Nyumbani » 06/06/2017 Entries posted on “Juni 6th, 2017”

Maji, amani na usalama havitengamani-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Maji, amani na usalama ni vitu vinavyohusiana. Wakati huu ambapo mahitaji ya maji safi yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 40 ifikapo katikati ya karne hii, na huku mabadiliko ya tabianchi yakiongeza athari, upungufu wa maji ni suala mtambuka linaloongeza hofu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye kikao cha baraza [...]

06/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Simulizi za wakimbizi wa ndani nchini Nigeria

Kusikiliza / Boussam Abdulahi, mmoja wa wakimbizi wa ndani nchini Nigeria waliopoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya Boko Harram. Picha: UNHCR/Video capture

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, watu zaidi ya milioni mbili katika maeneo ya bonde la ziwa Chad wamepoteza makazi yao kufuatia mashambuzizi ya Boko Haram. Wakimbizi na watu katika eneo hilo ikiwemo Nigeria wanahitaji msaada wa dharura, na makumi ya maelfu ya watoto wako hatari kupata magonjwa yanayosababishwa [...]

06/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nguli Grenier ateuliwa balozi mwema wa mazingira

Kusikiliza / Mcheza filamu nguli wa Marekani Adrian Grenier, ameteuliwa na UNEP  kuwa balozi mwema wa mazingira.(Picha:UNEP)

Mcheza filamu nguli wa Marekani Adrian Grenier, ameteuliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP kuwa balozi mwema wa mazingira. Nguli huyo anatarajiwa kupigia chepuo upunguzwaji wa matumizi ya plastiki na ulinzi wa viumbe vya baharini. Taarifa ya UNEP kuhusu uteuzi huo inasema kwamba mcheza filamu huyo mashuhuri kadhalika atawashawishi mashabiki wake kuwa [...]

06/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dunia inahitaji “mapinduzi” katika huduma ya afya ya akili:UM

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya afya , Dainius Pûras. Picha: UM/Jean-Marc Ferré

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya afya , Dainius Pûras, ametoa wito wa mabadiliko katika huduma ya afya ya akili kote duniani , akizitaka nchi na wataalamu wa afya ya akili kuchukua hatua kwa ujasiri kufanyia mapinduzi mfumo uliokumbwa na mtafaruku ambao umejengeka katika hulka zilizopitwa na wakati. Akiwasilisha ripoti yake kwenye [...]

06/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu milioni watia saini kupinga matumizi ya plastiki-UM

Kusikiliza / Mkaguzi wa bahari wa UNEP akiogelea ndani ya bahari kuliko na taka taka.(Picha:UNEP)

Kampeni ya Avaaz imetoa wito kwa serikali za dunia kupiga marufuku matumizi ya plastiki katika miaka mitano ijayo. Kampeni hiyo ambayo imetiwa saini na watu milioni moja itawasilishwa kwa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP ili kuunga mkono harakati zake za kuwa na bahari safi kwa kukomesha uchafu baharini. Mkurugenzi wa UNEP Erik [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanasiasa wasio na aibu wanasigina katiba za nchi zao – Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Raa'd Al Hussein ameeleza masikitiko yake juu ya vitendo vya baadhi ya wanasiasa kutokuwa na aibu kutokana na matendo yao yanayoleta machungu kwa wananchi wao. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Masikitiko hayo ya Zeid yamo kwenye hotuba yake ya kurasa nane [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maamuzi kwenye mkutano wa UM kuhusu bahari ni ya muhimu sana

Kusikiliza / Douglas McCauley mwanabailojia na mtaalamu wa viumbe vya baharini , na Mkurugenzi wa mradi  wa Benioff Ocean katika chuo kikuu cha California. Picha: UM

Maamuzi yanayofanyika wiki hii kwenye mkutano wa kimataifa wa bahari yataweza kutoa muongozo wa mustakhbali wa mabadiliko ya bahari katika maelfu ya miaka ijayo. Huo ni mtazamo wa mmoja wa wanasayansi mahiri aliyeko kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa juma hili akihudhuria mkutano huo. Douglas McCauley mwanabailojia na mtaalamu wa viumbe vya baharini , [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada kwa ajili ya elimu wapungua mwaka wa sita mfululizo-UNESCO

Kusikiliza / Mtoto darasani.(Picha:UNESCO/ Florida Valle, Colombia)

Kiwango cha fedha za msaada kwa ajili ya elimu kimeporomoka kwa mwaka wa sita mfululizo imesema leo ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO iliyotolewa Jumanne. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Ripoti hiyo ya ufuatiliaji wa elimu kimataifa (GEM) iitwayo "Msaada kwa elimu unadorora na kutowafikia [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii imuandae mwanamke tangu utoto alete mabadiliko:Upendo

Kusikiliza / Upendo, mwanasiasa chipukizi nchini Tanzania. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Mtandao wa viongozi wanawake barani Afrika utawezesha wanawake kuwa wapatanishi wa amani katika jamii zao na kujenga viongozi bora amesema Mwakilishi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa mtandao wa viongozi wa Afrika uliomalizika mjini New York Marekani Upendo Peneza. Akizungumza katika mahojiano maalum baada ya kuhudhuria mikutano ya mtandao huo, [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahari ni ajira kwa vijana-Freeman

Kusikiliza / Bwana Freeman katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Vijana waweza kukuza kipato kupitia bahari na kufanikisha kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs amesema mwakilishi ni mwakilishi wa kudumu wa vijana wa Kenya katika ofisi za Umoja wa Mataifa Samuel Freeman. Katika mahojiano na idhaa kandoni mwa mkutano wa siku tano kuhusu bahari unaondelea mjini New York Marekani Bwana Freeman amesema uwepo wao katika [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031