Watu wa asili wana ujuzi na ukizingatiwa utakuza kipato: Mshiriki CSW61

Kusikiliza /

Lucy Mulenkei kutoka mtandao wa taarifa kwa watu wa asili IIN nchini Kenya akihojiwa na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. (Picha:Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)

Katika zama hizi ambazo ajira ni changamoto ya kimataifa, jamii ya watu wa asili na ujuzi wao asilia wanaweza kukuza ajira, amesema Lucy Mulenkei kutoka mtandao wa taarifa kwa watu wa asili IIN, nchini Kenya. Bi. Mulenkei anashiriki mkutano wa kamisheni ya hadhi ya wanawake CSW61 mjini New York Marekani. Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii, mshiriki huyo amesema watu wa asili hawanufaikiipasavyo kutokana na kuachwa nyuma na mfumo wa maisha, na kuzisihi serikali kuzitizama jamii hizo alizosema zina ujuzi ambao haujathaminiwa ipasavyo.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031