Nyumbani » 30/06/2017 Entries posted on “Juni, 2017”

Sanaa yaleta nuru na kujiamini kwa wakimbizi Kakuma

Kusikiliza / Sanaa yatumika kuinua vipaji vya wakimbizi huko Kakuma nchini Kenya. Picha: UNHCR/Video capture

Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeibuka na mbinu mpya ya kuwezesha wakimbizi kuondokana na tabia ya baadhi ya watu kuwaona wao si binadamu kwa kuwa ni wakimbizi. Mbinu hiyo ilibuniwa na mwanamuziki mashuhuri nchini humo na sasa inaleta siyo tu nuru kwa wakimbizi bali pia kujiamini na kujitambua. je [...]

30/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ndogo ndogo na mchango wake katika fursa za ajira

Kusikiliza / biz

Juni 27 ni siku ya kimataifa ya biashara ndogo ndogo na zile za wastani. Siku hii ambayo imeadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu wa 2017 baada ya kupitishwa na azimio la Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa inalenga kuhimiza umuhimu wa sekta ya biashara ndogo ndogo na zile za wastani katika kutimiza maendeleo endelevu. [...]

30/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini Cyprus licha ya ugumu uliopo- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kati) ashiriki mkutano wa kimataifa kuhusu Cyrpus. Picha: UM/Video capture

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameshiriki mkutano wa kimataifa kuhusu Cyprus na kuonyesha kuwepo na matumaini kwa nchi hiyo kurejea tena katika taifa moja. Akizungumza na waandishi wa habari huko Crans-Montana nchini Uswisi baada ya kuongoza mkutano huo, Bwana Guterres amenukuu washiriki wa mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana wakieleza kuwa [...]

30/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 1.7 Sudan Kusini hataraini kukumbwa na njaa

Kusikiliza / Raia nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Takribani watu milioni mbili nchini Sudan Kusini wako hatarini kukumbwa na njaa kali licha ya tangazo la hivi karibuni kuwa njaa si tishio tena katika baadhi ya maeneo nchini humo. Onyo hilo limetolewa na shirikisho la msalaba mwekundu duniani, IFRC, shirika ambalo ni mdau wa Umoja wa Mataifa, wakati huu ambapo mzozo unaendelea Sudan Kusini [...]

30/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Licha ya mzozo, wakimbizi wa Syria warejea nyumbani- UNHCR

Kusikiliza / Mjini Aleppo. wakimbizi warejea nyumbani. Picha: © UNHCR/Hameed Marouf

Idadi ya raia wa Syria wanaoishi ukimbizini nje ya nchi yao au wale walio wakimbizi wa ndani imeripotiwa kuimarika. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema wakimbizi hao wanarejea kwa hiari kwa mipango yao wenyewe ambapo sababu kubwa ni kuangalia makazi yao au familia zao huko Aleppo, Hama, Homs na Damascus baada [...]

30/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki- Songobingo, Sokomoko na Segemnege

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno songobingo, sokomoko na segemnege. Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Bwana Nuhu anasema Songobingo inatokea wakati ambapo hakuna uelewa wa kinachoendelea linatumika kuonyesha uzito wa jambo, na Sokomoko ni wakatia [...]

30/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe mpya wa UM Burundi akutana na Rais Nkurunziza

Kusikiliza / Mjumbe mpya maalumu wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Burundi Michel Kafando. Picha: UM/Ky Chung

Mjumbe mpya maalumu wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Burundi Michel Kafando amefanya ziara nchini humo kujitambulisha katika jukumu lake la kusaidia kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo. Kuangazia ziara hiyo hii hapa ni ripoti ya mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga akiripoti kutoka Bujumbura. (Taarifa ya Kibuga) Bwana Michel Kafando amekuwa [...]

30/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo endelevu bila kujali haki za binadamu ni bure- Mtaalamu

Kusikiliza / sdgsmall

Wakati dunia inaendelea na mchakato wa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, serikali na wafanyabiashara wametakiwa kuweka sheria na kanuni zinazoweka mbele maslahi ya watu na si faida. Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema hay oleo huko Paris, Ufaransa wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu maadili ya kibiashara ya uwajibikaji. Mmoja [...]

30/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu yaongezeka machafuko yakishika kasi CAR-UNHCR

Kusikiliza / Mvulana aliyefurushwa makwao akiwa kambini ya Bria nchini CAR.(Picha:UNHCR/Cassandra Vinograd)

Kuzuka upya kwa machafuko yanayoshuhudiwa katika baadhi ya sehemu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kunalitia hofu shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Machafuko hayo mapya baina ya makundi ya ulinzi na makundi mengine yenye silaha yanaendelea katika miji ya Zemio, Bria na [...]

30/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wenyeji na wakimbizi wagombania rasilimali Bunj, Sudan Kusini-UNHCR

Kusikiliza / Watoto na wakazi wa Upper Nile nchini Sudan Kusini huku wafanyakazi wa UM wakiwa ziarani(Maktaba). Picha: UM/JC McIlwaine

Wakati mzozo wa Sudan Kusini ukizidi kushika kasi, katika mji mdogo uitwao Bunj,uliopo jimboni Uppern Nile, nuru inaangaza kwani msimu wa mvua umeleta ahueni kutokana na maporomoko ya maji yanaleta uzima kwa nyasi na mazao ambazo awali zilikauka. Lakini licha ya hayo,uwepo wa wakimbizi zaidi ya 140,000 waliojihifadhi humo kuanzia mwaka 2013 pale mapigano yalipoanza, [...]

30/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wachangia uchumi licha ya changamoto

Kusikiliza / Wakimbizi wa Mali

“Africa Shares” ni jukwaa la kimataifa la kutambua michango ya wakimbizi katika uchumi wa nchi zinazowahifadhi. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR tayari limetambua juhudi za wakimbizi katika nchi saba barani Afrika zikiwemo Kenya, Burkina Faso, Ethiopia, Rwanda, Zimbabwe, Malawi na Niger. Wakimbizi hawa walihudhuria mkutano wa Africa Shares,yaliyofanyika mjini Geneva Uswisi [...]

29/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa bado imejizatiti kusaidia Libya

Kusikiliza / Maria do Valle Ribeiro. Picha: UNDP

Umoja wa Mataifa umesema shambulio la gruneti dhidi ya msafara wa watendaji wake nchini Libya jana Jumatano halitateteresha azma ya kusaidia kusaka suluhu ya amani ya kudumu nchini humo. Shambulio hilo lilitokea wakati msafara wa magari ukiwa na watu 14 ambapo gruneti lililenga moja ya magari yao na kusababisha majeraha kwa dereva mmoja. Akihojiwa na [...]

29/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Nigeria wasilazimishwe kurejea makwao- UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Nigeria walioko Cameroon. Picha: © UNHCR/D. Mbaiorem

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeonya juu ya hatua yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi wa Nigeria walioko nchini Cameroon kurejea makwao. Katika taarifa yake ya leo, UNHCR imesema wakimbizi hao wanalazimishwa kurejea kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambako mazingira hayajawekwa sawa ili kuwapokea. Onyo hili la sasa limetolewa wakati tayari takribani wakimbizi 900 wa [...]

29/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Miaka 50 ya kukaliwa Palestina bado hakuna suluhu

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu mteule wa UM Bi. Amina J. Mohammed. (Picha:UM)

Katika kuadhimisha miaka 50 ya Israel kukalia eneo la Wapalestina tangu 1967, kamati ya utekelezaji wa haki zisizo na mjadala za watu wa Palestina imeandaa mkutano wa siku mbili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo na kesho Ijumaa ili kutathimini jinsi ya kumaliza ukaliaji huo wa Israel. Jukwaa hilo lililoandaliwa kwa mujibu wa [...]

29/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bila kuhusisha elimu ya mtoto wa kike SDG's haziwezi kufikiwa: UNESCO

Kusikiliza / Wanafunzi darasani. Picha: UNICEF

Elimu ya mtoto wa kike ni muhimu sana katika kusaidia kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG, ifikapo mwaka 2030. Hayo yamesemwa na mkuruguenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova kwenye mkutano maalumu unaofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, hii leo kuhusu lengo la maendeleo nambari 4 [...]

29/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukanda wa tropiki kujadili changamoto na fursa

Kusikiliza / Watoto wakipewa chanjo katika kituo cha afya. Picha: WHO/Video capture

Kwa mara ya kwanza kabisa, Siku ya kimataifa ya nchi zilizo kwenye ukanda wa tropiki inaadhimishwa leo, hizi ni nchi zilizo kati ya tropiki ya cancer na ile ya Capricorn. Maeneo ya Tropiki ni yale ambayo licha ya mabadilko ya hali ya hewa hushuhudia joto na mara chache hali ya hewa hubadilika kwa misimu, na [...]

29/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 6 DRC hawana uhakika wa kupata mlo- FAO

Kusikiliza / Mtoto mwenye utapiamlo nchini DRC.(Picha:UNICEF)

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hali ya chakula inaelezwa kuwa ni mbaya kwenye maeneo ya Kasai, Kivu na Tanganyika huku watu milioni Sita nchini humo wakiripotiwa kuhitaji msaada wa haraka. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC licha ya mzozo wa wenyewe kwa wenyewe kwenye maeneo [...]

29/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kasi yahitajika ili nchi 44 ziridhie CTBT

Kusikiliza / Magdalene Wangui ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi. Picha: Magdalene Wangui

Mkutano wa wataalamu wenye lengo la kubadilishana ujuzi juu ya ufuatiliaji majaribio ya nyuklia ukiendelea huko Vienna, Austria, mshiriki kutoka Kenya ametoa wito kwa ushirikiano zaidi ili nchi nyingi zaidi ziridhie mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya silaha hizo, CTBT. Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kando ya mkutano huo, mshiriki kutoka Kenya, Magdalene [...]

29/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlango wa UNOCI kufungwa rasmi Juni 30

Kusikiliza / Walinda amani wa UNOCI.(Picha:UNOCI/flickr)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha hatua ya kufungwa rasmi kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire (UNOCI) hapo kesho Juni 30 baada ya kupata mafanikio makubwa. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa , Guterres amepongeza juhudi za mpango huo na umakini wa kubadili ukurasa wa machafuko na [...]

29/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto waendelea kubeba gharama za zahma Sudan-UNICEF

Kusikiliza / Watoto katka kijiji cha Sewelinga Drfur Kaskazini nchini Sudan.(Picha:Mohamad Almahady, UNAMID.)

Dola milioni 22 zinahitajika haraka na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa zaidi ya watoto 100,000 nchini Sudan. Katika miezi kadhaa iliyopita shirika hilo linasema Sudan imekabiliwa na hali kadhaa za dharura ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa kuharaka katika majimbo 12 kati ya 18 ya [...]

29/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baada ya kuhutubia New York, mwanafunzi kutoka Tanzania apanga mwelekeo

Kusikiliza / Saul kwenye presser

Kijana Saul Mwame kutoka Tanzania ambaye ameshiriki mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba nne la elimu ametaja hatua atakazochukua pindi tu akirejea nyumbani. Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili jijini New York, Marekani Saul ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari [...]

29/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna hatua kubwa katika kupunguza hatari za silaha za maangamizi-UM

Kusikiliza / Izumi Nakamistu mwakilishi wa ngazi ya juu katika idara ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa.(Picha:UM/Manuel Elias)

Kuna hatua kubwa zilizopigwa na nchi wanachama katika miaka kadhaa iliyopita kwenye kupunguza hatari ya kuenea kwa silaha za maangamizi. Hayo yamesemwa leo na Izumi Nakamistu mwakilishi wa ngazi ya juu katika idara ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa akitoa taarifa kwenye baraza la usalama lililokuwa likijadili kudhibiti kuenea kwa silaha za maangamizi. (SAUTI [...]

28/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sarakasi yatumika kujenga amani na upendo Sudan Kusini

Kusikiliza / Wanafunzi wanaoshiriki sarakasi kwa ajili ya kuchagiza amani.(Picha:UNIfeed/video capture)

Nchini Sudan Kusini, shirika moja lisilo la kiserikali limeibuka na mbinu mpya ya kuimarisha amani, upendo na maridhiano baina ya jamii kwenye taifa hilo changa zaidi duniani. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimejenga chuki baina ya raia, na hivyo kukwamisha ndoto ya maendeleo ambayo wananchi walikuwa nayo tarehe 9, Julai 2011 walipotangazwa huru. Je nini [...]

28/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumieni fursa hii muhimu kwa ajili ya amani Cyprus-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Evan Schneider

Pande zote katika mazungumzo ya Cyprus lazima zitumie fursa hii ya kihistoria kufikia muafaka, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Jumatano. Ujumbe wake umewasilishwa Uswis na Jeffrey Feltman, msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa , katika mazungumzo yaliyoanza tena mjini in Crans-Montana kuhusu mgawanyiko wa kisiwa cha Cyprus. Bwana [...]

28/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia waliokwama Al-Raqqa wanahitaji ulinzi haraka

Kusikiliza / Wamama, wanaume na watoto waliokwama Al-Raqqa, Syria kutokana na kushika kasi kwa mashambulizi ya anga na ardhini. Picha: UNICEF/UN039561/Soulaiman

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein leo ameelezea hofu yake kuhusu hatma ya raia waliojikuta katikati ya mashambulizi ya kupinga ISIL mjini Al-Raqqa, Syria ambako watu takribani 100,000 wamekwama kutokana na kushika kasi kwa mashambulizi ya anga na ardhini. Idadi ya vifo na majeruhi ambao ni raia imeendelea kuripotiwa huku njia [...]

28/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi wa sera muhimu kuboresha ajira ya wahamiaji-ILO

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Guy Ryder. Picha: UM

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha utawala wa masuala ya uhamiaji na kupata njia mpya za kuboresha maisha na hali ya kazi ya wafanyakazi wahamiaji, amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Guy Ryder, akibainisha kuwa asilimia 74 ya wahamiaji wenye umri wa kufanya kazi wapatao milioni 150 wako katika soko la ajira na [...]

28/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wadau wakutana kujadili elimu jumuishi na yenye usawa

Kusikiliza / Saul Paul Mwame akihutubia kikao cha Baraza Kuu jijini New York.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu lengo namba nne la maendeleo endelevu SDGs linalotaka elimu jumuishi na yenye usawa pamoja na fursa kwa wote umeanza leo mjini New York Marekani, ukiwaleta pamoja wadau ili kutoa msukumo katika kutimiza lengo hilo. Flota Nducha na taarifa zaidi. (TAARIFA YA FLORA) Kwaya ya vijana kutoka Afrika Kusini ikitoa [...]

28/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa ustawi wa wahamiaji waanza Ujerumani

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria mpakani wakisaka uhifadhi nchini Iraq (Picha:UNHCR/G.Gubaeva)

Mkutano wa siku tatu kuhusu maendeleo ya wahamiaji hususani mitizamo chanya kwa kundi hilo umeanza mjini Berlin nchini Ujerumani, ambapo kiwa ni siku ya kwanza wito wa kuhakikisha wahamiaji wananufaika na jamii wanakoishi umetolewa. Viongozi katika ufunguzi wa mkutano huo wametoa ahadi za kuimarisha usimamizi kwa wakimbizi kimataifa, na ustawi wa kiuchumi kwa wahamiaji. Mkutano [...]

28/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwekeza kwa watoto masikini kuna thamani kubwa: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto mchanga. Picha: UNICEF

Kuwekeza katika afya kwa watoto masikini na jamii zao kuna thamani kubwa, na kunaokoa maisha karibu mara mbili kwa kila dola milioni moja zinazotumika kama uwekezaji mbadala kwa makundi yasiyojiweza. Hii ni kwa mujibu wa uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF hii leo. Utafiti huo unaonyesha [...]

28/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia wakumbwa na vikwazo- Wataalamu

Kusikiliza / Maandamano kwa ajili ya usawa wa kijinsia.(Picha:UN Women/maktaba)

Harakati za kusongesha haki za wanawake zinakabiliwa na vikwazo vikubwa maeneo mengi duniani, wamesema wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo. Katika taarifa yao iliyotolewa Geneva, Uswisi, wataalamu hao wa kikosi kazi cha udhibiti wa ubaguzi dhidi ya wanawake kisheria na kivitendo, wamesema dunai sasa iko njiapanda kwa kuwa hoja ya usawa wa kijinsia [...]

