Nyumbani » 31/07/2017 Entries posted on “Julai, 2017”

Mahakama ya watoto Zanzibar imenitendea haki

Kusikiliza / Picha:UNICEF/2014/Holt

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika ulinzi wa watoto baada ya kufungua mahakama mpya kwa ajili ya ulinzi wa watoto. Mahakama hiyo ni ya tatu kufunguliwa Zanzibar na hutumika kusikiliza na kutoa hukumu za kesi kati ya familia na mtoto, mtoto mtukutu, mtoto na mtu mzima [...]

31/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kisiwa cha Tonga chafanikiwa kutokomeza matende:WHO

Kusikiliza / Picha:WHO

Ufalme wa Tonga , kisiwa katika bahari ya Pacific ni kidogo na idadi ya watu wake ni wachache lakini kinafanikiwa kutimiza malengo makubwa ya kiafya umesema leo Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, limethibitisha kwamba nchi hiyo imetokomeza ugonjwa wa matende kama tatizo la afya ya umma. Matende ni ugonjwa [...]

31/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afisa wa haki za binadamu Gilmour kuzuru Liberia

Kusikiliza / Gilmour

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour, atazuru Liberia kuanzia Agosti Mosi hadi 3 katika jitihada za kutafuta kuungwa mkono ili kuanzisha ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo baada ya mpango wa Umoja wa Mataifa UNMIL kufungwa rasmi Machi 2018. Katika ziara hiyo bwana Gilmour atakutana na [...]

31/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani shambulio kwenye ubalozi wa Iraq , Kabul

Kusikiliza / 05-14-unama-kabul

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, umelaani vikali shambulio la leo dhidi ya ubalozi wa Iraq mjini Kabul. Shambulio hilo lililotokea katika makazi ya watu katikati mwa Kabul lilidumu kwa saa tano na lilihusisha watu kadhaa wenye silaha ambao waliwauwa raia wawili wa Afghanistan waliokuwa wakifanya kazi katika ubalozi huo na kumjeruhi afisa [...]

31/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Al-Shabaab yakatili maisha ya askari 12 wa Uganda Somalia

Kusikiliza / Askari wa AMISOM kutoka Uganda wakitembea katika daraja kwenye eneo la Janaale, Somalia. Picha: AU/UN/IST/Tobin Jones

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating, leo ametuma salamu za rambirambi kwa wafanyakazi na familia za askari kutoka Uganda wa kulinda amani wa muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM waliouawa katika shambulio kwenye jimbo la Lower Shabelle jana jumapili. Kundi la kigaidi la Al-Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo lililokatili maisha [...]

31/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Asilimia 80 ya vijana watumia intaneti: ITU

Kusikiliza / Picha:ITU

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la muungano wa habari na Tekinologia ya mawasiliano (ITU), inaonyesha kuwa idadi ya vijana wanaotumia mtandao wa intaneti inazidi kuongezeka, wakisalia na mchango wa asilimia kubwa zaidi ya watumiaji wa mtandao huo kote duniani, huku wanaotumia Mobile Broadbadn wakitarajiwa kufikia bilioni 4.3. Taarifa kamili na John Kibego. [...]

31/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita dhidi ya ubaguzi wa rangi lazima vifanikiwe:UM

Kusikiliza / Picha:UNICEF/Claudio Versiani

Vita dhidi ya mifumo yote ya ubaguzi wa rangi ni lazima vifanikishwe kwani mamilioni ya watu wanapitia mifumo mbalimbali ya ubaguzi wa rangi duniani pasi sababu yoyote. Grace Kaneiya na taarifa zaidi. (TAARIFA YA GRACE) Kauli hiyo imetolewa na Adam Andemoula mkurugenzi wa kitengo cha baraza na mifumo ya mikataba kwenye ofisi ya haki za [...]

31/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajenda ya 2030 inafahamika, lakini kuifanikisha ndio mtihani: Hongbo

Kusikiliza / Wu Hongbo, Msaidizi wa Katibu Mkuu kwa ajili ya idara ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii DESAPicha: Mbongiseni Mndebele.

Ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu inajadiliwa vyema kote duniani , lakini bado ni safari ndefu katika kuifanikisha. Huo ni mtazamo wa Msaidizi wa Katibu Mkuu katika Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, DESA, anayeondoka madarakani bwana Wu Hongbo. Leo ikiwa siku yake ya mwisho katika wadhifa huo amesema [...]

31/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa chuma cha pua warejea 2016:UNCTAD

Chuma cha pua nchini Liberia. Picha:UN Photo/B Wolff

Licha ya matumizi madogo nchini Uchina na gharama nafuu kwa takriban mwaka mzima sekta ya chuma cha pua imeshuhudia ongezeko la uzalishaji na usafirishaji nje wa bidhaa hiyo. Kwa mujibu wa ripoti mpyailiyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD , iitwayo "ripoti ya soko la chuma cha pua" sekta [...]

31/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu mpya wa UNSMIL kuisaidia Libya kutoka kwenye sokomoko

Kusikiliza / Mkuu mpya wa UNSMIL Ghassan Salamé. Picha: UM/Elma Okic

Kazi ya kuisaidia Libya kujikwamua kutoka kwenye sokomoko la kisiasa ndio kipaumbele cha kwanza cha mkuu mpya mteule wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL. Mwanadiplomasia mkongwe kutoka Lebanon na mwanazuoni Ghassan Salamé amekuwa hapa makao Makuu ya umoja wa Mataifa New York kuzungumza na maafisa wa Umoja wa Mataifa na mabalozi kabla [...]

31/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walindeni watoto wahamiaji dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu-UM

Kusikiliza / Usafirishaji haramu wa watoto.(Picha: UM/Alessandro Scotti )

Nchi zimetakiwa na wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa kuongeza juhudi za kuwalinda watoto wahamiaji dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu, kuuzwa na mifumo mingine ya unyanyasaji. Wawakilishi maalumu Maria Grazia Giammarinaro na Maud de Boer-Buquicchio wametoa wito huo kwa ajili ya siku ya kimataifa ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu ambayo huadhimishwa kila mwaka [...]

30/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Urafiki unaweza kutumika kwa ajili ya mustakabali bora wa dunia-UM

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Sophia Paris

Leo Julai 29 ni siku ya urafiki duniani, Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake siku hii umesema, wakati dunia inakabiliana na changamoto, majanga na migawanyiko kama vile: umasikini, mizozo na ukiukwaji wa haki za bindamu miongoni mwa mambo mengine yanayozorotesha amani, usalama, maendeleo na muungano wa kijamii miongoni mwa watu, urafiki huenda ndio muaorobaini. Katika [...]

29/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu alaani jaribio la kombora DPRK:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha na UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kurushwa tena kombora la masafa marefu lenye uwezekano wa kuvuka mipaka ya nchi lililofanywa na jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK leo. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Katibu Mkuu amesema kitendo hicho kwa mara nyingine ni ukiukaji wa maazimio ya baraza la [...]

28/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Suala la uzazi wa mpango nchini Uganda

Kusikiliza / Samuel na Kate Opio wanafurahia kuzaliwa kwa watoto wao mapacha nchini Uganda. Picha: © UNFPA Uganda / Prossy Jonker Nakanjako

Suala la uzazi wa mpango ni changamoto hususani kwa mataifa yanayoendelea na hususan  Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA takribani wanawake milioni 225 kote duniani ambao wanataka kuepuka mimba zisizotarajiwa hawatumii njia salama na muafaka za kupanga uzazi kwa [...]

28/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS imejenga mahabusu ya kwanza ya wasichana Sudan Kusini

Kusikiliza / Mahakama ya watoto nchini Sudan Kusini. Picha: UM.Video capture

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umejenga mahabusu ya kwanza ya aina yake ya wasicha nchini humo. Mahabusu hiyo Wau Juvenile Detention Centre ilikabidhiwa kwa serikali ili kuruhusu wasichana wahalifu kushikiliwa hapo na kesi zao kusikilizwa sambamba na vijana wenzao. UNMISS inasema ujenzi wa kituo hicho umegharimu dola za Marekani 35,000 na [...]

28/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bloga wa Vietnam aachiliwe baada ya mapungufu katika kesi:UM

Kusikiliza / Logo. Picha: OHCHR

Kufungwa kwa mmiliki wa blog kwenye mtandao nchini Vietnam mwezi mmoja baada ya mwanaharakati mwingine wa mtandaoni ajulikanaye kama Mother Mushroom kuwekwa kizuizini ni ishara ya kuongezeka kwa msako dhidi ya watetezi wa haki za binadamu umeonya leo Umoja wa Mataifa. Onyo hilo lililotolewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa limekuja [...]

28/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misaada ya kibinadamu Syria yafikia idadi ya chini kabisa: OCHA

Kusikiliza / Wakimbizi nchini Syria wanapokea msaada. Picha: UNHCR/Bassam Diab

Ufikishaji wa misaada ya kibinadamu kwa jamii zisizojiweza kabisa nchini Syria uko katika kiwango cha chini kabisa umesema leo Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA Jens Laerke, mwezi Julai hakujakuwa na misafara ya mashirika yoyote ya misaada katika maeneo yanayozingirwa nchini humo [...]

28/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutaimba na kucheza ngoma hadi amani irejee Darfur

Kusikiliza / Ngoma kwa ajili ya amani Darfur, Sudan. Picha: UM/Video capture

Mapigano baina ya vikundi vya waasi na serikali vya muda mrefu sasa yamepungua kutokana na jitihada za wadau wa kimataifa kusaidia nchi hiyo kurejesha tena amani. Baada ya miongo na miongo ya mateso na madhila ya vita hivyo, nuru ya amani inaangazia jimbo hilo na katika makala ifuatayo Amina Hassan anakupeleka huko kuangazia jinsi watu [...]

28/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Rehani na Dhamana

Kusikiliza / Neno la wiki: Rehani na Dhamana

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Rehani” na “Dhamana” Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Tukianza na Rehani, Bwana Zuberi anasema ukiwa na kitu ambacho unakipenda sana na unahitaji kukiweka rehani ili upate kitu kingine unachohitaji [...]

28/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

UM wahofia ghasia zaidi Venezuela

Kusikiliza / Bi. Liz Throssell, msemaji wa Ofisi ya UNHCR. Picha: UM/Video capture

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imesema inahofia ghasia zaidi nchini Venezuela, ambako uchaguzi wa bunge ulioitishwa na rais Nicolas Maduro unatarajiwa kufanyika Jumapili. Matakwa ya watu wa Venezuela kushiriki katika uchaguzi huo ama la ni lazima yaheshimiwe imesema ofisi hiyo, na kuongeza kuwa mtu yeyote asishinikizwe kupiga kura huku walio [...]

28/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ingawa mashambulizi yamepungua, albino bado wanaishi kwa hofu vijijini:Ero

Kusikiliza / Mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi , Ikponoswa Ero (Kushoto). Picha: UNIC/Tanzania

Watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino katika ameneo ya vijijini nchini Tanzania bado wanaendelea kuishi kwa hofu wakati hulka ya kutaka kuwashambulia ikienea amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi akihitimisha ziara yake nchini humo. Ikponwosa Ero, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es [...]

28/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita dhidi ya homa ya ini bado ni safari ndefu-WHO

Kusikiliza / Vita dhidi ya homa ya ini. Picha: WHO

Takwimu kutoka nchi 28 zinazobeba takriban asilimia 70 ya mzigo wa ugonjwa wa homa ya ini au Hepataitis zinaonyesha hatua zimepigwa katika kutokomeza ugonjwa huo. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya Ulimwenguni, WHO katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani mwaka huu kauli mbiu ikiwa "Tokemeza homa ya [...]

28/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame watishia hali ya utulivu mjini Lafon, Sudan Kusini

Kusikiliza / Wenyeji qa Lafon, Sudan Kusini. Picha: UM/Video capture

Madhila ya watu nchini Sudan Kusini kufuatia ukame unaoikumba nchi hiyo ni muhimu yatatuliwe kwani huenda yakatishia amani inayoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ikiwemo kaunti ya Lafon. Kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS eneo hilo ni tulivu lakini hali ya kutegemea zao moja kwa kilimo limesababisha  hali kuwa mbaya [...]

27/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na wadau waongeza kasi ya kudhibiti mlipuko wa surua Somalia

Kusikiliza / Watoto wawili waathirika wa ugonjwa wa surua katika wodi moja wa hospitali wa Kismayo huko Kismayo, Somalia.Picha: UNICEF Somalia/2016/Rich

Somalia inakabiliwa na mlipuko mbaya kabisa wa surua katika kipindi cha miaka minne , limesema leo shirika la afya duniani WHO. Ukame na tishio la baa la njaa ukiongezea na kiwango kidogo cha chanjo vimewaacha mamilioni ya watoto Somalia wakiwa dhaifu, wakikabiliwa na njaa na hususani hatari ya kukumbwa na mlipuko wa surua na maradhi [...]

