Nyumbani » 19/06/2017 Entries posted on “Juni 19th, 2017”

Nimetumikishwa kama kahaba, nashindwa kujinasua-Joy

Kusikiliza / Joy

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inasema mamilioni ya watoto wanavuka mipaka ya kimataifa wakikimbia vurugu na migogoro, majanga au umaskini wakitumainia kupata maisha bora ugenini. Shirika hilo linasema katika mwaka 2015 – 2016, Idadi ya watoto wakimbizi na wahamiaji waliotenganishwa na wasioambatana na wazazi wao ilifikia 300,000 kutoka nchi 80 ikilinganishwa [...]

19/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 4000 hawana makazi baada ya moto kuteketeza kambi ya Korma Darfur

Kusikiliza / Mkimbizi aliyefurushwa makwao na kuishia kambi ya Korma ilioko Darfur Kasakzini.(Picha:Owies Elfaki, UNAMID)

Watu 4, 000 wameachwa bila makazi na sasa wanaishi chini ya miti baada ya moto mkubwa kuteketeza kabisa kambi waliyokuwa wanaishi kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan. Tukio hilo lilitokea Ijumaa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Korma iliyoko kilometa 80 kutoka El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, umesema mpango wa [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikwazo vya kusafiri Cuba vitaathiri uchumi wa Marekani

Kusikiliza / Picha: UNWTO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, UNWTO limelaani vikali uamuzi wa utawala wa Marekani kurejesha vikwazo vya kusafiri nchini Cuba. UNWTO imesema hatua hii ni shambulio kubwa la uhuru wa kusafiri na inarudisha nyuma uhuru huo, na ingawa litaathiri utalii wa Cuba kwa kiasi, litaathiri zaidi uchumi na uwepo wa kazi nchini Marekani, [...]

19/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utii na utekelezaji wa sheria za kimataifa sio chaguo-Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu  Zeid Ra'ad Al Hussein. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema utii na kuhakikisha utekelezaji wa sheria za kimataifa sio chaguo, akiongeza kwamba ukiukwaji wa haki za binadamu haukua dalili ya mgogoro baina ya Israel na Palestina, bali kichocheo cha mzunguko wa machafuko ambayo sasa yanaendelea kwa zaidi ya nusu karne. [...]

19/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP kunadi uwezo wa kutoa misaada kwa anga kupitia maonyesho Paris

Kusikiliza / WFP kunadi uwezo wa kutoa misaada kwa anga kupitia maonesho Paris.(Picha:WFP)

Maonyesho ya safari za ndege yanaanza leo hadi June 25 mjini Paris, Ufaransa. Shirika la mpangowa chakula duniani WFP limesema litatumia fursa hiyo ikiwa ni mara yake ya saba kushiriki, kudhihirisha matumizi ya ndege, wafanyakazi na teknolojia kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu katika majanga. Katika taarifa yake WFP imesema itaonesha utaalamu, na uwezo wa [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono vitani ni tishio la haki ya kuishi kiutu-Guterres

Kusikiliza / Ubakaji na ukatili wa kingono hutumika kama silaha vitani.(Picha:MONUSCO)

Ubakaji na ukatili wa kingono vitani ni mbinu za kigaidi na za kivita zinazotumika kudhalilisha , kudharaulisha , kuharibu na mara nyingi kufanya kampeni ya kutokomeza watu wa kabila fulani. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono vitani, [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tujiandae kabla ya ukame ili kuokoa wakulima- FAO

Kusikiliza / Moja ya maeneo kunakoshuhudiwa ukame.(Picha:FAO/Giulio Napolitano)

Huko Roma, Italia kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kunafanyika semina ya kimataifa kuhusu ukame na kilimo ambapo serikali na wadau wa kilimo wametakiwa kuachana na mtindo wa kusubiri ukame ndio wachukue hatua za kusaidia wananchi. Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema tabia hiyo [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita, mateso, ghasia vyazidi kufurusha watu makwao- UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi kama hawa wa Sudan Kusini aliowatembelea Kamishna Mkuu wa UNHCR ni miongoni mwa waliofurushwa makwao.(Picha:UNMISS)

Idadi ya wakimbizi duniani imeongezeka mwaka 2016 na kufikia milioni 65.6, vichocheo vikitajwa kuwa ni vita, ghasia na mateso. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwelekeo wa wakimbizi duniani kwa mwaka 2016, ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkimbizi wa Syria Muzoon aweka historia kuwa balozi mwema wa UNICEF

Kusikiliza / Msichana Muzoon, mwenye miaka 19,mkimbizi wa Syria  aliyeteuliwa kuwa balozi mwema mdogo kabisa wa UNICEF. Ni mwanaharakati wa kupigania elimu ya wasichana. Picha na UNICEF

Katika kuelekea siku ya wakimbizi duniani hapo kesho , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limemteua Muzoon Almellehan, mwenye umri wa miaka 19 mwanaharakati wa masuala ya elimu na mkimbizi wa Syria kuwa balozi wake mwema mpya na mdogo kabisa. Uteuzi huo unamfaya Muzoon kuwa mtu wa kwanza mwenye hadhi ya ukimbizi [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031