28/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sharti la kufunga Al Jazeera ni pigo kwa uhuru wa habari- Mtaalamu

Kusikiliza / Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza David Kaye. Picha: UM/Manuel Elias

Kitendo cha nchi Nne za kiarabu kutaka Qatar ifunge chombo chake cha habari Al Jazeera kama moja ya masharti 13 ya kuondolewa vikwazo dhidi yake ni za kusikitisha. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza David Kaye amesema hayo leo akigusia sharti lililotolewa na Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Falme za kiarabu [...]

28/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wazazi timizeni wajibu wenu kwa watoto kuhusu elimu-Saul

Kusikiliza / Saul Mwame.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/video capture)

Saul Mwame, mwanafunzi wa kidato cha nne shule ye sekondari DCT Mvumi mkoani Dodoma, Tanzania, ni miongoni mwa watoa hotuba leo katika kusanyiko la kimataifa mjini New York, Marekani linalojadili lengo namba nne la maendeleo endelevu SDGs linalotaka elimu jumuishi na yenye usawa. Saul ni mwasisi wa taasisi ya kujenga mustakabali wa Afrika BAF, ambayo [...]

28/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bima ya afya ndio muarobaini wa afya kwa wote- Tanzania

Kusikiliza / Mhudumu wa afya na mgonjwa kwenye wodi moja hospitalini Tanzania. Picha: WHO

Jukwaa la afya barani Afrika likikunja jamvi hii leo huko Kigali nchini Rwanda, Tanzania imesema moja ya suluhu za kudumu ya afya kwa wote ni kuwa na bima ya afya kwa kila mwananchi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya  amesema hayo akihojiwa na Idhaa kutoka [...]

28/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres ziarani Washington DC

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:Jean-Marc Ferré/maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani kwenye mji mkuu wa Marekani, Washington DC akisaka kufahamisha wajumbe wa baraza la Kongresi la nchi hiyo kuhusu umuhimu wa kazi za umoja huo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephané Dujarric amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa hii leo Bwana Guterres amekutana na [...]

27/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto kubwa kwa wajane ni kusomesha

Kusikiliza / Mmoja wa wamama wajane kutoka Tanzania.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/N.Ngaiza)

Miongoni  mwa changamoto zinazowakabili wajane ni elimu kwa watoto, amesema mjane Elizabeth Mputa, mkazi wa Pangani, Tanga Tanzania. Mjane huyo mwenye umri wa miaka 42 amemweleza Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm, mkoani hapo,  mikasa aliyokumbana nayo baada ya mmewe kufariki ikiwemo kushitakiwa kutokana na madeni. Ungana naye katika mahojiano.

27/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ndani ya Syria ina taswira tofauti-De Mistura

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani nchini Syria.Picha: UN Photo/ Kim Haughton

Staffan de Mistura, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria ametoa taarifa hii leo kwenye baraza la usalama kuhusu mchakato wa amani katika taifa hilo la Mashariki ya Kati. Amesema hali ndani ya Syria ina taswira tofauti, na wakati kukiwa na maendeleo chanya kwa kiasi fulani, pia taifa hilo liko katika majaribio [...]

27/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya Cyprus ni fursa ya kipekee, Guterres atiwa matumaini-UM

Kusikiliza / Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa kuamua mustakhbali wa Cyprus, Espen Barth Eide.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Mazungumzo mapya ya kuamua mustakhbali wa Cyprus yafanyika kwa muda wowote utakaohitajika lakini sio hakikisho kwamba yatazaa matunda amesema leo mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mchakato huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis, Espen Barth Eide amesema mazungumzo hayo sio nafasi ya miwsho ya kufikia muafaka baina ya upande wa Cyprus [...]

27/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jukwaa la kupinga ugaidi mitandaoni limekuja wakati muafaka-UM

Kusikiliza / Uhuru wa kutumia mitandao. Picha: UNESCO

Umoja wa Mataifa umekaribisha jukwaa la kimataifa la mtandao wa intanet katika kukabiliana na ugaidi, juhudi ambazo zinawalenga watumiaji wa mitandao hiyo kutounga mkono  magaidi na wenye misimamo mikali kwa watumiaji wa mitandao mbalimbali. Kampuni inayounda jukwaa hilo ni Facebook, Twitter na YouTube na Microsoft. Akikaribisha hatua hiyo Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa [...]

27/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Habari njema, Kipindupindu chapungua Yemen-WHO

Kusikiliza / Watoa huduma wa afya wakihudumia mgonjwa nchini Yemen.(Picha:WHO)

Habari njema! Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema katika juma lililopita idadi ya visa vya kipindupindu nchini Yemen, taifa linalokabiliwa na machafuko imepungua, hata hivyo shirika hilo limeonya kwamba katika msimu wa sikukuu ya Eid al-Fitr watu wengi nchini humo husafiri hatua inayoweza kuongeza maambukizi. Zaidi ya watu 200,000 wameambukizwa ugonjwa huo, zaidi ya 1000 [...]

27/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ndogo ndogo ndio ziimarishwe kukwamua uchumi – UNCTAD

Kusikiliza / Biashara ndogo ndogo Kakuma, Kenya.(Picha:UN Habitat/Julius Mwelu)

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema maendeleo ya kidijitali yana fursa kubwa katika kuinua biashara ndogo na za kati duniani. Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii kuhusu siku ya kimataifa ya wajasiriamali wa kati na wadogo inayoadhimishwa hii leo. Amesema UNCTAD inaiga mfano [...]

27/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ILO yaunda mkakati wa kuinua vijana wajasiriamali

Kusikiliza / Wajasiriamali wadodo wadogo wachangia uchumi. Picha; ILO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wajasiriamali wa kati na wadogowadogo, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamezindua mkakati wa kimataifa wa kuhakikisha kazi bora kwa vijana ili kuinua ajira kwa kundi hilo. Makakati huo unasimamiwa na shirika la kazi ulimwenguni ILO, ambalo limesema kuwa ni jukwaa mahususi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya [...]

27/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubunifu katika afya waleta nuru Afrika

Kusikiliza / Jukwaa la kwanza la afya barani Afrika limeanza kikao chake cha siku mbili huko Kigali, Rwanda. Picha: WHO/Video capture

Jukwaa la kwanza la afya barani Afrika limeanza kikao chake cha siku mbili huko Kigali, Rwanda ambapo ubunifu katika kupatia suluhu magonjwa linapatiwa kipaumbele. Mkuu wa ofisi ya shirika la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti akifungua jukwaa hilo amesema ubunifu na afya mtandao vinasaidia kubadilishana taarifa kati ya watoa huduma na [...]

27/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 52 wafa jangwani Sahara:IOM

Kusikiliza / Wahamiaji jangwani Sahara. Picha: IOM

Wahamiaji 52 wafa jangwani Niger wakati operesheni ya uokozi ya shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM ikifanikiwa kuwanusuru wengine 600 waliokwama Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa shirika hilo Jumapili asubuhi Juni 25 wahamiaji 24 waliuarifu uongozi wa Niger kwamba wamekwama jangwani ingawa haijafahamika walikuwa wametembea kwa muda gani katika jangwa hilo la [...]

27/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tathimini ya hatua ya kupinga majaribio ya nyuklia yafanyika Vienna

Tathmini ya majaribio ya nyuklia Iran:Picha na CTBT

Wataalamu kutoka kila pembe ya dunia wanakutana mjini Vienna, Austria, wiki hii ili kubadilishana ujuzi na maendeleo ya teknolojia katika kufuatilia majaribio ya nyuklia. Mkutano huo wa sayansi na teknolojia 2017 ni miongoni mwa msururu wa mikutano yenye lengo la kuimarisha utekelezaji wa mkataba unaopinga majaribio ya nyuklia (CTBT) ambao unapiga marufuku milipuko ya nyuklia [...]

26/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ya kidijitali yanasua wakazi wa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Matumizi ya simu za rununu yameongezeka ikiwemo barani Afrika.(Picha:UM)

Hivi karibuni kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezindua ripoti yake kuhusu mwelekeo wa uwekezaji duniani kwa mwaka huu wa 2017. Kubwa lililomulikwa katika ripoti hiyo ni namna biashara ya kidijitali  inavyokuwa kwa kasi. mathalani watu hununua vitu mitandaoni na kufikishiwa majumbani kwao. UNCTAD imetaka wafanyabiashara hususani nchi zinazoendelea kutumia fursa [...]

26/06/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Safari ni ndefu lakini kuna matumaini kutokomeza madawa ya kulevya- Guterres

Kusikiliza / Eneo kunakoteketezwa madawa ya kulevya nchini Liberia.(Picha:UNMIL Photo/Staton Winter)

Kwa pamoja ni lazima tutimize ahadi ya wote ili kupunguza biashara, matumizi na madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye ujumbe wake kwa siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya inayoadhimishwa kila Juni 26. Guterres amesema, kwa uzoefu wake anafahamu [...]

26/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kitendo cha kutesa hakiwezi kuhalalishwa kamwe

Kusikiliza / Watoto nchini Syria wafanya maandamano kupinga mateso dhidi ya raia. Picha: UM (Maktaba)

Katika kuadhimisha Siku ya Kupinga Mateso hii leo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema hata kama mataifa yataendelea kutumia mateso kwa kisingizio cha ulinzi wa taifa, bado msimamo ni ule ule, wa kuwa mateso ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mataifa hayo ni lazima yatokomeze hali hiyo. Wamesema sheria za uzuiaji wa mateso [...]

26/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni muhimu kuheshimu na kuthamini mchango wa mabaharia-IMO

Kusikiliza / Bandari ya Felixtowe nchini Uingereza maarufu kwa kusafirisha makontena. Leo ni , Siku ya mabaharia duniani, picha na IMO

Likitanabaisha changamoto zinazowakabili mabaharia, wanawake kwa wanaume wanaosafiri na kufanyakazi ndani ya meli , shirika la kimtaifa la wanamaji IMO, liometoa wito wa kuthamnini mchango wa watu hao. Katika kuadhimisha siku ya mabaharia duniani ambayo kila mwaka huwa Juni 25, Katibu Mkuu wa IMO, Kitack Lim amesema "ingawa ubaharia unaweza kuwa msingi wa kutosheleza ajira [...]

25/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vifo na majeruhi kwenye ajali ya gari la mafuta Pakistan vimenistua:Guterres

Kusikiliza / Stephane Dujarric, Msemajiwa Katibu Mkuu Antonio Guterres kwenye mkutano na waandishi wa habari. 17 Juni 2014. Picha na UM / Jean-Marc FerrŽ

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi kufuatia kulipuka kwa lori la mafuta karibu na mji wa Ahmedpur Mashariki wilaya ya Bahawalpur jimbo la Punjab nchini Pakistan. Kupitia taarifa ya msemaji wake Katibu Mkuu ametuma salam za rambirambi kwa watu na serikali ya Pakistan kufuatia [...]

25/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Twaunga mkono mpango wa Katibu Mkuu kwa Haiti- Baraza

Kusikiliza / Picha: Minustah/Logan Abassi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza azma yake ya kufanikisha utekelezaji wa mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja huo katika kukabiliana na ugonjwa kipindupindu nchini Haiti. Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Juni Balozi Sacha Llorenti amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Port au Prince nchini Haiti, mwishoni [...]

24/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Uganda wapaza sauti wakati wa ziara ya Guterres

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanaosaka hifadhi nchini Uganda. Picha: UNHCR

Shamrashamra kwenye kambi ya Imvepi, iliyoko wilaya ya Arua kaskazini mwa Uganda! Kulikoni? Ni mapokezi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitembelea kambi hiyo wiki hii, katika nchi ambayo ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya milioni moja, wengi wakitoka Sudan Kusini. Uganda imepokea ugeni wa Guterres akiambatana na viongozi kadhaa wa bara [...]

23/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto milioni 5.6 ziwa Chad wamo hatarini

Kusikiliza / Watoto waliotenganishwa na wazazi wao nchini Nigeria baada ya mashambulizi ya Boko Haram. Picha: UNICEF

Zaidi ya watoto milioni 5.6 wako hatarini kupata magonjwa yatokanayo na maji machafu wakati msimu wa mvua ukinyemelea eneo la ziwa Chad, limesema leo Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Ukosefu wa usalama kutokana na migogoro katika ukanda huo pamoja na janga la kibinadamu linalosababishwa na kundi la kigaidi la Boko Haram linahatarisha zaidi hali hii, [...]

23/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya dola milioni 350 zaahidiwa kusaidia wakimbizi Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi wakiwa kambi ya Imvempi nchini Uganda.(Picha:UM/Mark Garten)

Mkutano wa mshikamano na wakimbizi nchini Uganda umekunja jamvi hii leo kwa ahadi za dola milioni 350 za kuisaidia Uganda kukabiliana na dharura ya wimbi la wakimbizi. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu idadi ya wakimbizi nchini humo imeongezeka zaidi ya mara mbili kutoka laki tano na kufikia zaidi ya milioni 1.25. Wengi wa watu [...]

23/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanandoa wenye ulemavu wa kuona wapinga njaa kwa watoto

Kusikiliza / Wanamuziki Amadou na Mariam kutoka Mali.(Picha:WFP/Video Capture)

Kuna usemi usemao, adui yako mwombee njaa! Usemi huu unabeba ujumbe kwamba njaa huangamiza, njaa ni adui mkubwa wa ustawi wa binadamu. Umoja wa Mataifa umeweka lengo la kukomesha njaa kuwa namba mbili katika ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Ili kupigia chepuo kutoweka kwa njaa hususani kwa watoto ambao ni nguvu [...]

23/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Hiba

Kusikiliza / Neno la wiki: Hiba

Wiki hii tunaangazia neno “Hiba” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema neno hiba lina maana mbili, moja ni kitu chochote anachopewa mtu kwa hiari au lengo la kuonyesha mapenzi, na lina maana sawa na idaya, adiya au azizi. Maana ya pili [...]

23/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Uchafuzi wa udongo ni hatari kwa mimea-FAO

Kusikiliza / Uchafuzi wa udongo unamulikwa. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya kuwa uchafuzi wa udongo utokanao na shughuli za kibinadamu una madhara ya moja kwa moja kwa chakula na afya ya binadamu. FAO imesema hayo wakati wa mkutano wa tano wa kimataiaf kuhusu ubia wa udongo uliofanyika mjini Roma Italia, ikitolea mfano wa kemikali kama vile zebaki na nyinginezo [...]

23/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutatua zahma ya wakimbizi Uganda vita lazima viishe Sudan Kusini:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa kwenye mkutano nchini Uganda. Picha: UM/Mark Garten

Suluhu ya wimbi kubwa la wakimbizi barani Afrika tangu mauaji ya Kimbari ya Rwanda ni kumaliza mgogoro wa Sudan Kusini amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres . John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA KIBEGO) António Guterres ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye siku ya pili ya mkutano wa kimataifa wa [...]

23/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jopo la kimataifa kuchunguza ukatili Kasai, Zeid apongeza

Kusikiliza / Timu ya Umoja wa Mataifa ikiwa Tshimbulu Kasai jimbo la kati, DRC,(Picha:MONUSCO/Biliaminou Alao/maktaba)

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio hii leo kuunda jopo la kuchunguza madai ya ukatili kwenye majimbo yaliyoko eneo la Kasai huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein amekaribisha hatua hiyo akisema itatoa fursa ya kuepusha ukwepaji sheria na ni matumaini [...]

23/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kilio cha wajane hakisikiki na hakijaliwi

Kusikiliza / Mama na mtoto katika kituo cha kijiji cha Tumaini cha kuwasaidia wajane, watoto na wanawake walioathiriwa na vita na Ukimwi huko Kigali nchini Rwanda. Picha: UN Women

Leo ni siku ya wajane duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ingawa jukumu la wajane ni kubwa na muhimu katika jamii, bado umuhimu wao hauonekani kwani wamesahaulika, hawamo katika utafiti wala takwimu zozote na haki zao zinapuuzwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi (Taarifa ya Assumpta) Nats.. Ni kilio cha Margaret, mjane mwenye watoto saba ambaye [...]

23/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yasaidia kuzima moto Korma, Darfur

Kusikiliza / Moto katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Korma yateketeza makazi ya wenyeji.(Picha: Lokraj Yogi, UNAMID.)

