajili ya wakimbizi wa Sahrawi

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sahrawi kambini Smara, Algeria. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni moja kutoka Marekani kwa ajili ya kusaidia wakimbizi walioko hatarini katika Mashariki mwa jangwa la Sahara nchini Algeria. Kwa takriban miaka 40, wakimbizi wa mzozo wa muongo mmoja wa eneo lililoko katikati ya Morocco wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu Kusini Mashariki mwa Algeria. [...]

09/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rasilimali zaidi zahitajika kuzinisuru nchi na baa la njaa:

Kusikiliza / Wanawake na watoto wao nchini Somalia wamebanwa na uhaba wa chakula
Picha: UN video capture

Rasilimali zaidi zahitajika haraka ili kuwalinda watu milioni 20 walio katika hatari ya baa la njaa Yemen, Somalia, Sudan Kusini na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa baraza la usalama hii leo , ambayo pia imetaja madhila kwa mamilioni ya watu yatokanayo na machafuko yanayoendelea kote duniani [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC yaalani mauaji ya watoa huduma wa msalaba mwekundu CAR

Kusikiliza / Picha:UNDOF

Shirika la Kimataifa la Hilali Nyekundu na Msalaba Mwekundu, ICRC, limeelezea kusikitishwa na vifo vya kikatili vya wafanyakazi wa kujitolea wa msalaba mwekundu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR wiki hii. Kwa mujibu wa taarifa, wafanyakazi hao walikuwa kwenye mkutano wa dharura katika kituo cha afya cha Gambo, Mbomou Kusini mashariki mwa CAR mnamo [...]

09/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanasanyansi DRC wazuia mlipuko wa mafua ya avian kwa kutumia nyuklia

Kusikiliza / Matumizi ya nyuklia DRC katika kutokomeza ugonjwa wa Avian.Picha:IAEA

Wanasayansi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamebaini mlipuko mpya wa mafua ya ndege aina ya avian kwa kutumia teknolojia ya nyuklia . Na kwa kubaini haraka na mapema mlipuko wa virusi hivyo kumesaidia kuchukua hatua za haraka na sasa mlipuko huo umedhibitiwa na kusalia tu katika jimbo la ziwa albert karibu na mpaka [...]

09/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado watu wa asili hawashirikishwi katika maamuzi-Dkt. Laitaika

Kusikiliza / Eli

Hatua kubwa zilizopigwa katika kutambua uwepo wa watu wa asili na kwamba wanastahili kupewa haki zao, lakini bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji wa haki hizo zilizopo katika azimio la watu wa asili. Hayo yamesemwa na Dr Elifuraha Laitaika kutoka Tanzania ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu mwakilishi wa UM Somalia ajadili usalama na viongozi

Kusikiliza / Raisedon Zenenga, Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia. Picha:UNSOM

Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Raisedon Zenenga leo amekuwa na mazungumzo na uongozi wa jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia kujadili hatua zilizopigwa na serikali katika sekta ya usalama. Ziara ya bwana Zenenga pia ilijikita katika ujenzi unaoendelea kwa makao makuu ya jeshi la Taifa la Somalia kikosi cha 60 na chuo [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSMA yachunguza makaburi ya pamoja na ukiukwaji wa haki Kidal

Kusikiliza / Picha: MINUSMA

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, katika ripoti yake iliyotolewa juma hili umesema unachunguza makaburi ya pamoja yaliyopatikana na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu katika jimbo la Kidal Kaskazini mwa Mali ambako machafuko na mapigano baina ya makundi mawili yenye silaha yaliyotia saini mkataba wa amani yameongezeka hivi karibuni na kutishia kuvuruga [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto ni zaidi, miaka 10 tangu kupitishwa kwa azimio la haki za watu wa asili

Kusikiliza / Mariam Wallet Aboubakrine, ambaye ni Rais wa Kikao cha Kudumu cha Umoja wa Mataifa juu ya Masuala ya watu wa Asili, UNPFII. Picha:UN Photo/Rick Bajornas

Ingawa ulimwengu unaadhimisha miaka 10 hii leo tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kuhusu haki za watu wa asili, Umoja wa Mataifa umesema kuwa kundi hili bado linabaguliwa, linatengwa na linakosa ulinzi ambao umedhihirishwa na ongezeko kubwa la mauaji ya watetezi wa haki za kibinadamu za watu wa asili na ongezeko la ukiukwaji wa haki [...]

