Nimestushwa na kusikitishwa na vifo vya moto Ureno:Guterres

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UM/Jean-Marc Ferr)

Nimeshtushwa na kusikitishwa na idadi ya watu waliopoteza maisha leo kutokana na moto wa mwituni uliolikumba eneo la Pedrógão jimbo la Grande nchini Ureno.

Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye mapema leo Jumapili amezungumza na Rais wa Ureno , Marcelo Rebelo de Sousa, na waziri mkuu, António Costa, kuelezea majonzi yake na kutoa rambirambi kwa serikali na watu wa Ureno.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa , bwana Guterres amewatakia nafuu ya haraka majeruhi. Katika kipindi hiki cha majonzi amewaambia watu wa Ureno kuwa fikra na sala zake ziko pamoja na familia za wahanga.

Ameipongeza serikali ya taifa hilo, wafanyakazi wa huduma ya zimamoto, kitengo cha huduma ya dharura na mashirika ya asasi za kiraia ambao wanajitahidi kwa kila njia kukabiliana na moto huo na kuwasaidia wanaohitaji msaada.

Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia katika njia yoyote inayowezekana. Watu Zaidi ya 60 wamepoteza maisha hadi sasa kutokana na moto huo.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031