Nyumbani » 13/06/2017 Entries posted on “Juni 13th, 2017”

Messi, Neymar wasaidia watoto wakimbizi-UNHCR

Kusikiliza / UNHCR kwa kushirkiana na klabu ya kandanda ya Barcelona wazindua #SignAndPass campaign yaani Tia sahihi na utoe pasi. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirkiana na klabu ya kandanda ya Barcelona, leo wametangaza kampeni kubwa ya pamoja ya kupigia chepuo usaidizi kwa watoto wakimbizi ijulikanayo kwa Kiingereza The #SignAndPass campaign yaani Tia sahihi na utoe pasi. Kampeni hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano wa wachezaji nyota akiwamo Leonel Messi na Neymar [...]

13/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushirika waleta nuru kwa wakimbizi Uganda

Kusikiliza / Kikundi cha wavuvi wakiwemo wakimbizi nchini Uganda. Picha: UNHCR/Video capture

Nchini Uganda, kitendo cha nchi hiyo kuwezesha wakimbizi kutangamana na wenyeji katika shughuli za kujikwamua kiuchumi, kimeleta ahueni kubwa kwa wakimbizi, fursa ambayo ni nadra sana kuipata kwingineko wanakopatiwa hifadhi,. Uganda pamoja na kuwezesha wakimbizi kupata ardhi ya kulima na hata kujenga makazi, sasa inaruhusu wenyeji na wakimbizi kujiunga katika vikundi vya ushirika ambavvyo kwavyo [...]

13/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia waendelea kuuliwa, kujeruhiwa Ukarine-UM

Kusikiliza / Wazee ni waathirka zaid wa vita vinavyoendelea Ukraine Mashariki. Picha: IOM/UN/Volodymyr Shuvayev

Uvunjifu wa makubaliano ya usitishaji wa mapigano umesababisha kuongezeka kwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mgogoro nchini Ukraine, Umoja wa Mataifa umesema leo. Ujumbe wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Ukraine (HRMMU), umesema kuwa kati ya Februari na Mei mwaka huu umesajili vifo 36 na majeruhi 157 vitokanavyo na [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki na sauti za watu wenye ulemavu vijumuishwe kwenye SDGs- Hungbo

Kusikiliza / disabilities 3

Mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu COSP10, umeanza leo mjini New York, Marekani ukiwaleta pamoja nchi wanachama 173 wa mkataba huo kutoka sehemu mbalimbali duniani. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu idara ya uchumi na masuala ya kijamii [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa ICT wabonga bongo kuhusu SDGs

Kusikiliza / Wasichana washikamana kuonyesha ujuzi wao katika teknolojia. Picha: ITU

Zaidi ya wataalamu 2,500 wa teknolojia ya habari na mawasiliano ICT wanakutana mjini Geneva, Uswisi, kwa siku tano kuanzia jumatatu juma hili, ambapo wanabadilishana ujuzi na uzoefu lengo likiwa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Mkutano huo wa kimataifa kuhusu upashanaji wa taarifa (WSIS Forum 2017 ) , kwa mwaka huu ukiwa chini ya uenyekiti [...]

13/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Takwimu sahihi za albino ni muhimu kufanikisha usaidizi- Al Shaymaa

Kusikiliza / Mwanaharakati Al Shaymaa Kwegyr kutoka Tanzania.(Picha:Idhaa ya Kiswahili kwa idhini ya Al Shaymaa)

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ulemavu wa ngozi au ualbino, mwanaharakati Al Shaymaa Kwegyr kutoka Tanzania ametaka tafiti zaidi juu ya takwimu kuhusu kundi hilo. Bi. Al Shaymaa ambaye alikuwa mbunge wa kwanza mwenye ulemavu wa ngozi, ameiambia idhaa hii kuwa.. (Sauti ya Al Shaymaa) Amesisitiza pia elimu akinukuu methali [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuwe makini udhibiti wa ugaidi usichochee machungu- Guterrres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kadri vitisho vitokanavyo na misimamo mikali vinavyozidi kuchanua, ni vyema kuhakikisha mbinu za kudhibiti hazileti matatizo. Bwana Guterres amesema hayo leo huko Ashgabat, Turkmenistan kwenye kikao cha ngazi ya juu cha kutathmini jinsi mataifa ya Asia ya Kati yanavyotekeleza mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makombora yakirindima Raqqa, UNHCR yahaha kufikia wahitaji

Kusikiliza / Mhuduhumu wa afya akiwa na watoto walionusurika kifo baada ya bomu la kutegwa ardhini kulipuka.(Picha:UNHCR/Areej Kassab)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetaka kupatia uwezo zaidi na endelevu wa kufikia makumi ya maelfu ya raia ambao wanahaha kupata msaada kwenye mji wa Raqqa nchini Syria. UNHCR imetoa ombi hilo wakati huu ambapo mapigano makali yanaendelea kwenye mji huo ikitajwa idadi ya wahitaji ni zaidi ya watu 430,000. Kila [...]

13/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini, japo kibarua bado kipo kukomesha ukatili dhidi ya albino:Ero

Kusikiliza / Haki za albino. Picha: UNHRC

Kuna kila sababu ya kuwa na matumaini katika kuhakikisha ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi unakomeshwa hususani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ambako tatizo hili limemea mizizi. Hayo ni kwa mujibu wa Ikponwosa Ero mtaalamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino akizungumza na [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumizi bora ya maji hukuza mahusiano baina ya nchi-Muigai

Kusikiliza / Mwanasheria Mkuu wa Kenya Githu Muigai.(Picha:Idhaa ya Kiswahili UM/G.Kaneiya)

Mkutano wa nchi wanachama kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria za bahari umeanza jana mjini New York, Marekani, ambapo nchi wanachama wa mkataba wa bahari zimekutana kutathimini utekelezaji wa sheria hizo. Kenya ni miongoni mwa washiriki wa mkutano ambapo Mwanasheria Mkuu wa taifa hilo Profesa Githu Muigai ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031