Nyumbani » 06/07/2017 Entries posted on “Julai 6th, 2017”

Mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kupitishwa Ijumaa

Kusikiliza / Mwenyekiti wa mkutano uliowezesha kupatikana kwa mkataba huo ambao unabeba maadili ya kimataifa kuhusu kutengeneza, kumiliki na kuhifadhi nyuklia Elayne Whyte GómezPicha: UM/Rick Bajornas

Mkataba wa aina yake wenye lengo la kutokomeza kabisa matumizi ya silaha za nyuklia unapitishwa kesho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inafuatia mashauriano ya wiki tatu baina ya serikali na pande mbali mbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na hivyo kufanikisha juhudi za zaidi ya miaka 20. Mwenyekiti wa mkutano uliowezesha [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu mkuu ziarani Uswisi kushiriki mazungumzo ya Cyprus

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa kwenye helikopta baada ya kushiriki mazungumzo juu ya Cyprus mapema mwezi Julai 2017.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesafiri kuelekea Uswisi Alhamisi ili kuendelea na mazungumzo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu Cyprus kwa ajili ya kuleta nchi hiyo kuwa taifa moja kufuatia kisiwa hicho kilicho kwenye bahari ya Mediteranea kugawanyika mapande kwa miaka 43. Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu iliyotolewa Jumatano imesema kwamba mkuu [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Astana imetupatia nuru ingawa ni kidogo- de Mistura

Kusikiliza / mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffa de Mistura akizungumza na waandishi wa habari huko Astan.(Picha:UM)

Mazungumzo kuhusu Syria yaliyofanyika huko Astana , Kazakhstan licha ya kuwa na maendeleo kidogo yamepiga hatua muhimu katika kusaka hatimaye suluhu ya mzozo unaoendelea nchini humo. Hiyo ni kwa mujibu wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura alipozungumza na waandishi wa habari huko Astana baada ya majadiliano kati ya serikali [...]

06/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bei ya vyakula imeongezeka hadi kiwango cha juu kabisa katika miaka miwili-FAO

Kusikiliza / Mkulima katika shamba la zao la mahindi Honduras.(Picha:FAO/Orlando Sierra)

Bei ya vyakula duniani imeongezeka na kufikia kiwango cha juu zaidi katika muda wa miaka miwili, ikichagizwa na bei ya juu ya siagi pamoja na kuongezeka kwa bei ya ngano na nyama. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO katika ripoti yake ya bei za vyakula kwa mwezi Juni ambayo [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dkt. Kituyi kuendelea kuongoza UNCTAD kwa miaka mingine minne

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi wakati akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii mwaka 2016.(Picha:UM/Video Capture)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limemthibitisha Dkt. Mukhisa Kituyi kuendelea kuongoza kamati ya biashara ya maendeleo ya umoja huo, UNCTAD kwa kipindi kingine cha miaka minne kuanzia tarehe mosi Septemba 2017. Uthibitisho huo umefanyika leo kufuatia kufuatia mapendekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mashauriano yake na nchi wanachama. Dkt. Kituyi ni [...]

06/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Myanmar isake suluhu kwa wasio na utaifa- Grandi

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi akutana na Masoota Hatu, mwanamke mwenye umri wa miaka 55 nchini Myanmar. Picha: © UNHCR/Roger Arnold

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya kwanza nchini Myanmar kwa kutoa wito kwa nchi hiyo kusaka suluhu ya endelevu na shirikishi juu ya suala la watu wasio na utaifa. Ametoa wito huo baada kutembelea maeneo ya Yangon, Naypyitaw pamoja na Sittwe na Maungdaw [...]

06/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mazingira duni ya kazi ni kikwazo katika utekelezaji wa majukumu kazini

Kusikiliza / Eunice, mmoja wa wanawake ambao wamepoteza ajira hivi karibuni nchini Kenya kama moja ya  juhudi za kupaza sauti za wanawake. Picha: Picha: UN Women/Video capture

Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yanalenga ikiwemo: kutokomeza umaskini uliokithiri, kumaliza utofauti wa usawa wa kijinsi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Usawa wa kijinsia ni miongoni mwa masuala muhimu kwa ajili ya kufikia ajenda ya 2030. Huku upatikanaji wa ajira ukiwa ni changamoto hususan katika nchi zinazoendelea mazingira duni ya [...]

06/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya gereza kuu la Kananga huko DRC ni ya kusikitisha

Kusikiliza / Jopo la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO limetembelea gereza kuu la Kananga.(Picha:UM/DRC

Jopo la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO limetembelea gereza kuu la Kananga kwenye jimbo la Kasai Mashariki ili kuweza kutathmini mahitaji yake kutokana na hali mbaya inayolikabili. Hivi sasa gereza hilo lililojengwa mwaka 1951 linakabiliwa na mlundikano wa wafugwa ambapo badala ya kuhifadhi wafungwa 300 hivi sasa [...]

06/07/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 30 wanakabiliwa na njaa- FAO

Kusikiliza / Mtoto anayeugua utapiamlo nchini Somalia katika kambi ya Salamey Idale.(Picha:UNICEF/Rich)

Dunia inakabiliwa na janga kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa, huku watu milioni 30 katika nchi nne wakikabiliwa na uhaba wa chakula na wengi wakiwa katka hatari ya ukame limesema Shirika la kilimo na chakula duniani FAO. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Akizungumza katika kongamano la FAO huko Roma, Italia Naibu [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zachukuliwa kusaidia waathirika wa mafuriko Darfur Kusini

Kusikiliza / Mafuriko nchini Sudan kwenye jimbo la Darfur Kusini kufuatia mvua kubwa. Picha: IOM

Huko nchini Sudan kwenye jimbo la Darfur Kusini mvua kubwa zilizonyesha tarehe 20 mwezi uliopita na kusababisha mafuriko zimeendelea kusababisha madhara kwa wakimbizi wa ndan wapatao 9,000. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu, OCHA imesema mvua hizo zilisababisha mamia ya makazi ya wakimbizi [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado kuna changamoto kubwa Afrika katika kujumuisha watu wenye ulemavu

Kusikiliza / Miundombinu2

Wakati mataifa yaliyoendelea yamepiga hatua kubwa katika kujumuisha mahitaji ya watu wenye ulemavu kwenye jamii, Afrika bado ni kitendawili hasa katika masuala kama miundombinu ambayo ilijengwa bila kumfikiria mtu mwenye ulemavu bila kusahau mila na tamaduni potofu kuhusu hali ya ulemavu. Akizungumza na idhaa hii  kuhusu changamoto hizo Dkt. Samuel Arap Tororee  kutoka tume ya [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930