27/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vanuatu kutumia drones kufikisha chanjo vijijini:UNICEF

Kusikiliza / Matumizi ya Drones kisiwani Vanuata. Picha: UNICEF

Serikali ya Vanuatu imesema itaaanza majaribio ya kutumia ndege zisizo na rubani au drones kufikisha chanjo za kuokoa maisha katika jamii za vijijini kwenye kisiwa hicho. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limethibitisha taarifa hizo leo na kusema ndege hizo zisizo na rubani zitajaribiwa kwa mara ya kwanza katika kisiwa hicho cha [...]

27/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia takriban 50,000 wakwama Raqqa-Mueller

Kusikiliza / Wanawake, wanaume na watoto wapoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya ISIL. Picha: UM

Takriban raia 50,000 bado wamekwama katika eneo la Raqqa lililokuwa likidhibitiwa na kundi la kigaidi la Daesh, au ISIL, bila njia yoyote ya kujinasua. Hayo yameelezwa na naibu msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu uratibu wa masuala ya kibinadamu (OCHA), alipohutubia baraza la usalama hii leo kuhusu hali nchini Syria. Bi Ursula Mueller akizungunmza kwa niaba [...]

27/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres akaribisha kutatuliwa mvutano Jerusalem

Kusikiliza / Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Manuel Elias

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha habari za kutatuliwa kwa mvutano kwenye mji wa kale wa Jerusalem kwa kuzingatia hadhi ya maeneo matakatifu iliyowekwa kabla ya Julai 14. Kupitia taarifa ya msemaji wake , Katibu Mkuu amesema anatumai kwamba majadiliano yataendelea na kuchangia kuweka mazingira ya uaminifu miongoni mwa jamii katika eneo [...]

27/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ajali ya helikopta yakatili maisha ya walinda amani wawili Mali

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix.(Picha:UM/Sylvain Liechti)

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix, amesikitishwa na taarifa za kuanguka kwa helikopta Jumatano karibu na Tabankort, eneo la Gao Kaskazini mwa Mali. Kwa mujibu wa taarifa, ajali hiyo iliyosababisha vifo vya walinda amani wawili kutoka Ujerumani ilitokea wakati wakifanya upelelezi Tabankort kufuatia mashambulizi kati ya vikundi viwili [...]

27/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamanda Cheka ajisalimisha DRC, UM wakaribisha

Kusikiliza / Sheka_accountabilitynew 1

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo bi Pramila Patten, ambaye anazuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, amekaribisha kujisalimisha hii leo kukikokuwa kukisubiriwa kwa muda mrefu kwa kamanda na mbabe wa kivita Ntabo Ntaberi Cheka. Cheka aliyejisalimisha kwa mpango wa Umoja wa mataifa nchini DRC, MONUSCO [...]

27/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yatoa muongozo mpya kuzisaidia nchi kufuatilia maliasili ya misitu

Kusikiliza / FAO limetoa muongozo mpya ya kuanzisha mfumo imara wa kitaifa ambao ni muhimu katika kupima hatua zilizopigwa kwenye mchakato wa kutimza SDGs katika suala la misitu. Picha: FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limetoa muongozo mpya wenye lengo la kuzisaidia nchi kuanzisha mfumo imara wa kitaifa ambao ni muhimu katika kupima hatua zilizopigwa kwenye mchakato wa kutimza malengo ya maendeleo endelevu, SDG's katika suala la misitu. Kwa mujibu wa FAO ili kutimiza ahadi zao chini ya mkataba wa [...]

27/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amina Mohammed na Rais Kabila wajadili nafasi ya mwanamke DRC

Kusikiliza / arriv+¬e +á Kinshsa le 24 07 B2017 (9)

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amehitimisha ziara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC alikopata fursa ya kuzungumza na serikali, wanawake, wakimbizi na wadau wengine. Grace Kaneiya na taarifa zaidi. (TAARIFA YA GRACE) Baada ya kukutana na wanwake na asasi za kiraia Bi Mohammed alikutana na Rais Joseph Kabila wa nchi [...]

27/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia lazima ijitahidi kulinda na kuhifadhi mikoko:UNESCO

Kusikiliza / Msitu wa Mikoko. Picha: UNESCO

Dunia inahitaji kufanya juhudi zaidi kulinda na kuhifadhi mikoko ya pwani ambayo ni miongoni mwa maliasili iliyohatarini duniani. Wito huo uliotolewa leo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO . UNESCO imetoa wito huo katika siku ya kimataifa ya uhifadhi wa mfumo wa mikoko inayoadhimishwa kila mwaka [...]

26/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kufungwa soko la London kutaathiri maisha ya kijamii:wataalam wa UM

Kusikiliza / Logo. Picha: OHCHR

Mipango ya kufunga soko la London kama sehemu ya mradi wa kuboresha maeneo duni inatishia maisha ya kijamii, limeonya leo kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Wataalamu hao wameongeza kuwa hatua hiyo pia itasababisha kutimuliwa kwa wakazi na wamiliki wa maduka katika maeneo hayo wanaoishi na kufanyia kazi. Soko hilo [...]

26/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vijana Uganda wakiwezeshwa ,wanajiweza

Kusikiliza / Vijana na ukulima. Picha: UM/Harandane Dicko

Kama zilizovyo nchi nyingi barani Afrika tatizo la ajira kwa vijana Uganda limekuwa donda ndugu, na fikra za kumaliza masomo na kuajiriwa zimesalia kuwa hadhithi za abunuwasi. Sasa vijana hao wametambua ili kujikimu sio lazima wategemee kuajiriwa bali kujiajiri kwa njia mbalimbali. Na hilo sio tu litawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuinua pato la taifa bali [...]

26/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaomba dola milioni 9.5 kusaidia watu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Kusikiliza / Magdelena, mkimbizi wa Nigeria mwenye umri wa miaka 35, na mtoto wake Musa mwenye umri wa wiki mbili tu warejea nchini Nigeria kutoka Cameoon. 
 Picha: UNHCR/Rahima Gambo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limezindua ombi la msaada kwa ajili ya kuongeza shughuli zake Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Shirika hilo linasema linahitaji dola milioni 9.5 zaidi kwa sababu ya kujerea kusikotarajiwa kwa wakimbizi wa Nigeria tangu mwanzo wa mwaka na wengi wa wakimbizi hao wanarejea kutoka Cameroon. Kwa mujibu wa [...]

26/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Juhudi za pamoja zinahitajika kutatua mzozo wa kisiasa Burundi-Kafando

Kusikiliza / Mjumbe maalumu wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Burundi Michel Kafando.(Picha:UM/Eric Kanalstein)

Juhudi zote ambazo zinaelekezwa kwa ajili ya kutatua mzozo wa kisiasa nchini Burundi lazima zishirikishe viongozi barani Afrika na hususan walioko katika ukanda huo. Hiyo ni kwa mujibu wa Mjumbe maalumu wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Burundi Michel Kafando akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Burundi. Bwana Kafando amesema [...]

26/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa kipindupindu Yemen; ni janga juu ya janga-UM

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wakipea matibabu watoto waaathirika wa ugonjwa wa kipindupindu. Picha: UNHCR/John Wessels

Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezuru Yemen kwa ajili ya kutathmini hali halisi ya janga la kibinadamu nchini humo na kuimarisha juhudi za pamoja kwa ajili ya kusaidi wananachi wa taifa hilo. Wakuu hao wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, la mpango wa chakula duniani, WFP na Shirika la [...]

26/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid ateua tume kutathimini hali ya Kasai DRC

Kusikiliza / Bernard, mkimbizi wa ndani mwenye umri wa miaka 25 anaketi chini kwenye kituo cha afya nchini DRC na watoto wake wawili wa kiume. Picha: UNHCR/John Wessels

Wakati baraza la usalama limekutana hii leo kujadili hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC kamishina Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein ametangaza uteuzi wa Bacre Ndiaye kutoka Senegal, Luc Côté kutoka Canada, na Fatimata M'Baye kutoka Mauritania kama jopo la kimataifa la wataalamu kutathimini hali ya Kasai nchini Jamhuri ya [...]

26/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauji ya walinda amani wengine wawili CAR yalaaniwa:UM

Kusikiliza / Walinda amani wa UM nchini CAR wanapiga Doria. Picha: MINUSCA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amelaani vikali mauaji ya walinda amani wengine wawili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. Mauji hayo ya walinda amani kutoka Morocco wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini CAR , MINUSCA yaliyotokea jana mjini Bangassou yanafanya idadi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliouawa [...]

26/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria yatokana na maendeleo duni: UNDP

Kusikiliza / Wanafunzi darasani kabla washambuliwe na kunaswa na Boko Haram. Picha: UNICEF/Video capture

Matatizo ya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kimsingi yanatokana na changamoto za maendeleo duni zilizochangiwa na uasi wa kundi la kigaidi la Boko Haram ambao umesababisha mgogoro wa kiwango cha kimataifa. Huo ni mtazamo wa mwakilishi na mratibu mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Nigeria , Edward Kallon. Karibu [...]

26/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto 1 kati ya 2 wanaokimbia Afrika hawataki kwenda Ulaya:UNICEF

Kusikiliza / Italy. Rescue at sea

Watoto wengi walio safarini kutoka Libya kwenda Italia wamekimbia machafuko na hawakutaka kwenda Ulaya walipoondoka makwao umesema leo Umoja wa Mataifa. Libya kwa muda mrefu imekuwa sumaku ya kuwanasa wahamiaji wanaotafuta kazi , lakini megene ya wasafirishaji haramu wa binadamu yameshika hatamu tangu kuenguliwa kwa Rais Muammar Ghadaffi 2011. Shirika la Umoja wa mataiofa la [...]

25/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko Jerusalem yana athari zaidi ya Mashariki ya Kati:Mladenov

Kusikiliza / Mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani Mashariki ya Katim, Nicholay Mladenov. Picha: UM/Loey Felipe (maktaba)

Machafuko yanayoendelea kwenye mji wa kale wa Jerusalem yana athari kubwa sio kwa Israel au Palestina pekee bali ni kwa dunia nzima. Hayo yamesemwa na mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati bwana Nickolay Mladenov katika mjadala maalumu kuhusu hali ya Mashariki ya Kati uliofanyika leo kwenye baraza [...]

25/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tanzania tumefanikiwa katika ukaguzi wa hesabu za serikali-Profesa Assad

Kusikiliza / Profesa Mussa Assad. Picha:UNNewsKiswahili

Tanzania imepiga hatua kubwa na kupata mafanikio katika zoezi la ukaguzi wa hesabu za serikali. Kauli hiyo imetolewa na Profesa Mussa Assad mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali wa Tanzania aliyeko hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhuduria mkutano unaotathimini ukaguzi wa hesabu za serikali na utekelezaji wa malengo ya maendeleo [...]

25/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yazinduaa mkakati mpya Tanzania kwa ajili ya SDG's

Kusikiliza / Hadija akivuna maharage katika shamba lake la acre moja nchini Tanzania. Picha:WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limezindua mkakati wa miaka mine wa kitaifa nchini Tanzania (CSP). Mkakati huo unakwenda sanjari na ajenda ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu kwa lengo la kutokomeza umasikini, kupunguza pengo la kutokuwepo usawa, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha [...]

25/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Amani na demokrasia ndio misingi ya kujenga upya DRC-Amina

Kusikiliza / Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed DRC. Picha: Twitter/Amina J.Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina J. Mohammed yuko ziarani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC kama sehemu ya ziara yake Afrika. John Kibego na taarifa kamili. (TAARIFA YA JOHN) Bi Mohammed akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano na wanawake viongozi amesema uwepo wake nchini humo ni kiashiria cha [...]

25/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kushambulia watu waliokimbia vita ni ukatili usiokubalika:Guterres

Kusikiliza / Picha:WFP Niger/Vigno Hounkanli,

Vitendo vya kigaidi vya kuwalenga watu ambao tayari wameshazikimbia nyumba zao kutokana na machafuko ya Boko Haram ni ukatili usiokubalika. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akilaani vikali mashambulizi ya kujitoa muhanga yaliyotokea jana katika kambi mbili za wakimbizi wa ndani karibu na Maiduguri , jimbo la Borno, nchini [...]

