Nyumbani » 14/03/2017 Entries posted on “Machi 14th, 2017”

Ni wakati wa malipo sawa kwa wanaume na wanawake:UN Women

Kusikiliza / Patricia Arquette mcheza filamu mashuhuri wa Marekani akizungumza katika mjadala wa malipo sawa baina ya wanawake na wanaume kwenye UM New Yoyk . Picha na UN Women Ryan Browm

Patricia Arquette nyota wa Marekani wa kucheza filamu amekuwa miongoni mwa wanaharakati mashuhuri waliotoa wito katika kikao cha 61 ya kamisheni ya hali ya wanawake duniani wa kumaliza tofauti za kijinsia imataifa na kuziba pengo la malipo baina ya wanaume na wanawake. Kikao hicho kilichofunguliwa Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New [...]

14/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kilimo cha buni chastawisha maisha ya wanawake Uganda.

Kusikiliza / Mama na kijana mvulana wakivuna buni. Picha: FAO

Ujasiriamali ni miongoni mwa mikakati bunifu ya kuwawezesha wanawake kuinuka kiuchumi wakati huu ambapo malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanapigia chepuo uwezeshaji wa wanawake katika kila ngazi. Nchini Uganda, licha ya changamoto kadhaa, Betty ni mfano wa wanawake waliofanikiwa kupitia kilimo cha mibuni. Ungana na John Kibego katika makala ya kumulika mafaniko ya mwanamke huyo.

14/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu wanahitaji msaada haraka baada ya kimbunga kuipiga Madagascar:IFRC

Kusikiliza / Kimbunga Enawo kikipiga Madagascar, kimeua, kuathiri mioundombinu na mashamba pia:Picha na WMO

Maelfu ya watu nchini Madagascar wanahitaji haraka misaada ya kibinadamu baada ya Kimbunga Enawo kupiga kisiwa hicho na kuharibu nyumba huku mafuriko ykiathiri mashamba na jamii ambapo shikisho la chama cha msalaba mwekundu IFRC limeanza kutoa msaada wa dharura. Inakadiriwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia, karibu watu 200 kujeruhiwa na wengine zaidi ya 84,500 kuyahama [...]

14/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ulaya na Asia ya Kati zaingia katika mfumo mpya wa utapia mlo:FAO

Kusikiliza / Picha: FAO

Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo FAO inasema Ulaya na Asia ya Kati inaingia katika mfumo mpya wa utapiamlo, ikiainisha ongezeko la utipwatipwa na maradhi mengine yanayoambatana na hali hiyo. Shirika hilo linasema ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa kipato vimesaidia kuondoa njaa katika kanda hizo lakini pia umesababisha mabadiliko ya mfumo kwa [...]

14/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi mkuu wa IOM azuru kituo cha wahamiaji Niger:

Kusikiliza / Jopo la IOM ziarani NIger. Picha:IOM

Mwishoni mwa juma, Mkurugeni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, William Lacy Swing ameanza ziara ya siku tatu nchini Niger ambako amekutana na viongozi wa kitaifa na kikanda , na pia kutembelea kituo cha muda cha wahamiaj kwenye mji mkuu wa taifa hilo Niamey. Bwana Swingi amekwenda pia katika mji wa jangwani wa [...]

14/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Syria, janga kubwa zaidi la kibinadamu tangu vita ya kuu ya pili ya dunia: Zeid

Kusikiliza / Mtoto aliye na umri wa miaka 7 anasimama mbemele ya shule yake iliyoboromoka huko Idleb, Syria. Picha: UNICEF

Akilihutubia  jopo la ngazi ya juu la baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi hii leo,  Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa   Zeid Ra’ad Al Hussein, amesema vita vya Syria ni janga baya zaidi la kibinadamu tangu vita pili ya dunia. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Sauti ya Flora) Zeid [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Buba waendelea kushambulia watoto duniani: WHO

Kusikiliza / Buba waendelea kushambulia watoto duniani. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema ugonjwa wa buba ambao hushambulia zaidi watoto bado unazishambulia nchi 13 duniani, licha ya shirika hilo kutangaza mwaka jana kuwa  India haina tena ua. Taarifa ya shirika hilo kuhusu ugonjwa huo inasema kuwa matibabu yake ni rahisi kwani dozi moja pekee ya kunywa ya dawa iitwayo kwa kitaalamu azithromycin, [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uikukwaji na ukatoili mkubwa unaendelea Libya:UM

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Jumanne kwamba imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, sheria za kimataifa za binadamu na ukatili kutoka pande zot e za mzozo tangu kuzuka tena kwa uhasama Machi 3 mwaka huu. Ofisi hiyo inasema habari za kuaminika zinaeleza kwamba mauaji ya [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wa kiume badilikeni, wajumuisheni wasichana-Kuria

Kusikiliza / Kelvin Machariya Kuria, Balozi wa vijana kutoka serikali ya Kenya. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Kelvin Macharia Kuria, Balozi wa vijana kutoka serikali ya Kenya, ni miongoni wa washiriki katika mkutano wa 61 wa kamisheni ya wanawake CSW, unaoendelea jijini New York, anasema mitizamo kwa vijana wa kiume kuhusu vijana wenzao wa kike ni nyenzo katika kuwawezesha wanawake kujumuishwa. Kuria ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa nchini Kenya kuna [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame umeyaweka rehani maisha ya watoto Somalia-UM

Kusikiliza / Ukame uliopo Somalia unahatarisha hali ya watoto.(Picha:UNIfeed/video capture)

Magonjwa yanayohusiana na ukame yamekatili maisha ya watoto 47 katika miiezi miwili iliyopita katika moja ya hospitali inayoendeshwa na serikali mjini Mohadishu Somalia. Rosemary Musumba na taarifa kamili (TAARIFA YA ROSE) Umoja wa Mataifa umetoa onyo kwa dunia kwamba athari za ukame ukichanganya na vita katika taiafa hilo la Pembe ya afrika zinaweza kuwa zahma [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Badala ya kutuhurunmia tuwezesheni watu wenye ulemavu: Seneta Omondi

Kusikiliza / Seneta Omondi ambaye ni mwanamke mwenye ulemavu akiwakilisha kundi la wanawake na wasichana wenye ulemavu. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake kinaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kikihusisha watu kutoka kila kundi kwenye jamii wakiwemo wenye ulemavu. Wakipaza sauti zao wanasema kuwahurumia wanawake na wasichana wenye ulemavu hakuna tija, tuzingatie nmana ya kuwawezesha, hii ni kauli ya mmoja wa washiriki wa mkutano wa 61 kamisheni [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031