Nchini Sudan katika jimbo la Darfur, walinda amani wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID waliwezesha kuepusha janga zaidi baada ya kushiriki kuzima moto katika kijiji cha Korma. Hivi sasa wakazi wa eneo hilo kwa usaidizi wa UNAMID wanajaribu kurejea katika maisha ya kawaida baada ya kunusurika na zahma [...]

22/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mbinu mpya yaepusha janga la kibinadamu Sudan Kusini

Kusikiliza / David Shearer Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na Mkuu wa UNMISS. Picha na UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umesema mbinu mpya ya ulinzi wa amani imesaidia kuzuia janga la kibinadamu kwenye jimbo la Upper Nile nchini humo. Mbinu hiyo inahusisha ushirikiano kati ya walinda amani na wafanyakazi wa misaada ambapo UNMISS imesema imetumika kwenye kijiji Aburoc ambako mzozo ulisababisha watu 70,000 kukimbia makazi yao. [...]

22/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani uharibifu wa mnara wa Al Hadba na msikiti wa Al Nuree Mosul

Kusikiliza / Mnara wa Al Hadba Minaret mjini Mosul nchini Iraq.(Picha:UNESCO)

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, Irina Bokova, amelaani uharibifu uliofanywa kwenye msikiti wa Al Nuree na mnara wa Al Hadba Minaret mjini Mosul nchini Iraq. Amesema msikiti na mnara huo ni miongoni mwa maeneo ya urithi ya mji wa Mosul na yalikuwa kama ishara ya utambulisho, [...]

22/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wafadhili wajitumbukize hatarini nasi kuokoa maisha

Kusikiliza /

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inasema kinachoshangaza na kushtua ni kwamba kuna mamia ya mashirika ya kibinadamu ya kutoa misaada katika maeneo yaliyoathirika na majanga ya asili lakini ni dazani moja tu yenye uwezo wa kutoa msaada katika maeneo hatari ya kivita ambayo kwayo watoto, wanawake na majeruhi wanauhitaji zaidi. Akiwasilisha ripoti [...]

22/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ziara ya Guterres Imvepi yawapa matumaini wakimbizi

Kusikiliza / sg 1

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres leo amezuru kambi ya wakimbizi ya Imvepi iliyoko Arua Kaskazini mwa Uganda. Kambi hiyo inahifadhi maelfu ya wakimbizi Kutoka Sudan Kusini. Amepata fursa ya kusikiliza kilio chao n ahata kuwagawia mgao wa chakula. Flora Nducha amezungumza na mwandishi wetu John Kibego aliyeko Imvepi kufuatilia ziara hiyo na anaeleza [...]

22/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame uliofuatiwa na mafuriko watishia uhakika wa chakula Sri Lanka

Kusikiliza / Uharibifu uliyosababishwa na mafuriko nchini Sri Lanka. Picha: IOM

Hali mbaya ya ukame iliyofuatiwa na mvua kubwa iliyoleta mafuriko nchini Sri Lanka imeathiri uzalishaji wa mazao, na kutishia uhakika wa chakula kwa takribani watu 900,000 kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la chakula na kilimo FAO na lile la mpango wa chakula duniani WFP. Hali hiyo iliyokithiri mwaka 2016 na mapema 2017 [...]

22/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uganda yapigwa jeki harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia

Kusikiliza / Hapa ni maandamano kwa ajili ya kupinga ukatili wa kijinsia.(Picha:UNFPA?Uganda)

Benki ya dunia imeidhinisha dola milioni 40 kwa ajili ya miradi ya kukabili shida za kijamii na ukatili wa kijinsia nchini Uganda. Fedha hizo ambazo ni mkopo wa masharti nafuu zitasaidia utekelezaji wa sera za miradi iliyoidhinishwa mwaka 2016 wakati huu ambapo ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kutoka kwa wenzi wa ndoa vinaonekana ni jambo [...]

22/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misri isitishe hima kunyonga watu sita-UM

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Manuel Elias

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Misri kusitisha hukumu ya kunyongwa kwa watu sita nchini humo baada ya mwenendo wa kesi zao kutokidhi viwango vya kimataifa vya haki. Jopo hilo katka taarifa yake limeeleza masikitiko yake likisema watu hao wanaume, wamehukumiwa kwa misingi ya kulazimishwa kukiri. Kuendelea kwa adhabu hiyo ya [...]

22/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma ya afya karibu watu huboresha ufanisi na imani: WHO

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNICEF anamhudumia mtoto nchini Sudan Kusini. picha: UNICEF

Licha ya juhudi za jumuiya ya kimataifa kuhakikisha watu hupata huduma za afya karibu na wanakoishi, shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kwamba takwimu zinaonyesha mtu mmoja kati ya 20 hawapati huduma za afya muhimu zinazoweza kutolewa katika  kiliniki badala ya hospitali. Katika ujumbe wake unaofafanuliwa kwa njia ya video, WHO imesema kwenye wavuti wake [...]

22/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya ini yachochea vifo vya watumiaji wa madawa ya kulevya- Ripoti

Kusikiliza / Yuri Fedotov, Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, akihutubia wanahabari jijini New York wakati wa kongamano la wadhamini katika kusaidia taasisi zinazopambana na uhalifu wa kuvuka mipala pwani ya Afrika Magharibi. (Picha:Maktaba/ UN /JC McIlwaine)

Watu milioni 29.5 maeneo mbali mbali duniani wanakabiliwa na madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC iliyotolewa leo. Imesema dawa aina za kupunguza maumivu za kundi la Opioids zikiwemo Heroine na zile [...]

22/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres kutembelea kambi ya Imvepi huko Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi-Uganda2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres yuko nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine leo atatembelea kambi ya Imvepi iliyoko wilaya ya Arua, kaskazini mwa nchi hiyo. Kambi hiyo ni inahifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwezi Disemba mwaka 2013 vimefurusha mamilioni ya watu. Hivi sasa Uganda [...]

22/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha G-5 ruksa kupambana na ugaidi Sahel:

Kusikiliza / Raia wa Sahel akiwa shambani , wakati ukame ukighubuika eneo hilo.Picha na FAO

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja Jumatano jioni limepitisha azimio la kuanzishwa kikosi cha pamoja cha nchi za Sahel zijulikanazo kama G-5. Mapema Februari mwaka huu nchi za G-5 ambazo ni Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger ziliamua kuunda kikosi cha pamoja ili kukabiliana na tishio la ugaidi na April [...]

22/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika iimarishe tahadhari na haki za binadamu kuepuka majnga-Grandi

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR akiwa nchini Ethiopia alikotembelea wakimbizi na vile vile kuhutubia kikao cha AU.(Picha:UNIfeed/Video Capture)

Bara la Afrika linahitaji kuwekeza zaidi katika tahadhari za mapema, kuongeza juhudi za kushughulikia uvunjifu wa haki za binadamu na ukwepaji wa sheria ili kuepuka migogoro inayozalisha wakimbizi, amesema Kamishana Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi. Akilihutubia baraza la amani na usalama la Muungano wa Afrika AU, katika [...]

21/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nilitembea kutwa kucha na wanangu kutoka Sudan Kusini hadi Uganda kunusuru maisha-Sehemu ya 2

Kusikiliza / Jane Kide, mkimbizi wa Sudan Kusini katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo nchini Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Kibego)

Kutana na Jade Kide katika sehemu ya pili ya mahojiano na John Kibego.  Yeye ni mama wa watoto wanne na amehaha kusaka hifadhi na kujikuta akitembea usiku na mchana kutoka Sudan Kusini kukimbia machafuko. Amewasili Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo, akiwa ametokea jimboni Equatoria Mashariki nchini Sudan Kusini. Anasilimulia kadhia zinazomakabili akikumbuka namna [...]

21/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kiwango cha madhila kwa watu wa Syria kinaendelea kutia hofu-Guterres

Kusikiliza / Mtoto msichana akiwa Aleppo nchini Syria.(Picha:OCHA/Josephine Guerrero)

Ninaendelea kushangazwa sana na kusikitishwa na kina cha mateso ya nayowaghibika watu wa Syria. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akionya kwamba maisha ya kila siku kwa mamilioni ya watu yako hatarini. Kupitia taarifa ya msemaji wake Guterres amesema raia wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kutawanywa katika kiwango cha kutisha, na [...]

21/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ombi la msaada wa kibinadamu 2017 lafikia bilioni 23.5:UM

Kusikiliza / Wamama na watoto wakimbizi barani Afrika. Picha: UNHCR

Watu milioni 141 katika nchi 37 duniani wanahitaji msaada wa kibinadamu hivi leo na idadi hiyo inatarajiwa kuongeza umesema Umoja wa Mataifa Jumatano. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) December mwaka 2016 Umoja wa mataifa na washirika wake walilizindua ombi la dola bilioni 22 za msaada wa kibinadamu kwa mwaka 2017 hadi sasa [...]

21/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi Tisa zikiwemo Tanzania na DRC kuchangia ongezeko la idadi ya watu duniani- Ripoti

Kusikiliza / Wakazi wa dunia wataongezeka kutoka bilioni 7.6 hivi sasa hadi bilioni 8.6 mwaka 2030.(Picha:UNDESA)

Katika miaka sita ijayo, India itaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani na hivyo kuipiku China. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo kama anavyoelezea Amina Hasssan. (Taarifa ya Amina) Kubwa katika ripoti hiyo inayoangazia makadirio ya idadi ya watu ni kwamba wakazi wa dunia wataongezeka kutoka [...]

21/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima Nigeria wapatiwa pembejeo za kilimo

Kusikiliza / Mbegu zinasambazwa nchini Nigeria ili kukabili janga la njaa katika siku za usoni. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesambaza mbegu za mazao na mbolea kwa zaidi ya wakulima zaidi ya milioni moja huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambako mashambulio ya Boko Haram yamesababisha uhaba wa chakula. Mwakilishi mkazi wa FAO nchini Nigeria Nourou Macki Tall amesema msaada huo wa pembejeo umewezekana baada ya Ujerumani kutoa dola milioni [...]

21/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umasikini waweza kupungua kwa nusu ikiwa watu wazima watahimitimu elimu ya sekondari-UNESCO

Kusikiliza / Umasikini waweza kupungua kwa nusu ikiwa watu wazima watahimitimu elimu ya sekondari.(Picha:UM/Isaac Billy

Sera mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO, inasema kwamba umasikini duniani waweza kupungua kwa nusu ikiwa watu wazima wote watahitimu elimu ya sekondari. Wakati sera hiyo ikisema hivyo, takwimu mpya za shirika hilo zinaonyesha kuwa kumekuwa na muendelezo wa idadi kubwa ya watu kutohudhuria shule, jambo linalotoa mwelekeo kwamba [...]

21/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda kuendesha mkutano wa mshikamano na wakimbizi, ambao idadi yao inaongezeka

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Sudan Kusini wakiwa kambini Ngoromoro nchini Uganda. Picha: © UNHCR/Rocco Nuri

Uganda inakuwa mwenyeji wa mkutano wa siku mbili wa mshikamano na wakimbizi , kwa msaada wa Umoja wa Mataifa katika wakati ambao mgogoro wa wakimbizi nchini humo unashika kasi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, wimbi kubwa la wakimbizi wa Sudan Kusini limeongeza karibu mara mbili idadi ya wakimbizi [...]

21/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Adama Dieng ziarani DRC kuangalia hali halisi Kasai

Kusikiliza / Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya halaiki Adama Dieng yuko ziarani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia hali ilivyo kwenye majimbo yaliyoko eneo la Kasai. Ziara hiyo ya siku sita inakuja wakati kumeripotiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo mauaji ya hata raia wasio na hatia. [...]

21/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaonya wakimbizi wa Nigeria wanaorejea makwao

Kusikiliza / Mkimbizi kutoka Nigeria aliyekimbilia Cameroon.(Picha:UNHCR/Alexis Huguet)

Umoja wa Mataifa umesikitishwa na taarifa kwamba idadi kubwa ya wakimbizi wa Nigeria waliohifadhiwa nchini Cameroon wanarejea Kaskazini mwa Nigeria huku kukiwa na hali tete isiyo rafiki kwa mapokezi ya wakimbizi hao. Kamishina Mkuu wa shirika la umoja huo la wakimbizi UNHCR Filippo Grandi amenukuliwa akisema majuam matatu yaliyopita UNHCR ilionya kuhusu hali mbaya mpakani [...]

21/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baa la njaa Sudan Kusini lapungua japo maelfu bado hawana uhakika wa chakula-WFP/UNICEF/FAO

Kusikiliza / Baa la njaa lashuhudiwa nchini Sudan Kusini.(Picha:UNICEF/Sebastian Rich)

Baa la njaa limepungua Sudan kusini baada ya juhudi kubwa za kibinadamu za kulikabili , umesema uchambuzi wa pamoja uliotolewa Jumatano na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, shirika la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la chakula na kilimo FAO. Hata hivyo hali inasalia kuwa mbaya nchini humo huku idadi ya watu wasio na [...]

21/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dini wana fursa kuhamasisha ukomeshwaji wa nyuklia-Linnet

Kusikiliza / Jaribio la nyuklia uliofanywa na Marekani katika Enewetak Atoll, Visiwa vya Marshall, Novemba 1, 1952. Picha: US Government

Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni Linnet Ng'ayu ambaye ni Mratibu wa mitandao kutoka baraza la viongozi wa dini barani Afrika ACRL-RfP lenye makao makuu mjini Nairobi Kenya, ambaye ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa umuhimu wa kufikiwa kwa mkataba huo ni. ( Sauti Linnet) Amesema mbinu ya kutumia dini kutimiza lengo hili ni [...]

21/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matangazo ya biashara yaondokane na fikra potofu za kijinsia – UNWomen

Kusikiliza / UNWomen_Phumzile-Mlambo-Ngcuka

Wiki ya tamasha la kazi za ubunifu likiendelea leo huko Cannes nchini Ufaransa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen, Phumzile Mlambo-Ngcuka ametaka sekta ya matangazo ya biashara iondokane na fikra potofu za kijinsia. Amesema hayo katika taarifa iliyotolewa na UN-Women akiongeza kuwa sekta ya matangazo ya biashara [...]

21/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jayathma Wickramanayake ndiye mwakilishi mpya wa vijana UM

Kusikiliza / jayathmaW

Jayathma Wickramanayake kutoka Sri Lanka ndiye mteule mpya wa kubeba bendera ya vijana kwenye Umoja wa Mataifa baada ya kutangazwa Jumanne na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Jayathma anakuwa mrithi wa Ahmad Alhendawi kutoka Jordan ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa kazi nzuri ya kushughulikia mahitaji na haki za vijana na kuzifikisha kazi [...]

20/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani shambulio la kigaidi Bamako Mali

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Evan Schneider

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulio la kigaidi lililofanyika kwenye hoteli nje kidogo ya mji wa Bamako nchini Mali Juni 18. Kupitia taarifa ya msemaji wake , Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga, serikali na watu wa Mali huku akiwatakia ahuweni ya haraka majeruhi. Pia amepongeza hatua [...]

20/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mamilioni Gaza wakwamuliwe, hali tete-Mladenov

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali. Picha: UM/Manuel Elias

Ukanda wa Gaza sasa ni vipandevipande na watu milioni mbili wanapaswa kukombolewa , amesema leo Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani Mashariki ya kati Nickolay Mladenov. Bwana Maldenov ameliambia baraza la usalama ambalo limekutana Jumanne kujadili hali katika ukanda huo, akisema ni muhimu viongozi wa Palestina na Israel kurejelea majadiliano kwa [...]

20/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mjadala mujarabu wa uhamiaji ni muarobaini kwa ukimbizi- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UN/Video Capture)

Idadi ya wakimbizi ikizidi kuongezeka kila uchao, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amependekeza mambo matano ambayo amesema yataweza kuboresha mustakhbali wa kundi hilo ambalo idadi yao hivi sasa imefikia milioni 65.6 Amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani katika mkutano wake wa kwanza [...]

20/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nilitembea kutwa kucha na wanangu kutoka Sudan Kusini hadi Uganda kunusuru maisha-Sehemu ya 1

Kusikiliza / Jane Kide, mkimbizi wa Sudan Kusini katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo nchini Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Kibego)

Kutana na Jade Kide, mama wa watoto wanne, ambaye amehaha kusaka hifadhi na kujikuta akitembea usiku na mchana kutoka SudanKusini kukimbia machafuko. Amewasili Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo, akiwa ametokea jimboni Equatoria Mashariki nchini Sudan Kusini. Anasilimulia kadhia zinazomakabili akikumbuka naman alivyompoteza mwanae na wazazi kufuatia mgogoro nchini mwake. John Kibego anazungumza naye [...]

