Nyumbani » 14/07/2017 Entries posted on “Julai 14th, 2017”

Utalii wanufaisha wakaazi nchini Tanzania

Kusikiliza / Bunga la wanyama nchini Tanzania.(Picha:UM/B Wolff)

Utalii!. Idadi ya watalii wa kutoka nje ya bara la Afrika imeongezeka tangu mwaka 1995. Mfano kati ya 1995 hadi 1998 idadi imeongezeka kutoka Milioni 24 hadi takribani watalii milioni 56 kati ya mwaka 2011-2014. Takwimu za baraza la kimataifa la safari na utalii linasema idadi ya watalii wa kigeni barani Afrika inatarajiwa kuongezeka na [...]

14/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kituo cha kudumu cha kulinda amani huenda kikaanzishwa Yei-UNMISS

Kusikiliza / UNHCR yaonya kuhusu hali ya Yei Sudan Kusini. Picha: UNHCR/Video capture

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, umesema unatathmini uwezekano wa kuanzisha kituo kipya cha kudumu cha ulinzi wa amani mjini Yei ili kuwalinda vyema raia katika jimbo hilo. Eneo hilo ambalo lilikuwa mwendeshaji wa Sudan Kusini na lenye kuzungukwa na udongo wenye rutuba lilisaidia sana biashara na kuvutia kundi kubwa la watu [...]

14/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani shambulio kwenye mji wa kale wa Jerusalem

Kusikiliza / Mtazamo wa mji wa Jerusalem.(Picha:UM/ Rick Bajornas)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres amelaani vikali shambulio lililotekelezwa leo asubuhi na washambuliaji watatu kwenye mji wa kale wa Jerusalem na kusababisha vifo vya maafisa wawili wa polisi na kumjeruhi mwingine. Kupitia taarifa ya msemaji wake, Katibu Mkuu amesema tukio hilo linaweza kuchochea ghasia zaidi na amezitaka pande zote kuchukua hatua stahiki kuzuia [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yang'ara katika mahindano ya shabaha ya UNAMID Darfur

Kusikiliza / Walenga shabaha wa UNAMID kikosi cha Tanzania.(Picha:UNAMID/Luteni Selemani Semenyu)

Tanzania yaibuka kidedea katika mashindano ya kulenga shabaha yaliyofanyika huko Darfur nchini Sudan. Mashindano hayo ya walinda amani wa mpango wa pamoja na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID yalijumuisha walinda amani kutoka nchi mbalimbali mjini Nyala. Luteni Selemani Semenyu alikuwa shuhuda na kutuandalia makala hii.

14/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki- Aidha, Ama, Ima, Au

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno aidha, ama, ima na au Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Bwana Zuberi anasema aidha maanake ni vile vile, Ima kwa upande wake inamaanisha kwa vyovyote vile. Je unafahamu matumizi [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa mvua kwa misimu mitatu waleta hofu ya njaa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Mfugaji nchini Kenya na mifugo wake walionusurika kifo kufuatia ukame uliosababisha vifo vya theluthi mbili ya mifugo yake.(Picha:FAO/Tony Karumba)

Tahadhari iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO imesema ukosefu wa mvua Afrika Mashariki umeongeza njaa zaidi na kusababisha mazao kuteketea, lishe kupungua na maelfu ya mifugo kufa, wafugaji wakibeba mzigo mkubwa wa ukosefu huo wa mvua. Tahadhari hiyo imeonya kwamba mfululizo wa tatu wa ukosefu wa msimu wa [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa amani umejeruhiwa lakini unaweza kutibika-Mogae

Kusikiliza / Bwana Festus Mogae akisalimiana na wakazi wa Bentiu. (Picha:UN/JC McIlwaine)

Mwenyekiti wa tume ya pamoja ya ufuatiliaji na tathmini, (JEMC) Festus Mogae, amejibu wito wa kumtaka kujiuzulu. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Juba Sudan Kusini bwana Festus Mogae, amesema anatambua kwamba jamii haijaridhika na kazi ya JMEC, lakini ameelezea dhamira yake ya kusaidia utekelezaji wa mchakatio wa amani nchini humo. (MOGAE CUT) "Nafahamu kwamba [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhil kwa raia Kasai DRC hayana dalili ya kupungua-UNHCR

Mkimbizi wa ndani Bernard akiwa mji wa Idiofa, jimbo la Kwilu na wanae.(Picha:UNHCR/John Wessels)

Madhila kwa maelfu ya watu wanaoendelea kutawanya na machafuko katika jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hayana dalili ya kupungua limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Katika eneo hilo linaloshuhudia machafuko tangu mwishoni mwa 2016, idadi ya watu waliotawanywa UNHCR inasema sasa imefikia milioni 1.3 na [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirika imara baina ya UM na nchi wanachama ni muhimu kukomesha ukatili wa kingono:

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu msaada mashinani  Atul Khare akihutubia nchi wanachama wa UM kupitia video. Picha: UM/Frédéric Fath

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo alhamisi amesisitiza umuhimu wa ushirika imara baina ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama katika kusonga mbele na juhudi za kuzuia na kushughulikia unyanyasaji wa kingono na ukatili. Bwana Atul Khare msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu msaada mashinani amesema "pamoja tumeimarisha juhudi zetu" ameuambia mkutano unaofanyika kwenye makao makuu [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dini wakaa kitako kuzuia mauaji mengine ya kimbari

Kusikiliza / Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji Mauaji ya Kimbari, Adama Dieng. Picha:UN/Photo

Viongozi wa dini ulimwenguni kote leo hii wamekusanyika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuanzisha mpango mpya wa utekelezaji wenye lengo la kuzuia mauaji mengine ya kimbari. Mpango huo ulichukua miaka miwili kuandaliwa na kuongozwa na Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji Mauaji ya Kimbari, Adama Dieng, na [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930