25/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Suala la mazingira ni kipengele muhimu, utekelezaji wa SDGs- UNEP

Kusikiliza / Nchini Iraq.(Picha: Hassan Partow/UNEP)

Uhusiano kati ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na mazingira ni dhahiri na hivyo ili kufikia malengo hayo lazima suala la mazingira litiliwe maanani, amesema Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Ibrahim Thiaw. Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, bwana Thiaw [Chow] amesema [...]

25/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ulengaji wa makusudi wa raia katika mashambulizi ni ukiukaji wa haki:Guterres

Kusikiliza / Picha:UNHCR/Ivor Prickett (file)

Ulengaji wa makusudi wa raia katika mashambulizi ni ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa ambao unahesabiwa kama uhalifu wa kivita. Hayo yamo katika taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kulaani vikali shambulio la kigaidi la kujitoa muhanga lililotokea leo nchini Afghanistan. Katika taarifa hiyo iliyowasilishwa na msemaji wake, Antonio [...]

24/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Australia ikomeshe usajili wa wahamiaji pwani-UNHCR

Kusikiliza / Picha:UNHCR/N. Wright

Kamishina Mkuu wa Wakimbizi, Filippo Grandi, ametoa taarifa isemayo sera ya Australia ya usajili kwenye pwani ya Papua New Guinea na Nauru, ambayo inawanyima fursa ya hifadhi nchini Australia wakimbizi wanaowasili kwa njia ya bahari bila visa, kwa muda mrefu imesababisha madhila makubwa yanayoweza kuizuilika. Ameongeza kuwa kwa miaka mine sasa zaidi ya watu 2000 [...]

24/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahusika wa shambulio la kigaidi Lahore wawajibishwe:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM/Evan Schneider

Wahusika wa shambulio la kigaidi lililofanyika leo mjini Lahore, Pakistan lazima wawajibishwe. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa ya msemaji wake akilaani vikali shambulio hilo. Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na kuwatakia ahuweni ya haraka wajeruhi. Takribani watu 26 wameuawa katika shambulio [...]

24/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kutumia biogesi kupikia ni faraja kwa wakazi, Yatta Kenya

Kusikiliza / biogas 2

Matumizi ya biogesi iliotengenezwa kutokana na kinyesi cha wanyama na taka za nyumbani yanaboresha maisha hususan ya wanawake ambao hutumia hadi saa tatu kila siku kusaka kuni. Mbinu hii inayojali mazingira na kuzuia kero itokanayo na matumizi ya kuni kupikia imeleta faraja kwa wakazi katika wilaya ya Yatta nchini Kenya. Kufahamu zaidi basi ungana na [...]

24/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama na haki za binadamu inaendelea kudorora Mynmar- Mtaalam

Kusikiliza / Picha:UNHCR /S. Kritsanavarin

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu ametoa ripoti inayoshtumu serikali ya Mynmar kuendeleza sera zinazofanana na zile za serikali ya kijeshi ya awali na kudumisha hali mbaya zaidi ya kiusalama na ukiukwaji wa haki za binadamu. Yanghee Lee akitoa ripoti yake kufuatia ziara ya siku kumi na mbili nchini Mynmar ameelezea [...]

24/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 20 wauawa katika shambulio, UNAMA yalaani vikali

Kusikiliza / 05-14-unama-kabul

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, umelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga lililotokea leo mjini Kabul, wakati nchi nzima ikiwa katika hali ya taharuki kutokana namachafuko yanayoathiri raia kwa kiasi kikubwa. Shambulio hilo la leo asubuhi limekuja wakati watu wakiadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja ya shambulio la 23 Julai 2016 kwenye uwanja wa [...]

24/07/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Nini mchango wa wahamiaji wa ughaibuni kwa SDG's:IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wakisubiri kupanda kivuko huko Ugiriki. (Picha:UNHCR/Socrates Baltagianis)

Wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa , mashirika ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia, wahamiaji na viongozi wa wahamiaji ughaibuni wanakutana hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo na kesho kujadili suala la wahamiaji. Amina Hassan na taarifa kamili (TAARIFA YA AMINA) Majadiliano hayo ni ya nne ya mchakato wa nchi [...]

24/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani mauaji ya mlinda amani wa MINUSCA:

Kusikiliza / MINUSCA_CentralAfrica

Mauaji ya mlinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, yaliyotokea jumapili yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Guterres amesema mauaji hayo yanashukiwa kufanywa na mwanamgambo wa anti-Balaka mjini Bangassou, Kusini Mashariki mwa CAR ambapo watu wengine [...]

24/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhusiano mzuri kati ya Eritrea na UM, ni faida kwa wananchi

Kusikiliza / John Ging ni mkurugenzi wa idara ya operesheni OCHA.(Picha:UM/Manuel Elias)

Mkataba wa miaka mitano kuanzia mwaka huu wa 2017 hadi 2021 kati ya Umoja wa Mataifa na uongozi wa Eritrea unalenga kuimarisha hali ya kibindamu nchini humo. Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa operesheni katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA John Ging amesema hii ni ishara [...]

24/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Visa vya kipindupindu Yemen vinatarajiwa kuongezeka na kufika 600,000

Kusikiliza / Watoa huduma wa afya wakihudumia mgonjwa nchini Yemen.(Picha:WHO)

Rais wa chama cha msalaba mwekundu ICRC,  Peter Maurer yuko katika ziara ya siku tano nchini Yemen wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na viwango vya juu vya mlipuko wa kipindupindu huku idadi ya waathirika ikipanda kila siku. Kwa mujibu wa ICRC idadi ya visa vya kipindupindu vinatarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwisho wa mwaka 2017 [...]

23/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani vifo vya Wapalestina watatu Jerusalem

Kusikiliza / Guterres4

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vifo vya Wapalestina watatu vilivyotolea leo kwenye makabiliano na wanajeshi wa usalama wa Israel , na kutoa wito wa matukioa hayo kuchunguzwa. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake , Guterres amesema fikra na sala zake ziko pamoja na familia za waathirika. Katibu Mkuu ameongeza kuwa anatiwa [...]

21/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa kibinadamu DRC wafurutu ada:O'Brien

Kusikiliza / Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa UM, bwana Stephen O'Brien akizungumza na baadhi ya wakimbizi wa ndani waathirika wa machafuko nchini DRC. Picha na OCHA/Yvon Edoumou

Kumekuwa na ongezeko kubwa la mgogoro wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa mtaratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Stephen O’Brien. Ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya siku nnne nchini DRC na kutoa wito kwa dunia kutoisahau nchi hiyo ambayo sasa ina idadi kubwa kabisa ya [...]

21/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji vigori wa Nigeria wanakabiliwa na unyanyasaji wa kingono Italia-IOM

Kusikiliza / Mfanyakazi wa IOM akikutana na mhamiaji.(Picha:IOM/2017)

Kuna ongezeko kubwa na wahamiaji wasichana vigori wanaowasili Ulaya sanjari na ongezeko la ukatili wa kingono unaohusishwa na uhalifu wa kupangwa. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita shirika hilo linasema limeshuhudia karibu ongezeko la asilimia 600 [...]

21/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tathimini ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo endelevu Afrika Mashariki

Kusikiliza / Wawakilishi kwenye mkutano wa kutathimini utekelezaji wa SDGs kutoka Kenya na Tanzania.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/G.Kaneiya)

Mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs umefunga pazia wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani. Mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu "tokomeza umaskini na chagiza maendeleo katika dunia inayobadiliki" umejikita katika kuangalia juhudi [...]

21/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Papa Francis atoa mchango kwa FAO kusaidia watu wanaokabiliwa na njaa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Papa Francis. Picha:UN Photo/Eskinder Debebe

Katika hatua isiyo ya kawaida, papa mtakatifu Francis ametoa mchango wa euro 25,000 kwa ajili ya mipango ya Shirika la kilimo na chakula duniani FAO wa kuwasaidia watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula na ukame Afrika Mashariki. Papa Francis amesema kwamba fedha hizo ni mchango wa mfano kwa ajili ya mradi wa FAO unaotoa pembejeo [...]

21/07/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki “Kilemba”

Kusikiliza / NenolaWiki

Neno la wiki hii ni  “KILEMBA” na mchambuzi wetu leo ni Onni Sigalla mhariri mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.

21/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Waafghanistan milioni 1 kupata haki ya kuishi Pakistan-UNHCR

Kusikiliza / Picha:UNHCR

Mipango ya Pakistan ya kuorodhesha hadi raia milioni moja wa Afghanistan wasio na nyaraka za kuishi nchini Pakistan itatoa afuweni kubwa inayohitajika kwa wakimbizi wengi ambao hawawezi kurejea nyumbani kutokana na sababu za kiusalama umesema leo Umoja wa Mataifa. Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR , limekaribisha mradi huo wa Pakistan ambao [...]

21/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Albino wamekosa nini hata wanyanyapaliwe na kuuawa?:Nyapinyapi

Kusikiliza / Azizi Kimindu Nyapinyapi. Picha:Kiswahili Unit

Watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino wamekosa nini hata wakatwe, viungo hata kuuwawa ? anahoji mwanamuziki wa Tanzania Azizi Kimindu Nyapinyapi katika kibao alichokitoa mahsusi kuelimisha jamii dhidi ya ukatili na mauaji ya watu hao. Kufahamu zaidi kwa nini aliamua kutunga kibao hico na wito wake kwa jamii ungana na Flora Nducha na mwanamuziki [...]

21/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen inakabiliwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu- WHO

Kusikiliza / Mtoto anahudumiwa katika hospitali ya Sab'een huko Sana'a nchini Yemen. Ni mmoja wa watoto waathirika wa kipindupindu. Picha: © UNICEF/UN065873/Alzekri

Yemen inakabiliwa na mlipuko mkubwa zaidi wa kipindupindu kuwahi kushuhudiwa duniani huku kukiwa na visa 368,207 vinvyoshukiwa na vifo 1,828 vilivyoripotiwa tangu Aprili 27 mwaka 2017. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Kwa mujibu wa Shirika la afya ulimwenguni WHO, kila siku waYemeni 5,000 zaidi wanaugua ugonjwa wa kuhara au kipindupindu, huku watoto [...]

21/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lacroix azuru Darfur Sudan:UNAMID

Kusikiliza / Picha:UNAMID

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix leo amewasili El Fasher mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan kwa ajili ya ziara ya siku mbili. Ziara yake imekuja wakati ambapo kuna mipango ya kufanya mabadiliko katika mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa [...]

21/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Je! Wahalifu dhidi ya Albino Tanzania wamehamia kwingine?

Kusikiliza / Mtaaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero. Picha: OHCHR/Christine Wambaa

Ingawa visa vya mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania vinashuka, na hiyo ni habari njema, cha kushangaza ni kuwa visa hivyo vimepanda zaidi nchini Malawi na Msumbiji na sababu yake haijulikani. Hilo ni kwa mujibu wa mtaaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero, ambaye amealikwa kuzuru [...]

21/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ili kufikia SDGs ni lazimwa kuwekeza kwa wanawake- Amina Mohammed

Kusikiliza / Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akizungumza na waandishi wa habari nchini Nigeria ambako ameandamana na viongozi mbali mbali.(Picha:UM/Lulu Gao)

Haitowezekana kufikia malengo ya maendeleo endelevu bila kuwekeza kwa wanawake, amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ambaye anazuru Nigeria na pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Bi. Amina ambaye anaongoza ujumbe katika ziara hiyo ya aina yake ameandamana na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na [...]

20/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ninatiwa hofu na ongezeko la mvutano Jerusalem: Mladenov

Kusikiliza / Mratibu maalumu wa UM kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov. (Picha:UM/Eskinder Debebe)

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati leo amesema kwamba anatiwa hofu na kuongezeka kwa mvutano katika maeneo matakatifu ya mji wa kale wa Jerusalem. Nickolay Mladenov ametoa taarifa akikaribisha hatua ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ya kujizuia na kuheshimu hadhi ya maeneo matakatifu ya mji [...]

20/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukame DPRK waathiri uzalishaji wa chakula:FAO

Kusikiliza / Picha:FAO

Uzalishaji wa chakula nchini Jamhuri ya watu wa Korea au DPRK umeathirika pakubwa na ukame mbaya kuwahi kuikumba nchini hiyo tangu mwaka 2001, limesema leo shirika la chakula na kilimo (FAO). Mvua katika maeneo muhimu ya uzalishaji wa chakula DPRK iliyonyesha chini ya kiwango kuanzia mwezi April hadi Juni mwaka huu imevuruga msimu wa upanzi [...]

