Nyumbani » 17/03/2017 Entries posted on “Machi 17th, 2017”

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake CSW61 waangaziwa

Kusikiliza / Washiriki wa kamisheni ya hadhi ya wanawake kikao cha 61 CSW New York.(Picha:UM/Idhaa ya Kiswahili.)

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake umeanza tarehe 13 mwezi huu wa Machi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Asasi za kiraia kutoka sehemu mbalimbali zinazojihusiha na masuala ya ustawi wa wanawake zimewakilishwa huku pia serikali zikituma wawakilishi wake kushiriki katika mikutano mbalimbali ya ndani kuhusu masuala [...]

17/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Calypso yarithishwa kizazi hadi kizazi

Kusikiliza / Wachezaji wa Calypso tamashani El Callao, Venezuela.(Picha:UNESCO/Video Capture)

Fasihi simulizi inaenezwa kutoka jamii moja hadi nyingine kwa njia mbali mbali ikiwemo matamasha. Miongoni mwa fasihi hizo ni utamaduni wa mtindo wa Calypso ambao huweka bayana historia ya jamii hususan ya nchi za Caribea. Mtindo huu umeorodheshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kama turathi za tamaduni zisizogusika [...]

17/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ijapokuwa hali ya usalama bado ni tete CAR, maendeleo makubwa yamepatikana-Onanga

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Parfait Onanga-Anyanga.(Picha:UM/JC McIlwaine)

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA, Parfait Onanga-Anyanga, amesema japokuwa hali ya usalama bado ni tete, lakini maendeleo makubwa yamepatikana tangu tangu uchaguzi wa serikali mpya mapema mwaka jana. Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Onanga-Anyanga [...]

17/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Guinea waliokwama Libya warejea nyumbani-IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Guinea waliokuwa Libya wakisafirishwa hadi Guinea Conakry.(Picha:IOM)

Wahamiaji 98 raia wa Guinea wakiwemo wanaume 96 na wanawake wawili waliokuwa wamekwama Libya sasa wamerejea nyumbani Conakry kwa msaada wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Ndege ndogo iliyoandaliwa kwa uratibu wa serikali ya Libya na uongozi wa Guinea iliondoka uwanja wa ndege wa Mitiga tarehe 14 mwezi huu, huku shirika la IOM likifanya [...]

17/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki- Gozigozi

Kusikiliza / Neno la wiki-gozigozi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia matumizi yasiyo sahihi ya neno gozigozi. Mchambuzi wetu  Nuhu Zubeir Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA anasema neno gozigozi linatumiwa likimaanisha upuuzi au mambo ya hovyo. Lakini kimsingi neno gozi linamaanisha ngozi ya mnyama iliyochunwa na [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Tunahitaji fedha za dharura kusaidia wakimbizi wa Iraq: UNHCR

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa ndani Iraq wanburuta magodoro na vifaa vingine kuelekea makazi yao katika kambi ya Hasansham, Iraq.Picha: © UNHCR/Ivor Prickett

Idadi ya wanaofurushwa makwao ikiongezeka Magharibi mwa Mosul nchini Iraq, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafungua kambi mpya sambamba na wito wa usaidizi kwa wafadhili kuongeza fedha kwa ajili ya ulinzi na malazi kwa wanaofurushwa. Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR, watu 255,000 wamefurushwa kutoka Mosul na maeneo ya karibu tangu [...]

17/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yakaribisha hatua kubwa ya kuwahamiasha waomba hifadhi 10,000 kutoka Ugiriki

Kusikiliza / Suleiman na familia yake walipata walihamishwa kutoka Ugiriki hadi Portugal.(Picha:IOM/2017)

Zaidi ya waomba hifadhi 10,000 sasa wamehamishwa kutoka Ugiriki na kwenda kwenye mataifa menmgine ya Muungano wa Ulaya . Grace Kaneiya na taarifa kamili (TAARIFA YA GRACE) Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM waomba hifadhi hao wamehamishwa chini ya utekelezaji wa mpango wa Muungano wa Ulaya ulioanza mwanzoni mwa Machi wa kuwahamisha [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Janga la wakimbizi wa Sudan Kusini laongezeka, msaada wahitajika-UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini wanaokimbia ghasai nchini mwao hapa wakiwa kambini.(Picha:UNHCR)

Miezi minane baada ya kuzuka upya machafuko Sudan Kusini , baa la njaa lililosababishwa na mchanganyiko wa vita na ukame sasa limefanya janga la wakimbizi nchini humo kuwa moja ya mgogoro wa wakimbizi unaokuwa haraka duniani. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Kwa mujibu wa shirik la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi Sudan Kusini wasindikizwa na polisi kufanya mitihani- UNMISS

Kusikiliza / Wanafunzi wa Sudan Kusini wanafanya mtihani yao ya kwawezesha kumaliza shule ya upili. Picha: UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS unawapatia wanafunzi wa kidato cha nne ulinzi wa polisi wanapokwenda kufanya mitihani yao ya mwisho wakati huu ambapo wanafunzi hao walikumbwa na hofu ya usalama. Msemaji wa UNMISS, Daniel Dicknson ameiambia Radio Miraya ya Umoja wa Mataifa kuwa wanafunzi hao ni wale waliopo kwenye kituo cha [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka mmoja baada ya kufungwa mpaka wa Balkan watoto wazidi kua hatarini:UNICEF

Kusikiliza / Watoto waongea juu ya matatiso yanaowakumba ukumbizini. Picha: UNICEF/Video capture

Mwaka mmoja baada ya mpaka wa mataifa ya Balkan kufungwa na Muungano wa Ulaya na serikali ya Uturuki kutoa tamko lenye lengo la kuzuia wimbi la wahamiaji, watoto wakimbizi na wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kurejeshwa kwa nguvu, kuwekwa rumande, kunyanyaswa na kunyimwa haki. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna pengo la mishahara baina ya wanawake na wanaume Tanzania: Kigwangalla

Kusikiliza / Dr Hamisi Kigwangalla (kushoto) akihojiwa na idhaa  ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Serikali ya Tanzania imesema injivunia hatua zilizopigwa katika suala la ukombozi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisheria, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii. Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto, Dr Hamisi Kigwangalla alipohojiwa na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa kikao cha 61 [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031