Nyumbani » 12/06/2017 Entries posted on “Juni 12th, 2017”

Kutoboka kwa kiatu si mwisho wa safari

Kusikiliza / Bosco Niyonkuru, muhudumu mkimbizi ambae amejitolea uhai wake kuwahudumia wengine nchini Uganda. Picha:  Picha: UNHCR/Video capture

Nchi ya Uganda inasifiwa kwa kupokea wakimbizi wengi na kuwajumuisha katika jamii kwa kuwapa kazi, ardhi na fursa za kujiendeleza. Mbali na changamoto nyingi anazokumbana nazo , mmoja wa wakimbizi hao anatumia fursa hiyo kujisaidia na kuwasaidia wengine. Sikiliza makala hii ya Amina Hassan yenye kusimulia zaidi.

12/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tusibabaike na kukosolewa kwa UNRWA bali tuiunge mkono:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM / Jean-Marc Ferré

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anawasiwasi na kukosolewa hadharani kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Palestina, UNRWA na uadilifu wake, lakini anaunga mkono na kupongeza mchango wake katika ulinzi wa haki za mamilioni ya wakimbizi wa Palestina walio Mashariki ya Kati. Amesema UNRWA inafanya kazi katika hali ngumu ya kivita, [...]

12/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mifumo ya hiari pekee haitoshi kulinda haki za wafanyakazi

Kusikiliza / Maria Grazia Giammarinaro.(Picha:UM/Paulo Filgueiras)

Mtaalamu huru wa Usafirishaji haramu wa binadamu hususan wanawake na watoto, Maria Grazia Giammarinaro, amewasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu hii leo, akisema ajira ya watoto na biashara ya watoto wahamiaji ndio iliyo ngumu zaidi kugundua na kugakua, na hivyo ataipa kipaumbele zaidi katika mamlaka aliyopewa. Wakati huo huo, wajumbe wa [...]

12/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali CAR bado tete, MINUSCA iendeleze wito wa amani-Anyanga

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu nchini CAR Parfait Onanga- Anyanga.(Picha:UM/Kim Haughton)

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kama ilivyo katika ripoti nambari (S/2017/473) ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kupitisha ajenda inayohusu CAR. Katika mkutano wa leo, baraza limeangazia hali ya kiusalama nchini CAR, husuani kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya raia pamoja na wafanyakazi wa Ujumbe [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ahadi ziende sanjari na vitendo katika kuwahifadhi wakimbizi-Grandi

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria Muhammed na nduguye Yousef  uhifadhi waliopata hifadhi  Gänserndorf, Austria, Novemba 2015.  (Picha© UNHCR/Mark Henley)

Wakati mahitaji ya makazi yakiongezeka kimataifa , sanjari na ongezeko la idadi ya wakimbizi, kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi Filippo Grandi, jumatatu ametoa wito wa kuongeza idadi ya maeneo kwa ajili ya kuhifadhi wakimbizi katika nchi ya tatu. Kwenye ufunguzi wa majadiliano ya kila mwaka na serikali na mashirika yasiyo [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hifadhi kwa wanawake wahanga sio hiari-Šimonoviæ.

Kusikiliza / Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonoviæ akihutubia mkutano wa 61 wa tume kuhusu hali ya wanawake CSW hapo machi 2017 jijini New York. Picha: UM/Rick Bajornas

Nchi zinapaswa kuwapatia hifadhi ya malazi wanawake ambao ni wahanga wa vitendo vya ukatili kulingana na sheria ya haki za binadamu, amesema leo Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonoviæ. Mtaalamu huru huyo ameliambia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi wakati akiwasilisha ripoti yake, kuwa amri ya [...]

12/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO na mwongozo mpya kuepusha ajira za watoto

Kusikiliza / FAO watoa mwongozo mpya kuepusha ajira za watoto. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limezindua mwongozo mpya unaoonyesha hatua zinazopaswa kuchukuliwa na watunga sera ili kuepusha watoto kutumikishwa mashambani pindi mizozo inapokumba jamii zao. Mwongozo huo umetangazwa hii leo ambayo ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto, FAO ikisema majanga yanapoibuka watoto wanatengana na familia zao na hivyo sekta ya [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kukomesha ukatili dhidi ya albino, nchi lazima zishirikiane-UM

Kusikiliza / mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi , Ikponoswa Ero (Kushoto).  Picha: UNI/Tanzania

Ukatili na ubaguzi unaowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi au albino hautomalizika hadi pale nchi zitakaposhirikiana kuukomesha. Onyo hilo limetolewa Jumatatu katika taarifa ya mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Ikponwosa Ero, katika kuelekea siku ya kimataifa ya kuelimisha dhidi ya ulemavu wa ngozi au Albino, inayoadhimishwa [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 65 zahitajika kunusuru wakimbizi wa DRC huko Angola:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wacongomani wawasili Chissanda, Lunda Norte, Angola wakitoroka vita vinavyaendelea Kasai, DRC. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake wanasaka dola milioni 65 ili kusaidia ongezeko la wakimbizi wanaowasili Angola kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , DRC. Tangu mwezi Aprili wakimbizi 30,000 wamewasili Angola katika mji wa Luanda jimbo la Norte, wakikimbia machafuko katika jimbo la Kasai. Mapigano baina ya [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majanga na vita ni kichocheo cha utumikishwaji watoto-ILO

Kusikiliza / Mtoto mchnugi mifugo Translyvania.(Picha:ILO/Marcel Crozet)

Takriban watoto milioni 168 wahanga wa utumikishwaji wa watoto wanaishi katika maeneo kunakoshuhudiwa vita na majanga. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la kazi ulimwenguni, ILO katika taarifa yake ya siku ya kimataifa ya kupinga utumikishwaji kwa watoto inayoadhimishwa kila mwaka Juni 12. Maadhimisho ya mwaka huu [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031