09/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Luteni jenerali Muriuki Ngondi kuongoza UNAMID:

Kusikiliza / Luten Jenerali Leonard Muiruki Ngondi. Kamanda mpya wa UNAMID. Picha na UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na mwenyekiti wa kamisheni ya muungano wa Afrika Moussa Faki Mahamat leo wametangaza uteuzi wa Luteni Jenerali Leonard Muriuki Ngondi wa kenya kuwa kamanda mkuu wa vikosi vya pamoja vya Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa kulinda amani Darfur, UNAMID . Ngondi anachukua nafasi ya Luteni [...]

08/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya Kwanza

Kusikiliza / Picha:UNICEF

Wiki ya unyonyeshaji duniani huadhimishwa na Umoja wa Mataifa kila mwaka kuanzia Agosti 1-7, ili kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora. Katika makala hii Amina Hassan amemhoji Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja [...]

08/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wadau Mauritania tatueni tofauti kwa njia ya amani:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres na msemaji wake Stephane Dujarric wakizungumza na waandishi wa habari. Picha na UM

Kufuatia kura ya maoni ya katiba iliyofanyika Agosti 5 mwaka huu katika Jamhuri ya Kiislam ya Mautitania, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewachagiza wadau wote kuhakikisha wanatatua tofauti zao kwa njia ya amani , kwa kuzingatia sheria na kuheshimu haki za uhuru wa kukusanyika na kujieleza. Kufuatia taarifa iliyotolewa na msemaji wake [...]

08/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa kipindupindu Sudan Kusini kuwa mbaya zaidi:IOM

Kusikiliza / Rais akipatiwa chanjo ya kipindupindu kambini Sudan Kusini. Picha na WHO

Mlipuko wa kipindupindu Sudan Kusini unatarajiwa kuwa mbya zaidi wakati msimu wa mvua ukiendelea limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Onyo hilo limekuja wakati kuna mgogoro mkubwa wa kibinadamu uliosababishwa na miaka ya vita na kutawanywa kuliko athari mamilioni ya watu. Zaidi ya visa 18,000 vya kipindupindu vimerekodiwa na karibu watu [...]

08/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zahma kwa waomba hifadhi Manus yaongezeka:UNHCR

Kusikiliza / Kituo kinachohifadhi waomba hifadhi Nauru. Picha na UNHCR

Wakimbizi na waomba hifadhi wanakabiliwa na hali mbaya na ongezeko la mgogoro katika kisiwa cha Manus, Papua New Guinea, ambako wanahifadhiwa katika kituo kinachomilikiwa na Australia. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) katika taarifa yake iliyotolewa leo ambayo inasema wakimbizi wanakabiliwa na msongo wa mawazo kabla ya [...]

08/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha kikanda Sudan Kusini ni fursa kwa UNMISS kushika majukumu mengine

Kusikiliza / Kikosi cha kikanda kilichowasili Sudan Kusini. Picha:UNMISS

Kuwasili kwa kikosi cha kikanda nchini Sudan kusini maana yake wanajeshi wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS ambao tayari wako juba wanaweza kupelekwa katika maeneo mengine nchini humo ili kulinda raia, kusaidia kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu, kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu haki za binadamu. Amina Hassan na taarifa zaidi (TAARIFA YA [...]

08/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wabaini ukiukwaji wa haki Venezuela

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva. Picha: UN Multimedia(UN News Centre)

Mahojiano 135 yaliyofanywa na timu ya haki za nbinadamu ya Umoja wa Mataifa yametoa taswira halisi ya kusambaa kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi na ukamataji kihiolela wa waandamanaji nchini Venezuela. Pia timu hiyo imebaini ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu ukiwemo msako wa kutumia nguvu kwenye nyumba za watu na utesaji wa watu walioko [...]

08/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yanusuru wahamiaji 1000 jangwa la Sahara:

Kusikiliza / Uokozi kwa wakimbizi kwenye pwani ya Italia.(Picha:IOM/Francesco Malavolta)

  Jumla ya wahamiaji 1000 wameokolewa tangu mwezi Aprili mwaka huu Kaskazini mwa Niger katika operesheni ya msako na uokozi inayofanywa na shirika la umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Tangu tarehe 19 hadi 25 Julai IOM imefanya tathimini ya safari za wahamiaji jangwa la Ténéré na eneo linalozunguka mpaka wa Niger na Libya, nia [...]

