Nyumbani » 14/06/2017 Entries posted on “Juni 14th, 2017”

Ukatili dhidi ya wazee waongezeka limeonya shirika la WHO

Kusikiliza / Wazee mara nyingi hutelekezwa wakati mwingine na ndugu zao. (Picha:UN/Logan Abassi)

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kwamba ukatili dhidi ya wazee unaongezeka kote duniani. Katika kuadhimisha siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee duniani, utafiti mpya uliofadhiliwa na WHO na kuchapishwa na jarida la kimataifa la afya la Uingereza, Lancet umebaini kwamba mzee 1 kati ya 6 anakabiliwa na ukatili. Takwimu hizo ni kubwa kuliko [...]

14/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wawatoa mamilioni katika umasikini kwa kutuma fedha nyumbani

Kusikiliza / Mfanyakazi wa duka la upokeaji fedha Somalia akihesabu noti. Picha na UM/Stuart Price.

Kiwango cha fedha kinachotumwa na wahamiaji kwa familia zao nyumbani kimeongezeka na kufikia asilimia 51 katika muongo uliopita kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa Jumatano na mfuko wa kimataifa wa ufadhili kwa maendeleo ya kilimo IFAD. Utafiti umejikita katika kipindi cha miaka kumi ya wahamiaji kutuma fedha nyumbani walikotoka ambacho ni kati ya 2007 hadi [...]

14/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake bado wana fursa ndogo katika ajira-ILO

Kusikiliza / Picha:ILO/Video Capture

Pengo la kijinsia limesalia moja ya changamoto inayokabili dunia katika masuala ya kazi, hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kazi duniani ILO inayosema kwamba wanawake wana fursa ndogo zaidi ya kushikiri kwenye soko la ajira ikilinganishwa na wanaume. Ripoti hiyo iitwayo Ajira duniani na mtizamo wa kijamii- Mwelekeo kwa wanawake 2017, [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyanya apanda mbegu ya imani kwa wakimbizi-Uganda

Kusikiliza / Nyanya ambaye alikaribisha wakimbizi katika shamba lake.(Picha:UNHCR/Video Capture)

Mgogoro na njaa nchini Sudan Kusini ukiendelea, wananchi wamelazimika kukimbilia nchi jirani zikiwemo Uganda, Sudan, Ethiopia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya kati kusaka hifadhi. Jamii nchini Uganda zimetoa mfano wa kuigwa kwa kufungua nyumba zao na kuwakirimu wakimbizi hao. Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon anakutana na mwanamke mwenye umri [...]

14/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Suluhu pekee ya vita Afghanistan ni amani-Guterres

Kusikiliza / sg

Vita nchini Afghanistan suluhu yake sio mtutu wa bunduki, amesema Jumatano Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipotoa wito kwa pande kinzani nchini humo kusaka kwa pamoja suluhu ya kiasa ya vita vinavyoendelea. António Guterres amefanya ziara ya kwanza nchini humo kama Katibu Mkuu ambako amekutana na maafisa wa serikali na watu waliotawanywa na machafuko [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Uchangiaji Damu, WHO inasema okoa maisha leo

Kusikiliza / Uchangiaji damu nchini Ethiopia.(Picha:WHO/Ethiopia)

Leo ni Siku ya Kuchangia Damu Duniani , ambapo Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mwaka huu linalenga uchangiaji damu katika dharura, hususan kwa wale wanaotaka kusaidia. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Unaweza kufanya nini? Changia damu. Changia sasa. Changia mara kwa mara “, yenye kuhamasisha [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takwimu zenye aina ya ulemavu zahitajika

Kusikiliza / Wawakilishi wa Tanzania mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/A.Massoi)

Haitoshi kuwa na takwimu za watu wenye ulemavu pekee, kinachohitajika ni takwimu za kina ili kuwezesha mipango, wamesema wawakilishi wa jamii za watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Zanzibar. Katika mahojiano kandoni mwa mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu unaoendelea mjini New York, Marekani, Haidari Madowea ambaye ni mwenyekiti wa [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo vya raia Syria inasikitisha-Pinheiro

Kusikiliza / Paulo Pinheiro, mwenyekiti wa Kamisheni ya Uchunguzi kuhusu Syria. Picha ya UN/Jean-Marc Ferré

Mgogoro nchini Syria unaendelea kusababisha madahara makubwa kwa raia ambao wanabeba gharama kubwa ya vita vilivyodumu kwa zaidia ya miaka sita sasa amesema mkuu wa tume ya uchunguzi kwa ajili ya Syria. Akitoa taarifa ya maendeleo kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis jumatano ,Paulo Pinheiro,mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi ametoa wito [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Picha mpya za setilaiti kusaidia kubaini baa la nzige

Kusikiliza / Picha:FAO/Carl de Souza

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema taarifa kutoka setilaiti zinatumika kama njia mpya ya kubaini mazingira bora ya nzige kuzaliana na hivyo kuweza kuchukua hatua mapema kabla wadudu hao hawajashambulia mazao na kusababisha uhaba wa chakula. Mbinu hiyo ambayo tayari imejaribiwa Algeria, Morocco na Mali, inafuatia ushirikiano kati ya wataalamu wa FAO na [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid atoa kauli sakata la kidiplomasia dhidi ya Qatar

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amezungumzia sakata la kidiplomasia dhidi ya Qatar akitaka hatua zichukuliwe haraka ili kuepusha kuzorota zaidi kwa haki za binadamu. Kamishna Zeid amenukuliwa akisema kuwa hivi sasa mvutano huo uliosababisha Falme za kiarabu, Misri na Bahrai kukata uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi [...]

14/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uongozi kwa wanawake wenye ulemavu bado ni safari ndefu- Seneta Omondi

Kusikiliza / Seneta Omondi ambaye ni mwanamke mwenye ulemavu akiwakilisha kundi la wanawake na wasichana wenye ulemavu. (Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili/J.Msami)

Licha ya kwamba hatua zimepigwa katika utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu katika nchi mbali mbali ikiwemo Kenya,  bado kuna walakin kwa baadhi ya watu wakiwemo wanawake wanoishi na ulemavu. Hayo ni kwa mujibu wa Seneta wa viti maalum kutoka Kenya Godliver Omondi katika mahojiano maalum na Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 10 [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031