20/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi dhidi ya misafara ya misaada ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa-OCHA

Kusikiliza / Wakimbizi wahitaji misaada Syria. Picha: UNHCR

  Shambulio dhidi ya msafara wa misaada Syria lililosababisha dereva mmoja kujeruhiwa limelaaniwa vikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na kusema ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Kwa mujibu wa Jens Laerke msemaji wa shirika hilo, majeruhi ambaye ni mfanyakazi wa shirika la hilali nyekundu nchini Syria alikuwa [...]

20/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Lazima tuyafikirie madhila na machungu kwa watoto wakimbizi-Jolie

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa UNHCR, Angelina Jolie alipowatembelea wakimbizi mjini Nairobi Kenya.(Picha:UNHCR/Mark Henley)

Lazima dunia ifikirie madhila na machungu wanayopitia watoto wakimbizi hususan wasichana. Wito huo umetolewa leo Jumanne siku ya wakimbizi duniani na mwakilishi maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Angelina Jolie alipowatembelea wasichana wakimbizi mjini Nairobi Kenya. Bi. Jolie amekutana na wasichana 20 ambao wako peke yao bila wazazi au walitenganishwa [...]

20/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

CAR lazima ichukue hatua sasa kulinda watu wake na haki:UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini CAR. Picha: UM

  Jamhuri ya Afrika la Kati CAR inashuhudia hali isiyo “endelevu” inayochangiwa na kuenea kwa vikundi vyenye silaha na kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, hivyo serikali inapaswa kuchukua hatua sasa kabla kitumbua hakijaingia mchanga ameonya , mtaalam wa Umoja wa Mataifa. Marie-Thérèse Keita Bocoum, mtaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa [...]

20/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tusaidie wakimbizi kwani wanachoomba ni kidogo- Guterres

Kusikiliza / Nyakong mwenye umri wa miaka 22 mkimbizi kutoka Sudan Kusini.(Picha:UNHCR / C. Tijerina)

Idadi ya wakimbizi duniani ikifikia milioni 65.6 mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka jamii ya kimataifa ionyeshe ukarimu kwa kuwasaidia. Katika ujumbe wake wa siku ya wakimbizi duniani hii leo, Guterres amesema wakimbizi hao aliosema ni majasiri, wanachoomba si kikubwa bali ni kitu kidogo tu cha kuwawezesha kuishi salama na [...]

20/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fikra za kufungia milango wakimbizi zimepitwa na wakati- Grandi

Kusikiliza / Grandi

Ikiwa leo ni siku ya wakimbizi duniani, Kamishna Mkuu wa shirika la wakimbizi duniani, UNHCR Filipo Grandi amesema ni wakati wa kutambua ujasiri wa watu zaidi ya milioni 65 ambao wanaendelea kukabilia na maisha baada ya kukimbia vita, mateso na ghasia. Amesema sambamba na hilo ni wakati wa kutambua jamii na watu kote ulimwenguni ambao [...]

20/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 130 wahofiwa kufariki dunia baharini Mediteranea

Kusikiliza / Wahamiaji waokolewa na wafanyakazi wa IOM baharini Medeterranea. Picha: IOM

Watu wapatao 130 wanahofiwa kufa maji katika bahari ya Mediteranea baada ya boti tatu kuripotiwa kuharibika majini na kuzama usiku wa Jumatatu. Shirika la wakimbizi duniani, UNHCR limesema tukio la kwanza linahusisha boti iliyoondoka Libya tarehe 15 mwezi huu ambapo manusura wamesema ilikuwa na watu 133 na hadi sasa 129 hawajulikani walipo. Tukio la pili [...]

20/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali yazidi kuwa mbaya Kasai DRC-Zeid

Kusikiliza / Walinda amani wahoji washukiwa katika eneo la tukio. Picha: MONUSCO

Hali ya kibinadamu imezidi kuzorota katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC huku baadhi ya watu wakichochea chuki za kikabila na kusababisha hofu na mashambulizi ya kupangwa dhidi ya raia. Hayo yamesemwa na Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein Jumanne akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha 35 cha [...]

20/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 1000 wa Sudan Kusini husaka hifadhi kila siku-UNICEF

Kusikiliza / ssudan

Wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya wakimbizi, watoto 1000 kila siku hufurushwa makwao kusaka hifadhi nchini Sudani Kusini limsema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF,na kuongeza kuwa sasa mgogoro huo ni janga kwa watoto. Katika taarifa yake leo, UNICEF imesema tangu kuanza kwa mgogoro huo mwaka 2013, zaidi ya watu miliomni 1.8 [...]

20/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nimetumikishwa kama kahaba, nashindwa kujinasua-Joy

Kusikiliza / Joy

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inasema mamilioni ya watoto wanavuka mipaka ya kimataifa wakikimbia vurugu na migogoro, majanga au umaskini wakitumainia kupata maisha bora ugenini. Shirika hilo linasema katika mwaka 2015 – 2016, Idadi ya watoto wakimbizi na wahamiaji waliotenganishwa na wasioambatana na wazazi wao ilifikia 300,000 kutoka nchi 80 ikilinganishwa [...]

19/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 4000 hawana makazi baada ya moto kuteketeza kambi ya Korma Darfur

Kusikiliza / Mkimbizi aliyefurushwa makwao na kuishia kambi ya Korma ilioko Darfur Kasakzini.(Picha:Owies Elfaki, UNAMID)

Watu 4, 000 wameachwa bila makazi na sasa wanaishi chini ya miti baada ya moto mkubwa kuteketeza kabisa kambi waliyokuwa wanaishi kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan. Tukio hilo lilitokea Ijumaa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Korma iliyoko kilometa 80 kutoka El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, umesema mpango wa [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikwazo vya kusafiri Cuba vitaathiri uchumi wa Marekani

Kusikiliza / Picha: UNWTO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani, UNWTO limelaani vikali uamuzi wa utawala wa Marekani kurejesha vikwazo vya kusafiri nchini Cuba. UNWTO imesema hatua hii ni shambulio kubwa la uhuru wa kusafiri na inarudisha nyuma uhuru huo, na ingawa litaathiri utalii wa Cuba kwa kiasi, litaathiri zaidi uchumi na uwepo wa kazi nchini Marekani, [...]

19/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utii na utekelezaji wa sheria za kimataifa sio chaguo-Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu Zeid Ra'ad Al Hussein. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema utii na kuhakikisha utekelezaji wa sheria za kimataifa sio chaguo, akiongeza kwamba ukiukwaji wa haki za binadamu haukua dalili ya mgogoro baina ya Israel na Palestina, bali kichocheo cha mzunguko wa machafuko ambayo sasa yanaendelea kwa zaidi ya nusu karne. [...]

19/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP kunadi uwezo wa kutoa misaada kwa anga kupitia maonyesho Paris

Kusikiliza / WFP kunadi uwezo wa kutoa misaada kwa anga kupitia maonesho Paris.(Picha:WFP)

Maonyesho ya safari za ndege yanaanza leo hadi June 25 mjini Paris, Ufaransa. Shirika la mpangowa chakula duniani WFP limesema litatumia fursa hiyo ikiwa ni mara yake ya saba kushiriki, kudhihirisha matumizi ya ndege, wafanyakazi na teknolojia kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu katika majanga. Katika taarifa yake WFP imesema itaonesha utaalamu, na uwezo wa [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono vitani ni tishio la haki ya kuishi kiutu-Guterres

Kusikiliza / Ubakaji na ukatili wa kingono hutumika kama silaha vitani.(Picha:MONUSCO)

Ubakaji na ukatili wa kingono vitani ni mbinu za kigaidi na za kivita zinazotumika kudhalilisha , kudharaulisha , kuharibu na mara nyingi kufanya kampeni ya kutokomeza watu wa kabila fulani. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono vitani, [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tujiandae kabla ya ukame ili kuokoa wakulima- FAO

Kusikiliza / Moja ya maeneo kunakoshuhudiwa ukame.(Picha:FAO/Giulio Napolitano)

Huko Roma, Italia kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kunafanyika semina ya kimataifa kuhusu ukame na kilimo ambapo serikali na wadau wa kilimo wametakiwa kuachana na mtindo wa kusubiri ukame ndio wachukue hatua za kusaidia wananchi. Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema tabia hiyo [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita, mateso, ghasia vyazidi kufurusha watu makwao- UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi kama hawa wa Sudan Kusini aliowatembelea Kamishna Mkuu wa UNHCR ni miongoni mwa waliofurushwa makwao.(Picha:UNMISS)

Idadi ya wakimbizi duniani imeongezeka mwaka 2016 na kufikia milioni 65.6, vichocheo vikitajwa kuwa ni vita, ghasia na mateso. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwelekeo wa wakimbizi duniani kwa mwaka 2016, ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkimbizi wa Syria Muzoon aweka historia kuwa balozi mwema wa UNICEF

Kusikiliza / Msichana Muzoon, mwenye miaka 19,mkimbizi wa Syria aliyeteuliwa kuwa balozi mwema mdogo kabisa wa UNICEF. Ni mwanaharakati wa kupigania elimu ya wasichana. Picha na UNICEF

Katika kuelekea siku ya wakimbizi duniani hapo kesho , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limemteua Muzoon Almellehan, mwenye umri wa miaka 19 mwanaharakati wa masuala ya elimu na mkimbizi wa Syria kuwa balozi wake mwema mpya na mdogo kabisa. Uteuzi huo unamfaya Muzoon kuwa mtu wa kwanza mwenye hadhi ya ukimbizi [...]

19/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nimestushwa na kusikitishwa na vifo vya moto Ureno:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UM/Jean-Marc Ferr)

Nimeshtushwa na kusikitishwa na idadi ya watu waliopoteza maisha leo kutokana na moto wa mwituni uliolikumba eneo la Pedrógão jimbo la Grande nchini Ureno. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye mapema leo Jumapili amezungumza na Rais wa Ureno , Marcelo Rebelo de Sousa, na waziri mkuu, António Costa, [...]

18/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishina Mkuu wa wakimbizi azuru Sudan Kusini-UNHCR

Kusikiliza / Kamishina Mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi akuwa katika eneo la ulinzi wa raia Juba Sudan Kusini akizungumza na wakimbizi wa ndani. Picha kutokana nha video ya UNHCR

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi amekuwa ziarani nchini Sudan Kusini. Akiwa nchini humo bwana Grandi amezuru eneo la ulinzi wa raia karibu na mji kuu Juba linalohifadhi watu zaidi ya 30,000. Katika eneo hilo amekutana na kundi la wanawake ambao wametembea kwa juma zima kufika katika [...]

18/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl afariki dunia

Kusikiliza / Helmut Kohl2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ameelezea masikitiko  yake kufuatia taarifa za kifo cha kansela wa zamani wa Ujerumani, Helmut Kohl, kilichotokea leo Ijumaa. Kolh atakumbukwa kwa mchango wake katika kufanikisha kuungana kwa Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi mwaka mmoja baada ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin. Halikadhalika alichangia katika muungano wa kiuchumi [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapewa taarifa ya maendeleo Mali

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la usalama kuhusu hali nchini Mali. Picha: UM/Kim Haughton

  Mwezi huu inatimia miaka miwli tangu kutiwa saini mkataba wa amani ulitotumainiwa kuwa wa kihistoria nchini Mali. Baraza la usalama Ijumaa ya leo limepewa taarifa ya hatua zilizopigwa nchini humo na changamoto ambazo bado zinaendelea. Umoja wa Mataifa ulianzisha operesheni Mali ili kusaidia taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya kushindwa kwa jaribio la [...]

16/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya Mtoto Zanzibar

Kusikiliza / Mwongozo kuhusu haki za watoto. Picha: UM

Mwaka 1989, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC. Mkataba huu ulilenga kusimamia misingi mikuu minne ya haki za mtoto ambayo ni Kuishi, Kuendelezwa, Kushirikishwa na Kulindwa. Ibara ya 3 ya mkataba huo inagusia haki ya mtoto kwenye masuala yote ya kisheria, ikitaka haki ya mtoto kulindwa. [...]

16/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za UM akamilisha ziara DRC

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix alipokutana na gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku.(Picha:MONUSCO/Myriam Asmani)

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix, leo Ijumaa amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Akiwa nchini humo amepata fursa ya kutembelea Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini na kukutana na gavana wa jimbo hilo Julien Paluku na wawili hao wakajadili hali ya usalama, [...]

16/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa fedha wanyima watoto wa Syria mahitaji muhimu-UNICEF

Kusikiliza / Watoto wakiwa mjini Aleppo nchini Syria.(Picha:UNICEF/Romenzi)

Ukosefu wa fedha za usaidizi kwa watoto una madhara ya kupindukia katika uokozi wa karibu watoto milioni tisa nchini Syria, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema leo. UNICEF imesema kwamba imepokea kiasi cha dola bilioni 1.4 pekee ambacho ni robo ya kiasi kinachohitajika kwa ajili ya operesheni za dharura mwaka huu [...]

16/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni

Kusikiliza / IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni.(Picha:IOM)

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM limezindua huduma za kibalozi mtandaoni katika juhudi za kutekeleza mpango wa kurejea makwao kwa hiari, na huduma za kibinadamu za dharura kwa wahamiaji ( AVRR) walioko Libya waliokwama. Kwa mujibu wa IOM, kwa mara ya kwanza mkutano wa huduma za ubalozi mtandaoni umefanyika mnamo Juni tano kupitia Skype kwa [...]

16/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulemavu sio ukosefu wa uwezo

Kusikiliza / Bogdana Petrova mwenye ulemavu wa kutoona kutoka nchini Bulgaria. Picha: UM/Video capture

  Ulemavu sio ukosefu wa uwezo, ndivyo unavyoweza  kusema ukisikiliza kipaji cha muziki cha mwanadada Bogdana Petrova mwenye ulemavu wa kutoona kutoka nchini Bulgaria. Nyota huyu aliyewashangaza wengi kwa uwezo wake bila kujali hali yake, ametoa burudani juma hili mjini New York. Joseph Msami amefuatilia tukio hilo na kukuandalia makala ifuatayo.

16/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Mchuuzi na Machinga

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno Mchuuzi na machinga. Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA Bwana Zuberi anasema kwamba mchuuzi ni mtu anyeuza vitu vidogo vidogo alivyoweka sehemu iwe ni matunda, vichana au mboga alimradi anuza [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Saidieni adha ya maji Yemen kuepusha janga la kipindupindu:UM

Kusikiliza / Selioua Muhammad, 25 akiwa ameketi ndani ya makazi yake ambayo yalikuwa shule huko Sheik Othman in Aden, Yemen.(Picha:IRIN/Lindsay Mackenzie)

  Yemen na jumuiya ya kimataifa ni lazima wachukue hatua haraka kutoa maji salama ya kunywa ili kuzuia kusambaa zaidi kwa mlipuko wa kipindupindu, wameonya wataalamu wa haki za binadamu Ijumaa. Zaidi ya watu 135,000 wanahofiwa tayari wameshapata kipindupindu , wakati taifa hilo bado linakabiliana na vita vinavyoendelea ,ambavyo vimechangia kusambaratika kwa miundombinu ya maji [...]

16/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nusu ya watoto hawana fursa ya kufurahia utoto wao na baba zao-UNICEF

Kusikiliza / UNICEF

Zaidi ya nusu au asilimia 55 ya watoto wa umri wa miaka 3 na 4 katika nchi 74 duniani ambao ni takribani watoto milioni 40 wana kina baba ambao hawachezi nao au kushiriki katika shughuli za elimu yao ya awali , kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa Ijumaa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yakusanya wabobezi kubongoa bongo kukabiliana na saratani

Kusikiliza / Picha:IAEA

Wataalamu wa afya zaidi ya 500 kutoka nchi 96 watakutana kwa siku tatu kubongoa bongo kuhusu namna ya kutumia mionzi ya atomiki katika kutibu saratani. Taarifa ya shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki AEA imesema kwamba kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni, mjini Vienna nchini Austria, watalaamu hao watajikita katika kujumuisha jukumu la tiba [...]