08/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha Rwanda cha kikanda chawasili Sudan Kusini

Kusikiliza / Raia nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Kundi la kwanza la wanajeshi wa Rwanda ambao ni sehemu ya kikosi cha ulinzi cha kikanda limewasili mjini Juba Sudan Kusini. Kwa mujibu wa msemaji wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS Daniel Dickinson wanajeshi 120 wa kikosi cha waenda kwa miguu wamewasili mwishoni mwa wiki. Wanajeshi hao wa Rwanda wanaungana na wenzao [...]

08/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa muhimu UM:

Kusikiliza / Kituo cha kutoa huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu nchini Yemen. Picha na WHO

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa na umuhimu mkubwa wakati huu wakikabiliwa na zahma kubwa ya kibinadamu. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York hii leo. Mwishoni mwa juma mashambulizi ya anga yaliarifiwa [...]

07/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanariadha wakimbizi nchini Kenya wajiandaa kung'aa Olimpiki London

Kusikiliza / Wanariadha wakimbizi. Picha:VideoCapture

Wachezaji wakimbizi nchini Kenya wamejiunga na wachezaji wengine chini ya Jumuiya ya Kimataifa ya shirikisho la riadha ili washiriki katika mazoezi na michuano. Wakimbizi hao kutoka nchi jirani ikiwemo Sudan Kusini na Somalia, wamewekwa katika timu ya wanariadha wakimbizi waliochaguliwa na mfuko wa Tekla Loroupe nchini Kenya. Tekla Loroupe ni mwanariadha mstaafu na anashikilia rekodi [...]

07/08/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi wa kesho Kenya uwe wa salama na haki:OHCHR

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Albert Gonzalez Farran

Wataalamu huru watatu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameisihi mamlaka nchini Kenya kuhakikisha hali ya utulivu na uchaguzi salama, pamoja na mchakato wa uchaguzi uliowazi na wa haki. Ili kutorejelea hali ya machafuko na ukatili wa mwaka 2007, wataalamu hao wametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwahimiza wadau wote katika uchaguzi [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia bado inasuasua na haki za watu wa asili miaka 10 baada ya azimio:

Kusikiliza / Moja ya makabila ya watu wa asili nchini Ethiopia Picha ya UN/Rick Bajornas

Watu wa asili duniani bado wanakabiliwa na changamoto kubwa muongo mmoja baada ya azimio la kihistoria kuhusu haki za watu wa asili kupitishwa na baraza kuu limeonya leo kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa. Wakizungumza kabla ya siku ya watu wa asili duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 9 , kundi hilo la wataalamu [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wawili wa Iraq

Kusikiliza / Waandishi wa habari.(Picha:UM/Casey Crafford)

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, leo amelaani vikali mauaji ya waandishi wawili wa habari nchini Iraq. Ripota Harb Hazaa al-Dulaimi na mpiga picha Soudad al-Douri, maiti zao zilikutwa katika kijiji cha Imam Gharbi Kusini mwa Mosul Julai 20 . Bi Bokova amesema vifo vyao [...]

07/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uchunguzi Syria lazima uendelee licha ya kujiuzulu del Ponte

Kusikiliza / Wanawake, wanaume na watoto wapoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya ISIL. Picha: UM

Juhudi za kimataifa za ukuorodhesha ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria ni lazima ziendelee baada ya kujiuzulu mmoja wa wajumbe wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi , wamesema leo wajumbe wawili waliosalia wa jopo hilo la uchunguzi. Katika taarifa yao mjumbe Paulo Pinheiro na Karen AbuZayd, wamemshukuru Carla Del Ponte kwa huduma yake [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna kinachoweza kuhalalisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto Kasai:UNICEF

Kusikiliza / Mkimbizi wa ndani Bernard akiwa mji wa Idiofa, jimbo la Kwilu na wanae.(Picha:UNHCR/John Wessels)

Dunia isifumbie macho hali mbaya ya watoto na familia katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC . John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA KIBEGO) Onyo hilo limetolewa na mkurugenzi wa kanda ya Afrika ya Kati na Magharibi wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Marie-Pierre Poirie(MARI-PIERI_PORII) akisema [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dunia imetakiwa kutosahau ukatili wa ISIL dhidi ya Wayazidi

Kusikiliza / Familia ya waYazidi wapokea mgao wa chakula, Erbil, Iraq.(Picha:WFP/Chloe Cornish)

Miaka mitatu iliyopita mwezi huu kundi la kigaidi la ISIL lilishambulia mji waSinjar nchini Iraq, maskani ya Wayazidi walio wachache nchini humo na kuua raia na kuwafanya maelfu kukimbia. Pia maelfu ya wanawake na wasichana wa jamii hiyo walitekwa na kupelekwa Syria walikolazimishwa kuingia katika utumwa wa ngono. Wengi wao bado wanashikiliwa hadi leo. Katika [...]