20/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya watoto Zanzibar ni msingi mzuri wa kumsaidia mtoto

Kusikiliza / Picha:UNICEF/2014/Holt

Zanzibar-Tanzania hatua kubwa imepigwa katika ulinzi wa watoto baada ya kufungua mahakama tatu mpya kwa ajili ya kuwalinda watoto na haki zao, mahakama ambazo zinatumika kusikiliza na kutoa hukumu za kesi zinazowahusu watoto chini ya umri wa miaka 18. Bi. Nyezuma Simai Issa, Afisa Hifadhi ya Mtoto katika Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii, [...]

20/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mizozo yapandisha bei za vyakula: WFP

Kusikiliza / Picha:WFP

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP, imesema mizozo,  misukosuko na mifumo duni ya chakula ni kiini cha kupanda kwa gharama za chakula, wakati huu ambapo mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka. Kwa mfano, WFP, yenyewe inasema imeshuhudia kupanada kwa gharama zake za chakula  kutoka dola bilioni 2.2 kaitka mwaka [...]

20/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yaangaza kwa MSMEs kufuatia uzinduzi wa programu ya UNCTAD Kenya

Kusikiliza / Mfanya biashara nchini Kenya.(Picha:World Bank/Video Capture)

Kenya inatarajiwa kujiunga na programu ya Umoja wa Mataifa ambayo inasaidia kujenga uwezo wa ujasiriamali kwa ajili ya kuwezesha biashara ndogo ndogo kote ulimwenguni, Empretec. Programu hiyo ambayo imezinduliwa leo nchini Kenya kwa ushirikiano wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD na wizara ya viwanda, biashara na vyama vya ushirika Kenya, [...]

20/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa chakula uliosahaulika DRC wahitaji kutupiwa jicho:FAO

Kusikiliza / Wakimbizi nchini DRC. Picha:PAM RDC‏ @PAMRDC

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kutosahau mamilioni ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao walikimbia vita na sasa wanakabiliwa na njaa. Ombi hilo limetolewa na afisa wa tathimini ya mgogoro wa chakula wa shirika la chakula na kilimo (FAO), Luca Russo. Amesema watu milioni sita raia wa DRC wako ukimbizini au wanaishi katika [...]

20/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzani uko juu katika mapambano dhidi ya VVU japo watu muhimu bado wako hatarini

Kusikiliza / Ukimwi haujaisha bado limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya ukimwi UNAIDS: Picha na UNAIDS.

Hatua kubwa imefikiwa katika vita dhidi ya virusi vya HIV kwa mujibu wa wataalamu wa afya wa Umoja wa Mataifa ambao wanasema zaidi ya nusu ya watu wote wanaougua ukimwi sasa wana fursa ya matibabu. Tangazo lililotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya ukimwi UNAIDS lina takwimu mpya zinazoonyesha kwamba takribani watu [...]

20/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajira kwa vijana bado ni chagamoto nchini Burundi

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Sebastian Villar

Moja ya changamoto kubwa inayowakumba vijana wengi duniani ni ukosefu wa ajira. Nchini Burundi, asilimia takriban 22 ya vijana waliohitimu vyuo vikuu hawajapata ajira. Kwa mujibu wa Serikali ukosefu wa kazi ni tishio kubwa kwa ustawi wa jamii nchini humo. Baadhi ya mashirika ya kiraia nchini Burundi yameanza kuwahamasisha vijana na kuwaelekeza jinsi ya kubuni [...]

19/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa lazima ihakikishe hakuna mtu wa LDC's anayesalia nyuma:

Kusikiliza / Fekitamoeloa Katoa Utoikamanu. Picha:UN/Photo:/Devra Berkowitz

Watu kutoka mataifa yenye maendeleo duni au LDC's wengi hawajiwezi , masikini na wako katika hatari ya kuachwa nyuma na treni ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG's ifikapo mwaka 2030. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New york Marekani leo, kuhusu uzinduzi wa ripoti yenye [...]

19/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zimeweka sera thabiti kulinda watu dhidi ya matumizi ya tumbaku-Ripoti, WHO

Kusikiliza / Mkurugenzi mpya mteule wa WHO akizungumza na waandishi wa habari Jumatano mjini Geneva Uswis.Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus.(Picha:UM/Daniel Johnson)

Ripoti ya Shirika la afya ulimwenguni, WHO kuhusu janga la tumbaku 2017, imebaini kuwa nchi nyingi zimeweka sera za kukabiliana na matumizi ya tumbaku iwe ni maandishi yanyopatikana katika makasha ya bidhaa hizo, marufuku ya matangazo au udhibiti wa maeneo ya kuvuta sigara. Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo watu bilioni 4.7 ambao ni [...]

19/07/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 316 warejeshwa Somalia kwa msaada wa IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Baada ya karibu miezi 5 ya kusubiri, wahamiaji 316 wa Kisomali wamerejea nyumbani kupitia Bahari ya Arabia wakisaidiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji , IOM katika kipindi cha siku nne zilizopita. Mnamo Februari mwaka huu, boti ya walanguzi iliokuwa imebeba Wasomali 150 ililipitia kweye Pwani ya Yemen ikielekea Ulaya. Kwa bahati mbaya [...]

19/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tubadili mtazamo na kubaini mizizi ya migogoro Afrika:Guterres

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Manuel Elias)

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kubadili mtazamo wake kuhusu bara ka Afrika na kuanzisha ushirika wa ngazi ya juu ambao utatambua uwezo na ahadi kubwa za bara hilo. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA YA AMINA) Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo kwenye mjadala maalumu wa baraza la usalama [...]

19/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulaya yaongeza msaada kupambana na utapiamlo Niger-WFP

Kusikiliza / Picha:OCHA/Franck Kuwonu

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limekaribisha mchango wa dola milioni 4.5 kutoka kwa tume ya Ulaya ambao utasaidia kuongeza ubora na upatikanaji wa chakula nchini Niger ambako takribani watoto milioni mbili wana utapia mlo. Fedha hizo kutoka tume ya Ulaya na ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo (DEVCO) itairuhusu [...]

19/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 11 zatolewa na Marekani kupambana na njaa CAR

Kusikiliza / Picha:WFP

Serikali ya Marekani imetoa dola milioni 11 zitakazowasaidia watu zaidi ya laki tano nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kupambana na tatizo la njaa linaloongezeka wakati machafuko mapya yakizuka. Likikaribisha mchango huo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema fedha hizo zilizotolewa na USAID, zaitaisaidia WFP kusaidia watu laki [...]

19/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

SDG's ni muhimu sana kwa FAO na mustakhbali wa dunia:Semedo

Kusikiliza / Naibu Mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO, Bi Maria Semedo. Picha na FAO.

Malengo yote ya maendeleo endelevu ni muhimu sana kwa shirika la chakula na kilimo FAO, lakini yanayopewa kipaumbele zaidi ni leongo nambari 1 kutokomeza umasikini, 2, kumaliza njaa, 13 la mabadiliko ya tabia nchi , 14 masuala ya viumbe baharini na namba 15 linalohusu maisha nchi kavu hasa bayoanuai. Hayo yamesemwa na Maria Helena Semedo [...]

19/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni muhimu kuendelea kuisaidia Haiti ikijiweka sawa: MINUSTAH

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Haiti MINUSTAH, Bi Sandra Honeree akiwasilisha taarifa kwenye varaza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu tathimini ya Haiti.

Msaada wa kimataifa kwa Haiti utakuwa muhimu sana wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea kukamilisha ufungaji wa mpango wake nchini humo ,amesema afisa wa ngazi ya juu wa mpango huo kwenye baraza la usalama hii leo. Sandra Honoré mkuu wa MINUSTAH, amesema mpango huo utafunga mlango wake kabisa mwezi Oktoba mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa [...]

18/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kutengeneza mkaa kupitia taka za minazi waleta nuru Mombasa, Kenya

Kusikiliza / Picha:Kencoco

Tuzo ya SEED inatolewa kila mwaka kwa miradi inayochagiza maendeleo endelevu na inayojali mazingira. Tuzo hiyo inatolewa kwa miradi bunifu katika nchi zinazoendelea ambayo ina uwezo wa kubadili maisha katika juhudi za kutokomeza umaskini na kuhifadhi mazingira. Mmoja wa washindi wa mwaka huu ni Shukry Said Twahir kutoka kampuni ya Kencoco ya Kenya, ambaye amehojiwa [...]

18/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mvua zaleta matumaini kwa wakulima wa Syria:FAO/WFP

Kusikiliza / Mjini Aleppo. wakimbizi warejea nyumbani. Picha: © UNHCR/Hameed Marouf

Uhakika wa chakula katika baadhi ya sehemu nchini Syria umeimarika kiasi ulilinganisha na wakati kama huu mwaka jana kutokana na kuimarika kwa usalama , mvua na kuwezesha kupatikana kwa fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu , lakini hali ya ujumla nchini humo bado ni mbaya zaidi kuliko kabla ya vita , yameonya leo mashirika mawili [...]

18/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 420 zahitajika kunusuru hali mbaya katika pwani za Libya

Kusikiliza / Wakimbizi wanalala katika chumba kimoja kizuizini huko Tripoli's Tariq al-Sikka. Picha: UNHCR/Iason Foounten

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema leo kuwa juhudi zaidi zinahitajika kukabiliana na maafa makubwa yanayotokana na safari za wakimbizi na wahamiaji katika pwani za Libya. Mjumbe Maalum wa UNHCR kuhusu hali kwenye Mediterenia ya Kati, Vincent Cochetel amewaambia waandishi wa habari jjini Geneva, Uswisi kwamba, watu 2,360 wamepoteza maisha yao [...]

18/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Unyongaji Libya lazima uchunguzwe:UM

Kusikiliza / Picha: OHCHR

Ripoti zinaonyesha kwamba washukiwa wa ugaidi wananyongwa na majeshi yanayohusiana na jeshi la taifa la Libya (LNA) lazima zifanyiwe uchunguzi huru umesema Umoja wa Mataifa leo. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa wito huo baada ya video kuonekana kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mahabusu wakipigwa riasi wakiwa wamepiga magoti na mikono [...]

18/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya watoto waongezeka CAR-UNICEF

Kusikiliza / Watoto nchini CAR waliosambaratishwa na vita na kuhitaji msaada wa haraka. Picha: WFP/Alexis Masciarelli

Visa vya ukatili dhidi ya watoto, ikiwemo ubakaji, kutekwa nyara mauaji na kusajiliwa watoto katika vikundi vilivyojihami, vimeongezeka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), sanjari na kuzuka upya kwa mapigano,  limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, kama atavyotujuza John Kibego katika ripoti ifuatayo. (Taarifa ya John Kibego) Shirika hilo limesema [...]

18/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kumuenzi vyema Mandela sio kwa maneno bali kwa vitendo-Guterres

Kusikiliza / Picha:UNPhoto

Nelson Mandela anaendelea kuchagiza dunia kupitia mifano aliyokuwa nayo ya ujasiri , utu na juhudi zake za kupigania haki za kijamii, kitamaduni na amani. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Nattss, Nelson Mandela…… Ni Nelson Mandela akizungumza alipohutubia baraza kuu Oktoba 3 , 1994 kama Rais wa kwanza kutoka Afrika Kusini kufanya hivyo [...]

18/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekelezaji wa SDGs Kenya unatia matumaini licha ya mapungufu

Kusikiliza / Irungu Nyakera, Katibu Mtendaji, wizara ya ugatuzi na mipango ya Kenya.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/G.Kaneiya)

Safari ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs licha ya kuwa ni ndefu inatia matumaini. Hiyo ni kauli ya Irungu Nyakera, Katibu Mtendaji, wizara ya ugatuzi na mipango ya Kenya alipozungumza na idhaa hii baada ya kuwasilisha ripoti ya nchi yake katika kongamano la ngazi ya juu la kisiasa linalotathimini utekelezaji wa SDGs kwenye makao [...]

18/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukombozi wa Mosoul haujamaliza changamoto zote Iraq: Kubiš

Kusikiliza / Mwakilishi wa UM nchini Iraq na mkuu wa UNAMI Bwana Kubis akihutubia baraza la usalama kuhusu hali nchini Iraq. Picha na UM

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema ukombozi wa kihistoria wa Mosul usifunike ukweli kwamba mustakhbali wa taifa hilo bado unakabiliwa na changamoto nyingi. Akihutubia baraza la usalama hii leo Ján Kubiš amesema ukombozi wa Mosul ulifanikiwa kwa juhudi kubwa za majeshi ya ukombizi ya Iraq na wadau wa kimataifa ili kuwaokoa na kuwalinda [...]

17/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wazindua mafunzo ya kitaifa ya mitaala ya mahakama Somalia

Kusikiliza / Picha:UNSOM

Serikali ya shirikisho ya Somalia kwa pamoja na Umoja wa Matafia wamezindua programu ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa sheria takriban 350 kote nchini katika juhudi za kusaidia kujenga upya mamlaka ya mahakama nchini humo. Akizindua programu hiyo, mwanasheria mkuu wa Somalia Ibrahim Idle Suleyman amesema mfululizo wa mafunzo utasaidia katika kuleta mabadiliko ya kisheria [...]