16/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kinachohitajika ni utekelezaji wa sera-Tanzania

Kusikiliza / Ahmad Kassim Haji ambaye ni Naibu Katibu Mkuu , ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Tanzania Zanzibar.(Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulamevu CRPD ukiwa umekamilika hapo jana mjini New York Marekani, Tanzania Zanzibar imesema kinachohitajika ni utekelezaji wa sera kuhusu kundi hilo. Katika mahojiano maaluma na idhaa hii, Ahmad Kassim Haji ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Tanzania [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumaini ya mtoto wa Afrika yanategemea wazazi-Mongella

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wakicheza nchini Haiti. Picha: UN Photo/Christopher Herwig

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa Juni 16 kila mwaka, mwaka huu maudhui ni Ajenda ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa watoto barani Afrika. Maudhui hayo yanataka kuchochea ulinzi, uwezeshaji na fursa sawa kwa watoto. Katika mahojiano na idhaa hii mwanaharakati wa wanawake, ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwaheri Babatunde ulikuwa mtu wa watu-Musoti

Kusikiliza / Babarunde-3

Mwendazake Dr Babatunde Osotmehin aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA leo anapewa mkono wa kwaheri kwa heshima zote kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa hapa New York Marekani . Assumpta Massoi na taarifa kamili. (TAARIFA YA ASSUMPTA) Miongoni mwa watakaoshiriki katika tukio hilo maalumu litakalofanyika leo [...]

16/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Natamani wasio walemavu wavae viatu vyetu: Mwakilishi walemavu Tanzania

Kusikiliza / Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

  Kila anayetunyima fursa tunatamani angevaa viatu vyetu, ahisi uchungu tunaopitia, ni kauli ya mmoja wa wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Zanzibar Bi Abeida Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu kwenye ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Bi Abeida anyehudhuria mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba [...]

15/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCHR yaorodhesha ukiukwaji wa haki za binadamu Eritrea

Kusikiliza / Mwanamke akichota maji kutoka kwenye kisima nchini Eritrea. Picha: UM/Milton Grant

Nasikitika kuripoti kwamba Eritrea haijafanya jitihada zozote za kukomesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao uchunguzi umebaini kuwa ni sawa na  uhalifu dhidi ya ubinadamu, amesema leo Mtaalamu Huru wa Haki za Binadamu nchini humo. Bi. Sheela Kitharuth amesema mateso wanayoyapitia raia hao ni pamoja na kukamatwa kiholela, kuwekwa mahabusu bila mawasiliano, kutoweka na [...]

15/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu watamalaki Burundi, huku hofu ikitanda-UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi wakisubiri mgao wa chakula katika kituo cha muda cha 
Kamvivira.(Picha:UNHCR /Eduardo Soteras Jalil)

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili mwingine uliofurutu ada nchini Burundi sasa wathibitishwa. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Hayo ni kwa mujibu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa ukiukaji wa haki za binadamu Burundi iliyowasilisha taarifa yake kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis Alhamisi. [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hata nchi tajiri zahaha kutimiza SDGs-UNICEF

Kusikiliza / Hata nchi tajiri zahaha kutimiza SDGs-UNICEF

Mtoto mmoja kati ya watoto watano katika nchi zilizoendelea wanaishi katika umasikini, ilihali mmoja kati ya wanane hawana uhakika wa chakula, umebaini utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Utafiti huo ulioko katika ripoti ya UNICEF iliyochapishwa leo, unasema kwamba, nchi zenye uchumi wa kiwango cha juu zaidi duniani , zinahaha [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kitendo cha dharau-UNSOM

Kusikiliza / Picha:UM/Tobin Jones

Nchini Somalia watu wapatao 19 wameuawa baada ya gari lililokuwa na vilipuzi kulipuka kwenye mgahawa wa Pizza na hoteli jirani ya Posh mjini Mogadishu. Kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab kimekiri kuhusika na shambulio la leo lililolenga wateja waliokwenda kufuturu kwenye mgahawa huo ambapo hata hivyo walinzi wa mgahawa huo waliua wanamgambo watano wa kikundi hicho. [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wazee waongezeka limeonya shirika la WHO

Kusikiliza / Wazee mara nyingi hutelekezwa wakati mwingine na ndugu zao. (Picha:UN/Logan Abassi)

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kwamba ukatili dhidi ya wazee unaongezeka kote duniani. Katika kuadhimisha siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee duniani, utafiti mpya uliofadhiliwa na WHO na kuchapishwa na jarida la kimataifa la afya la Uingereza, Lancet umebaini kwamba mzee 1 kati ya 6 anakabiliwa na ukatili. Takwimu hizo ni kubwa kuliko [...]

15/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Elimu ni haki ya binadamu

Kusikiliza / Brian Messenger.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/F.Nducha)

Matumaini yetu ni kuelimisha watoto milioni sita duniani kwa kutoa mafunzo kwa walimu milioni moja ifikapo mwaka 2030 kote ulimwenguni. Hiyo ni kauli ya Brian Messenger Afisa Masoko wa kimataifa kutoka shule ya kimataifa ya Perkins iliyoko mji wa Boston jimbo la Massachusetts, Marekani ambayo ni ya watu wenye ulemavu wa macho au wasioona, inayofanya [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji na wakimbizi wanyanyaswa na kushikiliwa bila ridhaa yao Libya-IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema linatiwa hofu na hali ya takribani wakimbizi na wahamiaji 260 wa Somalia na Ethiopia wakiwemo watoto wanaoshikiliwa na wasafirishaji haramu wa binadamu au magenge ya wahalifu nchini Libya bila ridhaa yao. Kwa mujibu wa IOM picha za video zilizosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa facebook Juni [...]

15/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wawatoa mamilioni katika umasikini kwa kutuma fedha nyumbani

Kusikiliza / Mfanyakazi wa duka la upokeaji fedha Somalia akihesabu noti. Picha na UM/Stuart Price.

Kiwango cha fedha kinachotumwa na wahamiaji kwa familia zao nyumbani kimeongezeka na kufikia asilimia 51 katika muongo uliopita kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa Jumatano na mfuko wa kimataifa wa ufadhili kwa maendeleo ya kilimo IFAD. Utafiti umejikita katika kipindi cha miaka kumi ya wahamiaji kutuma fedha nyumbani walikotoka ambacho ni kati ya 2007 hadi [...]

14/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake bado wana fursa ndogo katika ajira-ILO

Kusikiliza / Picha:ILO/Video Capture

Pengo la kijinsia limesalia moja ya changamoto inayokabili dunia katika masuala ya kazi, hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kazi duniani ILO inayosema kwamba wanawake wana fursa ndogo zaidi ya kushikiri kwenye soko la ajira ikilinganishwa na wanaume. Ripoti hiyo iitwayo Ajira duniani na mtizamo wa kijamii- Mwelekeo kwa wanawake 2017, [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyanya apanda mbegu ya imani kwa wakimbizi-Uganda

Kusikiliza / Nyanya ambaye alikaribisha wakimbizi katika shamba lake.(Picha:UNHCR/Video Capture)

Mgogoro na njaa nchini Sudan Kusini ukiendelea, wananchi wamelazimika kukimbilia nchi jirani zikiwemo Uganda, Sudan, Ethiopia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya kati kusaka hifadhi. Jamii nchini Uganda zimetoa mfano wa kuigwa kwa kufungua nyumba zao na kuwakirimu wakimbizi hao. Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon anakutana na mwanamke mwenye umri [...]

14/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Suluhu pekee ya vita Afghanistan ni amani-Guterres

Kusikiliza / sg

Vita nchini Afghanistan suluhu yake sio mtutu wa bunduki, amesema Jumatano Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipotoa wito kwa pande kinzani nchini humo kusaka kwa pamoja suluhu ya kiasa ya vita vinavyoendelea. António Guterres amefanya ziara ya kwanza nchini humo kama Katibu Mkuu ambako amekutana na maafisa wa serikali na watu waliotawanywa na machafuko [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Uchangiaji Damu, WHO inasema okoa maisha leo

Kusikiliza / Uchangiaji damu nchini Ethiopia.(Picha:WHO/Ethiopia)

Leo ni Siku ya Kuchangia Damu Duniani , ambapo Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mwaka huu linalenga uchangiaji damu katika dharura, hususan kwa wale wanaotaka kusaidia. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Unaweza kufanya nini? Changia damu. Changia sasa. Changia mara kwa mara “, yenye kuhamasisha [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takwimu zenye aina ya ulemavu zahitajika

Kusikiliza / Wawakilishi wa Tanzania mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/A.Massoi)

Haitoshi kuwa na takwimu za watu wenye ulemavu pekee, kinachohitajika ni takwimu za kina ili kuwezesha mipango, wamesema wawakilishi wa jamii za watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Zanzibar. Katika mahojiano kandoni mwa mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa watu wenye ulemavu unaoendelea mjini New York, Marekani, Haidari Madowea ambaye ni mwenyekiti wa [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo vya raia Syria inasikitisha-Pinheiro

Kusikiliza / Paulo Pinheiro, mwenyekiti wa Kamisheni ya Uchunguzi kuhusu Syria. Picha ya UN/Jean-Marc Ferré

Mgogoro nchini Syria unaendelea kusababisha madahara makubwa kwa raia ambao wanabeba gharama kubwa ya vita vilivyodumu kwa zaidia ya miaka sita sasa amesema mkuu wa tume ya uchunguzi kwa ajili ya Syria. Akitoa taarifa ya maendeleo kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis jumatano ,Paulo Pinheiro,mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi ametoa wito [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Picha mpya za setilaiti kusaidia kubaini baa la nzige

Kusikiliza / Picha:FAO/Carl de Souza

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema taarifa kutoka setilaiti zinatumika kama njia mpya ya kubaini mazingira bora ya nzige kuzaliana na hivyo kuweza kuchukua hatua mapema kabla wadudu hao hawajashambulia mazao na kusababisha uhaba wa chakula. Mbinu hiyo ambayo tayari imejaribiwa Algeria, Morocco na Mali, inafuatia ushirikiano kati ya wataalamu wa FAO na [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid atoa kauli sakata la kidiplomasia dhidi ya Qatar

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amezungumzia sakata la kidiplomasia dhidi ya Qatar akitaka hatua zichukuliwe haraka ili kuepusha kuzorota zaidi kwa haki za binadamu. Kamishna Zeid amenukuliwa akisema kuwa hivi sasa mvutano huo uliosababisha Falme za kiarabu, Misri na Bahrai kukata uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi [...]

14/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uongozi kwa wanawake wenye ulemavu bado ni safari ndefu- Seneta Omondi

Kusikiliza / Seneta Omondi ambaye ni mwanamke mwenye ulemavu akiwakilisha kundi la wanawake na wasichana wenye ulemavu. (Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili/J.Msami)

Licha ya kwamba hatua zimepigwa katika utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu katika nchi mbali mbali ikiwemo Kenya,  bado kuna walakin kwa baadhi ya watu wakiwemo wanawake wanoishi na ulemavu. Hayo ni kwa mujibu wa Seneta wa viti maalum kutoka Kenya Godliver Omondi katika mahojiano maalum na Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 10 [...]

14/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Messi, Neymar wasaidia watoto wakimbizi-UNHCR

Kusikiliza / UNHCR kwa kushirkiana na klabu ya kandanda ya Barcelona wazindua #SignAndPass campaign yaani Tia sahihi na utoe pasi. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirkiana na klabu ya kandanda ya Barcelona, leo wametangaza kampeni kubwa ya pamoja ya kupigia chepuo usaidizi kwa watoto wakimbizi ijulikanayo kwa Kiingereza The #SignAndPass campaign yaani Tia sahihi na utoe pasi. Kampeni hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano wa wachezaji nyota akiwamo Leonel Messi na Neymar [...]

13/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushirika waleta nuru kwa wakimbizi Uganda

Kusikiliza / Kikundi cha wavuvi wakiwemo wakimbizi nchini Uganda. Picha: UNHCR/Video capture

Nchini Uganda, kitendo cha nchi hiyo kuwezesha wakimbizi kutangamana na wenyeji katika shughuli za kujikwamua kiuchumi, kimeleta ahueni kubwa kwa wakimbizi, fursa ambayo ni nadra sana kuipata kwingineko wanakopatiwa hifadhi,. Uganda pamoja na kuwezesha wakimbizi kupata ardhi ya kulima na hata kujenga makazi, sasa inaruhusu wenyeji na wakimbizi kujiunga katika vikundi vya ushirika ambavvyo kwavyo [...]

13/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia waendelea kuuliwa, kujeruhiwa Ukarine-UM

Kusikiliza / Wazee ni waathirka zaid wa vita vinavyoendelea Ukraine Mashariki. Picha: IOM/UN/Volodymyr Shuvayev

Uvunjifu wa makubaliano ya usitishaji wa mapigano umesababisha kuongezeka kwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mgogoro nchini Ukraine, Umoja wa Mataifa umesema leo. Ujumbe wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Ukraine (HRMMU), umesema kuwa kati ya Februari na Mei mwaka huu umesajili vifo 36 na majeruhi 157 vitokanavyo na [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki na sauti za watu wenye ulemavu vijumuishwe kwenye SDGs- Hungbo

Kusikiliza / disabilities 3

Mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu COSP10, umeanza leo mjini New York, Marekani ukiwaleta pamoja nchi wanachama 173 wa mkataba huo kutoka sehemu mbalimbali duniani. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu idara ya uchumi na masuala ya kijamii [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa ICT wabonga bongo kuhusu SDGs

Kusikiliza / Wasichana washikamana kuonyesha ujuzi wao katika teknolojia. Picha: ITU

Zaidi ya wataalamu 2,500 wa teknolojia ya habari na mawasiliano ICT wanakutana mjini Geneva, Uswisi, kwa siku tano kuanzia jumatatu juma hili, ambapo wanabadilishana ujuzi na uzoefu lengo likiwa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Mkutano huo wa kimataifa kuhusu upashanaji wa taarifa (WSIS Forum 2017 ) , kwa mwaka huu ukiwa chini ya uenyekiti [...]

13/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Takwimu sahihi za albino ni muhimu kufanikisha usaidizi- Al Shaymaa

Kusikiliza / Mwanaharakati Al Shaymaa Kwegyr kutoka Tanzania.(Picha:Idhaa ya Kiswahili kwa idhini ya Al Shaymaa)

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ulemavu wa ngozi au ualbino, mwanaharakati Al Shaymaa Kwegyr kutoka Tanzania ametaka tafiti zaidi juu ya takwimu kuhusu kundi hilo. Bi. Al Shaymaa ambaye alikuwa mbunge wa kwanza mwenye ulemavu wa ngozi, ameiambia idhaa hii kuwa.. (Sauti ya Al Shaymaa) Amesisitiza pia elimu akinukuu methali [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuwe makini udhibiti wa ugaidi usichochee machungu- Guterrres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kadri vitisho vitokanavyo na misimamo mikali vinavyozidi kuchanua, ni vyema kuhakikisha mbinu za kudhibiti hazileti matatizo. Bwana Guterres amesema hayo leo huko Ashgabat, Turkmenistan kwenye kikao cha ngazi ya juu cha kutathmini jinsi mataifa ya Asia ya Kati yanavyotekeleza mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makombora yakirindima Raqqa, UNHCR yahaha kufikia wahitaji

Kusikiliza / Mhuduhumu wa afya akiwa na watoto walionusurika kifo baada ya bomu la kutegwa ardhini kulipuka.(Picha:UNHCR/Areej Kassab)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetaka kupatia uwezo zaidi na endelevu wa kufikia makumi ya maelfu ya raia ambao wanahaha kupata msaada kwenye mji wa Raqqa nchini Syria. UNHCR imetoa ombi hilo wakati huu ambapo mapigano makali yanaendelea kwenye mji huo ikitajwa idadi ya wahitaji ni zaidi ya watu 430,000. Kila [...]

13/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini, japo kibarua bado kipo kukomesha ukatili dhidi ya albino:Ero

Kusikiliza / Haki za albino. Picha: UNHRC

Kuna kila sababu ya kuwa na matumaini katika kuhakikisha ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi unakomeshwa hususani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ambako tatizo hili limemea mizizi. Hayo ni kwa mujibu wa Ikponwosa Ero mtaalamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino akizungumza na [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumizi bora ya maji hukuza mahusiano baina ya nchi-Muigai

Kusikiliza / Mwanasheria Mkuu wa Kenya Githu Muigai.(Picha:Idhaa ya Kiswahili UM/G.Kaneiya)

Mkutano wa nchi wanachama kuhusu mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria za bahari umeanza jana mjini New York, Marekani, ambapo nchi wanachama wa mkataba wa bahari zimekutana kutathimini utekelezaji wa sheria hizo. Kenya ni miongoni mwa washiriki wa mkutano ambapo Mwanasheria Mkuu wa taifa hilo Profesa Githu Muigai ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum [...]

