Nyumbani » 07/06/2017 Entries posted on “Juni 7th, 2017”

Mkataba wa amani Libya unafanyiwa marekebisho- Kobler

Kusikiliza / 03-18-2014-benghazi-Libya-07JUNE17-350-300

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler amesema hali ya amani nchini humo bado si shwari sana na mwelekeo wa utekelezaji wa mkataba wa amani una nuru kidogo. Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kutoka Tunis, Tunisia, Bwana Kobler amesema ingawa kuna muafaka [...]

07/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mama akisema ndio hakuna atakayesema hapana!

Kusikiliza / Kulea

Mila na desturi za baadhi ya makabila duniani zinataka mtoto wa kike aolewe tu punde baada ya kubalehe. Msingi mkuu wa mila hii ni fikra potofu ya kwamba mtoto wa kike hana msaada wowote kwa familia yake zaidi ya kwenda kuolewa na kuzaa watoto. Miongoni mwa makabila hayo ni wasamburu huko Afrika Mashariki na hususan [...]

07/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres atoa ujumbe kuhusu shambulizi Iran

Kusikiliza / Mtazamo wa bustani ya Nowruz, Tehran, Iran. Picha: UN Information Centre Tehran

Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa António Guterres amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika hii leo katika kaburi la Ayatollah Ruhollah Khomeini na jengo la bunge au Majlis katika mji mkuu wa Iran, Tehran. Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Iran na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi, akisema anatumai [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya matumaini bado kuna shaka ya uwekezaji wa kigeni duniani – UNCTAD

Kusikiliza / Uwekezaji wa kigeni unalenga sekta mbali mbali ikiwemo ya usafirishaji.(Picha:Benki ya Dunia/Video capture)

Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, FDI unatarajiwa kuongezeka duniani kwa asilimia Tano kwa mwaka huu wa 2017. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya kamati ya maendeleo na biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyochapishwa hii leo ikisema kuwa ongezeko hilo lina thamani ya dola trilioni 1.8. UNCTAD imesema ongezeko hilo limetokea [...]

07/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Teknolojia yaweza kusaidia maendeleo kwa amani na utu-Guterres

Kusikiliza / AI-WIPO 1

Wadau wakuu wa uwezo wa masuala ya teknolojia AI na wale wa mambo ya kibinadamu wanakutana na viongozi wa viwanda na taaluma katika mkutano wa kimataifa uliopewa jina Yote kwa wema. Mkutano huo unafanyika mjini Geneva, Uswisi, ambapo mjadala unahusu namna AI inavyoweza kusaidia juhudi za kukabili umasikini, njaa na kuwezesha elimu na afya pamoja [...]

07/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya watoto washamiri DRC- MONUSCO

Kusikiliza / Watoto nchini  DRC .(Picha:UNICEF/M.Gonzalez)

Jumla ya visa 40 vya ukatili dhidi ya watoto vimeripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kati ya tarehe 29 mwezi uliopita wa Juni na tarehe 5 mwezi huu vikitekelezwa na vikundi vilivyojihami. Mratibu wa mawasiliano ya umma wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, Théophane Kinda amewaeleza waandishi wa habari mjini [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa ajira kwa vijana duniani utatuliwe-Uganda

Kusikiliza / Mkutano wa 106 wa kila mwaka Shirika la kazi duniani ILO mjini Geneva.(Picha:ILO/Crozet / Pouteau)

Mkutano wa 106 wa kila mwaka Shirika la kazi duniani ILO unaendelea mjini Geneva Uswisi ambapo wafanyakazi, waajiri na wawakilishi wa serikali wanakutana kwa takribani majuma mawili wakijadili mambo kadhaa ikiwamo uhamaji wa wafanyakazi, usalama na afya kwa kundi hilo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Mada nyingine zinazojadiliwa katika mkutano huo ni [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki ya Dunia yaimarisha mtandao wa barabara Ghana

Kusikiliza / Wachuuzi wauza bidhaa zao katikati ya magari katika trafiki huko Tema, Ghana. Picha: Jonathan Ernst / World Bank (maktaba)

Benki ya Dunia imeridhia mkopo wa dola milioni 150 kwa ajili ya mradi wa kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini Ghana, TSIP. Fedha hizo zitasaidia ukarabati wa barabara zinazounganisha maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kutoka Tamale hadi Tatale ambako ni mji wa mashariki wa mpakani na Togo. Henry Kerali ambaye ni mkurugenzi wa benki hiyo [...]

07/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya 100,000 kufaidika na msaada wa China Chad:WFP

Kusikiliza / Msaada wa chakula wawasili nchini Chad.(Picha: WFP/Adel Sarkozi)

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha mchango wa kitita cha dola milioni 4 zilizotolewa na Uchina , ambazo zitawapa ahuweni watu zaidi ya laki moja wanaohitaji msaada nchini Chad. Eneo la ziwa Chad limeghubikwa na machafuko yaliyosababisha mgogoro wa kibinadamu, hivyo mchango huo wa Uchina kwa mujibu wa WFP [...]

07/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia bado ni changamoto katika elimu-UNESCO

Kusikiliza / Wanafunzi wasichana katika maabara ya sayansi. Picha: UNESCO

Licha ya hatua kubwa iliyopigwa katika kupanua fursa za elimu, usawa wa kijinsia katika elimu unasalia kuwa changamoto kubwa. Kwa mujibu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, wasichana wengi zaidi wako shule hii leo kuliko wakati mwingine wowote, lakini sababu za kijamii, kiuchumi na ubaguzi wa kijinsia zinawazuia wasichana hao kupata fursa sawa [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni wazi kuwa wanawake ndio wanaoteseka zaidi katika vita-Owusu

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Eugene Owusu akihutubia mkutano wa wanawake. (Picha:UNMISS)

Jukwaa la wazi Kimataifa kwa ajili ya Wanawake linafanyika wiki hii jijini Juba, Sudan Kusini kujadili usawa wa kijinsia, ukatili wa kijinsia, ubaguzi, ndoa za shuruti na za mapema ili hatimaye kuwawezesha wanawake katika ngazi zote kuleta amani. Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mifumo thabiti ya kimataifa ni muarobaini wa ulinzi wa bahari -DK Tizeba

Kusikiliza / Dkt. Tizeba2

Mfumo thabiti wa sheria za kimataifa unahitajika ili kulinda bahari ambayo ina manufaa katika uchumi hususani kwa nchi zinazoendelea , amesema Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba. Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa baada ya kuhutubia mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya bahari unaoendelea New York, Marekani, Dkt. [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031