17/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yamepitisha viwango vya matumizi ya dawa zitumikazo kwa mifugo

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Hien Macline

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia matumizi ya dawa katika bidhaa za mifugo zitumikazo kama chakula na kwa mimea wamepitisha viwango vinavyodhibiti matumizi ya dawa hizo, katika mkutano uliofanyika leo huko Geneva Uswisi. Muafaka huo umefikiwa kufuatia utafiti wa pamoja wa kamati ya Shirika la chakula duniani FAO na lile la afya ulimwenguni WHO kuhusu [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Gharama za vita kwa binadamu Afghanistan ni kubwa mno:UM

Kusikiliza / Kambi ya Samar Khel karibu na Jalalabad, ambako waAghanistan wamekimbil.(Picha: Bilal Sarwary/IRIN)

Gharama za vita vya Afghanistan kwa binadamu ni kubwa mno amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo , akitaja vifo, uharibifu na madhila kwa raia. Tadamichi Yamamoto ametoa kauli hiyo kufuatia ripoti ya mpango wa Umoja wa Mataifa UNAMA na ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu iliyotolewa leo. Ripoti imebaini [...]

17/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kazi ya kulinda amani si lele mama

Kusikiliza / Meja Cheche. Picha:UNMISS

Kazi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa si lele mama, mbali ya changamoto inatoa fursa pia kwa walinda amani hao kujifuinza mambo mengi kutoka kwa nchi na watu wanaowahudhumia. Lakini kikubwa zaidi kinawapa fursa ya kuthamini uhuru na kuishi kwa amani na usalama katika nchi watokako. Basi kwa undani zaidi ungana na Flora Nducha [...]

17/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto 1 kati ya 10 hakupata chanjo 2016 duniani

Kusikiliza / Picha: WHO

Kote ulimwenguni watoto milioni 12.9, sawa na mtoto mmoja kati ya kumi hawakuchanjwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya ulimwenguni WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF.Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Kwa mujibu wa mashirika hayo hii inamaanisha kwamba watoto hao walikosa dozi ya kwanza ya chanjo ya pepopunda (DTP) [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutimiza SDG's lazima kasi ya utekelezaji iongezeke:Guterres

Kusikiliza / Ripoti ya SDG's ya mwaka 2017. Picha: UN Photo

Kama dunia inataka kutokomeza umasikini, kukabili changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuwa na jamii jumuishi zenye amani kwa wote ifikapo 2030, basi wadau wote muhimu wakiwemo serikali, ni lazima waongeze kasi ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG's. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Wito huo umo katika ripoti mpya ya [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wawataka viongozi wa kisiasa kumaliza vita yei:UNMISS

Kusikiliza / Picha:UNMISS

Watoto wanaokabiliwa na madhila makubwa kutokana na vita vinavyoendelea Sudan Kusini na umasikini wamewataka viongozi wa kisiasa kurejesha amani kwenye mji wa Yei nchini humo. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS, hali ni mbaya jimboni Yei, asilimia 70 ya watu walikimbia mwaka jana baada ya machafuko kuzuka baina ya serikali [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunasonga kutokomeza umasikini Tanzania japo kuna changamoto:Mwasha

Kusikiliza / Anna Mwasha , Mkurugenzi idara ya kutokomeza umasikini katika wizara ya fedha na mipango ya Tanzania akihojia na Idhaa ya Kiswahili ya UM wa Mataifa New York.

Juhudi za kutokomeza usmasikini sanjari na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG's zinapiga hatua nchini Tanzania ingawa bado kuna changamoto kadhaa. Akizungumza na idhaa hii kandoni mwa kongamano la ngazi ya juu la kisiasa linalotathimini utekelezaji wa SDG's kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani Bi Anna Mwasha, ambaye ni [...]

17/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya ujuzi kwa vijana duniani

Kusikiliza / Picha:UNSOM

Wakati siku ya ujuzi kwa vijana ikiadhimishwa kote duniani , mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating, amesisitiza umuhimu wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi na teknolojia kwa vijana nchini Somalia. Amesema tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana Somalia ni kubwa sana na linatisha , huku kiwango cha chini cha elimu na [...]

15/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utalii wanufaisha wakaazi nchini Tanzania

Kusikiliza / Bunga la wanyama nchini Tanzania.(Picha:UM/B Wolff)

Utalii!. Idadi ya watalii wa kutoka nje ya bara la Afrika imeongezeka tangu mwaka 1995. Mfano kati ya 1995 hadi 1998 idadi imeongezeka kutoka Milioni 24 hadi takribani watalii milioni 56 kati ya mwaka 2011-2014. Takwimu za baraza la kimataifa la safari na utalii linasema idadi ya watalii wa kigeni barani Afrika inatarajiwa kuongezeka na [...]

14/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kituo cha kudumu cha kulinda amani huenda kikaanzishwa Yei-UNMISS

Kusikiliza / UNHCR yaonya kuhusu hali ya Yei Sudan Kusini. Picha: UNHCR/Video capture

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, umesema unatathmini uwezekano wa kuanzisha kituo kipya cha kudumu cha ulinzi wa amani mjini Yei ili kuwalinda vyema raia katika jimbo hilo. Eneo hilo ambalo lilikuwa mwendeshaji wa Sudan Kusini na lenye kuzungukwa na udongo wenye rutuba lilisaidia sana biashara na kuvutia kundi kubwa la watu [...]

14/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani shambulio kwenye mji wa kale wa Jerusalem

Kusikiliza / Mtazamo wa mji wa Jerusalem.(Picha:UM/ Rick Bajornas)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres amelaani vikali shambulio lililotekelezwa leo asubuhi na washambuliaji watatu kwenye mji wa kale wa Jerusalem na kusababisha vifo vya maafisa wawili wa polisi na kumjeruhi mwingine. Kupitia taarifa ya msemaji wake, Katibu Mkuu amesema tukio hilo linaweza kuchochea ghasia zaidi na amezitaka pande zote kuchukua hatua stahiki kuzuia [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yang'ara katika mahindano ya shabaha ya UNAMID Darfur

Kusikiliza / Walenga shabaha wa UNAMID kikosi cha Tanzania.(Picha:UNAMID/Luteni Selemani Semenyu)

Tanzania yaibuka kidedea katika mashindano ya kulenga shabaha yaliyofanyika huko Darfur nchini Sudan. Mashindano hayo ya walinda amani wa mpango wa pamoja na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID yalijumuisha walinda amani kutoka nchi mbalimbali mjini Nyala. Luteni Selemani Semenyu alikuwa shuhuda na kutuandalia makala hii.

14/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki- Aidha, Ama, Ima, Au

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno aidha, ama, ima na au Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Bwana Zuberi anasema aidha maanake ni vile vile, Ima kwa upande wake inamaanisha kwa vyovyote vile. Je unafahamu matumizi [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa mvua kwa misimu mitatu waleta hofu ya njaa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Mfugaji nchini Kenya na mifugo wake walionusurika kifo kufuatia ukame uliosababisha vifo vya theluthi mbili ya mifugo yake.(Picha:FAO/Tony Karumba)

Tahadhari iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO imesema ukosefu wa mvua Afrika Mashariki umeongeza njaa zaidi na kusababisha mazao kuteketea, lishe kupungua na maelfu ya mifugo kufa, wafugaji wakibeba mzigo mkubwa wa ukosefu huo wa mvua. Tahadhari hiyo imeonya kwamba mfululizo wa tatu wa ukosefu wa msimu wa [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa amani umejeruhiwa lakini unaweza kutibika-Mogae

Kusikiliza / Bwana Festus Mogae akisalimiana na wakazi wa Bentiu. (Picha:UN/JC McIlwaine)

Mwenyekiti wa tume ya pamoja ya ufuatiliaji na tathmini, (JEMC) Festus Mogae, amejibu wito wa kumtaka kujiuzulu. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Juba Sudan Kusini bwana Festus Mogae, amesema anatambua kwamba jamii haijaridhika na kazi ya JMEC, lakini ameelezea dhamira yake ya kusaidia utekelezaji wa mchakatio wa amani nchini humo. (MOGAE CUT) "Nafahamu kwamba [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhil kwa raia Kasai DRC hayana dalili ya kupungua-UNHCR

Mkimbizi wa ndani Bernard akiwa mji wa Idiofa, jimbo la Kwilu na wanae.(Picha:UNHCR/John Wessels)

Madhila kwa maelfu ya watu wanaoendelea kutawanya na machafuko katika jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hayana dalili ya kupungua limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Katika eneo hilo linaloshuhudia machafuko tangu mwishoni mwa 2016, idadi ya watu waliotawanywa UNHCR inasema sasa imefikia milioni 1.3 na [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirika imara baina ya UM na nchi wanachama ni muhimu kukomesha ukatili wa kingono:

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu msaada mashinani Atul Khare akihutubia nchi wanachama wa UM kupitia video. Picha: UM/Frédéric Fath

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo alhamisi amesisitiza umuhimu wa ushirika imara baina ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama katika kusonga mbele na juhudi za kuzuia na kushughulikia unyanyasaji wa kingono na ukatili. Bwana Atul Khare msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu msaada mashinani amesema "pamoja tumeimarisha juhudi zetu" ameuambia mkutano unaofanyika kwenye makao makuu [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dini wakaa kitako kuzuia mauaji mengine ya kimbari

Kusikiliza / Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji Mauaji ya Kimbari, Adama Dieng. Picha:UN/Photo

Viongozi wa dini ulimwenguni kote leo hii wamekusanyika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuanzisha mpango mpya wa utekelezaji wenye lengo la kuzuia mauaji mengine ya kimbari. Mpango huo ulichukua miaka miwili kuandaliwa na kuongozwa na Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji Mauaji ya Kimbari, Adama Dieng, na [...]

14/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania iko mstari sahihi, utekelezaji wa SDGs- Moshi

Kusikiliza / SDGs.(Picha:UNIC/Tanzania)

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs uko katika mstari sahihi nchini Tanzania kufuatia sera mpya zilizopo za kuhakikisha ulinzi wa mapato ya kitaifa kwa mujibu wa Celestine Moshi, mkurugenzi, idara ya ushrikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, akizungumza na Grace Kaneiya wa idhaa hii kandoni mwa mkutano wa [...]

13/07/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ujuzi wa kiuchumi wa miaka 70 ni somo kwa SDG’s

Kusikiliza / desa

Ripoti ya Kimataifa ya Kiuchumi na Kijamii ya 2017 iliyotolewa leo na idara ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA , imeweka bayana kuwa uchambuzi bado ni muhimu katika kuongoza mataifa wakati huu ambapo dunia inapitia hali ngumu ya kiuchumi na pia katika utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030. [...]

13/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Teknolojia ya habari na mawasiliano muhimu katika kutimiza SDGs

Kusikiliza / Watu wakitumia intaneti jijini Nairobi, Kenya.(Picha: ITU/G. Anderson)

Wakitanabaisha umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) katika ulimwengu wa sasa, ofisi na wakuu wa mashirika zaidi ya 20 ya Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kukumbatia teknolojia hizo ili kuchapusha utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu au SDG's. Wito huo upo katika ripoti mpya iliyozinduliwa leo mjini Geneva [...]

13/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Silaha za nyuklia ni mwiba unaopaswa kutolewa

Kusikiliza / Linnet Ng'ayu kutoka baraza la viongozi wa dini barani Afrika ACRL-RfP nchini Kenya.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J/Msami)

Silaha za nyuklia zimekuwa mwiba kwa wakazi wa dunia hii hasa kwa wale ambao silaha hizo zimetumika na kuwaletea madhara, mathalani huko Hiroshima na Nagasaki nchini Japan. Madhara kama vile watoto kuzaliwa na ulemavu wa viungo, wanawake kushindwa kubeba ujauzito ni miongoni mwa madhara lukuki yaliyosababisha Umoja wa Mataifa kupitia nchi wanachama wake kukutana kwenye [...]

13/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kifo cha mwanaharaki wa Uchina ni pigo kwa haki za binadamu duniani-Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu Zeid Ra'ad Al Hussein. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Mwanaharakati wa Uchina wa amani na demokrasia aliyeaga dunia , Liu Xiaobo ameenziwa na kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akisema alikuwa ni "Ufafanuzi wa ujasiri wa kiraia na heshima ya kibinadamu.” Bwana Liu, aliyekuwa na umri wa miaka 61, amekuwa akisumbuliwa na saratani ya ini na ameaga dunia leo Alhamisi [...]

