Nyumbani » 17/07/2017 Entries posted on “Julai 17th, 2017”

Ukombozi wa Mosoul haujamaliza changamoto zote Iraq: Kubiš

Kusikiliza / Mwakilishi wa UM nchini Iraq na mkuu wa UNAMI Bwana Kubis akihutubia baraza la usalama kuhusu hali nchini Iraq. Picha na UM

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema ukombozi wa kihistoria wa Mosul usifunike ukweli kwamba mustakhbali wa taifa hilo bado unakabiliwa na changamoto nyingi. Akihutubia baraza la usalama hii leo Ján Kubiš amesema ukombozi wa Mosul ulifanikiwa kwa juhudi kubwa za majeshi ya ukombizi ya Iraq na wadau wa kimataifa ili kuwaokoa na kuwalinda [...]

17/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wazindua mafunzo ya kitaifa ya mitaala ya mahakama Somalia

Kusikiliza / Picha:UNSOM

Serikali ya shirikisho ya Somalia kwa pamoja na Umoja wa Matafia wamezindua programu ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa sheria takriban 350 kote nchini katika juhudi za kusaidia kujenga upya mamlaka ya mahakama nchini humo. Akizindua programu hiyo, mwanasheria mkuu wa Somalia Ibrahim Idle Suleyman amesema mfululizo wa mafunzo utasaidia katika kuleta mabadiliko ya kisheria [...]

17/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yamepitisha viwango vya matumizi ya dawa zitumikazo kwa mifugo

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Hien Macline

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia matumizi ya dawa katika bidhaa za mifugo zitumikazo kama chakula na kwa mimea wamepitisha viwango vinavyodhibiti matumizi ya dawa hizo, katika mkutano uliofanyika leo huko Geneva Uswisi. Muafaka huo umefikiwa kufuatia utafiti wa pamoja wa kamati ya Shirika la chakula duniani FAO na lile la afya ulimwenguni WHO kuhusu [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Gharama za vita kwa binadamu Afghanistan ni kubwa mno:UM

Kusikiliza / Kambi ya Samar Khel karibu na  Jalalabad, ambako waAghanistan wamekimbil.(Picha: Bilal Sarwary/IRIN)

Gharama za vita vya Afghanistan kwa binadamu ni kubwa mno amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo , akitaja vifo, uharibifu na madhila kwa raia. Tadamichi Yamamoto ametoa kauli hiyo kufuatia ripoti ya mpango wa Umoja wa Mataifa UNAMA na ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu iliyotolewa leo. Ripoti imebaini [...]

17/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kazi ya kulinda amani si lele mama

Kusikiliza / Meja Cheche. Picha:UNMISS

Kazi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa si lele mama, mbali ya changamoto inatoa fursa pia kwa walinda amani hao kujifuinza mambo mengi kutoka kwa nchi na watu wanaowahudhumia. Lakini kikubwa zaidi kinawapa fursa ya kuthamini uhuru na kuishi kwa amani na usalama katika nchi watokako. Basi kwa undani zaidi ungana na Flora Nducha [...]

17/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto 1 kati ya 10 hakupata chanjo 2016 duniani

Kusikiliza / Picha: WHO

Kote ulimwenguni watoto milioni 12.9, sawa na mtoto mmoja kati ya kumi hawakuchanjwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya ulimwenguni WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF.Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Kwa mujibu wa mashirika hayo hii inamaanisha kwamba watoto hao walikosa dozi ya kwanza ya chanjo ya pepopunda (DTP) [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutimiza SDG's lazima kasi ya utekelezaji iongezeke:Guterres

Kusikiliza / Ripoti ya SDG's ya mwaka 2017. Picha: UN Photo

Kama dunia inataka kutokomeza umasikini, kukabili changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuwa na jamii jumuishi zenye amani kwa wote ifikapo 2030, basi wadau wote muhimu wakiwemo serikali, ni lazima waongeze kasi ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG's. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Wito huo umo katika ripoti mpya ya [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wawataka viongozi wa kisiasa kumaliza vita yei:UNMISS

Kusikiliza / Picha:UNMISS

Watoto wanaokabiliwa na madhila makubwa kutokana na vita vinavyoendelea Sudan Kusini na umasikini wamewataka viongozi wa kisiasa kurejesha amani kwenye mji wa Yei nchini humo. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS, hali ni mbaya jimboni Yei, asilimia 70 ya watu walikimbia mwaka jana baada ya machafuko kuzuka baina ya serikali [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunasonga kutokomeza umasikini Tanzania japo kuna changamoto:Mwasha

Kusikiliza / Anna Mwasha , Mkurugenzi idara ya kutokomeza umasikini katika wizara ya fedha na mipango ya Tanzania akihojia na Idhaa ya Kiswahili ya UM wa Mataifa New York.

Juhudi za kutokomeza usmasikini sanjari na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG's zinapiga hatua nchini Tanzania ingawa bado kuna changamoto kadhaa. Akizungumza na idhaa hii kandoni mwa kongamano la ngazi ya juu la kisiasa linalotathimini utekelezaji wa SDG's kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani Bi Anna Mwasha, ambaye ni [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930