07/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama laitandika vikwazo vigumu DPRK:

Kusikiliza / Wajumbe wa baraza la usalama la UM wakipiga kura kuiwekea vikwazo DPRK Jumamosi. Picha na UM

Wajumbe wa baraza la Usalama la UM wakipiga kura. Picha na UM Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo kwa kauli moja limepiga kura na kupitisha azimio nambari 2371 la kuongeza vikwazo kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK. Wajumbe wote 15 wa baraza wamepitisha azimio hilo linaloizuia DPRK kusafirisha nje [...]

05/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa maziwa na athari zake mkoani Kagera Tanzania

Kusikiliza / Mwanamke anakamua maziwa. Picha: UM/Eskinder Debebe (maktaba)

Shirika la afya ulimwenguni WHO, linasema maziwa ni miongoni mwa lishe muhimu hususani kwa ukuaji wa mtoto na afya ya mwanadamu. Kukosa maziwa hasa kwa watoto wa umri wa miaka mitano ni kukosa lishe muhimu na lishe duni huchangia vifo milioni 2.7 vya watoto kwa mwaka sawa na asilimia 45 ya watoto kote duniani. Binadamu [...]

04/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasanii Benin wapaza sauti dhidi ya ndoa za utotoni

Kusikiliza / Wasanii kutoka Benin. Picha:VideoCapture

Katika nchi zinazondelea, Umoja wa Mataifa unasema, msichana mmoja kati ya watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Ingawa kuna sheria kali dhidi ya hilo, desturi hizo bado zimetapakaa, zikisababishwa mara kwa mara na umasikini na ukosefu wa usawa wa kijinsia. Nchini Benin, wasanii kutoka jamii mbalimbali wamejitokeza na kushirikiana kwa pamoja kutumia [...]

04/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM kufunguliwa Liberia 2018

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour. Picha: MINUSCA

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu Andrew Gilmour leo amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Liberia. Lengo la zira yake ilikuwa ni kuanzisha ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini humo , na mkataba umetiwa saini na serikali kukubali kuanzishwa ofisi hiyo mpya mapema mwaka 2018. Mwisho wa ziara yake [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Venezuela lazima isitishe kuhukumu waandamanaji kijeshi na kuweka watu kizuizini

Kusikiliza / Waandamanaji wa amani nchini Libya. Picha: UNHCR

Serikali ya Venezuela ni lazima ikomeshe mfumo wa kuwakamata waandamanaji na ongezeko la matumizi ya mahakama za kijeshi kuwahukumu raia. Wito huo umetolewa leo na kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa . Kundi hilo pia limeitaka serikali ya Venezuela kuheshimu haki za waandamanaji wote na mahabusu na kuwahakikishia usalama wao [...]

04/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Libya yasalia kuwa kipaumbele cha IOM: Swing

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing zirani Libya. Picha: IOM

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing alienda Libya tena wiki hii ambako amerejelea kusema kwamba taifa hilo linasalia kuwa nchi inayopewa kipaumbele cha juu na IOM. Katika ziara hiyo ya pili mwaka huu ya Bwana Swing akiambatana na maafisa wengine wa IOM akiwemo mkuu wa ofisi yao [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki – KIAPO

Kusikiliza / NEnolaWikiKiapo

 Juma hili mchambuzi wetu ni Onni Sigalla mhariri mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akichambua neno “KIAPO”.

