Nyumbani » 15/03/2017 Entries posted on “Machi 15th, 2017”

Uganda, Kenya zimepiga hatua katika kuwawezsha wanawake:Mawaziri

Kusikiliza / Waziri wa Sicily Kariuki wa Kenya akishiriki vikao vya CSW61.(Picha:Sicily Kariuki)

Kikao cha ngazi ya mawaziri kilichoangazia uwezeshaji wa wanawake na uhusiano wake katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs, kimefanyika hii leo ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 61 tume ya hadhi ya wanawake CSW61 unaondelea mjini New York, Marekani. Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wamehutubia kikao hicho akiwamo waziri wa jinsia ,kazi na maendeleo ya jamii [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lajadili jinsi ya kukomesha usafirishaji haramu wa binadamu

Kusikiliza / Wasichana nchini Columbia ambao wamelazimishwa kufanya biashara ya kingono.  Picha: UNICEF/Donna DeCesare

barazauhalifu Takwimu bora na ufadhili vitakuwa muhimu sana katika vita vya kimataifa vya kukomesha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatano akihutubia baraza la usalama. Mabalozi kutoka nchi wanachama wamekutana kujadili njia za kuzuia mitandao ambayo inafaidika na uhalifu kama kazi za shutruti, uhalifu [...]

15/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake wadhihirisha kuwa kazi ni kazi bora iwe halali

Kusikiliza / wanawake11

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hali  ya wanawake duniani, CSW61 ukiendelea kushika kasi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania wanawake wa mashinani wameanza kuonyesha bayana kuwa zama za kazi fulani ni za wanaume na nyingine ni za kike zimepitwa na wakati. Mathalani udereva wa magari ya abiria, uwakala wa wasafiri na [...]

15/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Imarisheni sitisho la mapigano Syria tufikie walengwa- Guterres

Kusikiliza / Syria-3

Kwa miaka sita sasa, wananchi wa Syria wamekuwa wahanga wa moja ya majanga makubwa zaidi kukumba dunia zama za sasa. Ndivyo ilivyoanza taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António  Guterres aliyoitoa wakati huu ambapo vita hivyo vinaingia mwaka wa saba ambapo ametangaza maombi mawili ya dharura. Mosi ametaka pande husika kutumia ipasavyo sitisho [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maarifa ni sehemu kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani-WIPO

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa WIPO ni Francis Gurry.(Picha:WIPO/ Emmanuel Berrod)

Shughuli za uchumi kote duniani zina kipengee muhimu cha maarifa kuliko wakati mwingine wowote, kwa mujibu wa takwimu za karibuni zilizotolewa na shirika la kimataifa la hati miliki (WIPO). Katika Ripoti yake kwa mwaka 2016 shirika hilo linasema limeshuhudia idadi kubwa ya maombi ya kimataifa ya kulinda masuala ya ubunifu, nembo za biashara na mitindo [...]

15/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Somalia yaanza kutoa chanjo dhidi ya Kipindupindu

Kusikiliza / Utoaji wa chanjo nchini Somalia.(Picha:UNICEF)

Serikali ya Somalia kwa usaidizi wa shirika la afya duniani, WHO limeanza kutoka chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa watu zaidi ya 450,000 nchini humo. Mwakilishi wa WHO nchini Somalia Dkt. Ghulam Popal amesema watoto wenye umri wa kuanzia miaka miwili hadi watu wazima watapatiwa chanjo hiyo ya matone kwa awamu mbili kwenye maeneo [...]

15/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake wakishiriki katika uongozi huchochea maendeleo

Kusikiliza / wanawake- CSW61-2

Mkutano 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake duniani CSW, unaendelea  kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, leo pamoja na mambo mengine mjadala unajikita zaidi katika uwezeshaji wa wanawake na malengo ya maendeleo endelvu SDGs. Wawakilishi wa makundi ya wanawake kutoka mashinani hususani barani Afrika wanaeleza changamoto na mafaniko katika [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwakilishi wa wanawake kwenye serikali na bunge wadorora- IPU

Kusikiliza / Mkutano wa kando katika CSW61 kuhusu usawa wa kijinsia kwenye siasa. Picha: IPU

  Idadi ya wanawake walioko kwenye serikali na mabunge kote duniani inadorora licha ya matumaini kuwepo mwaka 2015. Hiyo ni kwa mujibu wa ramani mpya kuhusu wanawake katika siasa mwaka 2017 iliyozinduliwa hii leo jijini New York, Marekani na umoja wa mabunge duniani, IPU na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya wanawake, UNWomen [...]

15/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto wa Syria na wimbo #Heartbeat wa kuibua matumaini

Kusikiliza / Mtoto Syria

  Miaka sita ya vita nchini Syria ikiwa imetimu, watoto nchini humo wameimba wimbo uitwao Heartbeat au mapigo ya moyo kwa lengo la kutuma ujumbe wa matumaini licha ya madhila wanayokumbana nayo kila uchao. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Nats.. Wimbo unaanza kwa kuonyesha magofu yatokanayo  na mapigano ya miaka sita sasa [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wanawake Kigoma wapewa misaada

Kusikiliza / Sifa na wanae, Riziki na Yamlele, na mjukuu wake katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania.(Picha:UNHCR/T.Monboe)

Wanawake wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Tanzania wamepatiwa misaada ya vifaa vya kujisafi ikiwa ni sahemu ya kuhifadhi hadhi za wanawake ambao hukabiliwa na changamoto nyingi hususani wawapo ukimbizini. Katika mahojiano na Simavu Nangolo wa redio wa shirika Umoja Radio ya Nyarugusu Kigoma, Meneja wa shirika la Twesa Alex Ndondeye, shirika ambalo hufanya [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen yahitaji msaada wa dharura wa chakula- FAO

Kusikiliza / Mwanamke na mtoto wake kijijini nchini Yemen. Picha: FAO/Rawan Shaif

  Uhaba mkubwa wa chakula unatishia uhai wa zaidi ya watu milioni 17 nchini Yemen ambako mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanaendelea kushika kasi tangu mwaka 2015. Taarifa hizo zimo kwenye ripoti ya uchambuzi kuhusu uhakika wa chakula nchini humo, ripoti iliyochapishwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wa misaada ya [...]

15/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini imeanza kuwahamisha watu kwa kuzingatia makabila yao

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani katika kitua cha uhamishaji nchini Sudana Kusini. Picha: UNMISS

  Serikali ya Sudan Kusini imeanza kampeni ya kuorodhesha na kuhamisha watu kwa mujibu wa makabila yao amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Yasmin Sooka ambaye pia ni mwenyekiti wa tume maalumu ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa haki za binadamu Sudan Kusini, akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031