13/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutoboka kwa kiatu si mwisho wa safari

Kusikiliza / Bosco Niyonkuru, muhudumu mkimbizi ambae amejitolea uhai wake kuwahudumia wengine nchini Uganda. Picha: Picha: UNHCR/Video capture

Nchi ya Uganda inasifiwa kwa kupokea wakimbizi wengi na kuwajumuisha katika jamii kwa kuwapa kazi, ardhi na fursa za kujiendeleza. Mbali na changamoto nyingi anazokumbana nazo , mmoja wa wakimbizi hao anatumia fursa hiyo kujisaidia na kuwasaidia wengine. Sikiliza makala hii ya Amina Hassan yenye kusimulia zaidi.

12/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tusibabaike na kukosolewa kwa UNRWA bali tuiunge mkono:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM / Jean-Marc Ferré

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anawasiwasi na kukosolewa hadharani kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Palestina, UNRWA na uadilifu wake, lakini anaunga mkono na kupongeza mchango wake katika ulinzi wa haki za mamilioni ya wakimbizi wa Palestina walio Mashariki ya Kati. Amesema UNRWA inafanya kazi katika hali ngumu ya kivita, [...]

12/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mifumo ya hiari pekee haitoshi kulinda haki za wafanyakazi

Kusikiliza / Maria Grazia Giammarinaro.(Picha:UM/Paulo Filgueiras)

Mtaalamu huru wa Usafirishaji haramu wa binadamu hususan wanawake na watoto, Maria Grazia Giammarinaro, amewasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu hii leo, akisema ajira ya watoto na biashara ya watoto wahamiaji ndio iliyo ngumu zaidi kugundua na kugakua, na hivyo ataipa kipaumbele zaidi katika mamlaka aliyopewa. Wakati huo huo, wajumbe wa [...]

12/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali CAR bado tete, MINUSCA iendeleze wito wa amani-Anyanga

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu nchini CAR Parfait Onanga- Anyanga.(Picha:UM/Kim Haughton)

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kama ilivyo katika ripoti nambari (S/2017/473) ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kupitisha ajenda inayohusu CAR. Katika mkutano wa leo, baraza limeangazia hali ya kiusalama nchini CAR, husuani kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya raia pamoja na wafanyakazi wa Ujumbe [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ahadi ziende sanjari na vitendo katika kuwahifadhi wakimbizi-Grandi

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria Muhammed na nduguye Yousef uhifadhi waliopata hifadhi Gänserndorf, Austria, Novemba 2015.  (Picha© UNHCR/Mark Henley)

Wakati mahitaji ya makazi yakiongezeka kimataifa , sanjari na ongezeko la idadi ya wakimbizi, kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi Filippo Grandi, jumatatu ametoa wito wa kuongeza idadi ya maeneo kwa ajili ya kuhifadhi wakimbizi katika nchi ya tatu. Kwenye ufunguzi wa majadiliano ya kila mwaka na serikali na mashirika yasiyo [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hifadhi kwa wanawake wahanga sio hiari-Šimonoviæ.

Kusikiliza / Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonoviæ akihutubia mkutano wa 61 wa tume kuhusu hali ya wanawake CSW hapo machi 2017 jijini New York. Picha: UM/Rick Bajornas

Nchi zinapaswa kuwapatia hifadhi ya malazi wanawake ambao ni wahanga wa vitendo vya ukatili kulingana na sheria ya haki za binadamu, amesema leo Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonoviæ. Mtaalamu huru huyo ameliambia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi wakati akiwasilisha ripoti yake, kuwa amri ya [...]

12/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO na mwongozo mpya kuepusha ajira za watoto

Kusikiliza / FAO watoa mwongozo mpya kuepusha ajira za watoto. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limezindua mwongozo mpya unaoonyesha hatua zinazopaswa kuchukuliwa na watunga sera ili kuepusha watoto kutumikishwa mashambani pindi mizozo inapokumba jamii zao. Mwongozo huo umetangazwa hii leo ambayo ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto, FAO ikisema majanga yanapoibuka watoto wanatengana na familia zao na hivyo sekta ya [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kukomesha ukatili dhidi ya albino, nchi lazima zishirikiane-UM

Kusikiliza / mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi , Ikponoswa Ero (Kushoto). Picha: UNI/Tanzania

Ukatili na ubaguzi unaowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi au albino hautomalizika hadi pale nchi zitakaposhirikiana kuukomesha. Onyo hilo limetolewa Jumatatu katika taarifa ya mtalaamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Ikponwosa Ero, katika kuelekea siku ya kimataifa ya kuelimisha dhidi ya ulemavu wa ngozi au Albino, inayoadhimishwa [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 65 zahitajika kunusuru wakimbizi wa DRC huko Angola:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wacongomani wawasili Chissanda, Lunda Norte, Angola wakitoroka vita vinavyaendelea Kasai, DRC. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake wanasaka dola milioni 65 ili kusaidia ongezeko la wakimbizi wanaowasili Angola kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , DRC. Tangu mwezi Aprili wakimbizi 30,000 wamewasili Angola katika mji wa Luanda jimbo la Norte, wakikimbia machafuko katika jimbo la Kasai. Mapigano baina ya [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majanga na vita ni kichocheo cha utumikishwaji watoto-ILO

Kusikiliza / Mtoto mchnugi mifugo Translyvania.(Picha:ILO/Marcel Crozet)

Takriban watoto milioni 168 wahanga wa utumikishwaji wa watoto wanaishi katika maeneo kunakoshuhudiwa vita na majanga. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la kazi ulimwenguni, ILO katika taarifa yake ya siku ya kimataifa ya kupinga utumikishwaji kwa watoto inayoadhimishwa kila mwaka Juni 12. Maadhimisho ya mwaka huu [...]

12/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres asema utofauti ni mali na sio tishio

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika sanamu ya ukumbusho wa wahanga wa ghasia za kikabila ambao ulifanyika Kyrgyzstan mwaka 2010. Picha: UM/Vyacheslav Oseledko

  Jamii zinazidi kutofautiana zaidi na zaidi ulimwenguni kote na hili ni lazima lizingatiwe kama kitu chanya,  amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres wakati wa  ziara yake Kyrgyzstan. Guterres alitembelea  eneo la Osh na kuweka shada la maua katika sanamu ijulikanayao kama "Machozi ya Mama", iliyo kumbukumbu ya  mamia ya watu waliopoteza [...]

11/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jamii ya Wagungu yalinda utamaduni wake kupitia muziki

Kusikiliza / Ngoma za kitamaduni za nchini Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Kibego)

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni , UNESCO, linapigia chepuo ukuzaji wa tadamduni mbalimbali za makabila na jamii tofauti ili kulinda urithi. Nchini Uganda moja ya kabila dogo kwenye ufalme wa Bunyoro liitwalo Bagungu linalinda utamuduni wake kwa kuhifadhi nyimbo za kale. Ungana na John Kibego katika Makala ifuatayo.    

09/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhifadhi wa mazingira hususan Afrika

Kusikiliza / Uchafuzi kwenye msitu wa serikali nchini Tanzania. Picha: John Kibego

Mapema juma hili, dunia imeadhimisha siku ya mazingira, siku ambayo huadhimishwa Juni tano ya kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu ni utengamano na asili, ukilenga kuhakikisha ulinzi wa maliasili za mazingira ili kukuza uendelevu wa viumbe na sayari dunia. Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP na wadau  wake,  wametumia maadhimisho hayo [...]

09/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa bahari umefanikiwa, lakini kazi itaendelea:UM

Kusikiliza / Rais wa baraza kuu Peter Thomson. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Siku tano zilizoghubikwa na mikutano, mijadala na vikao takribani 150 na maonyesho 41 katika mkutano wa kimataifa wa bahari kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa hapa New York hatimaye zimefunga mlango hii leo ijumaa. Mkutano huo wa bahari uliowaleta pamoja wadau mbalimbali zaidi ya 1000, zikiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, watalaamu wa [...]

09/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Walinda amani 3 wauawa na 8 wajeruhiwa huko Mali

Kusikiliza / Maziko ya mlinda amani wa MINUSMA.(Picha: MINUSMA/Harandane Dicko)

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa wameuawa na wengine wanane wamejeruhiwa katika matukio mawili tofauti huko kidal, kaskazini mwa Mali. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari hii leo kuwa tukio la kwamza lilitokana na kituo cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Mali, MINUSMA kushambuliwa kwa kombora ambapo walinda [...]

09/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mipango ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu lazima iwe na ufanisi:UM

Kusikiliza / Kumbukumbu ya biashara ya utumwa. Picha: UM

Biashara nyingi lazima zijitoe kimasomaso kukabiliana na unyanyasaji kazini unaohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu amesema mtaalamu wa haki za binadamu Ijumaa. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Maria Grazia Giammarinaro, akihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis amesema hatua za hiyari zilizopo zinahitaji kufafanuliwa zaidi na ziwe zenye ufanisi. Kwa mujibu wa [...]

09/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kazakhstan ni muhimu katika ustawi wa Asia ya Kati- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM

Umoja wa Mataifa umesema unapenda kuona eneo la Asia ya Kati linakuwa na amani na ustawi, hivyo ushirikiano zaidi unatakiwa baina ya nchi za ukanda huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuanza ziara yake nchini Kazakhstan. Amesema udau kati ya Umoja [...]

09/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Mfasiri na Mkalimani

Kusikiliza / Picha :Idhaa ya Kiswahili

Wiki hii tunaangazia maneno Mfasiri na Mkalimani na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema mfasiri ni yule anayetafsiri neno au maneno kwa maandishi na mkalimani ni mtu anayeelezea kwa mdomo maneno yanayosemwa wakati ule ule kutoka lugha moja hadi nyingine .

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Ethiopia yaongoza katika baa la njaa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Wachungi nchini Ethipia watafutia mifugo lishe na maji. Picha: UNDP

Mamilioni ya watu Ethiopia, Djibouti, Kenya na Somalia wanakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kuonekana katika miongo, kutokana na ukosefu wa mvua na kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi wa ndani na mipakani, imesema leo ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM. Taarifa ya Amina Hassan inafafanua zaidi (TAARIFA YA AMINA) Mkurugenzi wa [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha ya watoto 40,000 shakani Ar Raqqa, Syria-UNICEF

Kusikiliza / Wakimbizi wanaokimbia kutoka eneno la Raqqa nchini Syria.(Picha:UNICEF/UN039561/Soulaiman)

Mashambulizi mazito mjini Ar-Raqqa nchini Syria yanatishia maisha ya zaidi ya watoto 40,000 ambao wanasalia mtegoni mwa hatari kubwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. UNICEF imesema imepokea taarifa za kutisha kwamba takribani watoto 25 wameuawa na kujeruhiwa katika mshambulizi ya hivi karibuni zaidi mjini humo, shule na hospitali zikiwa zimeshambuliwa, [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchunguzi wa kimataifa ufanyike dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu DRC- Zeid

Kusikiliza / Watu wakusanyika wakati wa maandamano nchini DRC mnamo Disemba 2016.(Picha:MONUSCO)

Tuna wajibu kwa wahanga na jukumu la kutuma ujumbe kwa wahusika wa uhalifu wa ukiukaji wa haki za binadamu na, kwamba tunawafuatilia na jumuiya ya kimataifa inatia uzito kuhakikisha ukwepaji wa sheria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC unakomeshwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Kauli hiyo imetolewa Ijumaa na kamishina mkuu [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanaoishi ufukweni Kenya kuneemeka- Karigithu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa idara ya kitaifa ya masuala ya bahari iliyoko chini ya wizara ya usafirsihaji nchini humo, Nancy Karigithu.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Wakati mkutano wa kimataifa kuhusu bahari ukifika ukingoni hii leo, Kenya imesema imeandaa mkakati maalum wa kuhakikisha jamii zinazoishi katika fukwe za bahari zinanufaika na uwepo wa bahari. Akizungumza na idhaa hii mjini New York Marekani, Katibu Mkuu wa idara ya kitaifa ya masuala ya bahari iliyoko chini ya wizara ya usafirsihaji nchini humo, Nancy [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wavuvi walalama kipato kidogo Tanzania

Kusikiliza / Boti za wavuvi. Picha: FAO

Mkutano wa kimataifa kuhusu bahari ukifikia tamati hii leo, nchini Tanzania wavuvi kutoka mkoani Tanga, wameesema kuwa sababaui kadhaa zikiwamo mabadiliko ya tabanchi zimesababaisha kupungua kwa samaki katika bahari ya Hindi. Katika mahojiano na Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo, wavuvi hao Rajabu Madaraka na Ali Mkada wamesema juhudi zaidi za [...]

09/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen si makazi salama kwa mtoto- UNICEF

Kusikiliza / Mtoto anahudumiwa katika hospitali ya Sab'een huko Sana'a nchini Yemen. Ni mmoja wa watoto waathirika wa kipindupindu. Picha: © UNICEF/UN065873/Alzekri

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema Yemen hivi sasa si pahala salama kwa makuzi ya mtoto kwa kuwa hali ni mbaya kupita kiasi. Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Geert Cappelaere amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani wakati huu ambapo inaelezwa [...]

08/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dunia itupie macho visiwa vya Afrika kulinda bahari: Dk Tizeba

Kusikiliza / Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba.Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Macho yote yameelekezwa kwenye visiwa vya Magharibi, hili lapaswa kukoma! Ni kauli ya Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba wakati akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu bahari unaoendelea mjini New York. Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii, Dk Tizeba ameitaka jumuiya ya kimataifa kutozisahau nchi zinazoendelea zenye visiwa [...]

08/06/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani Colombia:Guterres

Kusikiliza / Kitengo cha Umoja wa Mataifa nchini Colombia cha kukusanya silaha. Picha: UN Mission in Colombia

Natiwa moyo na hatua za utekelezaji wa mkataba wa amani nchini Colombia na hususani , kukamilika hapo jana kwa uwasilishaji wa asilimia 30 ya kwanza ya silaha za FARC-EP kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anonio Guterres Alhamisi kupitia taarifa ya msemaji wake, [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika ikamate fursa ya biashara za kidijitali- UNCTAD

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi.(Picha:UM/Jean-Marc Ferre)

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezindua ripoti yake kuhusu mwelekeo wa uwekezaji duniani kwa mwaka huu wa 2017. Ripoti hiyo pamoja na mambo mengine inaangazia kuongezeka kwa kasi ya uchumi utokanao na biashara ya kidijitali, biashara ambayo hufanywa kwa njia ya mtandao. Mathalani mtu kununua vitu kwenye tovuti na hatimaye [...]

08/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hongera Lesotho kukamilisha uchaguzi kwa amani-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akifungua jukwaa la kimataifa la kiuchumi huko St. Petersburg nchini Urusi. Picha: courtesy/TASS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres , amewapongeza watu wa ufalme wa Lesotho kwa kukamilisha uchaguzi wa bunge kwa amani na usalama. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu mkuu ameisifu kazi ya tume huru ya uchaguzi nchini humo kwa kuandaa uchaguzi huo kidemokrasia na pia jukumu la jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika [...]

08/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takataka zamwezesha kusomesha watoto wake

Kusikiliza / Sulubu Kisima Nzai.(Picha:UNIC Nairobi)

Mkutano kuhusu masuala ya bahari ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, nchini Kenya mkazi mmoja wa Malindi kwa miaka 12 amekuwa akiokota takataka baharini na ufukweni ambazo zimemwezesha kubadili maisha ya familia yake. Sulubu Kisima Nzai akihojiwa na Karim Said wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Gharama za uingizaji chakula kimataifa zapanda-FAO

Kusikiliza / Mchujo wa mpunga nchini Ufilipino.(Picha:FAO/Joseph Agcaoili)

Kimataifa soko la bidhaa za chakula limetengamaa kutokana na usambazaji mkubwa wa ngano, mahindi na mbegu. Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO ongezeko la gharama za usafirishaji na uingizaji wa kiasi kikubwa cha bidhaa , utaongeza gharama za usafirishaji wa bidhaa kimataifa na kufikia zaidi ya dola trilioni 1.3 kwa [...]

