Nyumbani » 09/06/2017 Entries posted on “Juni 9th, 2017”

Jamii ya Wagungu yalinda utamaduni wake kupitia muziki

Kusikiliza / Ngoma za kitamaduni za nchini Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Kibego)

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni , UNESCO, linapigia chepuo ukuzaji wa tadamduni mbalimbali za makabila na jamii tofauti ili kulinda urithi. Nchini Uganda moja ya kabila dogo kwenye ufalme wa Bunyoro liitwalo Bagungu linalinda utamuduni wake kwa kuhifadhi nyimbo za kale. Ungana na John Kibego katika Makala ifuatayo.    

09/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhifadhi wa mazingira hususan Afrika

Kusikiliza / Uchafuzi kwenye msitu wa serikali nchini Tanzania. Picha: John Kibego

Mapema juma hili, dunia imeadhimisha siku ya mazingira, siku ambayo huadhimishwa Juni tano ya kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu ni utengamano na asili, ukilenga kuhakikisha ulinzi wa maliasili za mazingira ili kukuza uendelevu wa viumbe na sayari dunia. Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP na wadau  wake,  wametumia maadhimisho hayo [...]

09/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa bahari umefanikiwa, lakini kazi itaendelea:UM

Kusikiliza / Rais wa baraza kuu Peter Thomson. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Siku tano zilizoghubikwa na mikutano, mijadala na vikao takribani 150 na maonyesho 41 katika mkutano wa kimataifa wa bahari kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa hapa New York hatimaye zimefunga mlango hii leo ijumaa. Mkutano huo wa bahari uliowaleta pamoja wadau mbalimbali zaidi ya 1000, zikiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, watalaamu wa [...]

09/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Walinda amani 3 wauawa na 8 wajeruhiwa huko Mali

Kusikiliza / Maziko ya mlinda amani wa MINUSMA.(Picha: MINUSMA/Harandane Dicko)

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa wameuawa na wengine wanane wamejeruhiwa katika matukio mawili tofauti huko kidal, kaskazini mwa Mali. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari hii leo kuwa tukio la kwamza lilitokana na kituo cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Mali, MINUSMA kushambuliwa kwa kombora ambapo walinda [...]

09/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mipango ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu lazima iwe na ufanisi:UM

Kusikiliza / Kumbukumbu ya biashara ya utumwa. Picha: UM

Biashara nyingi lazima zijitoe kimasomaso kukabiliana na unyanyasaji kazini unaohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu amesema mtaalamu wa haki za binadamu Ijumaa. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Maria Grazia Giammarinaro, akihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis amesema hatua za hiyari zilizopo zinahitaji kufafanuliwa zaidi na ziwe zenye ufanisi. Kwa mujibu wa [...]

09/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kazakhstan ni muhimu katika ustawi wa Asia ya Kati- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM

Umoja wa Mataifa umesema unapenda kuona eneo la Asia ya Kati linakuwa na amani na ustawi, hivyo ushirikiano zaidi unatakiwa baina ya nchi za ukanda huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuanza ziara yake nchini Kazakhstan. Amesema udau kati ya Umoja [...]

09/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Mfasiri na Mkalimani

Kusikiliza / Picha :Idhaa ya Kiswahili

Wiki hii tunaangazia maneno Mfasiri na Mkalimani na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema mfasiri ni yule anayetafsiri neno au maneno kwa maandishi na mkalimani ni mtu anayeelezea kwa mdomo maneno yanayosemwa wakati ule ule kutoka lugha moja hadi nyingine .

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Ethiopia yaongoza katika baa la njaa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Wachungi nchini Ethipia watafutia mifugo lishe na maji. Picha: UNDP

Mamilioni ya watu Ethiopia, Djibouti, Kenya na Somalia wanakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kuonekana katika miongo, kutokana na ukosefu wa mvua na kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi wa ndani na mipakani, imesema leo ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM. Taarifa ya Amina Hassan inafafanua zaidi (TAARIFA YA AMINA) Mkurugenzi wa [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha ya watoto 40,000 shakani Ar Raqqa, Syria-UNICEF

Kusikiliza / Wakimbizi wanaokimbia kutoka eneno la Raqqa nchini Syria.(Picha:UNICEF/UN039561/Soulaiman)

Mashambulizi mazito mjini Ar-Raqqa nchini Syria yanatishia maisha ya zaidi ya watoto 40,000 ambao wanasalia mtegoni mwa hatari kubwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. UNICEF imesema imepokea taarifa za kutisha kwamba takribani watoto 25 wameuawa na kujeruhiwa katika mshambulizi ya hivi karibuni zaidi mjini humo, shule na hospitali zikiwa zimeshambuliwa, [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchunguzi wa kimataifa ufanyike dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu DRC- Zeid

Kusikiliza / Watu wakusanyika wakati wa maandamano nchini DRC mnamo Disemba 2016.(Picha:MONUSCO)

Tuna wajibu kwa wahanga na jukumu la kutuma ujumbe kwa wahusika wa uhalifu wa ukiukaji wa haki za binadamu na, kwamba tunawafuatilia na jumuiya ya kimataifa inatia uzito kuhakikisha ukwepaji wa sheria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC unakomeshwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Kauli hiyo imetolewa Ijumaa na kamishina mkuu [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanaoishi ufukweni Kenya kuneemeka- Karigithu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa idara ya kitaifa ya masuala ya bahari iliyoko chini ya wizara ya usafirsihaji nchini humo, Nancy Karigithu.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Wakati mkutano wa kimataifa kuhusu bahari ukifika ukingoni hii leo, Kenya imesema imeandaa mkakati maalum wa kuhakikisha jamii zinazoishi katika fukwe za bahari zinanufaika na uwepo wa bahari. Akizungumza na idhaa hii mjini New York Marekani, Katibu Mkuu wa idara ya kitaifa ya masuala ya bahari iliyoko chini ya wizara ya usafirsihaji nchini humo, Nancy [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wavuvi walalama kipato kidogo Tanzania

Kusikiliza / Boti za wavuvi. Picha: FAO

Mkutano wa kimataifa kuhusu bahari ukifikia tamati hii leo, nchini Tanzania wavuvi kutoka mkoani Tanga, wameesema kuwa sababaui kadhaa zikiwamo mabadiliko ya tabanchi zimesababaisha kupungua kwa samaki katika bahari ya Hindi. Katika mahojiano na Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo, wavuvi hao Rajabu Madaraka na Ali Mkada wamesema juhudi zaidi za [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031