13/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitisho na mateso waliyoyapitia watoto Mosul havielezeki

Kusikiliza / Picha:©UNICEF 2017/Jenny Sparks

Ingawa vita vya miaka mitatu vya Mosul nchini Iraq vinakaribia kuisha, makovu ya mateso ya kimwili na kiakili walioachiwa watoto yatachukua muda kupona. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Hayo ni kwa mujibu wa Naibu Mwakilishi wa UNICEF nchini Iraq Bi. Hamida Ramadhani, ambaye amesema katika siku tatu zilizopita shirika lake na wadau [...]

13/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miradi ya Kenya, Uganda ni miononi mwa washindi 15 wa tuzo ya SWITCH-UNEP

Kusikiliza / Mshindi wa tuzo ya SEEDs kutoka Kenya.(Picha:UNEP)

Mradi wa mifuko itokanayo na shina la mgomba wa ndizi nchini Kenya, mradi wa madawati ya shule yaliyotengenezwa kwa taka za plastiki kutoka Burkina Faso, mradi wa kuboresha maisha ya wakulima wa kahawa na usalama wa sokwe wa mlimani Uganda ni miongoni mwa washindi 15 wa tuzo ya kifahari ya mwaka huu ijulikanayo kama SWITCH [...]

13/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulemavu sio kulemaa tunachotaka ni kuwezeshwa

Kusikiliza / Fatma Wangari (Kushoto) na Rebecca Altsi (Kulia) wakati wa mahojiano.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/G.Kaneiya)

Kuwa mlemavu haimanishi huwezi kushirikishwa katika maendeleo ya jamii na hasa katika umimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG's. Hayo yamesemwa na Rebecca Altsi kutoka shirika la kimataifa la IF linalojihusisha na walemavu wa mgongo wazi na wenye vichwa vikubwa Afrika ya Mashariki na Bi Fatma Wangari kutoka shirika la kimataifa la inclusion Africa [...]

13/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wayemen milioni 20 wanategemea hatua za baraza la usalama kusaidiwa

Kusikiliza / Mkuu wa kuratibu masuala ya kibinadamu wa Umoj wa Mataifa Stephen O'Brien.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Takriban Wayemeni milioni 20 wanategemea baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua mujarabu ili kusaidia kumaliza vita nchini Yemen ambavyo sasa vimechangia kusambaa kwa kashifa ya kipindupindu. Akizungumza kwenye kikao cha baraza la usalama hii leo mjini New York Marekani, mkuu wa kuratibu masuala ya kibinadamu wa Umoj wa Mataifa Stephen O'Brien, amesisitiza [...]

12/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kijana weka bunduki chini, chukua kalamu- Dor

Kusikiliza / Dor 2

Kijana Dor Achek kutoka Sudan Kusini, alikuwa mkimbizi, aliyeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Sasa kijana huyuni msomi na ana ndoto za kuwa balozi ili awasaidie wakimbizi hususani vijana. Kijana huyu ambaye amehudhuria mkutano wa ngazi za juu kuhusu elimu amezungumza na Joseph Msami wa idhaa hii kumuelezea alikotoka,aliko na zaidi ya [...]

12/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maeneo mapya 21 yaongezwa kwenye orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia

Kusikiliza / Eneo la urithi la Aphrodisias nchini Uturuki.(Picha:UNESCO)

Maeneo mapya 21 yameongezwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya urithi wa dunia na kufanya jumla ya maeneo ya urithi wa dunia kufikia zaidi ya 1000. Tangazo hilo limetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO wakati wa kufunga mkutano wa 41 wa kila mwaka wa kamati ya [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu bilioni 2 hawana maji salama ya kunywa:WHO/UNICEF

Kusikiliza / Upatikanaji wa maji safi na salama bado ni changamoto katika nchi nyingi duniani.(Picha:UNIC/Tanzania)

Watu 3 kati ya 10 kote duniani au watu bilioni 2.1 ,wanakosa fursa ya kupata maji salama nyumbani na mara mbili yao hawana huduma za kujisafi, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya duniani WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF. Ripoti hiyo imeongeza kuwa nyumba nyingi , vituo vya afya na shule [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Askari wa UNMISS wasitisha jaribio la utekaji nyara kwa wakimbizi

Kusikiliza / Walinda amani wakipiga doria nchini Sudan Kusini.(Picha:Isaac Billy/ UNMISS)

Nchini Sudan Kusini, askari wawili waliovaa sare za kijeshi na kubeba silaha walijaribu kuwateka nyara wakimbizi watatu karibu na kituo cha ulinzi wa raia cha Bentiu kinacholindwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Askari hao wanaodhaniwa kuwa ni wa SPLA waliwakaribia na kuanza kuwanyanyasa [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu kuhusu albino kuzuru Tanzania

Kusikiliza / Mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi , Ikponoswa Ero (Kushoto). Picha: UNIC/Tanzania

Mtaaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Ikponwosa Ero anafanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania wiki ijayo kuanzia Juali 18-28, ili kutathimini hali ya haki za binadamu za watu wenye ulemavu wa ngozi au albino. Bi Ero amesema ziara hiyo ni muhimu sana ukizingatia kwamba kumeripotiwa mashambulizi mengi dhidi ya watu [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utandawazi una mapungufu yake-WTO

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Kiuchumi Angel Gurria .(Picha:UNIfeed/Video Capture)

Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Kiuchumi (OECD) alisema kuwa kuna “upungufu dhidi ya utandawazi” na kuongeza kuwa “utandawazi hauna shingo ambayo unaweza kuegemea.” John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA KIBEGO) Akizungumza katika ufunguzi wa mwaka huu wa mkutano wa msaada wa tathimini ya kimataifa ya Biashara katibu mkuu huyo bwana [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uthubutu wa kutekeleza yanayosemwa utafanikisha SDGs- Moshi

Kusikiliza / SDGs.(Picha:UNIC/Tanzania)

SDGs.(Picha:UNIC/Tanzania) Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs uko katika mstari sahihi nchini Tanzania kufuatia sera mpya zilizopo za kuhakikisha ulinzi wa mapato ya kitaifa. Hiyo ni kauli ya Celestine Moshi, mkurugenzi, idara ya ushrikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, akizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano wa [...]

12/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa nishati ya jua wabadili maisha ya wakaazi Tanzania

Kusikiliza / Mradi wa nishati ya jua nchini Tanzania.(Picha:Benki ya dunia/video capture)

Upatikanaji wa huduma ya maji ni changamoto katika nchi nyingi hususan zilizo barani Afrika. Hata hivyo jamii, serikali na mashirika mbalimbali yakiwemo ya Umoja wa Mataifa kama vile benki ya dunia yanachukua hatua ili kupunguza adha hiyo. Nchini Tanzania waakazi wa mkoa wa Manyara wamepata muorubaini dhidi ya ukosefu wa maji na magonjwa yanayotokana na [...]

11/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waenzi waathirika wa mauaji ya Srebrenica

Kusikiliza / Ni mwaka 1995 mwanajeshi wa kitaifa akisoma orodha ya majina ya wanajeshi waliokimbia au manusura wa mji uliosambaratika wa SrebrenicaUNICEF/NYHQ1995-0553/LeMoyne

Umoja wa Mataifa leo Jumanne umewakumbuka na kuwaenzi maelfu ya wanaume na wavulana waliouawa kinyama miaka 22 iliyopita kwenye mji wa Srebrenica huko Bosnia na Herzegovina wakati wa vita vya Balkan. Mauaji ya halaiki ya Julai 11 mwaka 1995 yalikuwa ndio makubwa zaidi kutokea katika ardhi ya jumuiya ya Ulaya tangu jumuiya hiyo ilipoanzishwa baada [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwajibikaji na maridhiano ni muhimu kuponya majeraha ya ISIL Iraq

Kusikiliza / Familia iliyokimbia vita vya Mosul, nchini Iraq. Picha: Photo: UNHCR/Ivor Prickett

Kukombolewa kwa mji wa Mosul Iraq kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi la ISIL , kutokana na ushirika wa majeshi ya serikali ya Iraq yakisaidiwa na muungano wa wadau wa kimataifa , ni hatua muhimu ya kubadili ukurasa katika vita, Lakini Iraq inakabiliwa na mlolongo wa changamoto za haki za binadamu ambazo zisiposhughulikiwa , zinaweza [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekelezaji wa mkataba wa Disemba 2016 DRC hauridhishi-UM

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Utekelezaji wa mkataba uliotiwa saini mwaka 2016 mwezi Desemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hauridhishi huku hali ikiendelea kuwa tete katika maeneo mbalimbali hususani ya Mashariki na Magharibi mwa nchi hiyo. Hayo yamesemwa na Jean-Pierre Lacroix mkuu wa idara ya operesheni za ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa, akiwasilisha ripoti leo jumanne [...]

11/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Biashara ni nguzo muhimu kwa amani na ustawi wa kanda ya Maziwa Makuu Afrika-UNCTAD

Kusikiliza / Maisha ya kawaida jimbo la Tanganyika nchini DRC.(Picha:MONUSCO / Francois-Xavier Mybe)

Kuchagiza maendeleo, amani na usalama katika kanda ya Maziwa Makuu Afrika ndio mada kuu kwenye mkutano unaofanyika leo mjini Geneva Uswisi ulioandaliwa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD na kuhudhuriwa pia na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa eneo la maziwa makuu. John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA JOHN) [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila ya uzazi wa mpango umasikini utaendelea kuwa mfalme

Kusikiliza / Mama na mwanae katika hospitali nchini Liberia.(Picha:UNMIL Photo/Staton Winter)

Leo ni Siku ya Idadi ya Watu duniani ambayo mwaka huu inaenda sambamba na mkutano wa ngazi ya juu wa mpango wa uzazi FP2020 unaofanyika jijini London, Uingereza, mkutano ulioleta pamoja viongozi na watetezi kutoka mataifa mbalimblai kuahidi upatikanaji wa aina za kisasa za uzazi wa mpango kwa wanawake zaidi ya milioni 120 hususan wale [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msumbiji, Benki ya dunia na FAO wasaini mkataba kuinua sekta ya misitu

Kusikiliza / Naibu Mkurugenzi Mkuu Daniel Gustafson wa FAO na Augusta Pechisso wa maswala ya maendeleo endelevu ya kitaifa Msumbiji wakati wakutia saini mkataba.(Picha:FAO/Ricarrdo De Luca)

Serikali ya Msumbiji, Benki ya dunia na shirika la chakula na kilimo duniani FAO leo wametangaza mradi mpya ambao utaimarisha misitu endelevu na kuchangia kwa Msumbiji kutimiza lengo namba 15 la maendeleo endelevu yaani SDGs kuhusu misitu. Mradi huo utakaogharimu dola milioni 6 ni sehemu ya uwekezaji wa dola milioni 47 wa benki ya dunia [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Brigedi maalumu ya SADC yakabiliwa na changamoto DRC-Mwakibolwa

Kusikiliza / Luteni Jenerali James Mwakibolwa.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/F.Nducha)

Brigedi maalumu iliyoanzishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iliyo chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa ajili ya kufurusha makundi ya waasi (FIB) inakabiliwa na changamoto nyingi. Hayo ni kwa mujibu wa Luteni Jenerali James Mwakibolwa, mnadhimu mkuu wa majeshi wa ulinzi nchini Tanzania aliyeko makao makuu ya Umoja [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres akaribisha kuanzisha mpango mpya wa UM Colombia:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM/Evan Schneider

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha kuanzishwa kwa mpango mpya wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia utakaokuwa na lengo la kuhakiki utekelezaji wa mkataba wa amani unaohusiana na kulijumuisha katika jamii kundi la FARC-EP na pia utekelezaji wa hakikisho la usalama kwa kundi hilo na jamii zilizoathirika na machafuko. Mpango huo [...]

11/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utalii unatoa fursa za kipato kwa wengi ikiwemo wakulima- UNCTAD

Kusikiliza / Pwani ni moja ya kivutio cha watalii, hapa ni mvuvi nchini Tanzania.(Picha:UM/Milton Grant)

Utalii ni moja ya sekta ambazo inachangia mapato ya nchi huku ikielezwa kuwa mapato yatokanayo na sekta hiyo yameongezeka kutoka dola bilioni 69 kati ya mwaka 1995-1998 hadi dola bilioni 196 kati ya mwaka 2011-2014. Aidha nchi barani Afrika ni wanufaika wa sekta hii ambayo inatoa fursa za ajira za moja kwa moja katika sekta [...]