08/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi wa Sudan Kusini waingia Kenya

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini wanawasili kambini Kakuma nchini Kenya. Picha: UNHCR-Kenya-Nadapal-Kakuma

Idadi ya raia wa Sudan Kusini wanaongia nchini Kenya wakikimbia mzozo nchini mwao inazidi kuongezeka. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini humo limesema tangu mwezi Januari mwaka huu wakimbizi wapya 772 wamesajiliwa kwenye kituo cha muda cha Nadapal, ambacho hata hivyo uwezo wake ni wakimbizi 500. Kituo hicho kipo mpakani mwa [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ya afya kwa wananchi bado inasiginwa- Baraza

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wanapea chanjo watoto. Picha: UNICEF

Maeneo mbali mbali duniani hivi sasa haki ya msingi ya kupata huduma ya afya kwa binadamu bado inasalia ndoto. Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Kate Gilmore amesema hayo akihutubia kikao cha 35 cha Baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi hi leo ambacho kimeangazia haki ya msingi ya watu kupata huduma ya [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ISIL yakatili maisha ya mamia ya raia wanaokimbia Mosul-UM

Kusikiliza / Makazi mengi yameharibiwa Mosul, Iraq.(Picha: UNHCR/Ivor Prickett)

Taarifa za kuaminika zinaonyesha kwamba raia zaidi ya 231 waliokuwa wakijaribu kukimbia Mashariki mwa mji wa Mosul nchini Iraq wameuawa tangu Mei 26, wakiwemo 204 kati yao waliouawa katika kipindi cha siku tatu wiki iliyopita. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiorodhesha visa vya raia kutumiwa kama ngao ya vita na [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria na elimu visaidie kulinda bahari

Kusikiliza / Savana,14 (kushoto) na Kathryn 19, Kutoka Trinidad na Tobago ambao wanachagiza ulinzi wa bahari.(Picha:UM/Lulu Gao)

Bahari zetu, mustakhbali wetu, hiyo ndio kauli mbiu ya siku ya bahari duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 8. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (TAARIFA YA ASSUMPA) Katika hafla maalumu ya kuadhimisha siku hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa msukumo umetolewa katika kutambua uzuri, umuhimu na udhaifu wa bahari, na mikakati ya kuchua [...]

08/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa amani Libya unafanyiwa marekebisho- Kobler

Kusikiliza / 03-18-2014-benghazi-Libya-07JUNE17-350-300

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler amesema hali ya amani nchini humo bado si shwari sana na mwelekeo wa utekelezaji wa mkataba wa amani una nuru kidogo. Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kutoka Tunis, Tunisia, Bwana Kobler amesema ingawa kuna muafaka [...]

07/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mama akisema ndio hakuna atakayesema hapana!

Kusikiliza / Kulea

Mila na desturi za baadhi ya makabila duniani zinataka mtoto wa kike aolewe tu punde baada ya kubalehe. Msingi mkuu wa mila hii ni fikra potofu ya kwamba mtoto wa kike hana msaada wowote kwa familia yake zaidi ya kwenda kuolewa na kuzaa watoto. Miongoni mwa makabila hayo ni wasamburu huko Afrika Mashariki na hususan [...]

07/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres atoa ujumbe kuhusu shambulizi Iran

Kusikiliza / Mtazamo wa bustani ya Nowruz, Tehran, Iran. Picha: UN Information Centre Tehran

Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa António Guterres amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika hii leo katika kaburi la Ayatollah Ruhollah Khomeini na jengo la bunge au Majlis katika mji mkuu wa Iran, Tehran. Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Iran na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi, akisema anatumai [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya matumaini bado kuna shaka ya uwekezaji wa kigeni duniani – UNCTAD

Kusikiliza / Uwekezaji wa kigeni unalenga sekta mbali mbali ikiwemo ya usafirishaji.(Picha:Benki ya Dunia/Video capture)

Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, FDI unatarajiwa kuongezeka duniani kwa asilimia Tano kwa mwaka huu wa 2017. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya kamati ya maendeleo na biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyochapishwa hii leo ikisema kuwa ongezeko hilo lina thamani ya dola trilioni 1.8. UNCTAD imesema ongezeko hilo limetokea [...]

07/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Teknolojia yaweza kusaidia maendeleo kwa amani na utu-Guterres

Kusikiliza / AI-WIPO 1

Wadau wakuu wa uwezo wa masuala ya teknolojia AI na wale wa mambo ya kibinadamu wanakutana na viongozi wa viwanda na taaluma katika mkutano wa kimataifa uliopewa jina Yote kwa wema. Mkutano huo unafanyika mjini Geneva, Uswisi, ambapo mjadala unahusu namna AI inavyoweza kusaidia juhudi za kukabili umasikini, njaa na kuwezesha elimu na afya pamoja [...]

07/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya watoto washamiri DRC- MONUSCO

Kusikiliza / Watoto nchini DRC .(Picha:UNICEF/M.Gonzalez)

Jumla ya visa 40 vya ukatili dhidi ya watoto vimeripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kati ya tarehe 29 mwezi uliopita wa Juni na tarehe 5 mwezi huu vikitekelezwa na vikundi vilivyojihami. Mratibu wa mawasiliano ya umma wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, Théophane Kinda amewaeleza waandishi wa habari mjini [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa ajira kwa vijana duniani utatuliwe-Uganda

Kusikiliza / Mkutano wa 106 wa kila mwaka Shirika la kazi duniani ILO mjini Geneva.(Picha:ILO/Crozet / Pouteau)

Mkutano wa 106 wa kila mwaka Shirika la kazi duniani ILO unaendelea mjini Geneva Uswisi ambapo wafanyakazi, waajiri na wawakilishi wa serikali wanakutana kwa takribani majuma mawili wakijadili mambo kadhaa ikiwamo uhamaji wa wafanyakazi, usalama na afya kwa kundi hilo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Mada nyingine zinazojadiliwa katika mkutano huo ni [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki ya Dunia yaimarisha mtandao wa barabara Ghana

Kusikiliza / Wachuuzi wauza bidhaa zao katikati ya magari katika trafiki huko Tema, Ghana. Picha: Jonathan Ernst / World Bank (maktaba)

Benki ya Dunia imeridhia mkopo wa dola milioni 150 kwa ajili ya mradi wa kuimarisha sekta ya usafirishaji nchini Ghana, TSIP. Fedha hizo zitasaidia ukarabati wa barabara zinazounganisha maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kutoka Tamale hadi Tatale ambako ni mji wa mashariki wa mpakani na Togo. Henry Kerali ambaye ni mkurugenzi wa benki hiyo [...]

07/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya 100,000 kufaidika na msaada wa China Chad:WFP

Kusikiliza / Msaada wa chakula wawasili nchini Chad.(Picha: WFP/Adel Sarkozi)

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha mchango wa kitita cha dola milioni 4 zilizotolewa na Uchina , ambazo zitawapa ahuweni watu zaidi ya laki moja wanaohitaji msaada nchini Chad. Eneo la ziwa Chad limeghubikwa na machafuko yaliyosababisha mgogoro wa kibinadamu, hivyo mchango huo wa Uchina kwa mujibu wa WFP [...]

07/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia bado ni changamoto katika elimu-UNESCO

Kusikiliza / Wanafunzi wasichana katika maabara ya sayansi. Picha: UNESCO

Licha ya hatua kubwa iliyopigwa katika kupanua fursa za elimu, usawa wa kijinsia katika elimu unasalia kuwa changamoto kubwa. Kwa mujibu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, wasichana wengi zaidi wako shule hii leo kuliko wakati mwingine wowote, lakini sababu za kijamii, kiuchumi na ubaguzi wa kijinsia zinawazuia wasichana hao kupata fursa sawa [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni wazi kuwa wanawake ndio wanaoteseka zaidi katika vita-Owusu

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Eugene Owusu akihutubia mkutano wa wanawake. (Picha:UNMISS)

Jukwaa la wazi Kimataifa kwa ajili ya Wanawake linafanyika wiki hii jijini Juba, Sudan Kusini kujadili usawa wa kijinsia, ukatili wa kijinsia, ubaguzi, ndoa za shuruti na za mapema ili hatimaye kuwawezesha wanawake katika ngazi zote kuleta amani. Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mifumo thabiti ya kimataifa ni muarobaini wa ulinzi wa bahari -DK Tizeba

Kusikiliza / Dkt. Tizeba2

Mfumo thabiti wa sheria za kimataifa unahitajika ili kulinda bahari ambayo ina manufaa katika uchumi hususani kwa nchi zinazoendelea , amesema Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi wa Tanzania Dk Charles Tizeba. Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa baada ya kuhutubia mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya bahari unaoendelea New York, Marekani, Dkt. [...]

07/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maji, amani na usalama havitengamani-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Maji, amani na usalama ni vitu vinavyohusiana. Wakati huu ambapo mahitaji ya maji safi yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 40 ifikapo katikati ya karne hii, na huku mabadiliko ya tabianchi yakiongeza athari, upungufu wa maji ni suala mtambuka linaloongeza hofu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye kikao cha baraza [...]

06/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Simulizi za wakimbizi wa ndani nchini Nigeria

Kusikiliza / Boussam Abdulahi, mmoja wa wakimbizi wa ndani nchini Nigeria waliopoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya Boko Harram. Picha: UNHCR/Video capture

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, watu zaidi ya milioni mbili katika maeneo ya bonde la ziwa Chad wamepoteza makazi yao kufuatia mashambuzizi ya Boko Haram. Wakimbizi na watu katika eneo hilo ikiwemo Nigeria wanahitaji msaada wa dharura, na makumi ya maelfu ya watoto wako hatari kupata magonjwa yanayosababishwa [...]

06/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nguli Grenier ateuliwa balozi mwema wa mazingira

Kusikiliza / Mcheza filamu nguli wa Marekani Adrian Grenier, ameteuliwa na UNEP kuwa balozi mwema wa mazingira.(Picha:UNEP)

Mcheza filamu nguli wa Marekani Adrian Grenier, ameteuliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP kuwa balozi mwema wa mazingira. Nguli huyo anatarajiwa kupigia chepuo upunguzwaji wa matumizi ya plastiki na ulinzi wa viumbe vya baharini. Taarifa ya UNEP kuhusu uteuzi huo inasema kwamba mcheza filamu huyo mashuhuri kadhalika atawashawishi mashabiki wake kuwa [...]

06/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dunia inahitaji “mapinduzi” katika huduma ya afya ya akili:UM

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya afya , Dainius Pûras. Picha: UM/Jean-Marc Ferré

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya afya , Dainius Pûras, ametoa wito wa mabadiliko katika huduma ya afya ya akili kote duniani , akizitaka nchi na wataalamu wa afya ya akili kuchukua hatua kwa ujasiri kufanyia mapinduzi mfumo uliokumbwa na mtafaruku ambao umejengeka katika hulka zilizopitwa na wakati. Akiwasilisha ripoti yake kwenye [...]

06/06/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu milioni watia saini kupinga matumizi ya plastiki-UM

Kusikiliza / Mkaguzi wa bahari wa UNEP akiogelea ndani ya bahari kuliko na taka taka.(Picha:UNEP)

Kampeni ya Avaaz imetoa wito kwa serikali za dunia kupiga marufuku matumizi ya plastiki katika miaka mitano ijayo. Kampeni hiyo ambayo imetiwa saini na watu milioni moja itawasilishwa kwa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP ili kuunga mkono harakati zake za kuwa na bahari safi kwa kukomesha uchafu baharini. Mkurugenzi wa UNEP Erik [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanasiasa wasio na aibu wanasigina katiba za nchi zao – Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Raa'd Al Hussein ameeleza masikitiko yake juu ya vitendo vya baadhi ya wanasiasa kutokuwa na aibu kutokana na matendo yao yanayoleta machungu kwa wananchi wao. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Masikitiko hayo ya Zeid yamo kwenye hotuba yake ya kurasa nane [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maamuzi kwenye mkutano wa UM kuhusu bahari ni ya muhimu sana

Kusikiliza / Douglas McCauley mwanabailojia na mtaalamu wa viumbe vya baharini , na Mkurugenzi wa mradi wa Benioff Ocean katika chuo kikuu cha California. Picha: UM

Maamuzi yanayofanyika wiki hii kwenye mkutano wa kimataifa wa bahari yataweza kutoa muongozo wa mustakhbali wa mabadiliko ya bahari katika maelfu ya miaka ijayo. Huo ni mtazamo wa mmoja wa wanasayansi mahiri aliyeko kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa juma hili akihudhuria mkutano huo. Douglas McCauley mwanabailojia na mtaalamu wa viumbe vya baharini , [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada kwa ajili ya elimu wapungua mwaka wa sita mfululizo-UNESCO

Kusikiliza / Mtoto darasani.(Picha:UNESCO/ Florida Valle, Colombia)

Kiwango cha fedha za msaada kwa ajili ya elimu kimeporomoka kwa mwaka wa sita mfululizo imesema leo ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO iliyotolewa Jumanne. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Ripoti hiyo ya ufuatiliaji wa elimu kimataifa (GEM) iitwayo "Msaada kwa elimu unadorora na kutowafikia [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii imuandae mwanamke tangu utoto alete mabadiliko:Upendo

Kusikiliza / Upendo, mwanasiasa chipukizi nchini Tanzania. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Mtandao wa viongozi wanawake barani Afrika utawezesha wanawake kuwa wapatanishi wa amani katika jamii zao na kujenga viongozi bora amesema Mwakilishi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa mtandao wa viongozi wa Afrika uliomalizika mjini New York Marekani Upendo Peneza. Akizungumza katika mahojiano maalum baada ya kuhudhuria mikutano ya mtandao huo, [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahari ni ajira kwa vijana-Freeman

Kusikiliza / Bwana Freeman katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Vijana waweza kukuza kipato kupitia bahari na kufanikisha kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs amesema mwakilishi ni mwakilishi wa kudumu wa vijana wa Kenya katika ofisi za Umoja wa Mataifa Samuel Freeman. Katika mahojiano na idhaa kandoni mwa mkutano wa siku tano kuhusu bahari unaondelea mjini New York Marekani Bwana Freeman amesema uwepo wao katika [...]

06/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili wanaoushuhudia watoto Iraq ni wa kutisha:UNICEF

Kusikiliza / Mwanamke mkimbizi akimbeba mwanae kusini mwa Mosul. Picha:UNICEF/USA

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema leo kuwa limepokea ripoti za kushtua zenye idadi kubwa ya vifo vya watu, vikijumuisha watoto kaskazini mwa Mosul nchini Iraq, watoto ambao wanashuhudia visa vya kinyama ambavyo kamwe hakuna mtu anapaswa kushuhudia. UNICEF inasema takriban wasichana na wavulana 100,000 wamo katika hatari kubwa, wakijikuta [...]

05/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sasa si wakati wa kunawa mikono kuhusu Israel/Palestina

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, (Picha:UN/Jean-Marc Ferré)

Wakati huu sio wakati wa kukata tamaa katika kutafuta suluhu ya amani ya mataifa mawili katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanza kwa mapigano baina ya Waarabu na Waisrael ya mwaka 1967. Amesema miongo na miongo, kizazi [...]

05/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Afrika inahitaji mageuzi katika amani-Mongella

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi Gertrude Mongella.(Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Baada ya kuundwa na kukutana mjini New York Marekani kwa siku tatu, mtandao wa viongozi wanawake wa Afrika, umeazimia pamoja na mambo mengine kuhakikisha bara hilo linajikomboa katika migogoro kisha kupiga hatua za kimaendeleo. Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni mwanasiasa nguli kutoka Tanzania, aliye pia mwanaharakati wa wanawake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy [...]

05/06/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uhifadhi wa kompyuta au simu wachangia uhifadhi wa mazingira Burundi

Kusikiliza / Uhiadhi wa kompiuta au simu ni moja ya mikakati ya kuhifadhi vyema mazingira. Picha: UNEP

Kawaida likija swala la  kuhifadhi mazingira , katika nchi zinazoendelea  watu hufikiria haraka swala la  mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa hewa ikiwemo uhifadhi wa miti , mito na kadhalika. lakini je  unajua  kuwa uhifadhi wa komputa au simu ni moja  ya mikakati ya kuhifadhi vyema mazingira? Nchini Burundi , sehemu nyingi  na ofisini [...]

