Nyumbani » 09/03/2017 Entries posted on “Machi 9th, 2017”

Mkakati mpya unalenga kusaidia zaidi waathirika wa ukatili wa kingono

Kusikiliza / Presentation of the Sexual exploitation and abuse report

Umoja wa Mataifa umeweka bayana mkakati mpya wa kuzuia na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono vinavyotekelezwa na wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbali mbali duniani. Mapendekezo hayo yamo kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ripoti ikielezwa kuwa inaangazia zaidi waathirika wa vitendo hivyo. Katibu Mkuu aliwasilisha mapendekezo [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tukipata teknolojia wezeshi tutazalisha maradufu: Wajasiriamali Wanawake

Kusikiliza / Wanawake wajasiriamali nchini Tanzania.(Picha:ILO/Video capture)

Ukosefu wa teknolojia wezeshi unapunguza mapato kusudiwa kwa wanawake mkoani Kagera nchini Tanzania, hii ni kwa mujibu wa wajasiriamali mkoani humo ambao wanasema wakiwezeshwa kiteknolojia watazalisha maradufu. Nicolaus Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya Kagera nchini humo, amevinjari hadi wajasiriamali hao wanawake wanapofanya kazi zao ili kujionea. Ungana naye katika makala ifuatayo.

09/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini ya suluhu Burundi, nitaitisha mkutano wa dharura: Mkapa

Kusikiliza / Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi anayewakilisha Muungano wa Afrika AU, Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa. Picha: UM/Video capture

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo Machi tisa, limejadili hali ya kiusalama nchini Burundi, ambapo imeelezwa kuwa usalama umeendelea kuzorota na hofu imetanda miongoni mwa raia. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu kuzuia migogoro Jamal Benomar, ameliambia baraza hilo kuwa ikiwa ni miaka miwili tangu kuzuka kwa mgogoro nchini [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wagonjwa wa figo Yemen wahaha kupata tiba

Kusikiliza / Utoaji wa huduma wa afya kwa wagonjwa wa figo.(Picha:WHO)

Nchini Yemen, mapigano yakiwa yanaendelea kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Houthi miundombinu ya kiafya inazidi kusambaratika ikiacha wagonjwa taabani wakiwemo wale wa figo. Shirika la afya ulimwenguni WHO nchini humo linasema kutokana na mapigano, wagonjwa wa figo hivi sasa wanashindwa kupata huduma ya kusafisha damu katika vituo vingine na hivyo kulazimika kwenda [...]

09/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujasiri wa wakazi wa Ziwa la bonde Chad unatia matumiani -Balozi Rycroft

Kusikiliza / Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ambaye ni rais wa Baraza la Usalama mwezi Machi akihutubia kikao hicho.(Picha:UM/Manuel Elias)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo hapa makao makuu jijini New York kuwasilisha ripoti yake kufuatia ziara yao ya bonde la Ziwa Chad, Amina Hassan nataarifa kamili. (Taarifa ya Amina) Akihutubi kikao hicho Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ambaye ni rais wa baraza hilo mwezi huu wa Machi na pia kiongozi wa [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sitakubali anayepeperusha bendera ya UM atutie aibu- Guterres

Kusikiliza / Moja ya nukuu kutoka ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. (Picha:UN)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasilisha ripoti yake mbele ya Baraza Kuu inayotaja mikakati mipya mahsusi ya kuepusha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono kwenye operesheni za ulinzi wa amani za chombo hicho. Amesema mikakati hiyo ni muhimu kuhakikisha hakuna mtuhumiwa yeyote anakwepa sheria wakati huu ambapo watuhumiwa wa vitendo hivyo [...]

09/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yachukua hatua kuimarisha utoaji wa haki kwa watoto DRC

Kusikiliza / conference-MONUSCO

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa kushirikianana asasi isiyo ya kiraia AJEDEC na serikali wameanza ujenzi wa mahakama wilaya kwenye jimbo la Ituri. Mahakama hiyo inalenga kuimarisha usimamiaji wa haki na sheria kwa kesi zinazohusu watoto hususan visa vinavyohusiana na ulinzi wa mtoto. MONUSCO imegharimia [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka wa 7 wa vita, bado Syria iko njiapanda- UNHCR

Kusikiliza / Msichana Wafaa akiwa na mamake, yeye ni muathirka wa vita vya Syria.(Picha:UNHCR)

Wakati dunia inajiandaa kushuhudia vita nchini Syria vikiingia mwaka wa saba tangu vianze, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetaka jamii ya kimataifa iongeze maradufu usaidizi wake wakati huu ambao mamilioni ya raia wanaendelea kukumbwa na machungu. Grace Kaneiya na taarifa kamili. (Taarifa ya Grace) Filippo Grandi ambaye ni Kamishna Mkuu wa [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waalimu wa shule wasiwajibishwe kwa mipango ya majanga

Kusikiliza / Jair TORRES, Mtaalamu wa upunguzaji hatari ya majanga kwnye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Picha: UNESCO

Walimu wa shule wana majukumu ya kutosha darasani bila kutarajiwa kuwa wsimamizi wa kudhibiti hatari ya majanga pia. Mtazamo huo ni kwa mujibu wa Jair Torres, mtaalamu wa upunguzaji hatari ya majanga kwnye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO. Akiwasilisha mkakati wa tano wa UNESCO katika upunguzaji wa hatari ya [...]

09/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majanga ya kimya kimya yanayosambaratisha mazao mara nyingi hupuuzwa: FAO

Kusikiliza / jimbo la Tahoua nchini Niger, lililoathirika sana na Ukame na kuzusha hofu ya upungufu wa chakula.(Picha:WFP/Phil Behan)

Linapokuja suala la kulinda mazao na maisha ya kilimo, majanga ya kimyakimya mara nyingi hayaripotiwi na yanaweza kutokea mara nyingi na kufanya uharibifu mkubwa kuliko kimbunga au mafuriko. Hayo yamesemwa na Anna Ricoy, afisa wa shirika la chakula na kilimo FAO katika kanda ya Amerika ya Kusini ambaye ni mtaalamu wa hatari ya majanga. Bi [...]

09/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031