Nyumbani » 16/03/2017 Entries posted on “Machi 16th, 2017”

Usugu wa viuavijasumu ni tisho kwa kwa maendeleo endelevu: UM

Kusikiliza / Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed na Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Margaret Chan wakizungumza na waandishi wa habari mjini New York juu wa usugu wa viuavijasumu.
Picha: UN/Mark Garten

Usugu wa viuavijasumu au antimicrobial resistance AMR ni tisho kubwa la kutimiza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed. Amesema hayo hivi leo Alhamisi kwenye makau makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York walipokuwa wakijadili swala hilo na mkurugenzi mkuu wa shirika la afya [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu wa IOM alaani shambulio dhidi ya msafara wa wahudumu wa kibinadamu Sudan Kusini

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing

  Mkurugeni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing,  hivi leo amelaani shambulizi dhidi ya msafara wa wafanyi kazi wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini liotokea Machi 14 na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa. Wafanyi kazi hao walivamiwa na watu wenye silaha wasiojulikana walipokuwa  wanarudi Yirol [...]

16/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Heko Rais Touadéra kwa kuanzisha mahakama maalum CAR- Ladsous

Kusikiliza / Herves Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa. Picha: UN Photo/Loey Felipe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu hali ya amani, usalama na kibinadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo imeelezwa kuwa mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi,kumekuwepo na mafanikio hasa kurejeshwa kwa utawala wa serikali kwenye mji muhimu wa Bambari. Akihutubia kikao hicho, mkuu wa operesheni za ulinzi wa [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili na manyanyaso kazini ni ukiukaji wa haki za binadamu: ILO

Kusikiliza / Wanawake wafanyakazi katika sekta ya nguo nchini Cambodia. Picha:UN-Women/Cambodia/Charles-Fox

Ukatili na manyanyaso kazini dhidi ya wanawake ni tatizo kubwa na la kimataifa limesema shirika la kazi duniani ILO. Akizungumza kwenye mjadala maalumu kandoni mwa kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani uliojadidili ukomeshaji wa ukatili wa wanawake kazini, , Manuela Tomei ambaye ni mkurugenzi wa idara ya hali ya kazi na [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya raia 120,000 wamekimbia madhila magharibi mwa Mosul, Iraq

Kusikiliza / Wakimbizi wanaokimbia vita huko Mosul. Iraq.(Picha:UNHCR/Saif Al-Tatooz)

Tangu vikosi vya kijeshi nchini vianze mapigano ya kukomboa mji wa Mosul mwezi Oktoba mwaka, takribani raia 345,000 wamekimbia makwao, ambapo 275,000 kati yao wanahitaji usaidizi. Amesema mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Bi Lise Grande akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwa njia ya video kutoka Iraq. Ameongeza [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shilingi 5,000 zimebadili maisha yangu: Mjasiriamali

Kusikiliza / Nazi ni chakula cha thamani katika nchi nyingi. Picha: FAO

Mjasiriamali kutoka Tanzania Bi Amina Shaaban anasema amefanikiwa kusomesha watoto wake kwa kuanzia na mtaji wa shilingi 5,000 za Tanzania ambapo aliitumia kuuza nazi nakupata faida. Bi Amina ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania Zanzibar, hususani Pemba, ambao wamenufaika baada ya serikali kuelimisha wanawake namna ya kujikomboa kiuchumi ili kukabiliana na chnagamoto ya ajira. Ungana [...]