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Takribani asilimia 50 ya wanawake Tunisia waonja ukatili

Kusikiliza / Mkutano kati ya maafisa wa UN Women na ARP. Picha: UN Women

Tunisia imepiga hatua kubwa kwa kupitisha kwa mara ya kwanza sheria ya kitaifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake tarehe 26 July mwaka huu, ukatili unaoathiri asilimia 50 ya wanawake nchini humo, limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen . Taarifa kamili na Amina Hassan.. (Selina Amina) Sheria [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNDP, IOM na serikali kusaidia waathirika wa ukame Somalia

Kusikiliza / Mtoto kazaliwa wakati Somalia imepigwa na janga la ukame. Picha: IOM

Baada ya ukame mkali uliowatawanya na kuwaathiri watu zaidi ya laki nane nchini Somalia , sasa serikali ya nchi hiyo imeshikamana na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na shirika la Umoja wa Mataifa la mpangomwa maendeleo UNDP ili kuboresha juhudi na uwezo wa kukabiliana na ukame. Washirika hao watatu wameandaa mafunzo ya [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa Kasai DRC wachukua mwelekeo wa kikabila:UM

Kusikiliza / Eneo la Kasai. Picha: MONUSCO/Myriam Asmani

Machafuko katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yanaonekana kuchukua mwelekeo wa kikabila imeonya ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR. Taarifa kamili na John Kibego. (Sauti ya Kibego) Taarifa zilizokusanywa na timu ya uchunguzi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba baadhi [...]

04/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lacroix ahitimisha ziara ya siku tatu Sudan Kusini:

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, Jeane-Pierre Lacroix. Picha: UNMISS

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jeane-Pierre Lacroix, leo amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini. Akizungumza na waandishi wa habari amesema juhudi zinafanyika ili kuharakisha kufikisha jeshi la ulinzi la kikanda. Bwana Lacoix ameeleza kwamba kikosi cha Nepal na sehemu ya kikosi cha wahandisi wa Bangladesh tayari kiko [...]

03/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Walanguzi wa biashara haramu ya binadamu Niger wapigwa na butwaa

Kusikiliza / Kijana muathirika wa ulanguzi. Picha: UNHCR/Video capture

Nchini Niger, hali ya sintofahamu imewaghubika wafanya biashara wa usafirishaji haramu wa binadamu, ambao wamechukua fursa ya biashara hiyo, baada ya soko la watu wanaokimbia mateso, hali ya hatari na umasikini nchini mwao kutafuta maisha kwingine na pia sheria kushika mkondo wake. Ungana na Selina Jerobon kufahamu zaidi.

03/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulinzi wa haki za wanawake kufuatiliwa Samoa: UM

Serikali ya Samoa walipokuwa ziarani Si'upapa nchini Samoa, kijiji cha jamii ambao walipoteza makazi yao kufuatia migogoro. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, watafanya zaira ya siku kumi kuanzia tarehe 8 mwezi huu nchini Samoa, kwa ajili ya kubaini hatua zilizopigwa na serikali katika kupambana na ubaguzi dhidi ya wanawake, kuhakikisha ulinzi na kuinua haki zao. Kamala Chandrakirana, Mtaalamu wa haki za binadamu ambaye kwa sasa anaongoza kikundi shupavu [...]

03/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Machafuko kabla ya kura ya maoni Mauritania yatia hofu:UM

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema inatiwa wasiwasi na machafuko yaliyojitokeza kabla ya kura ya maoni ya katiba iliyopangwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii nchini Mauritania. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Ofisi hiyo inasema kibubwa ni ukandamizaji wa wale wanaopaza sauti zao na ripoti za matumizi ya nguvu [...]

03/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bei ya chakula yapanda kwa mwezi wa watu mfululizo:FAO

Wamama wapepeta mchele nchini Mauritania. Picha: FAO

Bei ya chakula duniani imepanda kwa mwezi wa tatu mfululizo mwezi Julai ikisukumwa zaidi na nafaka, sukari na bidhaa za maziwa. Kwa mujibu wa orodha ya bei ya vyakula inayotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO mwezi Julai bei imeongezeka kwa pointi 179.1 ikiwa ndio ongezeko kubwa kabisa tangu mwezi Januari 2015, na ni [...]

03/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwa mkimbizi haimaninishi maisha yako yamekwisha:UNHCR

Kusikiliza / Kijana Ahmed mkimbizi kutoka Syria anaeishi katika kambi ya wakimbizi ya Skaramagas mjini Athens nchini Ugiriki. Picha: UNHCR

Kuwa mkimbizi haimaninishi maisha yako yamekwisha au wewe huna maana tena wala matumaini. Hiyo ni kauli ya kijana Ahmed mkimbizi kutoka Syria anaeishi katika kambi ya wakimbizi ya Skaramagas mjini Athens nchini Ugiriki. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, badala ya kukata tamaa kijana Ahmed akaamua kuanzisha biashara ya [...]

