Nyumbani » 15/06/2017 Entries posted on “Juni 15th, 2017”

Natamani wasio walemavu wavae viatu vyetu: Mwakilishi walemavu Tanzania

Kusikiliza / Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

  Kila anayetunyima fursa tunatamani angevaa viatu vyetu, ahisi uchungu tunaopitia, ni kauli ya mmoja wa wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Zanzibar Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Bi Abeida anyehudhuria mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba [...]

15/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCHR yaorodhesha ukiukwaji wa haki za binadamu Eritrea

Kusikiliza / Mwanamke akichota maji kutoka kwenye kisima nchini Eritrea.  Picha: UM/Milton Grant

Nasikitika kuripoti kwamba Eritrea haijafanya jitihada zozote za kukomesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao uchunguzi umebaini kuwa ni sawa na  uhalifu dhidi ya ubinadamu, amesema leo Mtaalamu Huru wa Haki za Binadamu nchini humo. Bi. Sheela Kitharuth amesema mateso wanayoyapitia raia hao ni pamoja na kukamatwa kiholela, kuwekwa mahabusu bila mawasiliano, kutoweka na [...]

15/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu watamalaki Burundi, huku hofu ikitanda-UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi wakisubiri mgao wa chakula katika kituo cha muda cha 
Kamvivira.(Picha:UNHCR /Eduardo Soteras Jalil)

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili mwingine uliofurutu ada nchini Burundi sasa wathibitishwa. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Hayo ni kwa mujibu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa ukiukaji wa haki za binadamu Burundi iliyowasilisha taarifa yake kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis Alhamisi. [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hata nchi tajiri zahaha kutimiza SDGs-UNICEF

Kusikiliza / Hata nchi tajiri zahaha kutimiza SDGs-UNICEF

Mtoto mmoja kati ya watoto watano katika nchi zilizoendelea wanaishi katika umasikini, ilihali mmoja kati ya wanane hawana uhakika wa chakula, umebaini utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Utafiti huo ulioko katika ripoti ya UNICEF iliyochapishwa leo, unasema kwamba, nchi zenye uchumi wa kiwango cha juu zaidi duniani , zinahaha [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kitendo cha dharau-UNSOM

Kusikiliza / Picha:UM/Tobin Jones

Nchini Somalia watu wapatao 19 wameuawa baada ya gari lililokuwa na vilipuzi kulipuka kwenye mgahawa wa Pizza na hoteli jirani ya Posh mjini Mogadishu. Kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab kimekiri kuhusika na shambulio la leo lililolenga wateja waliokwenda kufuturu kwenye mgahawa huo ambapo hata hivyo walinzi wa mgahawa huo waliua wanamgambo watano wa kikundi hicho. [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wazee waongezeka limeonya shirika la WHO

Kusikiliza / Wazee mara nyingi hutelekezwa wakati mwingine na ndugu zao. (Picha:UN/Logan Abassi)

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kwamba ukatili dhidi ya wazee unaongezeka kote duniani. Katika kuadhimisha siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee duniani, utafiti mpya uliofadhiliwa na WHO na kuchapishwa na jarida la kimataifa la afya la Uingereza, Lancet umebaini kwamba mzee 1 kati ya 6 anakabiliwa na ukatili. Takwimu hizo ni kubwa kuliko [...]

15/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Elimu ni haki ya binadamu

Kusikiliza / Brian Messenger.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/F.Nducha)

Matumaini yetu ni kuelimisha watoto milioni sita duniani kwa kutoa mafunzo kwa walimu milioni moja ifikapo mwaka 2030 kote ulimwenguni. Hiyo ni kauli ya Brian Messenger Afisa Masoko wa kimataifa kutoka shule ya kimataifa ya Perkins iliyoko mji wa Boston jimbo la Massachusetts, Marekani ambayo ni ya watu wenye ulemavu wa macho au wasioona, inayofanya [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji na wakimbizi wanyanyaswa na kushikiliwa bila ridhaa yao Libya-IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema linatiwa hofu na hali ya takribani wakimbizi na wahamiaji 260 wa Somalia na Ethiopia wakiwemo watoto wanaoshikiliwa na wasafirishaji haramu wa binadamu au magenge ya wahalifu nchini Libya bila ridhaa yao. Kwa mujibu wa IOM picha za video zilizosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa facebook Juni [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031