Nyumbani » 10/03/2017 Entries posted on “Machi 10th, 2017”

Simulizi ya wanawake Afghanistan itabadilika wakishiriki kwenye uongozi – UNAMA

Kusikiliza / Wanawake nchini Afghanistan wakijadiliana
Picha: UNAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao chake kuhusu Afghanistan ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Tadamichi Yamamoto amesema katika nusu ya kwanza ya kipindi cha serikali ya umoja wa kitaifa, tayari hatua za maendeleo zimepigwa licha ya changamoto zinazotakiwa kupatiwa suluhu siku zijazo. Ametaja maeneo matatua ambayo yameonyesha [...]

10/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi Kigoma waadhiimisha siku ya wanawake

Kusikiliza / Wanawake wakimbizi nchini Tanzania.(Picha:UNFPA/Tanzania)

Maadhimisho ya siku ya wanawake nchini Tanzania yamefanyika sehemu mbalimbali licha ya kwamba kitaifa yamefanyika mkoani Singida. Mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, mvua kubwa iliyonyesha awali haikuwazuai wananchi kujitokeza kuhudhuria maadhimisho hayo yaliyotia fora kwa burudani na ujumbe. Tuungane na Mabamba Mpela Junior

10/03/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Jabari

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Wiki hii tunaangazia neno Jabari na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja, maana ya kwanza ni mtawala mkuu wa pekee, maana ya pili ni mtu shujaa asiye na woga na maana ya tatu ni jeuri.

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Kuelekea 2030, wanawake wamejizatiti kufikia #5050

Kusikiliza / Wanawake wanaohsikilia nafasi mbali mbali katika jamii,Afrika Mashariki.(Picha:UM)

Tarehe Nane mwezi Machi, kwa zaidi ya karne moja sasa, imekuwa ni siku  ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Siku hii ikiangazia harakati za kuweka usawa wa kijinsia kwa mustakhbali bora siyo tu wa kundi hilo ambalo ni zaidi ya asilimia 50 duniani, bali pia kwa ulimwengu wote kwani wahenga walisema ukimwendeleza mwanamke umeendeleza jamii [...]

10/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Burudani zasheheni wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Kusikiliza / Wanawake nchini Tanzania katika maadhimisho ya siku ya wanawake. Picha: UM

Wanawake wameshamiri juma hili. Mataifa mengi yameadhimisha siku ya wanawake duniani mnamo Machi nane, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka, lengo likiwa kupigia chepuo haki na ustawi wa kundi hilo katika nyanja mbalimbali. Katika makala ifuatayo Assumpta Massoi anamulika namna burudani ilivyotumiwa kufikisha ujumbe hususani nchi zenye mizozo, huku ikiwaliwaza washiriki, wakiongozwa na wanawake ambao ni [...]

10/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya makataba wa amani , machafuko yafurusha maelfu Colombia-UNHCR

Kusikiliza / Soko lilioko San Jose au San Jude jijini Buenaventura nchini Colombia. Picha © UNHCR/Juan Arredondo

Licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani baina ya serikali ya Colombia na kundi la upinzani liitwalo FARC, mwezi Novemba mwaka jana, machafuko nchini humo yanaendelea kufurusha maelfu ya watu, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Mapigano baina ya vikosi hivyo yamedumu kwa miaka 50. UNHCR licha ya kutambua juhudi za [...]

10/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatari zaidi ya Zika kwa nchi zenye mbu Aedes Aegypti- WHO

Kusikiliza / Mbu wa Aedes anayeambukiza virusi vya Zika. Picha ya WHO

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa mwongozo na orodha mpya ya nchi 70 ambazo ziko hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Zika. Mataifa hayo yako katika kanda mbali mbali ikiwemo Ulaya, Amerika, Asia na Afrika ambapo WHO imesema miongoni mwao ni nchi ambako mbu anayeeneza virusi hivyo Aedes Aegypti anapatikana, ingawa maambukizi hayajaripotiwa. Barani [...]

10/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaada wa chakula wawafikia maelfu ya wahitaji Sudan Kusini

Kusikiliza / Wakazi wa Sudan Kusini wapokea mgao wa chakula.9Picha:WFP/Peter Testuzza)

Zaidi ya watu Laki Tatu waliokuwa wanakabiliwa na njaa huko Sudan Kusini wamefikishiwa misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula. Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya kibinadamu Jens Laerke amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kutangazwa kwa baa la njaa lililotokana na ukame kwenye maeneo ya Leer na Mayendit tarehe 20 mwezi [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasichana 20 wauawa baada ya jengo la makazi kuteketea Guatemala

Kusikiliza / Msichana anacheza na kna mabati kutoka jengo liloloporomoka nchini Guatemala. Picha: © UNICEF/NYHQ2007-2316/Michael Kamber

Nchini Guatemala, wasichana 20 wameteketea kwa moto baada ya jengo lao la makazi kuungua kitendo ambacho kimehuzunisha shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) UNICEF inasema tukio hili la kutisha pia limejeruhi wengine wengi na imeitaka serikali ya Guatemala na na maeneo ya kikanda kuachana [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Salva Kiir atubu kwa niaba ya taifa lake

Kusikiliza / Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.(Picha:UNMISS/Isaac Billy)

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amongoza maelfu ya raia nchini humo kwa ajili ya maombi maalum ya toba. Grace Kaneiya na taarifa kamili. (TAARIFA YA GRACE) Nats! Ni sauti ya Rais Kiir, katika maombi maalum ya toba yaliyofanyika kwenye makumbusho ya kiongozi wa zamani wa taifa hilo John Garang, mjini Juba ambapo kwa niaba [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya Yemen yafurusha maelfu ya watu- UNHCR

Kusikiliza / Raia wa Yemen ambao wamekimbilia majimbo ya Taiz na Al-HudaydahPicha: © UNHCR/Shabia Mantoo

Mapigano mapya kwenye maeneo ya kati na magharibi mwa Yemen yamelazimisha watu zaidi ya elfu 60 wakimbie makazi yao. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mapigano hayo yanaendelea kwa wiki sita sasa na idadi kubwa ya raia wamekimbilia majimbo ya Taiz na Al-Hudaydah. Msemaji wa UNHCR William Spindler amesema wananchi hao [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Faida za wahamiaji za kiuchumi zitambulike: UM

Kusikiliza / Wahamiaji wajasiriamali kutoka Syria walioko nchini Turkey wapata mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya mshikamano ya kijamii. Picha: IOM

Likizingatia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi na wahamiaji wa hivi karibuni, baraza la haki za binadamu hii leo mjini Gweneva Uswisi, limekuwa na mjadala shirikishi kuhusu haki za kundi hilo katika muktadha wa kuhama kwa makundi makubwa. Wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza kuwa kuheshimu haki za binadamu kwa wahamiaji sio tu hitaji la [...]

10/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usawa hautakamilika iwapo hautajumuisha wanawake mashinani

Kusikiliza / Justine Uvuza. Picha: Idhaa ya Kiswahili/Amina Hassan

Ujumuishwaji wa wanawake mashinani ni dhana isiyokwepeka katika kutimizia dhima ya maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu ambayo ni wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika, inayokwenda sambamba na lengo nambari kumi la maendeleo endelevu yaani SDG’s, ambalo linachagiza ulimwengu kupunguza ukosefu wa usawa. Akihojiwa na Idhaa hii, Dkt. Justine Uvuza wa Shirika la asasi [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031