Nyumbani » 05/06/2017 Entries posted on “Juni 5th, 2017”

Ukatili wanaoushuhudia watoto Iraq ni wa kutisha:UNICEF

Kusikiliza / Mwanamke mkimbizi akimbeba mwanae kusini mwa Mosul. Picha:UNICEF/USA

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema leo kuwa limepokea ripoti za kushtua zenye idadi kubwa ya vifo vya watu, vikijumuisha watoto kaskazini mwa Mosul nchini Iraq, watoto ambao wanashuhudia visa vya kinyama ambavyo kamwe hakuna mtu anapaswa kushuhudia. UNICEF inasema takriban wasichana na wavulana 100,000 wamo katika hatari kubwa, wakijikuta [...]

05/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sasa si wakati wa kunawa mikono kuhusu Israel/Palestina

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, (Picha:UN/Jean-Marc Ferré)

Wakati huu sio wakati wa kukata tamaa katika kutafuta suluhu ya amani ya mataifa mawili katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanza kwa mapigano baina ya Waarabu na Waisrael ya mwaka 1967. Amesema miongo na miongo, kizazi [...]

05/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Afrika inahitaji mageuzi katika amani-Mongella

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi Gertrude Mongella.(Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Baada ya kuundwa na kukutana mjini New York Marekani kwa siku tatu, mtandao wa viongozi wanawake wa Afrika, umeazimia pamoja na mambo mengine kuhakikisha bara hilo linajikomboa katika migogoro kisha kupiga hatua za kimaendeleo. Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni mwanasiasa nguli kutoka Tanzania, aliye pia mwanaharakati wa wanawake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy [...]

05/06/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uhifadhi wa kompyuta au simu wachangia uhifadhi wa mazingira Burundi

Kusikiliza / Uhiadhi wa kompiuta au simu ni moja ya mikakati ya kuhifadhi vyema mazingira. Picha: UNEP

Kawaida likija swala la  kuhifadhi mazingira , katika nchi zinazoendelea  watu hufikiria haraka swala la  mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa hewa ikiwemo uhifadhi wa miti , mito na kadhalika. lakini je  unajua  kuwa uhifadhi wa komputa au simu ni moja  ya mikakati ya kuhifadhi vyema mazingira? Nchini Burundi , sehemu nyingi  na ofisini [...]

05/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yaomboleza kifo cha ghafla cha mkurugenzi mtendaji wake

Kusikiliza / Babarunde 4

Kwa masikitiko makubwa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA limetangaza kifo cha mkurugenzi wake mtendaji, Dr. Babatunde Osotimehin,kilichotekea ghafla usiku wa Jumapili nyumbani kwake . Alikuwa na umri wa miaka 68. UNFPA inasema hili ni pigo kubwa kwa shirika hilo na kwa watu wote hususani wanawake, wasichana na vijana aliojitolea [...]

05/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazibagui- Mugabe

Kusikiliza / Spokesman addresses the press on behalf of SG on the US withdraw from the Paris Agreetment

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amehutubia mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya bahari jijini New York, Marekani akisema kuwa ubia hasa usaidizi wa kiufundi ni muhimu ili kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yatokanayo na uchafuzi wa bahari. Amesema hata hivyo kwa nchi yake ubia huo hasa katika kutelekeza lengo namba 14 la malengo ya [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya mazingira duniani, asili ilindwe ili kulinda dunia:UNEP

Kusikiliza / Vijana wakazi wa msitu wa taifa la Tapajos waogelea katika mto wakati wa joto makali. Picha: UM/Eskinder Debebe (maktaba)

Utangamano na asili ndiyo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa leo kote duniani ikipigia chepuo uhifadhi na ulinzi wa maliasili za mazingira kwa mustakabali bora wa viumbe na sayari. Akizungumiza siku hiyo K atibi Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bahari ,ardhi, misitu , maji na hewa tunayovuta ni [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Kusikiliza / Mwendazake Babatunde Osotimehin! Amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 68.(Picha:UNFPA)

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin, amefariki dunia. Amina Hassan na taarifa zaidi. (Taarifa ya Amina) Nats.. Mwendazake Babatunde Osotimehin! Amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 68. Raia huyu wa Nigeria, ameongoza UNFPA tangu mwaka tarere Mosi Januari mwaka 2011 akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahari ina uhusiano na kila mmoja wetu inatufanya tuishi-Guterres

Kusikiliza / Watoto baharini nchini Timor Leste.(Picha:UN/DESA)

Bahari ina uhusiano na kila mmoja wetu, inatufanya tuendelee kuishi, lakini uhusiano huo sasa uko mahskani kuliko wakati mwingine wowote. Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatatu katika mkutano maalumu ulioanza leo Juni 5 kuhusu masuala ya bahari na hasa lengo la maendeleo endelevu nambari 14. Guterres amesema mkutano huo utakaomalizika [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin akihutubia jukwaa la maendeleo ya afya kwa wanawake ulimwenguni jijini New York Marekani. Picha: UN Photo/Loey Felipe

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin, amefariki dunia hii leo. Alikuwa na umri wa miaka 68. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kushtushwa na kifo hicho akisema kuwa Babatunde alikuwa bingwa wa utetezi wa ustawi wa wanawake na [...]

05/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tutamkomboa mwanamke katika maneo yenye migogoro-Gertrude Mongella

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi  Getrude Mongella ambaye ni mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa wanawake kutoka Tanzania. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Utatuzi wa amani katika maeneo yenye migogoro na ukombozi wa wanawake katika maeneo hayo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa na mtandao wa viongozi wa Afrika waliohitimisha mkutano wao mwishoni mwa juma mjini New York Marekani. Katika mahojiano na idhaa hii  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi  Getrude Mongella ambaye ni [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasiki:Guterres

Kusikiliza / Mandhari nzuri ikionesha malia asili ya duniania, mlima, mabonde na bahari. Katika siku ya Mazingira Duniani. Picha na UNEP

Bahari,  ardhi, misitu , maji na hewa tunayovuta ni mazingira yetu ambayo ni viungo muhimu katika mustakhbali dunia. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 5 na kuongeza (GUTERRES CUT 1) "Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasikini au [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031