Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl afariki dunia

Kusikiliza /

Mwaka 1997, Helmut Kohl akiwa Kansela wa Ujerumani, akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ameelezea masikitiko  yake kufuatia taarifa za kifo cha kansela wa zamani wa Ujerumani, Helmut Kohl, kilichotokea leo Ijumaa.

Kolh atakumbukwa kwa mchango wake katika kufanikisha kuungana kwa Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi mwaka mmoja baada ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.

Halikadhalika alichangia katika muungano wa kiuchumi na kisiasa wa nchi za Ulaya, mchakato unaoitwa kuwa ni kihistoria ambapo Bwana Guterres kupitia taarifa ya msemaji wake ameeleza kuwa Ulaya ya sasa ni matokeo ya dira na azma ya hayati Kohl katika mazingira magumu.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kansela huyo wa zamani pamoja na wananchi na serikali ya Ujerumani.

Kansela Kohl ambaye alizaliwa mwaka 1930, aliongoza Ujerumani kuanzia mwaka 1982 hadi 1998.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031