Nyumbani » 16/06/2017 Entries posted on “Juni 16th, 2017”

Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl afariki dunia

Kusikiliza / Helmut Kohl2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ameelezea masikitiko  yake kufuatia taarifa za kifo cha kansela wa zamani wa Ujerumani, Helmut Kohl, kilichotokea leo Ijumaa. Kolh atakumbukwa kwa mchango wake katika kufanikisha kuungana kwa Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi mwaka mmoja baada ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin. Halikadhalika alichangia katika muungano wa kiuchumi [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapewa taarifa ya maendeleo Mali

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la usalama kuhusu hali nchini Mali. Picha: UM/Kim Haughton

  Mwezi huu inatimia miaka miwli tangu kutiwa saini mkataba wa amani ulitotumainiwa kuwa wa kihistoria nchini Mali. Baraza la usalama Ijumaa ya leo limepewa taarifa ya hatua zilizopigwa nchini humo na changamoto ambazo bado zinaendelea. Umoja wa Mataifa ulianzisha operesheni Mali ili kusaidia taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya kushindwa kwa jaribio la [...]

16/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya Mtoto Zanzibar

Kusikiliza / Mwongozo kuhusu haki za watoto. Picha: UM

Mwaka 1989, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC. Mkataba huu ulilenga kusimamia misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambayo ni Kuishi, Kuendelezwa, Kushirikishwa na Kulindwa. Ibara ya 3 ya mkataba huo inagusia haki ya mtoto kwenye masuala yote ya kisheria, ikitaka haki ya mtoto kulindwa. [...]

16/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za UM akamilisha ziara DRC

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix alipokutana na gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku.(Picha:MONUSCO/Myriam Asmani)

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix, leo Ijumaa amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Akiwa nchini humo amepata fursa ya kutembelea Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini na kukutana na gavana wa jimbo hilo Julien Paluku na wawili hao wakajadili hali ya usalama, [...]

16/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa fedha wanyima watoto wa Syria mahitaji muhimu-UNICEF

Kusikiliza / Watoto wakiwa mjini Aleppo nchini Syria.(Picha:UNICEF/Romenzi)

Ukosefu wa fedha za usaidizi kwa watoto una madhara ya kupindukia katika uokozi wa karibu watoto milioni tisa nchini Syria, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema leo. UNICEF imesema kwamba imepokea kiasi cha dola bilioni 1.4 pekee ambacho ni robo ya kiasi kinachohitajika kwa ajili ya operesheni za dharura mwaka huu [...]

16/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni

Kusikiliza / IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni.(Picha:IOM)

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM limezindua huduma za kibalozi mtandaoni katika juhudi za kutekeleza mpango wa kurejea makwao kwa hiari, na huduma za kibinadamu za dharura kwa wahamiaji ( AVRR) walioko Libya waliokwama. Kwa mujibu wa IOM, kwa mara ya kwanza mkutano wa huduma za ubalozi mtandaoni umefanyika mnamo Juni tano kupitia Skype kwa [...]

16/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulemavu sio ukosefu wa uwezo

Kusikiliza / Bogdana Petrova mwenye ulemavu wa kutoona kutoka nchini Bulgaria. Picha: UM/Video capture

  Ulemavu sio ukosefu wa uwezo, ndivyo unavyoweza  kusema ukisikiliza kipaji cha muziki cha mwanadada Bogdana Petrova mwenye ulemavu wa kutoona kutoka nchini Bulgaria. Nyota huyu aliyewashangaza wengi kwa uwezo wake bila kujali hali yake, ametoa burudani juma hili mjini New York. Joseph Msami amefuatilia tukio hilo na kukuandalia makala ifuatayo.

16/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Mchuuzi na Machinga

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno Mchuuzi na machinga. Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA Bwana Zuberi anasema kwamba mchuuzi ni mtu anyeuza vitu vidogo vidogo alivyoweka sehemu iwe ni matunda, vichana au mboga alimradi anuza [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Saidieni adha ya maji Yemen kuepusha janga la kipindupindu:UM

Kusikiliza / Selioua Muhammad, 25 akiwa ameketi ndani ya makazi yake ambayo yalikuwa shule huko Sheik Othman in Aden, Yemen.(Picha:IRIN/Lindsay Mackenzie)

  Yemen na jumuiya ya kimataifa ni lazima wachukue hatua haraka kutoa maji salama ya kunywa ili kuzuia kusambaa zaidi kwa mlipuko wa kipindupindu, wameonya wataalamu wa haki za binadamu Ijumaa. Zaidi ya watu 135,000 wanahofiwa tayari wameshapata kipindupindu , wakati taifa hilo bado linakabiliana na vita vinavyoendelea ,ambavyo vimechangia kusambaratika kwa miundombinu ya maji [...]

16/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nusu ya watoto hawana fursa ya kufurahia utoto wao na baba zao-UNICEF

Kusikiliza / UNICEF

Zaidi ya nusu au asilimia 55 ya watoto wa umri wa miaka 3 na 4 katika nchi 74 duniani ambao ni takribani watoto milioni 40 wana kina baba ambao hawachezi nao au kushiriki katika shughuli za elimu yao ya awali , kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa Ijumaa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yakusanya wabobezi kubongoa bongo kukabiliana na saratani

Kusikiliza / Picha:IAEA

Wataalamu wa afya zaidi ya 500 kutoka nchi 96 watakutana kwa siku tatu kubongoa bongo kuhusu namna ya kutumia mionzi ya atomiki katika kutibu saratani. Taarifa ya shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki AEA imesema kwamba kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni, mjini Vienna nchini Austria, watalaamu hao watajikita katika kujumuisha jukumu la tiba [...]

16/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kinachohitajika ni utekelezaji wa sera-Tanzania

Kusikiliza / Ahmad Kassim Haji ambaye ni Naibu Katibu Mkuu , ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Tanzania Zanzibar.(Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulamevu CRPD ukiwa umekamilika hapo jana mjini New York Marekani, Tanzania Zanzibar imesema kinachohitajika ni utekelezaji wa sera kuhusu kundi hilo. Katika mahojiano maaluma na idhaa hii, Ahmad Kassim Haji ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Tanzania [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumaini ya mtoto wa Afrika yanategemea wazazi-Mongella

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wakicheza nchini Haiti. Picha: UN Photo/Christopher Herwig

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa Juni 16 kila mwaka, mwaka huu maudhui ni Ajenda ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa watoto barani Afrika. Maudhui hayo yanataka kuchochea ulinzi, uwezeshaji na fursa sawa kwa watoto. Katika mahojiano na idhaa hii mwanaharakati wa wanawake, ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwaheri Babatunde ulikuwa mtu wa watu-Musoti

Kusikiliza / Babarunde-3

Mwendazake Dr Babatunde Osotmehin aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA leo anapewa mkono wa kwaheri kwa heshima zote kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa hapa New York Marekani . Assumpta Massoi na taarifa kamili. (TAARIFA YA ASSUMPTA) Miongoni mwa watakaoshiriki katika tukio hilo maalumu litakalofanyika leo [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031