05/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yaomboleza kifo cha ghafla cha mkurugenzi mtendaji wake

Kusikiliza / Babarunde 4

Kwa masikitiko makubwa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA limetangaza kifo cha mkurugenzi wake mtendaji, Dr. Babatunde Osotimehin,kilichotekea ghafla usiku wa Jumapili nyumbani kwake . Alikuwa na umri wa miaka 68. UNFPA inasema hili ni pigo kubwa kwa shirika hilo na kwa watu wote hususani wanawake, wasichana na vijana aliojitolea [...]

05/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazibagui- Mugabe

Kusikiliza / Spokesman addresses the press on behalf of SG on the US withdraw from the Paris Agreetment

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amehutubia mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya bahari jijini New York, Marekani akisema kuwa ubia hasa usaidizi wa kiufundi ni muhimu ili kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yatokanayo na uchafuzi wa bahari. Amesema hata hivyo kwa nchi yake ubia huo hasa katika kutelekeza lengo namba 14 la malengo ya [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya mazingira duniani, asili ilindwe ili kulinda dunia:UNEP

Kusikiliza / Vijana wakazi wa msitu wa taifa la Tapajos waogelea katika mto wakati wa joto makali. Picha: UM/Eskinder Debebe (maktaba)

Utangamano na asili ndiyo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa leo kote duniani ikipigia chepuo uhifadhi na ulinzi wa maliasili za mazingira kwa mustakabali bora wa viumbe na sayari. Akizungumiza siku hiyo K atibi Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bahari ,ardhi, misitu , maji na hewa tunayovuta ni [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Kusikiliza / Mwendazake Babatunde Osotimehin! Amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 68.(Picha:UNFPA)

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin, amefariki dunia. Amina Hassan na taarifa zaidi. (Taarifa ya Amina) Nats.. Mwendazake Babatunde Osotimehin! Amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 68. Raia huyu wa Nigeria, ameongoza UNFPA tangu mwaka tarere Mosi Januari mwaka 2011 akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahari ina uhusiano na kila mmoja wetu inatufanya tuishi-Guterres

Kusikiliza / Watoto baharini nchini Timor Leste.(Picha:UN/DESA)

Bahari ina uhusiano na kila mmoja wetu, inatufanya tuendelee kuishi, lakini uhusiano huo sasa uko mahskani kuliko wakati mwingine wowote. Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatatu katika mkutano maalumu ulioanza leo Juni 5 kuhusu masuala ya bahari na hasa lengo la maendeleo endelevu nambari 14. Guterres amesema mkutano huo utakaomalizika [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Babatunde afariki dunia

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin akihutubia jukwaa la maendeleo ya afya kwa wanawake ulimwenguni jijini New York Marekani. Picha: UN Photo/Loey Felipe

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA Babatunde Osotimehin, amefariki dunia hii leo. Alikuwa na umri wa miaka 68. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza kushtushwa na kifo hicho akisema kuwa Babatunde alikuwa bingwa wa utetezi wa ustawi wa wanawake na [...]

05/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tutamkomboa mwanamke katika maneo yenye migogoro-Gertrude Mongella

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi Getrude Mongella ambaye ni mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa wanawake kutoka Tanzania. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Utatuzi wa amani katika maeneo yenye migogoro na ukombozi wa wanawake katika maeneo hayo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa na mtandao wa viongozi wa Afrika waliohitimisha mkutano wao mwishoni mwa juma mjini New York Marekani. Katika mahojiano na idhaa hii  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Advocacy for Women in Africa Bi  Getrude Mongella ambaye ni [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasiki:Guterres

Kusikiliza / Mandhari nzuri ikionesha malia asili ya duniania, mlima, mabonde na bahari. Katika siku ya Mazingira Duniani. Picha na UNEP

Bahari,  ardhi, misitu , maji na hewa tunayovuta ni mazingira yetu ambayo ni viungo muhimu katika mustakhbali dunia. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 5 na kuongeza (GUTERRES CUT 1) "Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasikini au [...]

05/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani shambulio la kigaidi London

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM / Jean-Marc Ferré

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali shambulio la ugaidi liliotokea jana mjini London chini Uingereza na kusababisha vifo na mejeruhi kadhaa. Vyombo vya habari vimeripoti kwamba watu saba wamefariki dunia, zaidi ya 40 wakijeruhiwa baada ya washambuliaji kuingia ndai ya umati wa watembea kwa miguu katika daraja kuu mjini London. Katika [...]

04/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Athari za matumizi ya tumbaku kwa jamii na watu binafsi

Kusikiliza / smoking_cameroon

Mei 31 kila mwaka ni siku ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni  "Tumbaku- tishio dhidi ya maendeleo". Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kwamba zaidi ya watu milioni 7 hufariki dunia kila mwaka huku ikigharimu familia na serikali takriban dola trilioni 1.4 kwa ajili ya matibabu na [...]

02/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterees asikitishwa na upungufu wa chakula kwa wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sahrawi kambini Smara nje ya Tindouf, Algeria. UN Photo/Evan Schneider

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres,amesikitishwa na hatma ya maelfu ya wakimbizi wa Sahrawi nchini Algeria ambao watapunguziwa mgao wao wa chakula kutokana na ukosefu wa chakula. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bwana Guterres amesema usaidizi wa kibinadamu ikiwamo chakula ni muhimu kwa ukanda huo wa jangwa la Sahara ambapo utafiti [...]

02/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maisha ya viumbe baharini ni moja ya wajibu wetu:FAO

Kusikiliza / Usafi baharini ni muhimu kwa viumbe vya bahari. Picha: UNEP

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari utafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New York Marekani . Mkutano huo utakaoanza Juni 5 hadi 9 utaenda sanjari na maadhimisho ya siku ya bahari duniani ambayo kila mwaka hua Juni 8. Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO [...]

02/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wimbo watumika kuelimisha kuhusu Fistula

Kusikiliza / (Mwanamke aliye na uchungu akionekana katika video hiyo ya wimbo wa Fistula: Picha:Video Capture)

Fistula ni ugonjwa ambao sasa ni mwiba kwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni mbili kuanzia Afrika, Asia, Mashariki ya Kati, Karibea hadi Amerika! Uchungu wa kupitiliza, kuchelewa kujifungua kwa wakati muafaka au kukatwa mrija wa kusafirisha mkojo wakati wa upasuaji wowote ule, vimetajwa kuwa ni sababu ya Fistula. Shirika la Umoja wa Mataifa la [...]

02/06/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Mchungi na Mchungaji

Kusikiliza / Neno la wiki:

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Mchungi” na “Mchungaji”. Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA Bwana Zuberi anasema “Mchungi” na “Mchungaji” ni manenno mawaili tofouti. Mchungi ni yule amabaye kazi yake ni kuchunga mifugo na Mchungaji [...]

02/06/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Tutawafikia wanawake mashinani: Dk Josephine

Kusikiliza / Dk Josephine Kulea ambaye ni mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wasichana wa jamii ya Samburu kutoka chini Kenya. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Mkutano wa mtandao wa wanawake viongozi barani Afrika uliozinduliwa wiki hii unafunga pazia leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani ambapo washiriki wameahidi kuwafikia wanawake mashinani. Katika mahojinao na idhaa hii, Dk Josephine Kulea ambaye ni mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wasichana wa jamii ya Samburu kutoka chini [...]

02/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya tabianchi hayapingiki-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:UM/Jean-Marc Ferr)

Mabadiliko ya tabianchi hayapingiki na ni moja ya tishio kubwa katika ulimwengu wa sasa na mustakhbali wa sayari hii. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António  Guterres Ijumaa mjini St Petersberg Urusi akizitaka serikali kuendelea kushikamana na kutimiza wajibu wao katika utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi, akisistiza kwamba [...]

02/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 50 wanaswa katika mtego wa kifo katika jangwa la Sahara

Kusikiliza / Wahamiaji kutoka Niger. Picha: IOM

Wahamiaji 44 kati ya 50 wanawake na watoto wamefariki dunia baada ya gari lao kuharibika katika jangwa la Sahara wakati wakielekea Libya kutoka Niger, taarifa za Umoja wa Mataifa zimesema leo. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Tukio hilo ambalo limetokea kati ya miji ya Agadez na Dirkou limetokana na joto kali na [...]

02/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 15 wafariki dunia baada ya chanjo ya surua kwenda mrama Sudan kusini

Kusikiliza / Watoto 15 wamekufa baada ya chanjo ya surua kwenda mrama Sudan kusini. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema limesikitishwa na taarifa ya vifo vya watoto 15 katika kijiji cha Nachodokopele Mashariki mwa Kapwete nchini Sudan Kusini, vinavyohusiana na kampeni ya chanjo ya surua ya tarehe 10 hadi 14 Mei kwenda mrama. Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Alhamisi na WHO, shirika la kuhudumia watoto UNICEF na [...]

02/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunahitaji kuimarisha usimamizi wa bahari:Thomson

Kusikiliza / oceans

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Peter Thomson amesema umuhimu wa uchumi wa bahari endelevu ni dhahiri hasa katika maeneo ya pwani ya Afrika na bara zima kwa ujumla na kuwa wakati umewadia kwa nchi zote kutimiza kwa uadilifu lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Thomson amesema hayo wakati wa [...]

02/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Twasikitishwa na Marekani kujitoa mkataba wa Paris- UM

Kusikiliza / Spokesman addresses the press on behalf of SG on the US withdraw from the Paris Agreetment

Umoja wa Mataifa umesema hatua ya Marekani kujitoa hii leo kutoka mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ni jambo la kusikitisha katika jitihada za kimataifa za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi na kuendeleza usalama wa ulimwenguni. Msemaji wa Umoja huo Stephane Dujarric amesema hayo alasiri hii mbele ya wanahabari akisema hatua hiyo imetangazwa na [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za upasuaji kwa wagonjwa Fistula -sehemu ya Pili

Kusikiliza / Tuwede ambaye alipokea matibabu ya Fistula na kurejelea maisha ya kawaida.(Picha:UNFPA Zimbabwe/Nikita Little)

Katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mtaalamu wa afya kutoka mkoani Kagera nchini Tanzania  Dk Martin Lwabilimbo, tunaelezwa kile ambacho kinafanyika baada ya upasuaji wa kurekebisha Fistula, ugonjwa ambao unaondoa utu wa mwanamke. Mathalani Dokta Lwabilimbo amemweleza Nicolaus Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM mkoani humo kuwa, mgonjwa akishafanyika upasuaji [...]

01/06/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IFAD yaelimisha uvuvi salama huko Indonesia

Kusikiliza / Mvuvi nchini indonesia. Picha: IFAD

Kuelekea mkutano wa kimataifa kuhusu bahari, tunaelekea huko nchini Indonesia, ambako mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD unashirikiana na jamii za wavuvi ili kulinda bahari ikiwemo matumbawe ambayo ni mazalia ya samaki. Indonesia ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa uvuvi na uuzaji nje wa samaki na uvuvi wote huo hufanyika na wavuvi [...]

01/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri na si porojo- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akifungua jukwaa la kimataifa la kiuchumi huko St. Petersburg nchini Urusi. Picha: courtesy/TASS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mabadiliko ya tabianchi ni wimbi kubwa linalokumba dunia hivi sasa na ni lazima lishughulikiwe ili kurejesha imani na usalama ulimwenguni. Akifungua jukwaa la kimataifa la kiuchumi huko St. Petersburg nchini Urusi amesema ingawa baadhi ya nchi zinaamini kuwa mabadiliko ya tabianchi ni porojo zisizo na msingi [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sasa siku za uvuvi haramu zahesabiwa- FAO

Kusikiliza / Boti za uvuvi. Picha: FAO

Harakati za kutokomeza uvuvi haramu zinazidi kung'ara baada ya Japan na Montenegro kutia saini mkataba wa kimataifa wa kudhibiti uvuvi huo. Makubaliano hayo yaitwayo Port State Measures , au PSMA yanahusisha zaidi ya theluthi mbili za sekta ya uvuvi duniani yakileta pamoja nchi wanachama zipatazo 50. PSMA imeundwa kuzuia meli za uvuvi kujihusisha na uvuvi [...]

01/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tusipomakinika viumbe hai watatoweka

Kusikiliza / Kuhakikisha mazingira bora pia ni haki ya binadamu. Picha: UNHCR

Hatuwezi kufurahia haki zetu za msingi za kibinadamu bila ya mazingira bora, huo ni ujumbe wa Mtaalamu Huru wa Haki za Binadamu kuhusu Mazingira, John H. Knox katika kuelekea Siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 05. Amesema wanasayansi wanahofu kwamba kwa mara ya kwanza katika miaka milioni 60, ulimwengu umo mwanzoni mwa awamu [...]

01/06/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pamoja na hatua katika vita dhidi ya AIDS, bado kuna pengo:Ripoti

Kusikiliza / Picha:UNAIDS

Wajibu wa kimataifa, kugawana jukumu la fedha, na mtazamo unaozingatia usawa miongoni mwa watu vimekuwa chachu kubwa ya mafanikio katika vita dhidi ya ukimwi, imesema ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iloyowasilishwa leo Alhamisi kwenye baraza kuu. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA YA AMINA) Ripoti hiyo "vita dhidi ya ukimwi kama chachu [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa wanawake viongozi Afrika wazinduliwa New York

Kusikiliza / Dkt. Asha-Rose Migiro,Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Msami)

Mtandao wa wanawake viongozi barani Afrika umezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ukileta pamoja viongozi wa kisiasa na kitaaluma kwa lengo la kuchagiza ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa na ile ya 2063 ya Muungano wa Afrika, AU. Lengo la mtandao huo unaochagizwa na Umoja wa Mataifa, AU na serikali ya Ujerumani ni [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani wa UNAMID auawa Nyala Sudan

Kusikiliza / Kamanda wa majeshi azuru eneo la tukio la kigaidi Darfur magharibi nchni Sudan. (Maktaba). Picha: UN Photo/Albert González Farran

Mlinda amani wa mpango wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNAMID ameuawa na kundi la watu wasiojulikana baada ya kuteka gari lao mjini Nyala jimbo la Darfur Kusini. UNAMID imelaani vikali shambulio hilo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Tukio hilo limeripotiwa kwa mamlaka ya Sudan na [...]

01/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sheria mpya Misri yakandamiza mashirika ya kiraia- Zeid

Kusikiliza / Raia nchini Misri wafanya maandamano kuomba haki zao. Picha: UNHCR

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ametaka serikali ya Misri ifute sheria mpya kuhusu utendaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo akisema ni kandamizi. Amenukuliwa na ofisi ya haki za binadamu akisema kuwa sheria hiyo namba 70 ya mwaka 2017 inabinya nafasi ya haki za binadamu [...]

01/06/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM inafanya uchunguzi Kakuma na Dadaab Kenya

Kusikiliza / Wafanyakazi wa IOM wakiendesha shughuli zake katika kambi nchini Kenya.(Picha:IOM)

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limesema Alhamisi linafanya uchunguzi dhidi ya shutuma za utovu wa nidhamu katika kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab nchini Kenya. Ofisi ya mkaguzi mkuu wa IOM ndio inayoendesha uchunguzi huo ikihusisha timu ya wataalamu wa upelelezi. Na endapo uchunguzi huo utathibitisha kuwepo kwa utovu wa nidhamu [...]

01/06/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini CAR sasa ukilinganisha na 2014-Gilmour

Kusikiliza / CAR 1-6-17car 1

Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ya mwaka 2014 iliyoghubikwa na hofu, machafuko, mauaji, kuporomoka kwa uchumi na zahma ya kibinadamu, sio CAR ya sasa inayotia matumaini. Kauli hiyo imetolewa na Andrew Gilmour msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu ambaye amehitimisha ziara ya siku nne nchini humo. Bwana Gilmour amesema ameshuhudia kuimarika kwa [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu juu ya maisha ya watoto walio kwenye nyumba za malezi- UNICEF

Kusikiliza / Romania_Anamaria Dinulescu ROMA_2016_MPS_002

Shirika Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema bado kuna pengo kubwa juu ya idadi halisi ya watoto wanaoishi kwenye makazi ya malezi. Katika ripoti yake hii leo, UNICEF imesema takwimu kutoka nchi 140 imeonyesha kuwa takribani watoto milioni 2.7 wanaishi katika nyumba hizo za malezi au familia za ulezi maeneo mbali mbali ulimwenguni, [...]

01/06/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930