10/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula kusalia chini hadi 2026-FAO

Kusikiliza / Picha:FAO

Gharama za mafuta ya mbogamboga ya kupikia , bidhaa za maziwa na bidhaa zingine za kimataifa za chakula zinatarajiwa kusalia chini katika miaka kumi ijayo. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyochapishwa leo na ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD) na shirika la chakula na kilimo FAO. Ripoti inasema akiba kubwa ya nafaka [...]

10/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

M-pesa yaokoa waathirika wa ukame, Kenya

Kusikiliza / M-pesa.(Picha:Video capture/World Bank)

Mpango wa kuhamisha fedha kwa tekinolojia ya simu za rununu umesaidia waathirka wa ukame zaidi ya 250,000 kuepuka njaa iliokithiri nchini Kenya, kando na kufikia mahitaji mengine mengi ya kila siku, limesema Shirka la Msalaba Mwekundu nchini Kenya (KRCS). Katika miezi mitatu iliopita, Shirika hilo limetoa shilingi za Kenya 3,000 za msaada wa kila mwezi, [...]

10/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uaminifu ni muhimu sana katika kuwalinda watoto walio pekee yao-UM

Kusikiliza / Watoto wacheza katika kambi ya Kara Tepe katika vitongonji vya Mytilini, Lesvos, Ugiriki.(Picha: UNICEF/UN057951/Gilbertson VII)

Mkakati kabambe umezinduliwa leo kwa ajili ya kuwalinda watoto wakimbizi na wahamiaji dhidi ya ghasia na ukatili wakati wanapoelekea na kusafiri ndani ya bara Ulaya. Mkakati huo uliotangazwa Jumatatu na Umoja wa Mataifa upo katika waraka uiitwao "Ramani ya mwelekeo" ambayo ni kazi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, shirika la [...]

10/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukombozi wa Mosul ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi-Guterres

Kusikiliza / Wakaazi wa Mosul nchini Iraq.(Picha:UNHCR)

Ukombozi wa mji wa Mosul ni hatua muhimu katika vita dhidi ya ugaidi na ghasia za itikadi kali. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA YA AMINA) Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres iliyotolewa Jumatatu kupitia msemaji wake, pia akiwashukuru watu na serikali ya Iraq kwa mchango [...]

10/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko Darfur yaleta zahma kambi ya wakimbizi wa ndani-OCHA

Kusikiliza / Mafuriko Darfur, Sudan.(Picha:UNAMID)

Mvua kubwa zinazonyesha katika sehemu mbaimbali kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan zimesababisha mafuriko na athari katika kambi ya wakimbizi wa ndani na miundombinu ikiwemo barabara ambazo nyingi sasa hazipitiki. Taarifa kamili na Selemeni Semunyu mwandishi wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika Darfur UNAMID (TAARIFA YA SELEMANI ) [...]

10/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bunge litunge sheria kwa mujibu wa Katiba ili kulinda wanawake- Katureebe

Kusikiliza / Wanawake nchini Uganda.(Picha:UNFPA)

Katiba ya Uganda imeweka bayana sheria za kulinda wanawake kwa ajili ya kuhakikisha wanalindwa dhidi ya tamaduni potofu, sasa changamoto ni kwa bunge kuweka sheria ili ziendane na katiba. Hiyo ni kauli ya mwanasheria mkuu wa Uganda Bart Katureebe alipohojiwa na Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano wa wafadhili wa shirika linalohusika na masuala ya [...]

10/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mbio zatumika Sudan Kusini kujenga maelewano baina ya jamii

Kusikiliza / Mbio zatumika Sudan Kusini kujenga maelewano baina ya jamii.(Picha:UNifeed/video capture)

Miaka sita ya uhuru wa Sudan Kusini ikitimu tarehe Tisa mwezi huu wa Julai, matumaini ya wananchi kuwa watakuwa na ustawi wa kudumu bado yako mashakani kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo tangu mwezi disemba mwaka 2013. Bado mamia ya watu ni wakimbizi wa ndani na wengine wanakimbilia nchi jirani, jamii mbali mbali zikiendelea kufarakana. [...]

07/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu nchini Kenya

Kusikiliza / Dkt. Samuel Arap Tororee kutoka tume ya kitaifa ya ardhi nchini Kenya ambaye ana ulemavu wa macho kutoona na Bi Marsela Odende wakati walihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa hii.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/G.Kaneiya)

Ikiwa ni zaidi ya miaka kumi tangu kupitishwa kwa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu CRPD, baadhi ya nchi zimepiga hatua katika kutekeleza na kuzingatia haki hizo. Mkataba huo uliopitishwa mnamo Disemba 13 mwaka 2016 unatoa muongozo kwa nchi wanachama katika utekelezaji wa sheria, mikakati, sera na programu za kuimarisha usawa na ujumuishwaji pamoja [...]

07/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yaangazia utokomezaji wa silaha za nyuklia

Kusikiliza / Balozi Elayne Whyte Gómez kutoka Costa Rica.(Picha:UM/Manuel Elias)

Mkataba wenye nguvu kisheriaa na ambao unalenga kutokomeza kabisa matumizi ya silaha za nyuklia umepitishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Wajumbe kutoka nchi 124 walioshiriki mkutano huo walipiga kura ambapo nchi 122 ziliunga mkono, ilhali Uholanzi ilipinga na Singapore haikuonyesha msimkamo wowote. Hata hivyo baadhi ya nchi kama vile Marekani, Uingereza, [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa lishe kwa watoto DRC wagharimu serikali mamilioni ya dola- Ripoti

Kusikiliza / rdc

Ripoti mpya iliyozinduliwa leo huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imebainisha jinsi lishe duni kwa watoto inavyoathiri uchumi wa nchi hiyo. Ikipatiwa jina la Gharama ya Njaa barani Afrika, COHA, ripoti hiyo mathalani imesema lishe duni miongoni mwa watoto husababisha DRC kupoteza dola zaidi ya bilioni moja kila mwaka kupitia gharama za tiba, [...]

07/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha Uingereza UNMISS chafungua hospitali Bentiu

Kusikiliza / Ufunguzi wa hospitali Bentiu na kikosi cha Uingereza kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS.(Picha:UNMISS)

Nchini Sudan Kusini, kikosi cha Uingereza kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS kimefungua hospitali kwenye mji wa Bentiu. Hospitali hiyo inalenga kutoa huduma ya matibabu kwa zaidi ya watu 1,800 wakiwemo askari na wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi kwenye kituo cha kuhifadhi raia lililo ndani zaidi. UNMISS inasema hospitali hiyo itaweza kutibu [...]

07/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Kifufumkunye

Kusikiliza / Neno la wiki 2

Wiki hii tunaangazia neno  Kifufumkunye na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema kwamba neno  kifufumkunye lina maana ya jambo lisilo fahamika bayana na ambalo halitiliwi maanani wala umuhimu.

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usugu wa dawa dhidi ya kisonono waongezeka- WHO

Kusikiliza / WHO imesema matumizi sahihi ya kondomu itasaidia kujikinga dhidi ya kisonono.(Picha:IRIN)

Shirika la afya duniani, WHO limesema tiba dhidi ya ugonjwa wa kisonono inazidi kuwa ngumu kila uchao kutokana na usugu wake kwa antibayotiki au viuavijasumu. Amina Hassan na ripoti kamili. (Taarifa ya Amina) Dkt. Teodora Wi kutoka WHO amesema kubadilika mara kwa mara kwa bakteria wanaosababisha ugonjwa huo pamoja na matumizi holela ya viuavijasumu ni [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Cyprus wamalizika bila muafaka

Kusikiliza / sg 1

Mazungumzo yaliyolenga kuweka mwelekeo wa kuwezesha Cyprus kuungana tena baada ya kuvunjika mapande mwaka 1974 yamemalizika bila maafikiano yoyote. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye aliombwa kurejea Crans Montana Uswisi jana ili kushiriki mazungumzo hayo amewaambia waandishi wa habari hii leo mjini humo kuwa.. [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukata watishia elimu kwa watoto wanaoishi kwenye mizozo- UNICEF

Kusikiliza / watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema ukata unakwamisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya elimu ya watoto wanaoishi kwenye mizozo. UNICEF imetoa taarifa hiyo wakati viongozi wa kundi la nchi 20 wakikutana huko Hamburg, Ujerumani huku ombi la dola milioni 392 zinazohitajika mwaka huu kwa miradi ya elimu kwenye nchi zenye [...]

07/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kupitishwa Ijumaa

Kusikiliza / Mwenyekiti wa mkutano uliowezesha kupatikana kwa mkataba huo ambao unabeba maadili ya kimataifa kuhusu kutengeneza, kumiliki na kuhifadhi nyuklia Elayne Whyte GómezPicha: UM/Rick Bajornas

Mkataba wa aina yake wenye lengo la kutokomeza kabisa matumizi ya silaha za nyuklia unapitishwa kesho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inafuatia mashauriano ya wiki tatu baina ya serikali na pande mbali mbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na hivyo kufanikisha juhudi za zaidi ya miaka 20. Mwenyekiti wa mkutano uliowezesha [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu mkuu ziarani Uswisi kushiriki mazungumzo ya Cyprus

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa kwenye helikopta baada ya kushiriki mazungumzo juu ya Cyprus mapema mwezi Julai 2017.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesafiri kuelekea Uswisi Alhamisi ili kuendelea na mazungumzo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu Cyprus kwa ajili ya kuleta nchi hiyo kuwa taifa moja kufuatia kisiwa hicho kilicho kwenye bahari ya Mediteranea kugawanyika mapande kwa miaka 43. Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu iliyotolewa Jumatano imesema kwamba mkuu [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Astana imetupatia nuru ingawa ni kidogo- de Mistura

Kusikiliza / mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffa de Mistura akizungumza na waandishi wa habari huko Astan.(Picha:UM)

Mazungumzo kuhusu Syria yaliyofanyika huko Astana , Kazakhstan licha ya kuwa na maendeleo kidogo yamepiga hatua muhimu katika kusaka hatimaye suluhu ya mzozo unaoendelea nchini humo. Hiyo ni kwa mujibu wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura alipozungumza na waandishi wa habari huko Astana baada ya majadiliano kati ya serikali [...]

06/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bei ya vyakula imeongezeka hadi kiwango cha juu kabisa katika miaka miwili-FAO

Kusikiliza / Mkulima katika shamba la zao la mahindi Honduras.(Picha:FAO/Orlando Sierra)

Bei ya vyakula duniani imeongezeka na kufikia kiwango cha juu zaidi katika muda wa miaka miwili, ikichagizwa na bei ya juu ya siagi pamoja na kuongezeka kwa bei ya ngano na nyama. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO katika ripoti yake ya bei za vyakula kwa mwezi Juni ambayo [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dkt. Kituyi kuendelea kuongoza UNCTAD kwa miaka mingine minne

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi wakati akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii mwaka 2016.(Picha:UM/Video Capture)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limemthibitisha Dkt. Mukhisa Kituyi kuendelea kuongoza kamati ya biashara ya maendeleo ya umoja huo, UNCTAD kwa kipindi kingine cha miaka minne kuanzia tarehe mosi Septemba 2017. Uthibitisho huo umefanyika leo kufuatia kufuatia mapendekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mashauriano yake na nchi wanachama. Dkt. Kituyi ni [...]

06/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Myanmar isake suluhu kwa wasio na utaifa- Grandi

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi akutana na Masoota Hatu, mwanamke mwenye umri wa miaka 55 nchini Myanmar. Picha: © UNHCR/Roger Arnold

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya kwanza nchini Myanmar kwa kutoa wito kwa nchi hiyo kusaka suluhu ya endelevu na shirikishi juu ya suala la watu wasio na utaifa. Ametoa wito huo baada kutembelea maeneo ya Yangon, Naypyitaw pamoja na Sittwe na Maungdaw [...]

06/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mazingira duni ya kazi ni kikwazo katika utekelezaji wa majukumu kazini

Kusikiliza / Eunice, mmoja wa wanawake ambao wamepoteza ajira hivi karibuni nchini Kenya kama moja ya juhudi za kupaza sauti za wanawake. Picha: Picha: UN Women/Video capture

Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yanalenga ikiwemo: kutokomeza umaskini uliokithiri, kumaliza utofauti wa usawa wa kijinsi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Usawa wa kijinsia ni miongoni mwa masuala muhimu kwa ajili ya kufikia ajenda ya 2030. Huku upatikanaji wa ajira ukiwa ni changamoto hususan katika nchi zinazoendelea mazingira duni ya [...]

