Nyumbani » 01/06/2017 Entries posted on “Juni 1st, 2017”

Twasikitishwa na Marekani kujitoa mkataba wa Paris- UM

Kusikiliza / Spokesman addresses the press on behalf of SG on the US withdraw from the Paris Agreetment

Umoja wa Mataifa umesema hatua ya Marekani kujitoa hii leo kutoka mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ni jambo la kusikitisha katika jitihada za kimataifa za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi na kuendeleza usalama wa ulimwenguni. Msemaji wa Umoja huo Stephane Dujarric amesema hayo alasiri hii mbele ya wanahabari akisema hatua hiyo imetangazwa na [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za upasuaji kwa wagonjwa Fistula -sehemu ya Pili

Kusikiliza / Tuwede ambaye alipokea matibabu ya Fistula na kurejelea maisha ya kawaida.(Picha:UNFPA Zimbabwe/Nikita Little)

Katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mtaalamu wa afya kutoka mkoani Kagera nchini Tanzania  Dk Martin Lwabilimbo, tunaelezwa kile ambacho kinafanyika baada ya upasuaji wa kurekebisha Fistula, ugonjwa ambao unaondoa utu wa mwanamke. Mathalani Dokta Lwabilimbo amemweleza Nicolaus Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM mkoani humo kuwa, mgonjwa akishafanyika upasuaji [...]

01/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IFAD yaelimisha uvuvi salama huko Indonesia

Kusikiliza / Mvuvi nchini indonesia. Picha: IFAD

Kuelekea mkutano wa kimataifa kuhusu bahari, tunaelekea huko nchini Indonesia, ambako mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD unashirikiana na jamii za wavuvi ili kulinda bahari ikiwemo matumbawe ambayo ni mazalia ya samaki. Indonesia ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa uvuvi na uuzaji nje wa samaki na uvuvi wote huo hufanyika na wavuvi [...]

01/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri na si porojo- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akifungua jukwaa la kimataifa la kiuchumi huko St. Petersburg nchini Urusi.  Picha: courtesy/TASS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mabadiliko ya tabianchi ni wimbi kubwa linalokumba dunia hivi sasa na ni lazima lishughulikiwe ili kurejesha imani na usalama ulimwenguni. Akifungua jukwaa la kimataifa la kiuchumi huko St. Petersburg nchini Urusi amesema ingawa baadhi ya nchi zinaamini kuwa mabadiliko ya tabianchi ni porojo zisizo na msingi [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sasa siku za uvuvi haramu zahesabiwa- FAO

Kusikiliza / Boti za uvuvi. Picha: FAO

Harakati za kutokomeza uvuvi haramu zinazidi kung'ara baada ya Japan na Montenegro kutia saini mkataba wa kimataifa wa kudhibiti uvuvi huo. Makubaliano hayo yaitwayo Port State Measures , au PSMA yanahusisha zaidi ya theluthi mbili za sekta ya uvuvi duniani yakileta pamoja nchi wanachama zipatazo 50. PSMA imeundwa kuzuia meli za uvuvi kujihusisha na uvuvi [...]

01/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tusipomakinika viumbe hai watatoweka

Kusikiliza / Kuhakikisha mazingira bora pia ni haki ya binadamu. Picha: UNHCR

Hatuwezi kufurahia haki zetu za msingi za kibinadamu bila ya mazingira bora, huo ni ujumbe wa Mtaalamu Huru wa Haki za Binadamu kuhusu Mazingira, John H. Knox katika kuelekea Siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 05. Amesema wanasayansi wanahofu kwamba kwa mara ya kwanza katika miaka milioni 60, ulimwengu umo mwanzoni mwa awamu [...]

01/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pamoja na hatua katika vita dhidi ya AIDS, bado kuna pengo:Ripoti

Kusikiliza / Picha:UNAIDS

Wajibu wa kimataifa, kugawana jukumu la fedha, na mtazamo unaozingatia usawa miongoni mwa watu vimekuwa chachu kubwa ya mafanikio katika vita dhidi ya ukimwi, imesema ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iloyowasilishwa leo Alhamisi kwenye baraza kuu. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA YA AMINA) Ripoti hiyo "vita dhidi ya ukimwi kama chachu [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa wanawake viongozi Afrika wazinduliwa New York

Kusikiliza / Dkt. Asha-Rose Migiro,Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Msami)

Mtandao wa wanawake viongozi barani Afrika umezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ukileta pamoja viongozi wa kisiasa na kitaaluma kwa lengo la kuchagiza ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa na ile ya 2063 ya Muungano wa Afrika, AU. Lengo la mtandao huo unaochagizwa na Umoja wa Mataifa, AU na serikali ya Ujerumani ni [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani wa UNAMID auawa Nyala Sudan

Kusikiliza / Kamanda wa majeshi azuru eneo la tukio la kigaidi Darfur magharibi nchni Sudan. (Maktaba). Picha: UN Photo/Albert González Farran

Mlinda amani wa mpango wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNAMID ameuawa na kundi la watu wasiojulikana baada ya kuteka gari lao mjini Nyala jimbo la Darfur Kusini. UNAMID imelaani vikali shambulio hilo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Tukio hilo limeripotiwa kwa mamlaka ya Sudan na [...]

01/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sheria mpya Misri yakandamiza mashirika ya kiraia- Zeid

Kusikiliza / Raia nchini Misri wafanya maandamano kuomba haki zao. Picha: UNHCR

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ametaka serikali ya Misri ifute sheria mpya kuhusu utendaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo akisema ni kandamizi. Amenukuliwa na ofisi ya haki za binadamu akisema kuwa sheria hiyo namba 70 ya mwaka 2017 inabinya nafasi ya haki za binadamu [...]

01/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM inafanya uchunguzi Kakuma na Dadaab Kenya

Kusikiliza / Wafanyakazi wa IOM wakiendesha shughuli zake katika kambi nchini Kenya.(Picha:IOM)

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limesema Alhamisi linafanya uchunguzi dhidi ya shutuma za utovu wa nidhamu katika kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab nchini Kenya. Ofisi ya mkaguzi mkuu wa IOM ndio inayoendesha uchunguzi huo ikihusisha timu ya wataalamu wa upelelezi. Na endapo uchunguzi huo utathibitisha kuwepo kwa utovu wa nidhamu [...]

01/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini CAR sasa ukilinganisha na 2014-Gilmour

Kusikiliza / CAR 1-6-17car 1

Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ya mwaka 2014 iliyoghubikwa na hofu, machafuko, mauaji, kuporomoka kwa uchumi na zahma ya kibinadamu, sio CAR ya sasa inayotia matumaini. Kauli hiyo imetolewa na Andrew Gilmour msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu ambaye amehitimisha ziara ya siku nne nchini humo. Bwana Gilmour amesema ameshuhudia kuimarika kwa [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu juu ya maisha ya watoto walio kwenye nyumba za malezi- UNICEF

Kusikiliza / Romania_Anamaria Dinulescu ROMA_2016_MPS_002

Shirika Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema bado kuna pengo kubwa juu ya idadi halisi ya watoto wanaoishi kwenye makazi ya malezi. Katika ripoti yake hii leo, UNICEF imesema takwimu kutoka nchi 140 imeonyesha kuwa takribani watoto milioni 2.7 wanaishi katika nyumba hizo za malezi au familia za ulezi maeneo mbali mbali ulimwenguni, [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031