Nyumbani » 07/07/2017 Entries posted on “Julai 7th, 2017”

Mbio zatumika Sudan Kusini kujenga maelewano baina ya jamii

Kusikiliza / Mbio zatumika Sudan Kusini kujenga maelewano baina ya jamii.(Picha:UNifeed/video capture)

Miaka sita ya uhuru wa Sudan Kusini ikitimu tarehe Tisa mwezi huu wa Julai, matumaini ya wananchi kuwa watakuwa na ustawi wa kudumu bado yako mashakani kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo tangu mwezi disemba mwaka 2013. Bado mamia ya watu ni wakimbizi wa ndani na wengine wanakimbilia nchi jirani, jamii mbali mbali zikiendelea kufarakana. [...]

07/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu nchini Kenya

Kusikiliza / Dkt. Samuel Arap Tororee  kutoka tume ya kitaifa ya ardhi nchini Kenya ambaye ana  ulemavu wa macho kutoona na Bi Marsela Odende wakati walihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa hii.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/G.Kaneiya)

Ikiwa ni zaidi ya miaka kumi tangu kupitishwa kwa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu CRPD, baadhi ya nchi zimepiga hatua katika kutekeleza na kuzingatia haki hizo. Mkataba huo uliopitishwa mnamo Disemba 13 mwaka 2016 unatoa muongozo kwa nchi wanachama katika utekelezaji wa sheria, mikakati, sera na programu za kuimarisha usawa na ujumuishwaji pamoja [...]

07/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yaangazia utokomezaji wa silaha za nyuklia

Kusikiliza / Balozi Elayne Whyte Gómez kutoka Costa Rica.(Picha:UM/Manuel Elias)

Mkataba wenye nguvu kisheriaa na ambao unalenga kutokomeza kabisa matumizi ya silaha za nyuklia umepitishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Wajumbe kutoka nchi 124 walioshiriki mkutano huo walipiga kura ambapo nchi 122 ziliunga mkono, ilhali Uholanzi ilipinga na Singapore haikuonyesha msimkamo wowote. Hata hivyo baadhi ya nchi kama vile Marekani, Uingereza, [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa lishe kwa watoto DRC wagharimu serikali mamilioni ya dola- Ripoti

Kusikiliza / rdc

Ripoti mpya iliyozinduliwa leo huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imebainisha jinsi lishe duni kwa watoto inavyoathiri uchumi wa nchi hiyo. Ikipatiwa jina la Gharama ya Njaa barani Afrika, COHA, ripoti hiyo mathalani imesema lishe duni miongoni mwa watoto husababisha DRC kupoteza dola zaidi ya bilioni moja kila mwaka kupitia gharama za tiba, [...]

07/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha Uingereza UNMISS chafungua hospitali Bentiu

Kusikiliza / Ufunguzi wa hospitali Bentiu na kikosi cha Uingereza kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS.(Picha:UNMISS)

Nchini Sudan Kusini, kikosi cha Uingereza kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS kimefungua hospitali kwenye mji wa Bentiu. Hospitali hiyo inalenga kutoa huduma ya matibabu kwa zaidi ya watu 1,800 wakiwemo askari na wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi kwenye kituo cha kuhifadhi raia lililo ndani zaidi. UNMISS inasema hospitali hiyo itaweza kutibu [...]

07/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Kifufumkunye

Kusikiliza / Neno la wiki 2

Wiki hii tunaangazia neno  Kifufumkunye na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema kwamba neno  kifufumkunye lina maana ya jambo lisilo fahamika bayana na ambalo halitiliwi maanani wala umuhimu.

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usugu wa dawa dhidi ya kisonono waongezeka- WHO

Kusikiliza / WHO imesema matumizi  sahihi ya kondomu itasaidia kujikinga dhidi ya kisonono.(Picha:IRIN)

Shirika la afya duniani, WHO limesema tiba dhidi ya ugonjwa wa kisonono inazidi kuwa ngumu kila uchao kutokana na usugu wake kwa antibayotiki au viuavijasumu. Amina Hassan na ripoti kamili. (Taarifa ya Amina) Dkt. Teodora Wi kutoka WHO amesema kubadilika mara kwa mara kwa bakteria wanaosababisha ugonjwa huo pamoja na matumizi holela ya viuavijasumu ni [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Cyprus wamalizika bila muafaka

Kusikiliza / sg  1

Mazungumzo yaliyolenga kuweka mwelekeo wa kuwezesha Cyprus kuungana tena baada ya kuvunjika mapande mwaka 1974 yamemalizika bila maafikiano yoyote. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye aliombwa kurejea Crans Montana Uswisi jana ili kushiriki mazungumzo hayo amewaambia waandishi wa habari hii leo mjini humo kuwa.. [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukata watishia elimu kwa watoto wanaoishi kwenye mizozo- UNICEF

Kusikiliza / watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema ukata unakwamisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya elimu ya watoto wanaoishi kwenye mizozo. UNICEF imetoa taarifa hiyo wakati viongozi wa kundi la nchi 20 wakikutana huko Hamburg, Ujerumani huku ombi la dola milioni 392 zinazohitajika mwaka huu kwa miradi ya elimu kwenye nchi zenye [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930