Nyumbani » 11/07/2017 Entries posted on “Julai 11th, 2017”

Mradi wa nishati ya jua wabadili maisha ya wakaazi Tanzania

Kusikiliza / Mradi wa nishati ya jua nchini Tanzania.(Picha:Benki ya dunia/video capture)

Upatikanaji wa huduma ya maji ni changamoto katika nchi nyingi hususan zilizo barani Afrika. Hata hivyo jamii, serikali na mashirika mbalimbali yakiwemo ya Umoja wa Mataifa kama vile benki ya dunia yanachukua hatua ili kupunguza adha hiyo. Nchini Tanzania waakazi wa mkoa wa Manyara wamepata muorubaini dhidi ya ukosefu wa maji na magonjwa yanayotokana na [...]

11/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waenzi waathirika wa mauaji ya Srebrenica

Kusikiliza / Ni mwaka 1995 mwanajeshi wa kitaifa akisoma orodha ya majina ya wanajeshi waliokimbia au manusura wa mji uliosambaratika wa SrebrenicaUNICEF/NYHQ1995-0553/LeMoyne

Umoja wa Mataifa leo Jumanne umewakumbuka na kuwaenzi maelfu ya wanaume na wavulana waliouawa kinyama miaka 22 iliyopita kwenye mji wa Srebrenica huko Bosnia na Herzegovina wakati wa vita vya Balkan. Mauaji ya halaiki ya Julai 11 mwaka 1995 yalikuwa ndio makubwa zaidi kutokea katika ardhi ya jumuiya ya Ulaya tangu jumuiya hiyo ilipoanzishwa baada [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwajibikaji na maridhiano ni muhimu kuponya majeraha ya ISIL Iraq

Kusikiliza / Familia iliyokimbia vita vya Mosul, nchini Iraq. Picha: Photo: UNHCR/Ivor Prickett

Kukombolewa kwa mji wa Mosul Iraq kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi la ISIL , kutokana na ushirika wa majeshi ya serikali ya Iraq yakisaidiwa na muungano wa wadau wa kimataifa , ni hatua muhimu ya kubadili ukurasa katika vita, Lakini Iraq inakabiliwa na mlolongo wa changamoto za haki za binadamu ambazo zisiposhughulikiwa , zinaweza [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekelezaji wa mkataba wa Disemba 2016 DRC hauridhishi-UM

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Utekelezaji wa mkataba uliotiwa saini mwaka 2016 mwezi Desemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hauridhishi huku hali ikiendelea kuwa tete katika maeneo mbalimbali hususani ya Mashariki na Magharibi mwa nchi hiyo. Hayo yamesemwa na Jean-Pierre Lacroix mkuu wa idara ya operesheni za ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa, akiwasilisha ripoti leo jumanne [...]

11/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Biashara ni nguzo muhimu kwa amani na ustawi wa kanda ya Maziwa Makuu Afrika-UNCTAD

Kusikiliza / Maisha ya kawaida jimbo la Tanganyika nchini DRC.(Picha:MONUSCO / Francois-Xavier Mybe)

Kuchagiza maendeleo, amani na usalama katika kanda ya Maziwa Makuu Afrika ndio mada kuu kwenye mkutano unaofanyika leo mjini Geneva Uswisi ulioandaliwa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD na kuhudhuriwa pia na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa eneo la maziwa makuu. John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA JOHN) [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila ya uzazi wa mpango umasikini utaendelea kuwa mfalme

Kusikiliza / Mama na mwanae katika hospitali nchini Liberia.(Picha:UNMIL Photo/Staton Winter)

Leo ni Siku ya Idadi ya Watu duniani ambayo mwaka huu inaenda sambamba na mkutano wa ngazi ya juu wa mpango wa uzazi FP2020 unaofanyika jijini London, Uingereza, mkutano ulioleta pamoja viongozi na watetezi kutoka mataifa mbalimblai kuahidi upatikanaji wa aina za kisasa za uzazi wa mpango kwa wanawake zaidi ya milioni 120 hususan wale [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msumbiji, Benki ya dunia na FAO wasaini mkataba kuinua sekta ya misitu

Kusikiliza / Naibu Mkurugenzi Mkuu Daniel Gustafson wa FAO na Augusta Pechisso wa maswala ya maendeleo endelevu ya kitaifa Msumbiji wakati wakutia saini mkataba.(Picha:FAO/Ricarrdo De Luca)

Serikali ya Msumbiji, Benki ya dunia na shirika la chakula na kilimo duniani FAO leo wametangaza mradi mpya ambao utaimarisha misitu endelevu na kuchangia kwa Msumbiji kutimiza lengo namba 15 la maendeleo endelevu yaani SDGs kuhusu misitu. Mradi huo utakaogharimu dola milioni 6 ni sehemu ya uwekezaji wa dola milioni 47 wa benki ya dunia [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Brigedi maalumu ya SADC yakabiliwa na changamoto DRC-Mwakibolwa

Kusikiliza / Luteni Jenerali James Mwakibolwa.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/F.Nducha)

Brigedi maalumu iliyoanzishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iliyo chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa ajili ya kufurusha makundi ya waasi (FIB) inakabiliwa na changamoto nyingi. Hayo ni kwa mujibu wa Luteni Jenerali James Mwakibolwa, mnadhimu mkuu wa majeshi wa ulinzi nchini Tanzania aliyeko makao makuu ya Umoja [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres akaribisha kuanzisha mpango mpya wa UM Colombia:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres. Picha: UM/Evan Schneider

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha kuanzishwa kwa mpango mpya wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia utakaokuwa na lengo la kuhakiki utekelezaji wa mkataba wa amani unaohusiana na kulijumuisha katika jamii kundi la FARC-EP na pia utekelezaji wa hakikisho la usalama kwa kundi hilo na jamii zilizoathirika na machafuko. Mpango huo [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930