16/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunawasaka waliotekwa nyara DRC-Dujarric

Kusikiliza / Msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo Stéphane Dujarric akihutubia waandishi habari.(Picha:UM/Mark Garten)

Umoja wa Mataifa umesema unaendelea na msako dhidi ya wataalamu wa kimataifa wawili na wafanyakazi watatu raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC ambao walitekwa nyara na watu wasiojulikana jimboni Kasai nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo Stéphane Dujarric amesema malalamiko ya [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Guterres azungumzia mapendekezo ya bajeti ya Marekani 2018

Kusikiliza / Walinda amani katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS waadhimisha siku ya walinda amani. Picha: UM/JC McIlwaine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ameazimia kufanyia marekebisho chombo hicho na kuhakikisha kuwa kinakidhi malengo na kuleta matokeo bora kwa gharama yenye unafuu. Bwana Guterres amesema hayo kufuatia Ikulu ya Marekani kuweka wazi mapendekezo ya bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka wa 2018, mapendekezo ambayo inaelezwa yanalenga kupunguza matumizi kwenye maeneo [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya haki kwa Sudan Kusini ni muhimu zaidi hivi sasa- Mogae

Kusikiliza / Mogae 2

Mwenyekiti wa tume ya pamoja ya ufuatiliaji na tathmini ya hali ya Sudan Kusini, JMEC, Festus Mogae ameshutumu vikali ghasia, mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu unaotekelezwana vikundi vyote vilivyojihami nchini humo. Akifungua mkutano wa wazi wa JMEC kwenye mji mkuu Juba, Bwana Mogae ambaye ni rais mstaafu wa Botswana ametaka wale wote wanaohusika [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yaleta unafuu kwa wanawake wanaofuga kuku Gambia

Kusikiliza / Mwanamake mjasiriamali anakusanya mayai. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema miradi yake katika nchi za Afrika imeanza kukwamua wanawake wajasiriamali kwa kuwawezesha kuinua vipato na wakati huo huo kuhakikisha upatikanaji wa chakula. Afisa mwandamizi FAO anayehusika na usawa wa kijinsia na maendeleo vijijini Thacko Ndiaye amesema hayo katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila kwa wajawazito ni kama siri ya mtungi ajiuaye ni kata-Dr Tshanda

Kusikiliza / Mama Madeleine Kanku aliamua kujifungua katika kituo cha afya huko DRC.(Picha:UNFPA DRC

Kikao cha 61 cha kamisheni ya hadhi ya wanawke duniani leo mbali na mada zingine kimesikiza taarifa kutoka asasi za kiraia. Miongoni mwa wanaoshiriki kikao hicho ni Dr Micrette Ngalula Tshanda kutoka Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Yeye ni daktari bingwa wa masuala ya wanawake kwa ushirikiano na mumewe wameanzisha shirika lililo [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukwepaji sheria ndio adha kubwa Sudan kusini-UM

Kusikiliza / Huku mapigano yakiendelea baadhi ya watu wanafurushwa makwao kama wakimbizi hawa waliomba hifadhi kanisani huko Wau, Sudan Kusini.(Picha:UNICEF/UN027524/Ohanesian)

Tume ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Sudan Kusini, imesema hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota nchini humo, huku uvunjaji wa sheria, watu kuswekwa rumande kiholela, utesaji, ubakaji na mauaji vikigeuka kuwa kasumba. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Mwenyekiti wa tume hiyo Yasmin Sooka ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutia [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani endelezeni usaidizi kwa CAR, hali inadorora

Kusikiliza / Raia na watoto nchini CAR. Picha: MINUSCA

Hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR inazidi kudorora tangu kuanza upya kwa mapigano mwezi Septemba mwaka jana hadi mwezi huu wa Machi. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Kaimu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Michel Yao amesema hayo wakati wa kikao cha wahisani [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake ni kikwazo katika mazingira ya sasa ya ajira

Kusikiliza / Fundi viatu1

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW61 ukiingia siku ya nne hii leo, mmoja wa washiriki amesema ukatili dhidi ya wanawake unaendelea kuwa kikwazo cha wanawake kushiriki ipasavyo katika mazingira ya ajira hivi sasa yanayobadilika. Akihojiwa na Idhaa hii jijini New York, Marekani kando mwa CSW, Maureen Mukalo wa shirika la [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031