03/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Polisi wanawake wana mchango mkubwa kwenye UM:Appelblom

Kusikiliza / Maria Appelblom, mkuu wa kitengo cha polisi wa akiba cha Umoja wa Mataifa akisalimiwa na Maafisa wa Polisi wakati wa ziara yake MINUSCA huko Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Picha: UN / MINUSCA

Polisi wanawake wana mchango mkubwa katika miakakati ya ulinzi na usalama ya Umoja wa Mataifa hasa kwenye maeneo mbalimbali duniani waliko na operesheni za ulinzi wa amani. Kauli hiyo imetolewa na Bi Maria Appelblom mkuu wa kitengo cha polisi wa akiba cha Umoja wa Mataifa akizungumza na UN News amesema .. (MARIA CUT 1) "Katika [...]

03/08/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa UM wasaidia tiba ya majeruhi wa shambulio la msikitini Afghanistan

Kusikiliza / Ali Ahmed, mmoja wa majeruhi aliyekuwa akisali msikitini, yuko katika hospitali wa Herat's nchini Afghanistan. Picha: UNAMA

Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa masuala ya kibinadamu umetenga dola 35,000 kwa ajili ya hospitali nchini Afghanistan inayotibu waathirika wa shambulio la kigaidi la msikitini umesema leo Umoja wa Mataifa. Fedha hizo zimekabidhiwa kwa hospitali kuu ya Herat iliyoko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambako takriban watu 44 waliuawa katika shambulio dhidi [...]

02/08/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni lazima kuhakikisha magaidi hawamili silaha:Fedotov

Kusikiliza / Yuri Fedotov, Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, akihutubia wanahabari jijini New York wakati wa kongamano la wadhamini katika kusaidia taasisi zinazopambana na uhalifu wa kuvuka mipala pwani ya Afrika Magharibi. (Picha:Maktaba/ UN /JC McIlwaine)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili tishio la ugaidi katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Baraza hilo ambalo limepitisha kwa kauli moja azimio nambari 2370 la mwaka 2017 la kuwazuia magaidi kumiliki silaha limesema ili kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa lazima nchi zishikamane kupambana na vitendo vyote vya kigaisi [...]

02/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana washirikishwe katika kutimiza SDGs: Sauli

Kusikiliza / Sauli 1

Umoja wa Mataifa unaendelelea kupigia chepuo ushirikishwaji wa vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Malengo hayo ni mtambuka ambapo vijana wana nafasi kubwa ya kuyafanikisha malengo yote iwapo watapewa fursa. Katika mahojiano na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kijana Sauli Paul Mwame wa kidato cha nne katika shule [...]

02/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yahimiza kuheshimu uhuru na haki ikiwataka wadau wote kujizuia na ghasia

Kusikiliza / Maman Sidikou, Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na mkuu wa MONUSCO.Picha:UM/Mark Garten

Maman S. Sidikou, mwakilishi maalimu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO, ameelezea hofu yake dhidi ya watu kukamatwa kiholea na kuwekwa rumande kunakofanyika katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo. Amesema kamatakamata hiyo ni kufuatia asasi za kiraia kuchagiza kuandamana [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama, kisiasa na changamoto Burundi yajadiliwa na baraza la usalama

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo kujadili hali nchini Burundi. Picha: UM/Manuel Elias

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali nchini Burundi. Katika kikao hicho kilichofanyika mjini New York Marekani wamezungumzia hali ya kisiasa, usalama, hali ya haki za kibinadamu na changamoto za haki za binadamu nchini humo. Akizungumza na waandichi wa habari kuhusu mkutano huo balozi wa kudumu wa Uingereza kwenye Umoja wa [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo na Kiir yamekuwa mazuri lakini bado tunawasiwasi: Lacroix

Kusikiliza / Jeane-Pierre Lacroix akikutana na Rais Salva Kiir. Picha:UNMISS

Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jeane-Pierre Lacroix, amesisitiza haja ya ushirikiano wa serikali ya Sudan Kusini katika kuhakikisha uhasama nchini humo unafikia ukomo. Akizungumza na waandishi wa habari,baada ya kukutana leo hii na rais Salva Kiir katika makao makuu ya jeshi la SPLA huko Bilpha Lacroix amesema baadhi ya [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq: FAO

Kusikiliza / Simu za rununu zasaidia kutuma fedha kwa familia zilizoathirika na vita Iraq. Picha: FAO

