Nyumbani » 12/07/2017 Entries posted on “Julai 12th, 2017”

Wayemen milioni 20 wanategemea hatua za baraza la usalama kusaidiwa

Kusikiliza / Mkuu wa kuratibu masuala ya kibinadamu wa Umoj wa Mataifa Stephen O'Brien.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Takriban Wayemeni milioni 20 wanategemea baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua mujarabu ili kusaidia kumaliza vita nchini Yemen ambavyo sasa vimechangia kusambaa kwa kashifa ya kipindupindu. Akizungumza kwenye kikao cha baraza la usalama hii leo mjini New York Marekani, mkuu wa kuratibu masuala ya kibinadamu wa Umoj wa Mataifa Stephen O'Brien, amesisitiza [...]

12/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kijana weka bunduki chini, chukua kalamu- Dor

Kusikiliza / Dor 2

Kijana Dor Achek kutoka Sudan Kusini, alikuwa mkimbizi, aliyeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Sasa kijana huyuni msomi na ana ndoto za kuwa balozi ili awasaidie wakimbizi hususani vijana. Kijana huyu ambaye amehudhuria mkutano wa ngazi za juu kuhusu elimu amezungumza na Joseph Msami wa idhaa hii kumuelezea alikotoka,aliko na zaidi ya [...]

12/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maeneo mapya 21 yaongezwa kwenye orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia

Kusikiliza / Eneo la urithi la Aphrodisias nchini Uturuki.(Picha:UNESCO)

Maeneo mapya 21 yameongezwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya urithi wa dunia na kufanya jumla ya maeneo ya urithi wa dunia kufikia zaidi ya 1000. Tangazo hilo limetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO wakati wa kufunga mkutano wa 41 wa kila mwaka wa kamati ya [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu bilioni 2 hawana maji salama ya kunywa:WHO/UNICEF

Kusikiliza / Upatikanaji wa maji safi na salama bado ni changamoto katika nchi nyingi duniani.(Picha:UNIC/Tanzania)

Watu 3 kati ya 10 kote duniani au watu bilioni 2.1 ,wanakosa fursa ya kupata maji salama nyumbani na mara mbili yao hawana huduma za kujisafi, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya duniani WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF. Ripoti hiyo imeongeza kuwa nyumba nyingi , vituo vya afya na shule [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Askari wa UNMISS wasitisha jaribio la utekaji nyara kwa wakimbizi

Kusikiliza / Walinda amani wakipiga doria nchini Sudan Kusini.(Picha:Isaac Billy/ UNMISS)

Nchini Sudan Kusini, askari wawili waliovaa sare za kijeshi na kubeba silaha walijaribu kuwateka nyara wakimbizi watatu karibu na kituo cha ulinzi wa raia cha Bentiu kinacholindwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Askari hao wanaodhaniwa kuwa ni wa SPLA waliwakaribia na kuanza kuwanyanyasa [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu kuhusu albino kuzuru Tanzania

Kusikiliza / Mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi , Ikponoswa Ero (Kushoto). Picha: UNIC/Tanzania

Mtaaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Ikponwosa Ero anafanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania wiki ijayo kuanzia Juali 18-28, ili kutathimini hali ya haki za binadamu za watu wenye ulemavu wa ngozi au albino. Bi Ero amesema ziara hiyo ni muhimu sana ukizingatia kwamba kumeripotiwa mashambulizi mengi dhidi ya watu [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utandawazi una mapungufu yake-WTO

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Kiuchumi Angel Gurria .(Picha:UNIfeed/Video Capture)

Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Kiuchumi (OECD) alisema kuwa kuna “upungufu dhidi ya utandawazi” na kuongeza kuwa “utandawazi hauna shingo ambayo unaweza kuegemea.” John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA KIBEGO) Akizungumza katika ufunguzi wa mwaka huu wa mkutano wa msaada wa tathimini ya kimataifa ya Biashara katibu mkuu huyo bwana [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uthubutu wa kutekeleza yanayosemwa utafanikisha SDGs- Moshi

Kusikiliza / SDGs.(Picha:UNIC/Tanzania)

SDGs.(Picha:UNIC/Tanzania) Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs uko katika mstari sahihi nchini Tanzania kufuatia sera mpya zilizopo za kuhakikisha ulinzi wa mapato ya kitaifa. Hiyo ni kauli ya Celestine Moshi, mkurugenzi, idara ya ushrikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, akizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano wa [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930