Nyumbani » 08/06/2017 Entries posted on “Juni 8th, 2017”

Yemen si makazi salama kwa mtoto- UNICEF

Kusikiliza / Mtoto anahudumiwa katika hospitali ya Sab'een huko Sana'a nchini Yemen. Ni mmoja wa watoto waathirika wa kipindupindu. Picha: © UNICEF/UN065873/Alzekri

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema Yemen hivi sasa si pahala salama kwa makuzi ya mtoto kwa kuwa hali ni mbaya kupita kiasi. Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Geert Cappelaere amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani wakati huu ambapo inaelezwa [...]

08/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dunia itupie macho visiwa vya Afrika kulinda bahari: Dk Tizeba

Kusikiliza / Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba.Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Macho yote yameelekezwa kwenye visiwa vya Magharibi, hili lapaswa kukoma! Ni kauli ya Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba wakati akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu bahari unaoendelea mjini New York. Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii, Dk Tizeba ameitaka jumuiya ya kimataifa kutozisahau nchi zinazoendelea zenye visiwa [...]

08/06/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani Colombia:Guterres

Kusikiliza / Kitengo cha Umoja wa Mataifa nchini Colombia cha kukusanya silaha. Picha: UN Mission in Colombia

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani nchini Colombia na hususani , kukamilika hapo jana kwa uwasilishaji wa asilimia 30 ya kwanza ya silaha za FARC-EP kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anonio Guterres Alhamisi kupitia taarifa ya msemaji wake, [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika ikamate fursa ya biashara za kidijitali- UNCTAD

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi.(Picha:UM/Jean-Marc Ferre)

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezindua ripoti yake kuhusu mwelekeo wa uwekezaji duniani kwa mwaka huu wa 2017. Ripoti hiyo pamoja na mambo mengine inaangazia kuongezeka kwa kasi ya uchumi utokanao na biashara ya kidijitali, biashara ambayo hufanywa kwa njia ya mtandao. Mathalani mtu kununua vitu kwenye tovuti na hatimaye [...]

08/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hongera Lesotho kukamilisha uchaguzi kwa amani-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akifungua jukwaa la kimataifa la kiuchumi huko St. Petersburg nchini Urusi.  Picha: courtesy/TASS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres , amewapongeza watu wa ufalme wa Lesotho kwa kukamilisha uchaguzi wa bunge kwa amani na usalama. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu mkuu ameisifu kazi ya tume huru ya uchaguzi nchini humo kwa kuandaa uchaguzi huo kidemokrasia na pia jukumu la jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika [...]

08/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takataka zamwezesha kusomesha watoto wake

Kusikiliza / Sulubu Kisima Nzai.(Picha:UNIC Nairobi)

Mkutano kuhusu masuala ya bahari ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, nchini Kenya mkazi mmoja wa Malindi kwa miaka 12 amekuwa akiokota takataka baharini na ufukweni ambazo zimemwezesha kubadili maisha ya familia yake. Sulubu Kisima Nzai akihojiwa na Karim Said wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Gharama za uingizaji chakula kimataifa zapanda-FAO

Kusikiliza / Mchujo wa mpunga nchini Ufilipino.(Picha:FAO/Joseph Agcaoili)

Kimataifa soko la bidhaa za chakula limetengamaa kutokana na usambazaji mkubwa wa ngano, mahindi na mbegu. Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO ongezeko la gharama za usafirishaji na uingizaji wa kiasi kikubwa cha bidhaa , utaongeza gharama za usafirishaji wa bidhaa kimataifa na kufikia zaidi ya dola trilioni 1.3 kwa [...]

08/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi wa Sudan Kusini waingia Kenya

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini wanawasili kambini Kakuma nchini Kenya. Picha: UNHCR-Kenya-Nadapal-Kakuma

Idadi ya raia wa Sudan Kusini wanaongia nchini Kenya wakikimbia mzozo nchini mwao inazidi kuongezeka. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini humo limesema tangu mwezi Januari mwaka huu wakimbizi wapya 772 wamesajiliwa kwenye kituo cha muda cha Nadapal, ambacho hata hivyo uwezo wake ni wakimbizi 500. Kituo hicho kipo mpakani mwa [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ya afya kwa wananchi bado inasiginwa- Baraza

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wanapea chanjo watoto. Picha: UNICEF

Maeneo mbali mbali duniani hivi sasa haki ya msingi ya kupata huduma ya afya kwa binadamu bado inasalia ndoto. Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Kate Gilmore amesema hayo akihutubia kikao cha 35 cha Baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi hi leo ambacho kimeangazia haki ya msingi ya watu kupata huduma ya [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ISIL yakatili maisha ya mamia ya raia wanaokimbia Mosul-UM

Kusikiliza / Makazi mengi yameharibiwa Mosul, Iraq.(Picha: UNHCR/Ivor Prickett)

Taarifa za kuaminika zinaonyesha kwamba raia zaidi ya 231 waliokuwa wakijaribu kukimbia Mashariki mwa mji wa Mosul nchini Iraq wameuawa tangu Mei 26, wakiwemo 204 kati yao waliouawa katika kipindi cha siku tatu wiki iliyopita. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiorodhesha visa vya raia kutumiwa kama ngao ya vita na [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria na elimu visaidie kulinda bahari

Kusikiliza / Savana,14 (kushoto) na Kathryn 19, Kutoka Trinidad na Tobago ambao wanachagiza ulinzi wa bahari.(Picha:UM/Lulu Gao)

Bahari zetu, mustakhbali wetu, hiyo ndio kauli mbiu ya siku ya bahari duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 8. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (TAARIFA YA ASSUMPA) Katika hafla maalumu ya kuadhimisha siku hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa msukumo umetolewa katika kutambua uzuri, umuhimu na udhaifu wa bahari, na mikakati ya kuchua [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031