Familia nyingi za vijijini nchini Iraq sasa zinafaidika na njia salama na ya uhakika ya kupokea fedha, asante kwa teknolojia ya kutuma fedha kupitia simu za rununu, iliyoanza kutumiwa kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo kama sehemu ya mpango wa malipo ya fedha kwa [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya 40 wafariki dunia kwenye shambulio msikitini Afghanistan:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa Antonio Guterres. Picha: UM

Waumini zaidi ya 40 wamearifiwa kuuawa wakiwemo watoto wawili na kujeruhiwa wengine zaidi ya 80 katika shambulio dhidi ya msikiti mjini Herart nchini Afghanistan. Amina Hassan na taarifa kamili (TAARIFA YA AMINA) Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio hilo la Agost Mosi na kusema mashambulizi ya makusudi dhidi ya raia [...]

02/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini yemen bado ni tete:UNDP

Kusikiliza / Hali nchini Yemen bado ni tete. Picha: UNDP

Hali nchini Yemen bado ni tete na inahitaji kuendelea kutupiwa jicho zaidi. Hayo ni kwa mujibu wa Auke Lootsma mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Yemen alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York kwa njia ya video. Bwana Lootsma amesema hivi sasa Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba [...]

01/08/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Busara na uzoefu wa wazee na vijana ni muhimu kwa SDG:Guterres

Kusikiliza / mjadala wa rika mbalimbali  wenye lengo la kuchagiza mchango muhimu wa wazee na vijana katika utekelezaji wa SDGs. Picha: UM/Manuel Elias

Busara, uzoefu, ari na mawazo ya wazee na vijana ni muhimu katika kuhakikisha utimizaji wa malengo yote 17 ya maendeleo endelevu yaani SDG's. Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, katika mwanzo wa siku ya mjadala wa rika mbalimbali wenye lengo la kuchagiza mchango muhimu wa wazee na vijana katika [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM uko hapa kuwasaidia Wasudan Kusini kupata amani: Lacoix

Kusikiliza / Mkutano kuhusu mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacoix leo amewasili Juba nchini Sudan kusini ili kutathimini hali halisi na mikakati ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS katika kuhakikisha taifa hilo linafikia lengo la amani ya kudumu. Lacoix amekutana na maafisa wa serikali na kujadili masuala mbalimbali [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkakati wa WFP Tanzania utasaidia kutokomeza njaa

Kusikiliza / WFP kutokomeza umasikini nchini Tanzania. Picha: WFP/Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP hivi karibuni limezindua mkakati wa miaka mine wa kitaifa nchini Tanzania (CSP). Walengwa wakubwa wakiwa watanzania wenyewe hasa wakulima wadogo wadogo na wakimbizi kutoka nchi jirani. Ili kuchambua zaidi kuhusu mkakati huo, faida na madhumini yake Flora Nducha amezungumza na Juvenal Kisanga afisa wa [...]

01/08/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumeshuhudia madhila ya Boko haramu kwa watu:IOM

Kusikiliza / Mtoto akiwa katika kambi ya Assaga, karibu na Diffa, Niger.(Picha:UNICEF/Sylvain Cherkaoui)

Tumeshuhudia madhila kwa watu yalkiyosababishwa na uasi wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing baada ya kuzuru eneo hilo. Karibu watu milioni mbili wamezikimbia nyumba zao sababu ya Boko Haram, huku zaidi ya nusu ya watu waliotawanywa [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji umewaangusha mama na mtoto katika unyonyeshaji:UNICEF/WHO

Kusikiliza / Watoto watano kati ya sita hawapati lishe muafaka. Picha: UNICEF/UNI116106/Pirozzi

Unyonyeshaji ni moja ya njia muafaka na uwekezaji wa gharama nafuu unaoweza kufanywa na taifa lolote katika afya ya kizazi kipya na mustakhbali bora wa kiuchumi na jamii amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataiofa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake. Katika mwanzo wa wiki ya unyonyeshaji duniani ambayo kila mwaka huwa Agost [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lacroix yuko CAR kusaka suluhu ya machafuko mapya

Kusikiliza / Jean-Pierre-Lacroix

Mkuu wa operesheni za amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ili kusaidia kupata suluhu ya kuzuia kuendelea kwa machafuko yanayotishia mchakato wa amani. Katika ziara hiyo ya siku tatu inayomalizika leo Jumanne Lacoix amekutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo, viongozi wa serikali na [...]

01/08/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031