06/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya gereza kuu la Kananga huko DRC ni ya kusikitisha

Kusikiliza / Jopo la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO limetembelea gereza kuu la Kananga.(Picha:UM/DRC

Jopo la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO limetembelea gereza kuu la Kananga kwenye jimbo la Kasai Mashariki ili kuweza kutathmini mahitaji yake kutokana na hali mbaya inayolikabili. Hivi sasa gereza hilo lililojengwa mwaka 1951 linakabiliwa na mlundikano wa wafugwa ambapo badala ya kuhifadhi wafungwa 300 hivi sasa [...]

06/07/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 30 wanakabiliwa na njaa- FAO

Kusikiliza / Mtoto anayeugua utapiamlo nchini Somalia katika kambi ya Salamey Idale.(Picha:UNICEF/Rich)

Dunia inakabiliwa na janga kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa, huku watu milioni 30 katika nchi nne wakikabiliwa na uhaba wa chakula na wengi wakiwa katka hatari ya ukame limesema Shirika la kilimo na chakula duniani FAO. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Akizungumza katika kongamano la FAO huko Roma, Italia Naibu [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zachukuliwa kusaidia waathirika wa mafuriko Darfur Kusini

Kusikiliza / Mafuriko nchini Sudan kwenye jimbo la Darfur Kusini kufuatia mvua kubwa. Picha: IOM

Huko nchini Sudan kwenye jimbo la Darfur Kusini mvua kubwa zilizonyesha tarehe 20 mwezi uliopita na kusababisha mafuriko zimeendelea kusababisha madhara kwa wakimbizi wa ndan wapatao 9,000. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu, OCHA imesema mvua hizo zilisababisha mamia ya makazi ya wakimbizi [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado kuna changamoto kubwa Afrika katika kujumuisha watu wenye ulemavu

Kusikiliza / Miundombinu2

Wakati mataifa yaliyoendelea yamepiga hatua kubwa katika kujumuisha mahitaji ya watu wenye ulemavu kwenye jamii, Afrika bado ni kitendawili hasa katika masuala kama miundombinu ambayo ilijengwa bila kumfikiria mtu mwenye ulemavu bila kusahau mila na tamaduni potofu kuhusu hali ya ulemavu. Akizungumza na idhaa hii  kuhusu changamoto hizo Dkt. Samuel Arap Tororee  kutoka tume ya [...]

06/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sauli aeleza ndoto zake za kubadlisha maisha ya vijana na jamii Tanzania

Kusikiliza / Sauli 1

Umoja wa Mataifa hivi sasa unapigia chepuo ushirikishaji wa vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Malengo hayo ni mtambuka ambapo vijana wanaweza kushiriki katika kufanikisha malengo yote iwapo watajiongeza. Mathalani huko Tanzania kijana mmoja amejiongeza na kupigia chepuo lengo namba nne la linalotaka elimu jumuishi na yenye usawa. Kijana huyo Saul Mwame wa [...]

05/07/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa vijijini ni muarobaini kutokomeza njaa na umaskini-FAO

Kusikiliza / Kilimo barani Afrika.(Picha:IFAD)

Wanawake wa vijijini ni kiungo muhimu cha mabadiliko katika kutokomeza njaa na umaskini uliokithiri, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula na kilimo duniani FAO José Graziano da Silva leo katika kongamano huko Roma, Italia. Bwana da Silva amesema majukumu yao ni zaidi ya uzalishaji wa kilimo na yanakwenda mbali ya uzalishaji wa chakula na [...]

05/07/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni muhimu nchi kuwalinda wahamiaji na wakimbizi- Ruteere

Kusikiliza / Mutuma Ruteere, Mtaalamu wa haki za binadamu kuhusu ubaguzi wa zama za kisasa.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/G.Kaneiya)

"Mgeni wa leo ni mwenyeji wa kesho," hiyo ni kauli ya ufunguzi wa mahojiano kati ya mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu mifumo ya kisasa ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na hali zingine za kutovumiliana, Mutuma Ruteere na Flora Nducha wa Idhaa hii. Ungana naye.  

05/07/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

WTO yashirikiana na watangazaji kudhihirisha ajenda ya mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Mmoja wa watangazaji wa masuala ya hali ya hewa ambaye video yake imezinduliwa leo.(Picha:WTO/video capture)

Shirika la hali ya hewa duniani, WTO linashirikiana na taasisi ya masuala ya hali ya hewa nchini Marekani, Climate Central kuonyesha jinsi viwango vya joto vitakavyozidi kuongezeka katika miji mbali mbali duniani kutokana na mabadiliko ya tabianchi. WTO imesema kupitia ushirikiano huo, watangazaji wa televisheni wanaohusika na masuala ya hali ya hewa pamoja na wataalamu [...]

05/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM watoa wito wa kusitishwa kunyongwa kwa Morva

Kusikiliza / 20170705_Agnes_Callamard_JMFerre_350300

Hukumu ya kifo ya mwanamume anayesubiri kunyongwa jimbo la Virginia nchini Marekani inapaswa kusitishwa kwa kuzingatia ulemavu wake wa akili, wamesema wataalam wa haki wa Umoja wa Mataifa Jumatano. Katika ombi lao kwa mamlaka, wataalamu hao Agnes Callamard na Danius Puras wamesema hali ya kiakili ya mwanamume huyo William Morva raia wa Hungary, haikuwekwa bayana [...]

05/07/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko thabiti ya UM yahitajika kukidhi SDGs- Guterres

Kusikiliza / SG-Report4

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwasilisha ripoti ya mapendekezo yake kuhusu mabadiliko ya mfumo wa Umoja wa Mataifa. (Picha: UN/Kim Haughton)   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo amewasilisha ripoti yake inayopendekeza mabadiliko makubwa ya muundo wa utendaji wa chombo hicho ili kiweze kutekeleza kwa ufanisi ajedna ya maendeleo [...]

05/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utalii watoa fursa za ajira milioni 21 Afrika- UNCTAD

Kusikiliza / Utalii

Ripoti mpya ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kuhusu maendeleo ya uchumi Afrika imebaini kuwa sekta ya utalii ina nafasi kubwa katika kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Mathalani imebaini kuwa mapato yatokanayo na sekta hiyo yameongezeka kutoka dola bilioni 69 kati yam waka 1995-1998 hadi dola bilioni 196 kati [...]

05/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nusu ya wahamiaji milioni 12 ni watoto- UNICEF

Kusikiliza / Watoto wakimbizi. Picha: UM/Video capture

Zaidi ya nusu ya wahamiaji milioni 12 kila mwaka ni watoto, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyochapishwa hii leo ikipatiwa jina -Kutafuta fursa: Sauti za watoto walio safarini katika Afrika ya Magharibi na ya kati. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Nats… [...]

05/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia lazima ijue mgeni wa leo ni mwenyeji wa kesho-Rutere

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa Bwana Mutuma Ruteere. UN Photo/Evan Schneider

Ni muhimu dunia ikatambua kwamba katika mabara yote asilimia kubwa ya watu ni wageni na wahamiaji, hata kama ni wahamiaji wa ndani waliotoka sehemu moja kwenda nyingine na hilo si jambo baya na la kuchochea ubaguzi. Kauli hiyo imetolewa na Bwana Mutuma Ruteere mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu mifumo ya kisasa ya ubaguzi, [...]

05/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi DPRK acheni vitendo vinavyozorotesha hali ya sasa- Guterres

Kusikiliza / Launch of the Regional Flash Appeal Folowing recent events in Libyan Arab Jamahiriya.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK leo imefanya jaribio la kombora la masafa marefu, kitendo ambacho kimeshutumiwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akisema kuwa kitendo hicho ni hatua nyingine ya ukiukwaji mkubwa wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa [...]

04/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa na mchango wake katika maendeleo

Kusikiliza / Mama mkulima kama huyu hunufaika na vyama vya ushirika.(Picha:Dasan Bobo / World Bank)

Leo tarehe Nne Julai ni siku ya mapumziko hapa Marekani kwa kuwa ni sikukuu ya Uhuru wa taifa hili, kwa hivyo tunakutelea jarida maalum. Jarida hili maalum linaangazia vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa na mchango wake katika maendeleo. Tunaangazia siku hii kwani huadhimishwa kila tarehe Mosi Julai kwa lengo la kutathmini umuhimu wa [...]

04/07/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa usalama na hali ngumu ya uchumi vyafurusha wakimbizi Libya

Kusikiliza / Hwa ni miongoni mwa wakimbizi na wahamiaji walioko nchini Libya wanaosaka maisha bora Ulaya.(Picha:UNHCR)

Utafiti mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR umebaini kuwa nusu ya wageni wanaokimbilia Libya, wanafanya hivyo wakiamini kuwa watapata ajira na hatimaye maisha yao kuwa bora. Hata hivyo utafiti huo uliokuwa unaangalia mienendo ya wakimbizi na wahamiaji umebaini kuwa baada ya kufikia Libya, wengi wao hubaini kuwa mazingira ni hatarishi, [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wa Tanzania wakuza Kiswahili Darfur

Kusikiliza / TZ

Walinda amani wa Tanzania kwenye mpango wa kulinda amani wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni Darfur UNAMID, mbali ya kutoa mchango mkubwa wa kuhakikisha raia wa eneo hilo wanaishi kwa amani na utulivu, wanachangamana na wenyeji katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwafunza lugha ya Kiswahili. Ungana na mwandishi wa UNAMID Luteni [...]

03/07/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa fursa wachochea vijana kuwa mamluki- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM/Manuel Elias

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema suala la ukosefu wa ajira hivi sasa siyo tu janga kwa vijana pekee bali pia ni janga kwa usalama duniani. Bwana Guterres amesema hayo wakati akihutubia huko Lisbon, Ureno kwenye jukwaa la kujadili mikakati ya maendeleo mwaka huu likiangazia jinsi ya kuweka mikakati ya kufanikisha ajenda [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki ya Dunia yapatia mkopo Tanzania kupanua bandari ya Dar

Kusikiliza / Bandari ya Dar Es Salaam, Tanzania.(Picha: FAO)

Benki ya Dunia imeipatia Tanzania jumla ya dola milioni 357 kwa ajili ya mradi wa kupanua bandari ya Dar es salaam wa DSMGP. Taarifa ya benki hiyo imesema kati ya fedha hizo dola milioni 345 ni mkopo ilihali kiwango kinachosalia cha dola milioni 12 ni mkopo wa masharti nafuu. Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuwekeza katika vijana ndio muarobaini wa bara bora la kesho- Amina

Kusikiliza / PC

Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohamed amechagiza ushirikiano wa wote ili kujenga Afrika thabiti kwa ajili ya vijana na vizazi vijavyo. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi na viongozi wa AU kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Bi. Mohamed amesema ajenda ya 2063 ya AU [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa Ebola DRC watokomezwa- WHO

Kusikiliza / Wahudumu wa afya nchini DRC. Picha: WHO/Video capture

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetangaza kutokomezwa kwa mlipuko wa hivi karibuni zaidi wa ugonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Tangazo hilo linafuatia kutokuwepo kwa kisa kipya cha Ebola ndani ya siku 42 tangu kisa cha mwisho kiripotiwe kwenye jimbo la Bas-Uélé. Tarehe 11 mwezi Mei mwaka huu WHO ilijulishwa kuhusu [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wenye njaa duniani yaongezeka- FAO

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva na Waziri Mkuu wa Italia, Paolo Gentiloni. Picha: FAO

Idadi ya watu wenye njaa duniani imeongezeka tangu mwaka 2015 na hivyo kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika kuondokana na tatizo hilo. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema hayo huko Roma, Italia wakati akifungua mkutano mkuu wa wa siku [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wawekeze katika huduma za afya badala ya kusaka matibabu nje ya nchi

Kusikiliza / Kijana Ezechiel Ndayisaba.(Picha kwa idhini ya Ezechiel Ndayisaba )

Suala ya afya sio tu linawahusu wauguzi na wahudumu wa sekta ya afya pekee lakini ni jambo ambalo linajumuisha sekta zote za jamii ikiwemo sekta ya uchumi, viongozi na serikali kwa ujumla ili kuhakikisha huduma ya afya kwa wote hususan barani Afrika. Hii ni kwa mujibu wa kijana Ezechiel Ndayisaba ambaye ni mwanafunzi kutoka Burundi [...]

03/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu mpya wa WHO Dk Tedros aanza majukumu rasmi

Dk Tedros Ghebreyesus wa Ethiopia, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Hii leo Julai mosi, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus amenza kazi rasmi akiwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, akichukua nafasi ya Dk Margaret Chan ambaye ameshikilia wahdifa huo kwa miaka kumi. Dk Tedros mzaliwa wa Ethiopia, atakayeshikilia wadhifa huo kwa miaka mitano, alichaguliwa na nchi wanachama katika uchaguzi wa baraza kuu la WHO [...]

01/07/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031